28/05/2026
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Government apex body coordinating sectoral and multi sectoral economic empowerment initiatives in the country.
28/05/2026
27/05/2026
27/05/2026
26/05/2026
Kikao cha 11 cha wadau wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogondogo za kifedha kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Midland Hotel mkoani Dodoma, kikilenga kuimarisha ushirikiano na kujadili mikakati ya kukuza huduma ndogo za kifedha kwa wananchi kupitia vikundi vya kifedha vya kijamii
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), CCT, Centre for VICOBA microfinance and Enterprise Development and Community Educator Empowerment Development (CEVEDE-CEED), Shirikisho la Vikcoba Tanzania (VIKOBA-FETA), Benki kuu ya Tanzania (BOT) pamoja na Dodoma Jiji.
Washiriki walijadili namna ya kuendelea kuimarisha uwezo wa vikundi vya kijamii katika usimamizi wa huduma ndogondogo za kifedha, kuongeza uelewa wa masuala ya fedha na kuweka mazingira bora ya wananchi kunufaika na fursa za uwezeshaji wa kiuchumi.
Aidha, kikao kilisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za serikali, taasisi za dini na mashirika ya maendeleo katika kuhakikisha vikundi vya kijamii vinaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
19/05/2026
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) limeendesha mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo Watoa huduma za Maendeleo ya Biashara, Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Biashara kutoka halmashauri mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utekelezaji wa programu za uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Mafunzo hayo yamewakutanisha washiriki kutoka Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Halmashauri ya Kilolo, Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Halmashauri ya Mji wa Babati pamoja na Mji wa Gairo, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu namna bora ya kutoa huduma za maendeleo ya biashara na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za kiuchumi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kaimu Katibu Mtendaji wa NEEC Bw. Gwakisa Bapala, alisisitiza umuhimu wa wataalamu hao kuwa chachu ya maendeleo kwa kuhakikisha elimu na huduma zinazotolewa zinafikia walengwa kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya katika jamii.
Aidha, Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania Bi. Neema Mwakatobe alieleza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa NEEC wa kujenga mazingira wezeshi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, huku akisisitiza matumizi ya maarifa na mbinu zinazolenga kuongeza tija katika biashara na miradi ya maendeleo.
Kwa upande wao, Wakufunzi wa Watoa huduma waliongoza vipindi vya mafunzo kwa kutoa maarifa kuhusu mbinu za utoaji huduma za maendeleo ya biashara, ushauri kwa wajasiriamali, pamoja na namna ya kuunganisha fursa za kiuchumi na mahitaji ya jamii katika maeneo yao ya kazi.
NEEC imeendelea kusisitiza kuwa uwezeshaji wa kiuchumi unahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Taasisi za serikali, wataalamu wa maendeleo na jamii ili kuhakikisha wananchi wanapata fursa stahiki za kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Dodoma
