06/09/2025
*CROWN FM - LEO*
Usikose kusikiliza kipindi kinachokupa michongo ya jinsi ya kupata tenda za Serikali kupitia Mfumo wa NeST, Jumamosi, Septemba 6, 2025. Kimepewa nguvu na
Mtangazaji:
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from PPRA_Tanzania, Government Organization, Kambarage Tower, 9th floor, PSPF Road, Dodoma.
06/09/2025
*CROWN FM - LEO*
Usikose kusikiliza kipindi kinachokupa michongo ya jinsi ya kupata tenda za Serikali kupitia Mfumo wa NeST, Jumamosi, Septemba 6, 2025. Kimepewa nguvu na
Mtangazaji:
13/07/2025
*PPRA YASHINDA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA SABASABA 2025*
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameikabidhi Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Tuzo ya Mshindi wa Kwanza kwa Mamlaka za Udhibiti katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu k**a Sabasaba 2025.
Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Meneja wa PPRA Kanda ya Pwani, Bi. Vicky Mollel, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Dennis Simba, Julai 13, 2025, wakati wa hafla ya kufunga rasmi maonesho hayo yaliyofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Mollel alisema kuwa PPRA imepokea tuzo hiyo kwa heshima kubwa kwa niaba ya wadau wote wa ununuzi wa umma waliotembelea banda la Mamlaka hiyo na kupata huduma katika kipindi chote cha maonesho. Aliongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na maandalizi bora na huduma zilizotolewa, ambazo zinaakisi utamaduni wa uwajibikaji na uchapakazi miongoni mwa watumishi wa PPRA, pamoja na uongozi madhubuti kutoka Wizara ya Fedha, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya PPRA.
Aidha, Bi. Mollel alitumia fursa hiyo kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake makubwa, hususan katika kuanzisha Mfumo wa NeST ambao umeongeza uwazi na usawa katika michakato ya ununuzi wa umma, na kuifanya sekta hiyo kuwa rafiki kwa Watanzania wote.
07/07/2025
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akisikiliza maelezo kuhusu kazi za PPRA na mafanikio ya Mfumo wa NeST yaliyotolewa na mtumishi wa Mamlaka hiyo, baada ya Mwenge wa Uhuru kufika jijini Arusha, leo.
28/06/2025
27/06/2025
Tukuhudumie
06/06/2025
Usikose kusikiliza Kasri la Kikeke, leo kuanzia saa 12 jioni kupitia
02/06/2025
MATUKIO KATIKA PICHA:
wa Uhuru 2025 - Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila (katikati) akiwa na Meneja wa PPRA Kanda ya Pwani, Bi. Vicky Mollel (wa pili kulia) na viongozi wengine wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani humo.
PPRA imeweka banda maalum la kutoa huduma kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na Mfumo wa NeST katika maeneo hayo.
Mwenge huo utakimbizwa katika wilaya zote za Mkoa huo kuanzja Juni 1-5, 2025, ukikagua miradi mbalimbali pamoja na ukidhi wa Sheria katika matumizi ya Mfumo wa NeST.
28/05/2025
Meneja wa PPRA Nyanda za Juu Kusini, Bw. Paschael Manono akitoa elimu kuhusu fursa za zabuni kwa wananchi waliotembelea banda la PPRA, katika kampeni maalum ya Malkia wa Nguvu iliyoandaliwa na Clouds Media Group, jijini Mbeya, Mei 28, 2025.
| Monday | 08:00 - 16:00 |
| Tuesday | 08:00 - 16:00 |
| Wednesday | 08:00 - 16:00 |
| Thursday | 08:00 - 16:00 |
| Friday | 08:00 - 16:00 |