Tanzania Meteorological Authority

Website Contact the organization

Tanzania Meteorological Authority Ukurasa Rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania - Official page of the Tanzania Meteorological Authority

www.meteo.go.tz

11/09/2026

NAIBU WAZIRI MHE. KIHENZILE ATOA RAI KWA WANANCHI KUHUSU EL NIÑO

Asisitiza ushawishi wa wasanii na watu mashuhuri

11/09/2026
25/08/2026

MHE. MBARAWA: MVUA KUBWA ZISISIMAMISHE KAZI ZINAZOWEZEKANA KUFANYIKA

22/08/2026

MHE. RAIS SAMIA AELEKEZA WAKUU WA MIKOA, WAKUU WA WILAYA NA WADAU MBALIMBALI KUJIANDAA KUKABILIANA NA MVUA KUBWA KUTOKANA NA UWEPO WA HALI YA ELNINO.

MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI (OKTOBA-DISEMBA),2026
19/08/2026

MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI (OKTOBA-DISEMBA),2026

TMA YATOA ANGALIZO DHIDI YA EL NINO, MSIMU WA VULI 2026Dar Es Salaam – 18 Agosti, 2026Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (...
18/08/2026

TMA YATOA ANGALIZO DHIDI YA EL NINO, MSIMU WA VULI 2026

Dar Es Salaam – 18 Agosti, 2026
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba – Desemba) 2026, ikitoa angalizo la msimu huo kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa iliyotokana na joto la bahari kuwa Juu ya Wastani katika Bahari ya Pasifiki, hali itakayochagiza ongezeko la Mvua za Vuli 2026 kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

Akizungumza juu ya utabiri huo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a alisema:-
"Msimu wa mvua za Vuli 2026 unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa, hivyo mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma”. Aliongezea kusema kuwa Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba hadi wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba 2026 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria, na kusambaa taratibu katika maeneo mengine katika mwezi Oktoba 2026, aidha alifanunua kuwa kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Desemba japo katika msimu wa Vuli 2026 mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Januari 2027, na ongezeko la mvua likitarajiwa hasa katika kipindi cha mwezi Novemba 2026.

Akielezea juu ya athari zinazotarajiwa, Dkt. Chang’a ametahadharisha kuwa "vipindi vya unyevu kwenye udongo wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo," pia aliongezea kusema kuwa ongezeko la kina cha maji katika mabwawa na mito linaweza kuathiri miundombinu ya rasilimali za maji na nishati, huku magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji. Magonjwa ya mazao yanayosababishwa na kuvu, bakteria na virusi yanaweza kuathiri uzalishaji wa viazi mviringo, alizeti, maharage, ufuta pamoja na matunda na mbogamboga, huku sekta za usafiri, ujenzi na utalii zikitarajiwa kukumbwa na changamoto za mmomonyoko wa barabara, uharibifu wa madaraja na kuhama kwa wanyamapori kutokana na mafuriko.

Katika hitimisho lake, Dkt. Chang’a amewashauri Wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia taarifa mahususi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA ikiwa ni pamoja na kuvuna maji ya mvua, kuimarisha miundombinu, kutoa tahadhari za mapema na kudhibiti mazalia ya mbu ili kupunguza magonjwa ya mlipuko.

Kwa taarifa zaidi tembelea:

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑODodoma, 14 Agosti 2026: Mwenyekiti wa...
14/08/2026

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Dodoma, 14 Agosti 2026:

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mheshimiwa Jaji Mshibe Ali Bakari, amezitaka sekta zote nchini kutumia ipasavyo taarifa za hali ya hewa katika kufanya maandalizi ya kisekta ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na uwepo wa El Niño.
Mhe. Jaji Mshibe aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 25 wa kujadili Utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli, Oktoba hadi Disemba 2026, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF, Dodoma.
“Tunapojiandaa kupokea taarifa ya utabiri wa mvua za Vuli, Oktoba hadi Disemba 2026, ni muhimu kila mmoja wetu kuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu na kuelewa taarifa hizo ili kuanza maandalizi ya hatua za kuchukua katika kukabiliana na athari za hali ya hewa zinazotarajiwa kujitokeza katika sekta yake, kwa kutambua kuwa upo uwezekano mkubwa kwa El Niño kuendelea kuimarika kuelekea mwishoni mwa mwaka 2026,” alisisitiza Mhe. Jaji Mshibe.

Mhe. Jaji mshibe aliongeza kuwa Tanzania, k**a ilivyo kwa nchi nyingine duniani, inaendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayodhihirishwa kupitia ongezeko la joto, ukame, upepo mkali, vimbunga na vipindi vya mvua kubwa vinavyoweza kusababisha mafuriko, hivyo amewataka wadau wasiishie katika kupokea taarifa za utabiri wa hali ya hewa, bali wazitumie katika kufanya maamuzi yanayozingatia mazingira ya sekta na maeneo yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a, alisema TMA imeendelea kuboresha utoaji wa taarifa za hali ya hewa, ikiwemo kuandaa utabiri mahususi kwa maeneo madogo kwa wilaya 86 zilizopo katika mikoa inayopata mvua za Vuli, hatua inayolenga kuhakikisha kila wilaya na sekta husika zinaweza kutumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya maamuzi na kupanga shughuli zao.

Aidha, Dkt. Chang’a alimalizia kwa kusisitiza kuwa taarifa za utabiri na tahadhari zinapaswa kuzingatiwa katika sekta zote za kiuchumi na kijamii, kwa lengo la kuongeza tija na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa itakayotokana na uwepo wa El nino nchini.

“Nitumie fursa hii kuwajulisha kuwa mwaka huu 2026 tunakabiliwa na changamoto ya El Nino ambayo inatarajiwa kuendelea kuimarika kuelekea mwishoni mwa mwaka na hivyo kuchagiza mvua za VULI, hivyo basi matumizi sahihi na kwa wakati ya taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa Kila sekta katika kukabiliana na changamoto hii”. Alisema Dkt.Chang’a.

Naye, mwakilishi wa wadau mbalimbali kutoka Zanzibar, Bw. Makame Kh Makame, Mkurugenzi wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar, Alisema "Utabiri wa hali ya hewa ni jambo moja muhimu mno hasa katika kipindi cha El -Nino ambapo jamii na sekta zote muhimu zinahitaji kujikinga, kujiandaa, kukabiliana na majanga au maafa yanayoweza kutokea sambamba na kurejesha hali baada ya maafa".

Mkutano huo uliobeba kaulimbiu: “Kupunguza Pengo la Uelewa wa Tahadhari za Hali ya Hewa kwa Pamoja.” ulihusisha pia utoaji wa mrejesho kutoka kwa wadau kuhusu utabiri wa msimu wa mvua za Masika uliokuwa na usahihi wa asilimia 94.1.

TMA inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2026 tarehe 18 Agosti 2026.

TANZIA
10/08/2026

TANZIA

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Meteorological Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Meteorological Authority:

Shortcuts

Share