Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Share

Karibu Katika ukurasa rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

13/05/2026
Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu's post 13/05/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba Mkoani Dodoma leo Mei 13,2026.

Aidha, Katika ukaguzi huo Waziri Sangu aliambatana na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Dkt.Evaline Munisi pamoja na Viongozi wa Wizara hiyo.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu's post 08/05/2026

WAFANYAKAZI WALIOPOTEZA AJIRA KULIPWA MKUPUO NDANI YA SIKU 90

Na. OWM-KAM

Serikali imeendelea kuboresha Mifumo ya Hifadhi ya Jamii nchini kwa kufanya maboresho ya kanuni za ulipaji wa mafao ili kuongeza ulinzi na ustawi wa wafanyakazi wanaopoteza ajira wakiwa kazini.

Hayo yamebainishwa Mei 8, 2026 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Mhe. Ado Shaibu Ado, lililohoji kauli ya serikali juu ya Fao la kujitoa kwa Waajiriwa na lini Serikali inafikiria kuanzisha Fao hilo.

Akijibu swali hilo, Dkt. Munisi amesema Serikali imefanya maboresho ya kanuni za fao la kukosa Ajira ili kumpa mwanachama uchaguzi wa namna ya kunufaika baada ya kupoteza ajira ambapo mtumishi sasa anaweza kuamua kulipwa mkupuo maalumu au kuendelea kulipwa asilimia 33.3 ya mshahara wake kwa kipindi cha miezi sita. Utaratibu huo unaolenga kumwezesha kuendelea kuwa na sifa za kupata pensheni atakapostaafu.

Amesema maboresho hayo yanaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha watumishi wanaopoteza Ajira wanapata kinga ya kiuchumi bila kuathiri mafao yao ya muda mrefu ya uzeeni.

Sambamba na hayo Dkt. Munisi ameeleza kuwa Serikali tayari imesaini kanuni mpya mwaka 2025 zinazomruhusu Mwajiriwa aliyepoteza Ajira kulipwa mafao yake kwa mkupuo ndani ya siku tisini tangu kupoteza ajira hiyo.

*Katika mifuko ya hifadhi ya jamii hakuna fao la kujitoa kwa mwanachama anapopoteza ajira, bali kinachotambuliwa kwa sasa ni fao la kukosa ajira lililoboreshwa mwaka 2025 ili kuendana na mahitaji ya wafanyakazi na hali ya soko la ajira nchini.* amesema.

Hatua hiyo ya Serikali inaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii na kuhakikisha wafanyakazi wanapata usalama wa kipato wanapokumbwa na changamoto ya kupoteza ajira.

MWISHO

08/05/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi leo Mai 8, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.

07/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. M***a Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi pamoja na Mawaziri wa Sekta mbalimbali katika picha na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt. Evaline Wilbard Munisi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.

07/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. M***a Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi katika picha na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt. Evaline Wilbard Munisi pamoja na Viongozi wengine wa ofisi hiyo, tarehe 6 Mei, 2026 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.

Photos from Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu's post 06/05/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Ajira na Mahusiano Mhe.Deus Sangu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kwa watumishi wa Ofisi hiyo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Mhe. Sangu amesema hayo wakati ya mapokezi ya Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Dkt. Evaline Munisi leo tarehe 6 Mei, 2026, Jijini Dodoma na kueleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita imeweka mkazo kwenye uwajibikaji na kutoa huduma bora hivyo amewataka watumishi wote wafanye kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo ya ofisi hiyo.

Aidha, Waziri Sangu amewataka viongozi na watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana kwa karibu na Naibu Waziri, Evaline Munisi.

Vilevile, amewahakikishia watumishi kuwa wataendelea kuimarisha mazingira ya kazi, ajira na Mahusiano ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wananchi zinakwenda sambamba na malengo ya Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Evaline Wilbard Munisi amewapongeza na kuwashukuru watumishi wa Ofisi hiyo kwa mapokezi mazuri na kuwaahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ili kufanikisha malengo ya ofisi hiyo.

MWISHO

06/05/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Mji Wa Serikali, Mtumba
Dodoma