Duwasatz

Duwasatz

Share

Sambamba na hayo DUWASA pia inatoa huduma ya maji bure kwa watu wasiojiweza.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Mjini Dodoma-DUWASA inatoa huduma ya usambazaji wa maji safi pamoja na uondoshaji wa majitaka ikiwa ni usafi wa mazingira Jijini Dodoma.

Photos from Duwasatz's post 09/05/2026

SERIKALI KUMALIZA KERO YA MAJI KIBAIGWA - KONGWA

Serikali imewahakikishia wakazi wa Kata ya Kibaigwa, Wilayani Kongwa, kumalizika kwa changamoto ya upatikanaji wa majisafi, kufuatia mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kununua mitambo ya kisasa ya kuchimbia visima kwa kila mkoa nchini.

​Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mei 08, 2026.

​Akifafanua jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya maji, Dkt. Nchemba alibainisha kuwa hatua ya awali ya upatikanaji wa mitambo imekamilika, na sasa Serikali inaelekeza nguvu kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa.

​"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshakamilisha ununuzi wa mitambo ya kuchimbia visima kwa kila mkoa. Hatua inayofuata sasa ni kutenga Bajeti mahususi ya kununua vifaa na kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya maji itakayomaliza kero hii kwa wananchi wa Kibaigwa na maeneo ya jirani," alisema Dkt. Nchemba.

​Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, ameshiriki kikamilifu kuhakikisha maelekezo ya Serikali yanatekelezwa kwa manufaa ya Wananchi wa Kibaigwa.

​Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili katika Wilaya za Kongwa (Kibaigwa) na Mpwapwa. Lengo kuu la ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Photos from Duwasatz's post 07/05/2026

KIKAO KAZI CHA WAKURUGENZI WATENDAJI WA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), Leo tarehe 07 Mei, 2026 amekutana na kuzungumza na Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji NCHINI Jijini Dodoma juu ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 iliyopitishwa Mei 06,2026.

Waziri Aweso amewasisitiza Wakurugenzi katika uwajibikaji, ufanisi na usimamizi madhubuti wa miradi ya maji kwa kuzingatia matokeo yenye manufaa kwa wananchi.

Aidha, Waziri Aweso amewataka Wakurugenzi hao kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na ushirikiano ili kuendelea kuisogeza mbele sekta ya maji nchini sambamba na kutekeleza maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu ya maji.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amewasisitiza Wakurugenzi hao Watendaji wa Mam amesisitiza kufanya kazi kwa weledi, ushirikiano na nidhamu ili kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwa kwa ufanisi na huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati.

Photos from Duwasatz's post 06/05/2026

DUWASA YASHIRIKI WASILISHO LA BAJETI YA WIZARA YA MAJI KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Fadhili Chibago na Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi Aron Joseph, imeshiriki Mkutano wa 13 wa Bunge, Kikao cha 22 na 23, uliohusisha Wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma Mei 05 – 06, 2026.

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti hiyo, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amesema, katika Jiji la Dodoma hadi kufikia Disemba 2025, Serikali kupitia Mamkaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imetekeleza miradi 18 yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.7 na itasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milioni 54 hadi 88 kwa siku.

Amesema, mahitaji ya ya sasa ni Lita Milioni 159.9 kwa siku, ili kuongeza uzalisha wa maji kutoka Lita Milioni 88 hadi 127 kwa siku ambayo itakuwa ni sawa na asilimia 75 ya mahitaji kwa siku, na kwamba Serikali imeanza utekelezaji wa miradi sita (6) yenye thamani ya shilingi Bilioni 51. Miradi hiyo ni pamoja na Nzuguni PhaseII, Nala Phase II, Zuzu, Mradi wa kuboresha maji Chuo Kikuu cha Dodoma na Hospital ya Benjamini Mkapa.

Mhe. Aweso ameitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na Kisasa-Njedengwa na Mradi wa Maji katika Mji wa Serikali (Magufuli City), ambapo kukamilika kwa miradi hii kutaongeza uzalishaji wa maji na kupunguza migao maeneo ya Mkonze, Miganga, Chidachi, Michese, Kinyambwa Extension, Zuzu, Nala, Nkuhungu, Ilazo, Ipagala, Swaswa, Mpamaa, Kisasa, Iyumbu, Njedengwa, Ihumwa na Mtumba.

Akizungumza baada ya wasilisho hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya DUWASA, Bw. Chibago, amesema bajeti hiyo inatoa matumaini kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kwa kuwa inalenga kutatua changamoto ya maji katika maeneo yanayohudumiwa na DUWASA.

Chibago amesisitiza dhamira ya kuimarisha huduma kwa wateja kwa kupunguza Upotevu wa Maji, kuongeza vyanzo vya maji na kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan walio pembezoni mwa Jiji.

Waziri Aweso ameomba Bunge kuidhinisha kiasi cha takriban shilingi Trilioni 1.12 kwa ajili ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Photos from Duwasatz's post 02/05/2026

*Mhandisi Aron Joseph Ahimiza Bidii na Mashirikiano Kuboresha Huduma ya Maji Mpwapwa*

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amewataka watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mpwapwa (MPWUWSA) kufanya kazi kwa bidii, weledi, na ushirikiano ili kuhakikisha huduma ya maji inaimarika kwa wakazi wa mji huo.

Mhandisi Joseph ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo, wakati akimtambulisha Meneja mpya wa Mamlaka ya MPWUWSA.

Hatua hiyo inafuatia mabadiliko ya hivi karibuni ya uongozi yaliyofanywa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb), yenye lengo la kuongeza ufanisi katika sekta ya maji nchini.

"Lengo letu kuu ni kuona mabadiliko chanya. Huduma ya maji ni hitaji la msingi, hivyo ushirikiano kati yenu na Meneja mpya ndio utakaowezesha kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara," alisisitiza Mhandisi Joseph.

Mabadiliko haya ya uongozi yanatarajiwa kuleta chachu mpya katika usimamizi wa miradi ya maji na kutatua changamoto za upatikanaji wa maji ambazo zimekuwa zikiwakabili wakazi wa wilaya ya Mpwapwa kwa muda mrefu.

Photos from Duwasatz's post 01/05/2026

TUGHE DUWASA YAPONGEZWA KWA KUSIMAMIA MASLAHI YA WATUMISHI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amewashauri Watumishi kuhakikisha wanajiunga na Chama cha Wafanyakazi -TUGHE kwani kimekuwa msaada mkubwa kwa watumishi.

Mha. Aron ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa DUWASA kwenye Hafla ya Jioni katika kusherehea Siku ya Wafanyakazi Diniani.

Amewataka Watumishi kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi kutimiza wajibu wao katika kutoa Huduma Bora kwa wananchi.

"Lazima tuendelee kushindana kutimiza wajibu kwa kuhakikisha kila mtu anatimiza majukumu yake, mimi nitatimiza wajibu wangu na atakae tuangusha huyo hatakuwa mwenzetu . Amesema Mhandisi Aron

Pia Mhandisi Aron amewapongeza Wafanyakazi Hodari kwa kufanya kazi vizuri mpaka wakachaguliwa katika nafasi hiyo.

Photos from Duwasatz's post 01/05/2026

Wafanyakazi wa DUWASA washiriki MEI MOSI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph ameshiriki pamoja na watumishi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani - MEI MOSI, 2026, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule ameongoza Matembezi ya Wafanyakazi katika Viwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yamefanyika Kimkoa katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma, ambapo DUWASA imeshiriki katika Matembezi na kutoa Elimu ya Usomaji Mita Shirikishi kupitia Gari la Maonesho lililopita mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa.

Kauli Mbiu ya Mei Mosi, 2026 ni "Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050".

01/05/2026
Photos from Duwasatz's post 27/04/2026

OFISI YA RAIS - UTUMISHI YATOA MAFUNZO YA PEPMIS KWA WATUMISHI WA DUWASA

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Leo Aprili 27, 2026 wamepatiwa Mafunzo ya Utekelezaji wa Mfumo wa e- Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Mafunzo hayo yametolewa na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambapo Afisa Rasilimaliwatu Mkuu Bw. Kassim Dihenga na Afisa Rasilimaliwatu Msaidizi Bw. Peter Kapitingana wamewataka Watumishi kuzingatia na kufuata maelekezo ya Ujazaji wa PEPMIS kwa ufasaha kwa faida yao katika upimaji wa utendaji kazi.

Photos from Duwasatz's post 26/04/2026

DUWASA YAENDELEA KUTOA ELIMU NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Aprili 25, 2026, Maafisa kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wameshiriki katika kikao cha wananchi wa Mtaa wa Miganga Kata ya Mkonze ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali za maji.

Kikao hicho kilichoandaliwa na serikali ya Mtaa kilikuwa na agenda tofauti ikiwemo ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo hivyo waliitaji ufafanuzi Zaidi.

DUWASA ikiongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. Antony Maro alieleza miradi inayoendelea katika eneo hilo ukiwemo mradi wa Majisafi wa Zuzu – Miganga.

Naye Mhandisi Uzalishaji DUWASA, Mha. Evance Wilhemu amewaambia wananchi kuwa wakati DUWASA inaendelea kusubiri ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Maji ya Bwawa la Farkwa na Ziwa Victoria pia kuna miradi midogo midogo ya uchimbaji visima ikiwemo huo wa Zuzu – Miganga.

Photos from Duwasatz's post 26/04/2026

MHANDISI MWAJUMA WAZIRI ATUNUKIWA TUZO YA UTUMISHI WA UMMA ‘MALKIA WA NGUVU’

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, ametunukiwa Tuzo ya Utumishi wa Umma katika kilele cha utoaji wa Tuzo za Malkia wa Nguvu kwa Kanda ya Kati, zilizofanyika jijini Dodoma.

Tuzo hiyo imetolewa na Kampuni ya Habari na Burudani ya Clouds (Clouds Media Group) Aprili 26, 2026, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wanawake walioonesha utendaji uliotukuka katika sekta mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Balozi Emmanuel Nchimbi, alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizowakutanisha wadau wa maendeleo, viongozi wa serikali na wanawake wajasiriamali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewapongeza washindi wote na kuishukuru Clouds Media Group kwa kuendelea kuibua na kutambua juhudi za wanawake nchini.

Aidha, amewataka Watanzania kuachana na dhana potofu ya kumchukulia mwanamke k**a kiumbe dhaifu, badala yake watambue mchango mkubwa wa wanawake katika kukuza uchumi wa Taifa.

Akimtaja Mhandisi Mwajuma Waziri k**a mfano, amesema ni kielelezo cha mwanamke shupavu aliyebadilisha utendaji kazi na kuleta matokeo chanya katika sekta ya maji.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake kushika nafasi za uongozi na kufanya vizuri katika utumishi wa umma.

Tuzo za Malkia wa Nguvu kwa mwaka huu zimejikita katika kuwatambua wanawake walioleta mabadiliko makubwa katika jamii kupitia nyanja za uongozi, biashara na huduma za kijamii.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Salmin
Dodoma