Magereza Tanzania

Magereza Tanzania

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Magereza Tanzania, Prison & Correctional Facility, Dodoma.

Photos from Magereza Tanzania's post 04/06/2026

🇹🇿

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hezron Komba Norbeth, Juni 04, 2026 amekagua shamba la mahindi la mkoa huo lililopo Kambi Mwisa, lenye ukubwa wa Hekari 75, ikiwa ni mkakati wa kujitosheleza kwa chakula ndani ya Magereza Mkoa wa Kagera.

ACP Norbeth, ameridhishwa na maendeleo ya uzalishaji katika shamba hilo, akisisitiza kuendelea kutumika kikamilifu Kwa mtaalamu wa kilimo wa Kambi hiyo katika kulihudumia shamba kwa hatua zote ili kuongeza uzalishaji ambao utakidhi kuhudumia vituo vya Magereza Mkoa Kagera kwa chakula.

04/06/2026

🇹🇿

RPO IRINGA ATEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI WA MKOMBOZI PAWAGA

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Abdallah Missanga, tarehe 02 Juni 2026 ametembelea Mradi wa Umwagiliaji wa Mkombozi Pawaga kwa lengo la kukagua ufanisi wa mradi huo unavyosafirisha maji kuelekea katika mashamba ya mpunga ya Gereza Pawaga.

Katika ziara hiyo, ACP Missanga alipata fursa ya kuona hali ya upatikanaji wa maji kupitia mifereji ya mradi huo pamoja na mifereji ya asili iliyokuwa ikitumika hapo awali, ili kujiridhisha kuwa Gereza Pawaga linaendelea kuwa na uhakika wa maji yanayotosheleza mahitaji ya uzalishaji wa mpunga kwa tija na ufanisi.

Aidha, alikagua mashamba ya mpunga na mifugo yanayomilikiwa na gereza hilo na kusisitiza matumizi bora ya utaalamu ili kuhakikisha malengo ya uzalishaji yaliyowekwa na Jeshi yanafikiwa.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mkuu wa Gereza Pawaga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Jawadu Hassan Abdallah, alimshukuru RPO kwa ziara hiyo yenye tija na kuahidi kuendelea kusimamia kwa karibu shughuli za kilimo na ufugaji ili kuongeza uzalishaji na kuchangia kikamilifu utekelezaji wa dira ya Jeshi la Magereza katika kujitosheleza kwa chakula.

Photos from Magereza Tanzania's post 04/06/2026

🇹🇿

CP KAVIRONDO: KAZI ZA UREKEBISHAJI ZIFANYWE KWA KUZINGATIA SHERIA NA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Na. INSP. Nurdin Nanyanga - TCTA

Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, (CP) Amina Jumanne Kavirondo, ameendesha semina kwa wanafunzi wa kozi ya Sayansi ya Urekebishaji (PCT & BMT), katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

Katika semina hiyo, CP Kavirondo alieleza umuhimu wa kufanya kazi za urekebishaji kwa kuzingatia sheria na viwango vinavyokubalika kimataifa, huku akisisitiza nidhamu, uwajibikaji na kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha dhana ya urekebishaji wa wafungwa inafanikiwa.

Alisema mafanikio ya urekebishaji wa wafungwa huchangia kuifanya jamii kuwa salama na kusaidia maendeleo ya shughuli za kiuchumi nchini.

Aidha, alikumbusha kuwa Jeshi la Magereza lilizindua mitaala ya Sayansi ya Urekebishaji wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Agosti 26, 2025 katika chuo hicho, lengo la mitaala hiyo ni kuandaa maafisa wa urekebishaji watakaotoa huduma za urekebishaji kwa wafungwa magerezani.

CP Kavirondo, pia alieleza kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu na mafunzo ikiwemo Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), VETA pamoja na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), ili kuwajengea wafungwa maarifa na stadi zitakazowasaidia kurejea kwenye jamii wakiwa raia wema.

Pia alisisitiza kuwa hakuna mtu anayezaliwa akiwa mhalifu, bali mazingira, malezi na changamoto mbalimbali za maisha vinaweza kuchangia mtu kuingia kwenye vitendo vya uhalifu na kujikuta gerezani, hivyo kupitia mwongozo wa Programu za Urekebishaji, Jeshi la Magereza linaendelea kutoa huduma bora kwao.

Vilevile, alieleza umuhimu wa kufanya tathmini ya wafungwa wanaorudia makosa ili kubaini sababu zinazowafanya kurejea kwenye uhalifu na kuzifanyia kazi kupitia mifumo bora ya urekebishaji.

Aliongeza kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kuimarisha mifumo ya kufuatilia na kutunza kumbukumbu za wafungwa kwa ajili ya kuboresha huduma za urekebishaji nchini.

Photos from Magereza Tanzania's post 04/06/2026

🇹🇿

TAKUKURU YAZINDUA OFISI MPYA MOROGORO, MAGEREZA YAPONGEZWA KWA UJENZI BORA

Na. Sgt Salome Mwakitalima - MOROGORO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ndg. Crispin Francis Chalamila, Juni 1, 2026 amezindua ofisi mpya ya TAKUKURU iliyojengwa eneo la Kihonda, Morogoro. Mradi huo umetekelezwa na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA).

Chalamila amesema, ushirikiano kati ya taasisi za umma ni kielezo cha namna watumishi wa umma wanavyoweza kuunganisha nguvu za kitaaluma na kiujuzi ili kutoa huduma bora kwa wananchi. Amesema ushirikiano huo unapaswa kuigwa na taasisi nyingine za umma katika kuwatumikia Watanzania.

Aidha, Chalamila, alimpongeza Mkuu wa Jeshi la Magereza CGP. Jeremiah Yoram Katungu kwa kazi nzuri iliyofanywa na SHIMA akieleza kuwa ujenzi huo umezingatia viwango vya kitaalamu, ubora wa hali ya juu na thamani halisi ya fedha, jambo lililowezesha kupatikana kwa miundombinu imara na inayokidhi mahitaji ya taasisi hiyo.

“Kama alivyoeleza Mkurugenzi wa Milki, si hapa tu; pia wamefanya kazi kubwa na nzuri k**a hii mkoani Iringa na Mkoa wa Shinyanga, tunatarajia kuzindua hivi karibuni. Kwa hiyo tunawashukuru sana Magereza,” alisema Chalamila

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro SACP. Peter Anatory alimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa Jengo hilo.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa, wakiwemo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi Tanzania, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Idara ya Uhamiaji Tanzania.

Photos from Magereza Tanzania's post 03/06/2026

🇹🇿

DKT. JINGU APONGEZA USHIRIKIANO WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA JESHI LA MAGEREZA

Na. SSGT. Mawazo Mtondo - DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. John Jingu, amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na Jeshi la Magereza katika kuimarisha upatikanaji wa haki na huduma za msaada wa kisheria kwa Wafungwa na Mahabusu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.

Dkt. Jingu alitoa kauli hiyo leo Juni 3, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria uliopo Mtumba jijini Dodoma, wakati wa kikao cha pamoja kati ya viongozi wa Wizara hiyo na Jeshi la Magereza kilicholenga kujadili na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya utoaji haki na huduma za msaada wa kisheria magerezani.

Aidha, Dkt. Jingu amesema kuwa, Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Magereza katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kuwajengea uwezo wataalamu wa sheria, kuimarisha utekelezaji wa vifungo mbadala, utoaji haki pamoja na kuboresha mifumo ya ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa zinazohusu huduma za msaada wa kisheria na ufuatiliaji wa haki za wafungwa na mahabusu.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP. Jeremiah Yoram Katungu, amesema ushirikiano kati ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Jeshi la Magereza ni nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo na kufikia malengo ya Serikali ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Ameeleza kuwa, maeneo ya ushirikiano yanajumuisha utoaji wa mafunzo kwa maafisa wa sheria, uimarishaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu, pamoja na kushughulikia changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili watu waliopo magerezani.

Photos from Magereza Tanzania's post 01/06/2026

🇹🇿

CGP KATUNGU 'ATETA' NA WAJUMBE WA BODI YA TPS SACCOS LTD JIJINI DODOMA

Na SGT. Geofrey Jacka - DODOMA

Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, CGP. Jeremiah Yoram Katungu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza (TPS SACCOS LTD), katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Magereza, Msalato jijini Dodoma, Juni 01, 2026.

Akizungumza katika kikao hicho, CGP. Katungu, ameipongeza Bodi hiyo na uongozi wa chama kwa usimamizi, uendeshaji na utoaji huduma bora, jambo linalopelekea kutokuwa na malalamiko kutoka kwa wanachama.

Aidha, CGP. Katungu, ameitaka Bodi kuendelea kuwa wabunifu katika utoaji huduma, kutumia vizuri rasilimali za chama, pamoja na kutoa elimu kwa Maafisa na Askari ili waone umuhimu wa kutumia huduma za chama hicho na si vinginevyo.

Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TPS SACCOS LTD, Kamishna wa Fedha na Mipango, CP. Chacha Bina Jackson, amemshukuru CGP. Katungu kwa malezi mazuri ya Chama hicho, akieleza kuwa ushirikiano anaoutoa kwa Bodi umekuwa chachu ya mafanikio yanayopatikana, ikiwa ni pamoja na ongezeko la akiba za wanachama na mali za chama.

Akisoma Taarifa fupi ya Chama kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Mei 10, 2026, Meneja wa TPS SACCOS LTD, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) John Itambu, amesema kumekuwa na ongezeko la wanachama ambao wamechangia zaidi ya bilioni Mbili, ikiwa ni kiwango cha juu ukilinganisha na bilioni moja zilizopokelewa katika kipindi k**a hicho Mwaka 2025.

31/05/2026

🇹🇿

WAKAGUZI WARIDHISHWA HATUA ZA UJENZI OFISI YA MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SONGWE

Wakaguzi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiongozwa na Bi. Singwa Mokiwa, Mei 29,2026 wamefanya ziara ya kikazi Mkoa wa Songwe kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Songwe, unaoendelea katika eneo la Nselewa Wilaya ya Mbozi.

Baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi huo kutoka kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Wilson Asukenye Mwasomola, pamoja na mambo mengine Bi. Singwa Mokiwa alieleza kuridhishwa na hatua nzuri iliyofikiwa katika ujenzi wa ofisi hiyo.

Aidha, Bi. Mokiwa amemtaka msimamizi wa mradi huo Mhandisi wa Magereza Dimoso Rajabu Chigwasi, kufanya kazi kwa uadilifu na umakini ili mradi huo ulete matokeo chanya

Photos from Magereza Tanzania's post 31/05/2026

🇹🇿

JESHA LA MAGEREZA LAJIKITA KATIKA KUTUMIA ZANA BORA ZA KISASA ZA KILIMO

Kamishna wa Fedha na Mipango wa Jeshi la Magereza, CP. Chacha Bina Jackson, pamoja na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango na Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanefanya ziara ya kikazi Gereza Kilimo Kitete wilaya ya Nkasi mkoa wa Rukwa.

Lengo la ziara hiyo ni kujionea jinsi Jeshi la Magereza linavyotekeleza maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya Magereza kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa.

Aidha, CP. Chacha, amesema Serikali imeendelea kuliwezesha Jeshi la Magereza zana za kilimo kwajili ya urahisishaji wa kilimo, ikiwa ni pamoja na kupanda, kuvuna na kupuliza dawa, hivyo ameagiza uongozi wa Magereza mkoa huo kuhakikisha zana hizo zinatunzwa na zinatumika kwa maslahi mapana ya Jeshi na Taifa k**a ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, mtaalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Said Kitenge, amelipongeza Jeshi la Magereza kwa jitihada kubwa zinazofanywa na maafisa na askari katika usimamiaji wa raslimali za serikali na uzalishaji wa zao la mahindi na maharage, akiahidi ushirikiano ili kufikia mafanikio ya kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu.

(Picha Na CPL. Dotto Buswelu)

31/05/2026

🇹🇿

RPO ARUSHA AWEKA MKAKATI KUANZISHA MFUKO WA KUWASAIDIA WAFUNGWA WANAOMALIZA VIFUNGO

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Frank Mwakijungu, Mei 28, 2026 amefanya kikao na Wakuu wa Magereza, Viwanda pamoja na Maafisa Urekebu kwa lengo la kujadili namna ya kuanzisha mfuko maalumu wa urekebu, utakaowasaidia wafungwa wanaomaliza vifungo vyao kupata mtaji na kujitegemea baada ya kurejea kwenye jamii.

ACP. Mwakijungu, amesema kuwa Jeshi la Magereza linaendelea kutoa elimu ya ujasiriamali na stadi za maisha kwa wafungwa, huku wahitimu wakipatiwa vyeti kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo VETA na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA). Hata hivyo, changamoto kubwa imekuwa ni ukosefu wa mitaji ya kuanzisha shughuli za kujitegemea wanapomaliza vifungo vyao.

Mfuko huo unalenga kuwawezesha wahitimu hao kwa kuwapatia mitaji na vifaa mbalimbali vya kazi k**a mashine ndogondogo kwa mafundi seremala, mafundi uashi, washonaji, mafundi wa kuchomelea, wahunzi pamoja na waokaji.

Aidha, ACP. Mwakijungu amewataka viongozi hao kuweka utaratibu wa kuwafuatilia wafungwa wanaomaliza vifungo vyao ili kuona namna wanavyotumia elimu na mafunzo waliyopewa wakiwa gerezani.

Photos from Magereza Tanzania's post 31/05/2026

🇹🇿

CP CHACHA ASISITIZA UMUHIMU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Kamishna wa Fedha na Mipango Jeshi la Magereza CP. Chacha Bina Jackson Mei 29, 2026 ametembelea Gereza la Kilimo Mollo mkoani Rukwa, pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT ), kwa lengo la kukagua eneo la kuanzisha mradi wa kielelezo wa kilimo cha umwagiliaji.

CP. Chacha, amesema kupitia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Gereza Mollo limetengewa Shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji cha mahindi na maharage kuanzia msimu wa 2026/2027 ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kuiwezesha Magereza kujitegemea zaidi.

Aidha, amesema mradi huo utasaidia kuwajengea wafungwa ujuzi wa kilimo cha kisasa kupitia mpango wa urekebu ili wanapotoka magerezani waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Dodoma