Tanzania Dairy Board

Tanzania Dairy Board

Share

Ukurasa rasmi wa Bodi ya Maziwa Tanzania

14/05/2026
Photos from Tanzania Dairy Board's post 14/05/2026

Watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, iliyokuwa ikiwasilishwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, tarehe 14 Mei 2026, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uelewa wa vipaumbele na mwelekeo wa maendeleo ya sekta ya mifugo na Tasnia ya Maziwa nchini.

@

14/05/2026



Photos from Tanzania Dairy Board's post 13/05/2026

Habari picha zikionesha Sehemu ya Wajumbe wa Kikao cha Kitaifa cha Maandalizi ya Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa nchini kilichoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Iringa, Bw. Elias Luvanda, kikiwakutanisha wadau mbalimbali kujadili mikakati na maandalizi ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo kuanzia tarehe 25 Mei hadi 01 Juni 2026.

Kikao hicho kimefanyika Mei 13, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, kikilenga kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa ufanisi kuelekea maadhimisho yenye mafanikio makubwa kwa Tasnia ya Maziwa nchini.

Photos from Tanzania Dairy Board's post 13/05/2026

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Iringa Bw. Elias Luvanda, akiongoza kikao cha kitaifa cha maandalizi ya Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa nchini kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa tarehe 13 Mei 2026.

Katika kikao hicho, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwajibikaji katika maandalizi hayo ili kuhakikisha maadhimisho yanafanyika kwa mafanikio, sambamba na kutumia jukwaa hilo kuhamasisha urasimishaji wa biashara ya maziwa, kuongeza matumizi ya maziwa salama na kukuza uchumi kupitia sekta ya maziwa.

13/05/2026


13/05/2026

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. George Msalya, akiendesha mafunzo kuhusu ubora na usalama wa maziwa kwa wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa kutoka Wilaya za Muheza na Mkinga mkoani Tanga.

Mafunzo hayo ni sehemu ya programu ya kuwajengea uwezo wadau kuhusu dhana ya Afya Moja (One Health) na mbinu za kukabiliana na magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia maziwa. Mafunzo hayo yanaendelea kwa siku sita kuanzia tarehe 12 hadi 17 Mei 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa VETA, Tanga.

Photos from Tanzania Dairy Board's post 13/05/2026

Matukio mbalimbali katika picha yakionesha wataalamu kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania wakiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa thamani wa maziwa kuhusu dhana ya Afya Moja (One Health) pamoja na mbinu za kukabiliana na magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 12 hadi 17 Mei 2026 katika ukumbi wa VETA, mkoani Tanga.

Photos from Tanzania Dairy Board's post 11/05/2026

Bodi ya Maziwa Tanzania imekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi katika kikao maalum kilichofanyika tarehe 08 Mei, 2026 kwenye Ofisi Ndogo za Wizara, Jengo la Kambarage Tower jijini Dodoma, kwa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu ushiriki wao katika Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa 2026.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Nyumba 300
Dodoma
P.O.BOX17029