Tangamano

Tangamano

Share

Tangamano is a Government Institution that provides peer education to youths

07/11/2024

YAKOBO 4:7-8

⁷ Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

⁸ Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

HILO NDILO NENO LA MUNGU

06/11/2024

ISAYA 54:17

¹⁷ Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.

HILO NDILO NENO LA MUNGU

02/11/2024

MARKO 7:14-15

¹⁴ Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu.

¹⁵ Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu.

HILO NDILO NENO LA MUNGU

Photos from Tangamano's post 20/05/2024

Katika kusubiria Bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara 2024/2025

26/12/2023
16/08/2023

Man Okinyi

Photos from Tangamano's post 21/01/2022

*TANTRADE KUHAMASISHA MFUMO UTOAJI CHETI CHA USALAMA WA MIMEA KIMTANDAO TANZANIA*

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania( TanTrade) kwa kushirikiana na *Ubalozi wa Uholanzi* nchini Tanzania, Wizara za Kilimo na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanatarajia kufanikisha zoezi lautoaji vyeti vya kidigitali(E- Certificates)

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade *Bi.Latifa Mohamed Khamis* alipokutana na *Bw.Alexander Moret* ambaye ni Mtaalam wa Masuala ya vyeti Mtandao ( E-Certification) kutoka nchini Uholanzi.

*Bw.Moret* ambaye aliambatana na *Bi.Agnes Tengia* kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na *Bw.Abdalah Mwambachi* ambaye ni Mtaalam wa Masuala ya Kilimo kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini.

Mazungumzo hayo yalilenga katika kuiwezesha Tanzania kuingia katika mfumo wa utoaji cheti cha Usalama wa Afya ya Mimea inayojulikana kitaalam k**a *Phytosanitary Certificate*.

Hatua Hiyo itawezesha Upatikanaji wa cheti cha Usalama wa Mimea kimtandao katika hatua zote hapa nchini tofauti na sasa ambapo wafanyabiashara wanalazimika kujaza fomu mtandaoni na kisha kuhitajika kupata nakala ngumu (hard copy) mara baada ya kujaza fomu Hiyo.

Katika mazungumzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade *Bi.Latifa Mohamed* ambaye aliambatana na baadhi ya wakuu wa Idara, alisema mfumo huo utarahisisha taratibu za ufanyaji Biashara nchini Tanzania.
"Sisi k**a Mamlaka inayosimamia Biashara nchini, "tupo tayari kushirikiana na wadau wote wanaolenga kurahisisha njia za ufanyaji Biashara Nchini" aliongeza *Bi.Latifa*

18/01/2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi tarehe 17 Januari, 2022 ametembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya EXPO 2020 Dubai yanayoendelea katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE)

Rais Mwinyi ambaye yupo katika ziara ya Kiserikali nchini humo ametembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya Expo Dubai2020 kwa ajili ya kujionea jinsi Tanzania inavyotumia fursa ya Maonesho hayo ya Makubwa Duniani kutangaza Biashara na Uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uchumi wa Bluu, Utalii, Madini, Nishati na Kilimo.

Mhe. Rais Mwinyi amepongeza ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo ikiwa ni miongoni mwa Nchi 192 zinazoshiriki katika Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 1 Oktoba , 2021 na yanatarajiwa kukamilika tarehe 31 Machi, 2022 ambapo, Ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho hayo unaratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

Pia Mhe. Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ametembelea Kituo cha Polisi cha mtandao “ Smart Police Station “ kwenye Maonesho hayo ambapo alipewa maelezo kuhusu kifaa maalum kinachotumika kuwasilisha kesi kwa njia ya mtandao.

Katika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

18/11/2021

Karibuni katika Maonesho ya Expo2020 Dubai

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dodoma