Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Share

Karibu katika ukurasa rasmi wa Facebook wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ni Wizara inayoendeleza utambulisho wa Taifa kwa kuwezesha upatikanaji stahiki wa Habari, kukuza Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuleta maendeleo ya jamii na kiuchumi.

06/06/2026
05/06/2026

Mhe. Mwinjuma: Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga uwe mfano kwa Wadau wanaotaka kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo.

Photos from Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo's post 05/06/2026

Naibu Waziri Mwinjuma Aridhishwa na Ufungaji Viti Mkwakwani

Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali vya michezo nchini ili viweze kutumika katika michuano ya kimataifa hata baada ya Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, mara baada ya kutembelea na kukagua usimikaji wa Viti katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga leo Juni 3, 2026.

Mhe. Mwinjuma ameupongeza Uongozi wa uwanja huo chini ya Meneja Nassoro Makau, kwa kufanya ubunifu mkubwa wa kuvipanga vizuri viti kwa rangi, ikiwa ni viti vilivyotolewa na Serikali katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hatua inayoupendezesha uwanja huo wa kihistoria.

Amesema, uboreshaji wa viwanja vya michezo nchini ni sehemu ya maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye Serikali yake ya Awamu ya Sita imewekeza kwa kiwango cha hali ya juu katika ukarabati wa viwanja k**a Uhuru na Mkapa, pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa Arusha.

"Zoezi la usimikaji wa viti hapa Mkwakwani limefanyika kwa ukamilifu mkubwa. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaona namna ya kukamilisha sehemu iliyobaki kadiri rasilimali zitakavyopatikana. Nawaomba wananchi na wapenda michezo kutunza miundombinu hii na kuepuka uharibifu ili viwanja vyetu viwe endelevu," amesisitiza Mwinjuma.

Ametoa wito kwa sekta binafsi na wadau mbalimbali wa soka nchini kujitokeza kushirikiana na Serikali ili kuweka nguvu ya pamoja katika kukamilisha maeneo madogo yaliyobaki uwanjani hapo ili kuendana na kasi ya soko la soka la kisasa duniani.

Akiwasilisha taarifa ya ukarabati huo, Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani, Nassoro Makau, alisema kuwa katika awamu ya kwanza, Serikali iliwaletea jumla ya viti 6,500 ambavyo vimeshafungwa kikamilifu, huku kukiwa na upungufu wa viti 2,500 ili kukamilisha maeneo yote.

Makau alifafanua kitalamu kuwa viti hivyo vimeshafungwa kwenye Jukwaa Kuu (Main Stand), jukwaa la Reli Moja na Reli Mbili, huku jukwaa maarufu la "Urusi" likiwa ndilo eneo pekee lililobaki ambalo halijafungwa viti kwa sasa. Baada ya ukarabati huu, uwezo wa uwanja huo sasa utakuwa ni kubeba watazamaji 9,000 waliokaa kwenye viti.

Photos from Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo's post 04/06/2026

Naibu Waziri Mwinjuma Apongeza PBZ Kufikisha Huduma Tanga

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa pongezi kwa Benki ya PBZ (Ikhlas) kwa kufikisha huduma zake mkoa wa Tanga.

Mhe. Mwinjuma ametoa pongezi hizo, Juni 3, 2026 alipozindua tawi jipya la Benki hiyo ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ikhlas) katila Mkoa wa Tanga, ambao ulienda sambamba na Maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo nchini mwaka 1966.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Mwinjuma alisema, hatua hiyo ni kielelezo tosha cha uaminifu na sifa ya Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar, ambao umepanua wigo wa huduma kupitia mfumo wa PBZ Ikhlas.

"Ufanisi huu mkubwa wa PBZ unaenda sambamba na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambao kwa pamoja wanasimamia mageuzi ya kiuchumi yanayojenga soko shindani kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kibenki," alisisitiza Mhe. Mwinjuma.

Aliongeza kuwa, Mkoa wa Tanga una umuhimu mkubwa wa kimkakati kupitia miradi mikubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza kwenye miundombinu ya bandari, barabara, reli na nishati, jambo linalofungua milango kwa ustawi wa sekta binafsi, akitoa wito kwa wananchi kutumia huduma za PBZ Ikhlas kuongeza akiba, kupata mikopo, na kuwekeza ili kukuza uchumi wao wa kila siku.

Naye Meneja Masoko na Kuendeleza Biashara wa PBZ, Seif Suleiman, alisema ujio wa tawi hilo unalenga kuchochea fursa za kiuchumi kwa sababu Tanga ni lango kuu linalokua kwa kasi na linapakana na Jiji la Mombasa, nchini Kenya.

"Tunajivunia miaka 60 ya uaminifu nchini. Uamuzi wa kuleta PBZ Ikhlas Tanga umechochewa na fursa za kiuchumi na mshabihiano mkubwa wa kitamaduni kati ya Tanga na Zanzibar. Benki hii si ya Waislamu pekee, ni chombo cha watu wote," alisema Suleiman.

Suleiman aliongeza kuwa kwa sasa PBZ ni benki ya sita kwa ukubwa nchini ikiwa na vituo na matawi ya kutolewa huduma yapatayo 50 Bara na Visiwani. Katika hatua hiyo, uongozi ulimshukuru Muasisi Marehemu Abeid Amani Karume kwa maono yake yaliyowezesha taasisi hiyo kuzaliwa.

03/06/2026

WAZIRI MAKONDA: NAWASHUKURU SANA WAKOSOAJI SABABU LENGO NI KUIMARISHA TIMU ZETU

03/06/2026

MAKONDA: MSIWABEZE MASHABIKI WALIOKWENDA MOROCCO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amewataka Watanzania kuacha kuwabeza mashabiki waliokwenda nchini Morocco kuishangilia Serengeti Boys, akisisitiza kuwa uwepo wao ulikuwa sehemu muhimu ya kuipa timu morali katika hatua ya fainali ya AFCON U-17.

Makonda amesema mashabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani kwa kuwa uwepo wao huwapa wachezaji nguvu, hamasa na kujiamini wanapoiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

“Hakuna timu inayokwenda mashindanoni bila mashabiki. Senegal na mataifa mengine yalikuwa na mamia ya mashabiki waliokwenda kuziunga mkono timu zao. Nasi tunapaswa kuthamini wale waliopata nafasi ya kwenda kuiwakilisha Tanzania na kuwapa nguvu vijana wetu,” amesema Makonda.

Ameongeza kuwa badala ya kubezana, Watanzania wanapaswa kuendelea kuungana katika kuunga mkono timu za taifa na kuhamasisha ushiriki mkubwa zaidi wa mashabiki katika mashindano yajayo.

Makonda amesema mafanikio ya Serengeti Boys ni mafanikio ya Watanzania wote na kwamba safari ya maendeleo ya soka la Tanzania inaendelea.

📍 Dar es Salaam, Tanzania
🗓️ Juni 2026

03/06/2026

KARIA: VIJANA HAWA TUNAWAPATA KWENYE MICHEZO YA UMITASHUMTA NA UMISETA NA KUWAENDELEZA

Photos from Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo's post 03/06/2026

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, akizungumza na umati wa Wananchi waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuipokea na kuipongeza Timu ya Taifa ya Wavulana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, baada ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA U-17 na kutwaa nafasi ya pili katika Mashindano ya AFCON U-17.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

S. L. P 25 Mtumba
Dodoma
00000

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30