Geita Municipal Council

Geita Municipal Council

Share

Geita Municipal Council is one of the two council forming Geita District, other Council is Geita District Council.

Geita District is one of the five (5) districts in Geita Region. It gained the status of being a district in 1961 being combined with Sengerema District, by then being known as Geita Province. It had 16,638 Km2 of which dry land was 10,123.94Km2 and water was 6,514.06Km2. n 1975 the province was divided forming two districts namely Geita and Sengerema. The main ethnic groups in the district are Su

03/12/2025

MANISPAA YA GEITA YASAMBAZA MBEGU ZA VIAZI LISHE KATIKA SHULE 41 KUBORESHA LISHE YA WANAFUNZI

Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeanza rasmi zoezi la usambazaji wa mbegu za viazi lishe katika shule 41 za msingi na sekondari ndani ya manispaa hiyo. Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuimarisha lishe ya wanafunzi kupitia kilimo cha bustani na mashamba yanayomilikiwa na shule husika.

Mbegu zinazotolewa ni za aina ya Kabode, Jewel, Irene na Kakamega, ambazo zinatambulika kwa kuwa na virutubisho muhimu k**a vile vitamini A, madini ya chuma na nyuzinyuzi, vinavyosaidia katika ukuaji wa mwili na kuimarisha kinga ya mwili.

Mpango huu unatekelezwa k**a sehemu ya afua za lishe na mpango wa chakula shuleni, kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata angalau mlo mmoja wenye virutubisho anapokuwa shuleni. Hili linaenda sambamba na azma ya serikali ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji na kupunguza changamoto za kiafya zinazotokana na lishe duni kwa watoto wa shule.

Zoezi hili linafanikishwa kupitia ushirikiano wa karibu baina ya idara za Afya, Kilimo na Elimu (Msingi na Sekondari), jambo linaloonesha nguvu ya mshik**ano wa kiutendaji katika kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora na endelevu ya chakula shuleni.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manispaa ya Geita

Photos from Geita Municipal Council's post 03/12/2025

MANISPAA YA GEITA YAKABIDHI KOMPYUTA MPAKATO KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NGAZI YA KATA KUONGEZA UFANISI WA KAZI

Leo, 3 Desemba 2025 – Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya zoezi la kukabidhi kompyuta mpakato (laptop) tano kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata, ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa kutumia teknolojia.

Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo, likiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa, Ndugu Yefred Myenzi.

Akitoa taarifa hiyo Ndugu Robert J. Sungura Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii, amesema kuwa idara imeona umuhimu wa kugawa vifaa hivyo ili kuwawezesha watumishi kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya teknolojia, jambo litakalosaidia kuboresha utoaji huduma kwa jamii.

Amezitaja kata zilizonufaika katika awamu hii ya kwanza kuwa ni Kalangalala, Nyankumbu, Buhalahala, Shiloleli na Ihanamilo, huku akibainisha kuwa mpango uliopo ni kufanikisha upatikanaji wa vifaa kwa kata nyingine zilizobaki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Myenzi ameipongeza Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kwa namna inavyotekeleza majukumu yake kwa ushirikiano na viongozi wa ngazi zote. Ameeleza kuwa kompyuta hizo zitaongeza usiri wa taarifa, kupunguza matumizi yasiyo rasmi ya steshenari, na kuongeza ubora wa kazi.

“Vifaa hivi vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa, hasa katika kuchakata taarifa za waombaji mikopo na shughuli nyingine za kiofisi. Hii ni mali ya Serikali, hivyo tunatarajia itatunzwa kwa uadilifu ili viweze kutumika na wengine watakao kuja,” amesema Mkurugenzi Myenzi.

Amesisitiza kuwa hatua hii ni sehemu ya kuimarisha mifumo ya utendaji kazi kwa Maafisa wa ngazi ya kata, sambamba na kupunguza muda wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Photos from Geita Municipal Council's post 03/12/2025

MADIWANI WA MANISPAA YA GEITA WALA KIAPO NA KUJIELEKEZA KULETA MAENDELEO KWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI

Mapema leo tarehe 2 Desemba 2025, katika Ukumbi wa EPZ Bombambili, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imefanya kikao chake cha kwanza cha Baraza la Madiwani.

Katika kikao hicho maalum, Madiwani wote wamekula kiapo cha utii, wakiahidi kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi pamoja na za Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Wameeleza dhamira yao ya dhati ya kushirikiana kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Geita.

Kikao hicho pia kimeashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Baraza jipya, ambapo viongozi na watendaji wa Halmashauri wameonyesha mshik**ano na matarajio chanya katika kipindi hiki kipya cha utawala.

03/12/2025

MHE. ELIAS CHARLES NGOLE ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA WA MANISPAA YA GEITA KWA KURA ZOTE KATIKA KIKAO CHA KWANZA CHA BARAZA LA MADIWANI

Tarehe 2 Desemba 2025, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita limeendelea kuonesha mshik**ano na umoja baada ya kumchagua Diwani wa Kata ya Nyanguku, Mhe. Elias Charles Ngole, kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani, Mhe. Ngole amepata kura zote 20 kati ya 20 zilizopigwa na wajumbe wa baraza, jambo linaloonesha imani kubwa waliyonayo kwake katika kuendeleza ajenda za maendeleo kwa ushirikiano na Meya pamoja na uongozi wa Manispaa.

Mhe. Ngole ameahidi kushirikiana kwa karibu na viongozi wenzake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha ustawi wa jamii ya Geita unaimarika.

Wajumbe wa baraza wamempongeza kwa ushindi huo na kumtakia kila la heri katika kutimiza majukumu yake mapya kwa weledi na uadilifu.

03/12/2025

MHE. LEONARD BUGOMOLA KIGANGA APEWA KURA ZOTE NA KUCHAGULIWA KUWA MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA GEITA KATIKA KIKAO CHA KWANZA CHA BARAZA LA MADIWANI

Tarehe 2 Desemba 2025, Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeandika historia mpya baada ya Diwani wa Kata ya Bombambili, Mhe. Leonard Bugomola Kiganga, kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo.

Uchaguzi huo umefanyika katika kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa EPZ Bombambili, ambapo Mhe. Kiganga amepata kura zote 20 kati ya 20 zilizopigwa na wajumbe wa baraza hilo, ikiwa ni ishara ya kuungwa mkono kwa kauli moja.

Ushindi huo wa kishindo ni kielelezo cha imani kubwa waliyonayo madiwani kwa uongozi na maono ya Mhe. Kiganga katika kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Geita.

Wajumbe wa baraza wamempongeza kwa ushindi huo na kumtakia mafanikio mema katika kusimamia maendeleo ya Manispaa kwa ushirikiano, uwazi na uwajibikaji.

01/12/2025
Photos from Geita Municipal Council's post 24/11/2025

MKUU WA WILAYA GEITA AFANYA KIKAO KAZI NA MAAFISA KILIMO NA MIFUGO WA KATA ZOTE 50 - ATOA MAELEKEZO KUIMARISHA SEKTA ZA UZALISHAJI

Leo tarehe 24 Novemba 2025, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Hashim Komba, ameongoza kikao kazi maalum kilichowakutanisha Maafisa Kilimo na Mifugo kutoka kata zote 50 za Wilaya ya Geita. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa EPZ Bombambili na kuhudhuriwa pia na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Komba amezitaka Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuwekeza kwa nguvu katika sekta kuu tatu za uzalishaji – Kilimo, Ufugaji na Uvuvi – ambazo tayari zimechangia zaidi ya Shilingi bilioni moja katika mapato ya Wilaya.

Katika kuhakikisha sekta hizi zinatoa matokeo zaidi, Mhe. Komba ametoa maagizo matatu muhimu:

1. Pembejeo kwa Bei Elekezi

Amesisitiza kuwa maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuongeza tija katika sekta ya kilimo. Hivyo, wauzaji wa pembejeo wanapaswa kuzingatia bei elekezi na kuhakikisha pembejeo hizo zinawafikia wakulima kwa wakati.

2. Maafisa Kilimo Kata Kuwafuata

Amewataka Maafisa Kilimo wa Kata kuwafuata wakulima mashambani na kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwa ukaribu na kwa wakati.

3. Ramani Maalum ya Kilimo Geita

Ameelekeza kuandaliwa kwa ramani maalum ya kilimo itakayobainisha mazao yanayostawi kulingana na mazingira ya kila eneo, ili kusaidia kupanga kwa ufanisi aina ya mazao kulingana na maeneo.

Aidha, kwa upande wa sekta ya mifugo, Mkuu wa Wilaya amewaagiza Maafisa Mifugo kuhakikisha wanadhibiti wizi wa mifugo kwa kuhakikisha kila mnyama anayesafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine anakuwa na kibali halali cha serikali.

Mhe. Komba ameahidi kuwa balozi wa sekta hizo kwa kushirikiana na wakulima na wafugaji katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuimarisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Wiki ya Unyonyeshaji 2025 | Elimu ya Unyonyeshaji Yatolewa kwa Wazazi Geita Manispaa 11/08/2025

Wiki ya Unyonyeshaji 2025 | Elimu ya Unyonyeshaji Yatolewa kwa Wazazi Geita Manispaa

KUSOMA ZIADI >>>

Wiki ya Unyonyeshaji 2025 | Elimu ya Unyonyeshaji Yatolewa kwa Wazazi Geita Manispaa Katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Duniani 2025, elimu juu ya umuhimu wa kunyonyesha watoto maziwa ya mama imetolewa kwa wazazi katika Zahanati ya Geita Town na Kituo cha Afya Nyankumbu.   Afisa Lishe wa Manispaa ya Geita, kwa kushirikiana na watoa huduma wengine wa afya, wameendesha ma

Photos from Geita Municipal Council's post 11/08/2025

WACHEZAJI 43 WA MANISPAA YA GEITA WAPEWA HAMASA KUELEKEA MASHINDANO YA SHIMISEMITA 2025

Wachezaji 43 wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita walioteuliwa kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA mwaka huu, wamepewa hamasa maalum kabla ya kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mashindano hayo ya kitaifa.

Katika tukio hilo maalum la kuwaaga wachezaji, viongozi mbalimbali wa manispaa wamewatakia kila la heri na kuwahimiza kushiriki kwa bidii, wakitambua kuwa wanawakilisha nembo ya Manispaa ya Geita pamoja na Mkoa kwa ujumla.

Akizungumza na wachezaji hao, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita, Bi. Ellah Makese aliwapongeza kwa kuchaguliwa kushiriki mashindano hayo, akisisitiza kuwa ana imani kubwa na uwezo wao. “Michezo ni afya, lakini pia ni heshima kwa taasisi. Nendeni mkaonyeshe uwezo wenu, mkipata ushindi katika kila mchezo ikiwezekana,” alisema.

Bi. Ellah alisisitiza umuhimu wa kurejea na ushindi, kwani kufanya hivyo kutajenga taswira chanya kwa Halmashauri ya Manispaa ya Geita na Mkoa mzima wa Geita.

Akihitimisha hotuba yake kwa ari na matumaini, alihamasisha: “Twendeni Tanga, turudi na ushindi!”

Mashindano ya SHIMISEMITA yanatarajiwa kuanza Tarehe 15/08/2025 na kumalizika tarehe 29/08/2025 yanajumuisha watumishi kutoka sekta mbalimbali za serikali, yakilenga kuimarisha afya, mshik**ano, na motisha kazini kupitia michezo.

11/08/2025

KARIBU NANE NANE 2025!


KATIBU TAWALA MKOA WA GEITA APONGEZA UBUNIFU NA MAANDALIZI YA NANENANE 11/08/2025

KATIBU TAWALA MKOA WA GEITA APONGEZA UBUNIFU NA MAANDALIZI YA NANENANE

KUSOMA ZAIDI >>>>

KATIBU TAWALA MKOA WA GEITA APONGEZA UBUNIFU NA MAANDALIZI YA NANENANE Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndg. Mohamed Gombati, mapema leo ametembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo, jijini Mwanza, ambapo ameeleza kufurahishwa na maandalizi mazuri na ushiriki wa halmashauri kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo n

Want your business to be the top-listed Government Service in Geita?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Municipal Director, Geita Municipal Council, 11 Geita MC Road, P. O. Box 384 Geita
Geita

Opening Hours

Monday 01:30 - 15:30
Tuesday 01:30 - 15:30
Wednesday 01:30 - 15:30
Thursday 01:30 - 15:30
Friday 01:30 - 15:30