Handeni Town Council

Handeni Town Council

Share

Imeanzishwa, Julai 2015
Ipo Mkoa wa Tanga,
Wilaya ya Handeni

02/06/2026
29/05/2026

Karibu Mwenge wa Uhuru 2026 Halmashauri ya Mji Handeni Tarehe 18/06/2026.

Mapokezi yatafanyika Kata ya Kwamagome katika uwanja wa Shangwe

Tutaukimbiza na utafanya shughuli mbalimbali za Kuzindua,kuweka jiwe msingi,kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo

Mkesha utakuwa Kata ya Chanika katika Uwanja wa Kigoda

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mapokezi, kuukimbiza na katika mkesha.

Kaulimbiu "Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo"

27/05/2026

Eid Al - Adha Mubarak

Photos from Handeni Town Council's post 24/05/2026

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese ameungana na wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni katika Bonanza la Siku ya Afya lililofanyika tarehe 23 Mei 2026, likiwa na lengo la kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kuzingatia afya bora.

Bonanza hilo limewakutanisha viongozi, watumishi pamoja na wananchi mbalimbali walioshiriki shughuli za mazoezi na michezo kwa ajili ya kuimarisha afya na mshikamano wa kijamii. Aidha, wagonjwa waliolazwa hospitalini walipatiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuwaonesha upendo katika kipindi cha matibabu yao.

Akizungumza katika bonanza hilo, Mhe. Salum Nyamwese amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya pamoja na kudumisha mshikamano wa kijamii kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii.

@

14/05/2026

Wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni wamehamasishwa kujitokeza kufanya uchunguzi wa Saratani ya Matiti ili kubaini ugonjwa huo mapema na kupata matibabu kwa wakati. Zoezi hilo linaloendelea katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni kwa ushirikiano na Jhpiego chini ya ufadhili wa The Pfizer Foundation linatarajiwa kuwafikia wananchi zaidi ya 500 na huduma hiyo inatolewa bure kwa jinsia zote.

ya afya

Photos from Handeni Town Council's post 14/05/2026

WANANCHI HANDENI MJI WAHAMASISHWA KUFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI

Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa Saratani ya Matiti ili kubaini ugonjwa huo mapema na kupata matibabu kwa wakati.

Wito huo umetolewa na Dkt. Rashid Suleiman kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakati wa zoezi la uchunguzi wa awali wa Saratani ya Matiti linaloendelea katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni, linalofanywa ushirikiano na Shirika la Jhpiego chini ya ufadhili wa The Pfizer Foundation na linahusisha jinsia zote.

Dkt. Rashid amesema zoezi hilo lilianza rasmi Mei 13 na linatarajiwa kuhitimishwa Mei 15, 2026 na kwamba Saratani ya Matiti ni miongoni mwa magonjwa yanayoendelea kuathiri wananchi wengi, hivyo uchunguzi wa mapema ni muhimu katika kuokoa maisha.

Aidha, amesema kuwa mwaka 2025 zaidi ya wanawake 10,000 katika Mkoa wa Tanga walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya Matiti ambapo asilimia 2.3 walibainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.

“Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa wananchi kujitokeza mapema kwa ajili ya uchunguzi na tiba,” amesema Dkt. Rashid.

Kwa upande wake, Dkt. Lawrence Victoria kutoka Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni amesema wanatarajia kuhudumia wananchi wapatao 500 katika kipindi cha zoezi hilo.

Amebainisha kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wananchi huku vifaa vya kisasa vikitumika kuhakikisha uchunguzi unafanyika kwa ufanisi na usahihi zaidi.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo wameishukuru Serikali pamoja na wadau wa afya kwa kupeleka huduma hiyo karibu yao, wakisema hatua hiyo itasaidia kuongeza uelewa na kuwafanya wananchi wengi zaidi kujitokeza kwa uchunguzi.

Wananchi hao pia wameomba huduma ya uchunguzi wa Saratani ya Matiti iwe endelevu ili kusaidia jamii kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati.

ya afya

14/05/2026

Kuelekea mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, Mama Lishe na wajasiriamali wa Halmashauri ya Mji Handeni wanaendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi na Salama katika kupikia ikiwa ni sehemu ya ajenda muhimu ya mambo mtambuka yanayobebwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026.

Matumizi ya nishati safi yana mchango mkubwa katika kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kuchochea maendeleo endelevu ya jamii.

Tanzania ni yetu sote, Tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo

09/05/2026

TAARIFA KWA UMMA
Huduma ya Mkoba ya Uchunguzi wa Awali wa Saratani ya Matiti
Mei 13 ,2026 Zahanati ya Misima
Mei 14&15 Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni
Huduma hii ni bure

Photos from Handeni Town Council's post 05/05/2026

HANDENI MJI YAPIGA HATUA KUDHIBITI UTAPIAMLO KWA WATOTO

*Watoto wanaolazwa wapungua kutoka 32 hadi 7 kwa robo mwaka

Na Augusta Njoji

IDADI ya watoto wanaokabiliwa na utapiamlo mkali katika Halmashauri ya Mji Handeni imepungua kwa kiasi kikubwa, kutoka watoto 32 waliokuwa wakilazwa hospitalini kwa robo mwaka 2024/25 hadi wastani wa watoto watano hadi saba kwa robo mwaka 2025/26.

Mafanikio hayo yanatajwa kuchangiwa na mikakati madhubuti ya utoaji elimu ya lishe kwa jamii inayotekelezwa na Hospitali ya Halmashauri hiyo, ikilenga kupunguza lishe duni hususan kwa watoto.

Akizungumza Mei 5, 2026 katika kikao cha tathmini ya shughuli za lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025/26, Afisa Tarafa ya Chanika, Julieth Mushi, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amepongeza juhudi hizo na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mkataba wa lishe.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe pamoja na Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kuhamasisha jamii kuanzisha bustani za mboga majumbani na kufuga wanyama ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa watoto.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Dkt.Hudi Shehdadi, amesema mikakati inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na kushirikiana na Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari pamoja na kamati za lishe za kata kuhamasisha upandaji wa miti ya matunda na uanzishaji wa bustani za mboga, huku kila shule ikitakiwa kutenga angalau hekari mbili kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

Aidha, amebainisha kuwa juhudi zimeongezwa katika kuhamasisha wajawazito kuhudhuria huduma za afya mapema ili kupata elimu ya lishe pamoja na virutubisho vya madini chuma, hatua inayolenga kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na uzito pungufu.

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025/26, Kaimu Afisa Lishe wa Halmashauri hiyo, Getruda Kasabaja, amesema jumla ya wazazi na walezi 9,571 wamefikiwa na elimu ya lishe, huku watoto 17,390 wakifanyiwa tathmini ya hali ya lishe.




Want your business to be the top-listed Government Service in Handeni?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

P. O. BOX 51
Handeni
21801

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30