Innovation Family Together

Innovation Family Together

Share

Usilaumu kwamba Tanzania hakuna ajira wakati hakuna wa kuzifanya ziwepo. Njoo tuk**ate fursa kisha tutoke pamoja.

01/07/2018

Unakaribishwa mdau katika ukurasa huu waweza jiunga nasi kwa kupiga 0712238545 hiki ni chama cha wajasiliamali. Karibu

28/06/2018

Tunapenda kuwakaribisha vijana wa kitanzania kwenye chama cha innovation family together tujenge urafiki wa kimtandao katika kupeana mawazo na mitazamo mbali mbali ya kimaisha kusudi tuweze kujikwamua kiuchumi na kutoka kimaisha. Like page hii kisha waweza kuwasiliana nasi kwa 0712238545 nyote mnakaribishwa.

29/03/2017

Napenda kuwa salimu wapendwa wetu wa ukurasa huu,kuanzia sasa nakaribisha mawazo na idea, mbalimbali kutoka kwenu ili kutengeneza timmu ya vijana yenye mitazamo na fikra pevu. nakaribisha mapendekezo pia maoni ktk kuboresha ukurasa wetu huu. KARIBUNI.

01/03/2017

hello frnd mambo niaje?

Photos 30/01/2017

TANGAZO TANGAZO

Kutakuwa na kikao cha wana vission family wote waishio dar es salaam, siku ya j,mosi saa kumi kamili jioni karibu kabisa na USESI CLUB, kituo cha daladala kinaitwa gereji ukitokea ubungo kwenda buguruni baada ya mabibo external/ au baada ya mwananchi tabata relini ukitokea buguruni kwenda ubungo kwa kutumia Barbara ya Mandela.

Fika bila kukosa hata k**a ndio Mara yako ya kwanza na ungependa kujiunga na chama hiki cha vission family tz, unakaribishwa sana.

Hakutakuwa na kiingilio kwa wale watakao kuja kwenye kikao.

Nyote mnakaribishwa

By.
G.Chirwa

Director of Vission family tz.

15/01/2017

Wapendwa naomba kuwafahamisha wadau wa page yetu hii, kwamba kwa sasa vission family tz, inatimiza mwaka mmoja tangu kuundwa kwake k**a kundi ndani ya mitandao ya kijamii yaani face book na Whatsup.

Hivyo basi tumeona ili umoja wetu huu uwe na mantiki kiuhalisia tumeamua kuunda chama cha wajasiliamali katika nyanja mbali mbali za kibiashara, ili kuifanya mitandao hii ya kijamii iwe na manufaa kwetu badala ya kuitumia kwa kupiga porojo zisizo na maana mwaka mzima.

Sasa basi endapo utapenda kujumuika nasi katika kuunda chama hiki, thibitisha hapa kwa maandishi ukianza kwa kujitambulisha Jina na utokako, itapendeza zaidi ukiweka na namba ya simu. Admin atarekodi taarifa zako na baadaye atakupatia muongozo mwingine. Aidha ingia whatsap kwa namba hii..0712 238545.
Lengo la kufanya hivi ni kutaka kupata idadi kamili ya wenye nia ya kwenda nasi katika malengo ya pamoja k**a.

Karibuni.
By.
G. Chirwa : Admin

05/01/2017
Photos 02/12/2016

Je wewe ni mdau katika nyanja za kilimo, Ufugaji na Biashara??

Nakukaribisha katika chama cha wajasiliamali wenye fikra za kutoka kimaisha kwa kutumia fursa zilizopo kwenye Sekta ya kilimo hapa nchini.

Waweza kuthibitisha hapa k**a ungependa kujumuika ndani ya chama hiki kipya kabisa, chenye malengo ya kuinua vijana kifrika na kuachana na tabia za kulalamika kuhusu ukosefu wa ajira hapa nchini.

Kwa mawasiliano zaidi:
0712 238545/ 0786 515828

Email: Vission [email protected]

Nyote mnakaribishwa.

Photos 13/11/2016

Njoo tukae pamoja tujadili biashara ya kilimo na kutatua kero ya ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini.

Chama Vission Family Tz, kina furaha ya kukukaribisha uje kujiunga na chama hiki cha wajasiliamali katika sekta ya kilimo kwa lengo la kutengeneza mikakati kadha wa kadha katika kukuza kilimo chetu, biashara ya kilimo (Sekta ya viwanda na uzalishaji mali??

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi piga: 0712238545 & whatsap.

Email: [email protected]

Photos 24/10/2016

ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA.
(JICHO LA TOFAUTI)

Hivi kwa nini tunazani kwamba "ELIMU NI MUHIMU ZAIDI KULIKO VINGINE??"

Karibu tena mdau wa page yetu ili tuweze kujifunza na kupeana dondoo mbalimbali za kimaisha ili tuweze kujitambua.

Tuanze basi mada yetu kwa kujiuliza tu swali hili:-
Kwanini tunalazimika kuwa na elimu?
Au tunasoma ili iweje??

Majibu ya haraka haraka tunayoweza kupata katika msingi wa swali hili ni:-

Tunasoma ili tuwe na maisha mazuri.
Tunasoma ili tupate kazi na ujira mzuri.
Tunasoma ili kutengeneza maisha ya baadaye. n.k

Yote haya yanaweza kuwa majibu sahihi kulingana na mtazamo wa mtu binafsi.

Sasa basi, ebu tuingie kwa pamoja kiundani zaidi kutambua thamani ya elimu kwa binadamu.

Elimu ni k**a afya tu. Ni kitu muhimu tu k**a afya ili binadamu aweze kukua na kupanua mawazo yake kulingana na mazingira yanayomzunguka.

Tunahiitaji Elimu kwa sababu ya Kuitawala dunia. Pia ni Amri tunayopewa hata katika vitabu vya Kidini BIBLIA/ MSAHAFU. Enendeni duniani mkaitawale dunia.
Sasa unawezaje kuitawala Dunia wakati huijui dunia??
Ili uweze kuitawala dunia ni lazima kupambana na mazingira yanayokuzuia kufikia yale unayotamani kuyafikia kimaisha.

Na kazi ya elimu ni moja tu ambayo ni kuviondoa vikwazo hivyo.

Kwa mfano:-
Binadamu tumeumbwa na njaa, ili uweze kuitibu njaa yako ni lazima upate chakula kilichopikwa vizuri.

Je, Ungejuaje leo kwamba, eti ukichukua nyanya ukachanganya na kitunguu na kuweka chumvi kidogo, utapata ladha Fulani itakayokuwezesha kuiona thamani ya chakula chako k**a kusingekuwa na mtu aliyekufundisha au kukuelekeza??
Hiyo ni elimu.

Ungejuwaje leo kwamba kuiba ni dhambi endapo husingefundishwa hivyo??
Hiyo pia ni kazi ya elimu.

Kwa hiyo tunapozungumzia elimu atuzungumzii kitu kikubwa sana cha kutisha, Bali tunazungumza kuhusu TIBA ya asili ya akili ya mwanadamu.

Hvyo Tunaposema kwamba Elimu ni Ufunguo wa maisha tunamaanisha kwamba, ili uweze kufanya jambo lolote hapa duniani ni lazima uwe na uelewa juu ya jambo lenyewe. Na uelewa huo hauji hivi hivi tu bila kupata mtu wa kukufundisha na kukuelewesha, ndiyo tafsili ya elimu.

Sasa tena jiulize:-
Kuna watu wangapi wamesoma lakini maisha yao hadi sasa hayaeleweki??

Maana yake ni nini??
Hapa inamaanisha kwamba, wapo baadhi ya watu wanaidhani kwamba kusoma au kupata elimu ndio mafanikio yenyewe. La hasha!! Yaani unakuta mtu anachanganya elimu na mafanikio akizani kwamba ni kitu kimoja.

Elimu ni Uelewa wa Jambo fulani.

Bali mafanikio hutokana na faida ya kile ulichokielewa wakati unafundishwa. Lakini utayaona mafanikio endapo tu utatenda kwa umakini yale uliyoyaelewa baada ya kufundishwa (UJUZI).

Fikiria k**a umepata shahada ya udaktari alafu uk**aliza masomo yako ukakaa tu nyumbani bila kutumia taaluma uliyonayo katika kuwa hudumia wengine, lakini ukawa unajivunia mafanikio ya kupata shahada tu; unadhani shahada hiyo inaweza kukuletea mafanikio hapo ulipo?

Misingi ya Elimu ni hii-

Elewa, kisha hudumia wengine kwa lile ulichokielewa. Hapo ndipo utayaona mafanikio.

WITO

Wito wangu kwenu hasa kwa wazazi na walezi; URITHI pekee utakaoweza kumfanya mwanao aweze kumudu maisha ndani ya ulimwengu huu ni ELIMU. ni usimpe mtoto wako Mali kwani kwa kufanya hivyo ni kumuangamiza akiwa bado angali hai.

NB;
Endelea kutembelea ukurasa wetu wa Vission family tz, ili kujiifunza mambo mbali mbali ya kimaisha yatakayo kufanya uimarike kiakili.

Ni katika kuelekea kwenye kampeni yetu ya VISSION FAMILY FURSA.

NIWATAKIE SIKU NJEMA ILIYOJAA BARAKA TELE.

By. GEOFREY CHIRWA

18/10/2016

JICHO LA TOFAUTI (By Captain G)

Katika muendelezo wa makala yetu ya jicho la tofauti ni k**a ifuatavyo:-

Vitu pekee unavyotakiwa kuvizingatia katika kujitengenezea alama binafsi ya utambulisho wako (Individual Identification mark) ni;-

1) Kujitambua kuwa wewe ni nani? Uwezo wako ni upi? Unahitaji nini maishani? Malengo yako yanahusiana na kile unachohitaji kwenye maisha??

Ili kupata majibu sahihi ya maswali haya, inakubidi utenge muda wa kutosha ikiwezekana siku nzima, tafuta sehemu tulivu ambayo hukuizoea kukaa au kushinda mara kwa mara.

Unapokuwepo katika mazingira hayo hakikisha Simu yako unazima kabisa wala usihitaji rafiki wala kampani yoyote bali uwe peke yako kiuhalisia, ukiwa na notes book/dially, kisha ingia ndani ya dhamira yako kifrikra na uanze kuteta na nafsi yako na kusikiliza sauti ya upole itokayo ndani ya mtima wa moyo wako kisha rekodi (andika) Yale mawazo muhimu yanayokujia katika akili yako.

Kwani Mara nyingi hata Mungu uteta na watu wake kwa njia hiyo.

Hivyo ninaamini kwamba sauti itokayo ndani ya moyo wako huwa ni Sauti ya ki Mungu. Ukimaliza siku hiyo anza kuyafanyia kazi polepole yale uliyoyaandika katika kijitabu chako cha kumbukumbu, ndipo majibu hupatikana hapo.

Pia zingatia kupata matokeo katika kila jambo unalolipanga kwenye maisha.

Penda kushirikiana na kushirikishana na wenzio hasa kwa yale mambo yenye tija kwenye jamii na kwako pia.

Epuka sana mtu mwingine hasikupotezee muda katika shughuli zako.

Siku zote kuwa bize kufuatilia ndoto zako za kimaisha ulizojiwekea.

Okoa muda na fedha kwa kufanya matumizi ya fedha bila tija au kukaa sehemu moja tu inayokulazimu utumie pesa nyingi kuliko zile unazoingiza katika mfuko.

YOTE TISA, MTANGULIZE MUNGU KATIKA KILA JAMBO, NAYE ATAFANYA NJIA PASIPO NJIA.

NIKUTAKIE SIKU NJEMA.

Asante.

(By Geofrey Chirwa/ Captain G)

Want your business to be the top-listed Government Service in Ifakara?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Email: Geofreychirwa6@@gmail. Com
Ifakara