Water is essential thing in your body ,
make sure it's your daily routine 🙏🙏
Maji ni mhimu kwa mwili wako hakikisha unapata kila siku
AFYA YAKO kwanza
JayE.S.M�, public health service
02/04/2023
Dalili kuu za kifua kikuu ni zipi??
Hizi ndizo dalili kuu za kifua kikuu;
Mgonjwa wa TB anaweza akapata dalili kati ya hizi
1.kukohoa kohozi zaid ya wiki 2
2.homa zaidi ya wiki 2
3.kukohoa damu
4.kupungua uzito
5.kutokwa na jasho usiku
6.uchovu na
Zingne k**a kukosa hamu ya kula na kutokua kwa watoto na kifua kuuma,
Ukishagundua au kuona dalili hizi chukua hatua nenda kituo Cha kutolea huduma ya afya
Je wajua ??aina kuu mbili (2,) za kifua kikuu,T.B
Kuna aina kuu mbili za T.B ;
1.kifua kikuu Cha mapafu,TB ya ndani ya viungo vya kupumua( pulmonary T.B)
Ni aina ya kifua kikuu , TB ambacho huathiri zaidi mapafu ya binadamu( huathiri watu wote wenye kinga nzuri ya mwili na wale wenye kinga ndogo ya mwili)
2.kifua kikuu Cha nje ya viungo vya kupumua ,mapafu( Extapulimonary TB)
Ni aina ya kifua kikuu ambacho huathiri zaidi ndani ya mwili lakini mbali na mapafu k**a vile mgongo,ubongo,mifupa, na sehemu zingine za mwili
Aina hii ya TB mara nyingi huwaathiri au huwapata zaidi wagonjwa wenye kinga ndogo ya mwili mfano wagonjwa wa Virusi vya UKIMWI,VVU
02/04/2023
Je wajua habari njema kuhusu kifua kikuu?TB
Habari njema ni kwamba kuugua TB ni kitu ambacho hutokea mara chache sana sio kwasababu wagonjwa ni wachache kiasi Cha kushindwaa kusambaza hawa bacteria hapana ni kwasababu tunavuta hawa bacteria lakini kinga zetu ni ziko imara na inaweza kupambana na bacteria hawa.
Lakini pia kwa wagonjwa wa kifua kikuu wakishatumia dozi ya dawa kwa muda wa siku 14 ,mgonjwa huyu hawezi kuambukiza mtu mzima wa afya
Habari wapendwa,
Leo tuendelee kujua(kujifunza) zaidi TB
Leo tujifunze zaidi kuhusu kifua kikuu( TB);
TB ni nini na husababishwa na nini??
T.B ni kifupi Cha neno tuberculosis
Tuberculosis ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa Mycobacterium Tuberculosis. Ni ugonjwa ambao huambukizwa kwa njia ya hewa unaishambulia zaidi mapafu.TB pia inaweza kushambulia sehemu zingine za mwili k**a ubongo,Figo,mifupa, na uti wa mgongo .
Endelea kufuatilia katika page hii na kujifunza zaidi kuhusu ugonjwa wa TB,dalili,aina,visababishi na mazngra hatarishi ,tiba na njia za kujikinga dhidi ya Tb🙏🏽
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Iringa Town Tz , Kazimotojames8@gmail. Com
Iringa
