04/06/2023
HEKARI 100 ZATENGWA KATA YA MGAMA, IRINGA VIJIJINI KUWEZESHA UJENZI WA HOSPITALI KUPITIA UMOJA WA WAZAZI, JUMUIYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Uchungu wa MWANA?
Jana Umoja wa Wazazi Iringa Vijijini tumefanikiwa kutembelewa na Katibu Mkuu wa Wazazi Ndugu Gilbert Kalima akiwa amefika kwa dhumuni la kutembelea eneo la HEKARI Mia Moja lililotengwa Ili KUWEZESHA UJENZI WA HOSPITALI katika eneo hilo
Mwenyekiti wa Halmashauri Iringa Vijijini akiwa ameongozana na Diwani na Viongozi wengine wa Kijiji alisema kuwa litakua jambo jema Sana k**a Mradi huo utafanikiwa na kuishukuru Jumuiya ya Wazazi kwa kuwa tayari kujenga Hospital katika Eneo hilo
Katibu mkuu aliwashukuru Viongozi wote wa Kata ya MGAMA na Viongozi wote wa Halmashauri ya Iringa Vijijini kwa kuwa tayari kulitoa Eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Wazazi aliwahakikishia Viongozi na Wananchi kuwa Suala la Afya ni Moja ya Eneo Muhimu ambalo Jumuiya ya Wazazi inajihusisha nalo
Na itakua ni Heshima kubwa Kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa
Uongozi wa Wazazi Iringa Vijijini unawashukuru Viongozi wote kwa kuja na kuungana pamoja nasi katika Kumpokea Katibu mkuu na Kwenda kuliona eneo hilo
Mungu Ibariki Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini
Mungu Kibariki Chama Cha Mapinduzi
By
Maryline Mamuya
Katibu Elimu, Malezi na Mazingira Iringa Vijijini.
