Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa

Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa

Share

Halmashauri ya wilaya ya Iringa ni taasisi ya kiserikali inayohudumia jamii ya wakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa,na ilianzishwa rasmi mwaka 1964.

18/03/2022

Usichukulie poa nyumba ni choo. Ujenzi wa vyoo bora na matumizi sahihi yatasaidia kutokuwepi na homa za matumbo na maradhi mengine yanayoendezwa na kutapakaa hovyo kwa kinyesi.

Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inawakumbusha wananchi wote kuwa suala la vyoo bora na matumizi sahihi ni lazima wakati wote ili kuwezesha kaya zote kuwa katika hali ya usafi wa Mazingira.

Timu za afya zinaendelea kupita na kukagua kila kaya ili kubaini wanaokiuka na kuvunja sheria ama kukaidi agizo la Ujenzi wa vyoo bora.

22/02/2022

Taarifa kwa Umma, Mh.Rais alitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikiana na Jamii

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 22/02/2022

Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano, Iringa-DC)

Iringa-DC inatekeleza agizo la Mh.Rais Samia.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Mohamed Moyo tarehe 16 Februari 2022 amefungua mafunzo ya Anwani za makazi yaliyotolewa kwa Wenyeviti wa Vijiji,Wetendaji wa Kata na Vijiji.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amewataka Viongozi hao kufanya kazi hiyo kwa weledi ili kufukia lengo la serikali na ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ibara ya 61 (m).

Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati ni lazima wawe wanaishi mahala panapo tambulika na kufikika kwa urahisi lakini pia kuwezesha kufanya biashara kwa njia ya mtandao, kurahisisha suala zima la Ulinzi na Usalama.

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 17/02/2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupitia kwa Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Kisanga anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kuomba kotesheni ya Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa katika shule ya Msingi Kisanga kuomba kotesheni ya Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa katika shule takes hapo juu.

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 17/02/2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupitia kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Pawaga anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kuomba kotesheni ya Ujenzi katika shule ya Sekondari Pawaga ambazo ni Ujenzi wa vyumba vya madarasa,maabara za masomo ya Sayansi na Ofisi za Walimu

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 07/02/2022

Mkrugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kupitia kwa Mganga Mfawidhi:
- Kituo cha Afya Mgama,
- Zahanati ya Wasa,
- Zahanati ya Usengelendeti,
- Zahanati ya Mikong’wi,
- Zahanati ya Migoli,
- Zahanati ya Ikengeza,
- Zahanati ya Iguluba.
Anawatangazia kazi za ufundi zifuatazo:- 👇

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 05/02/2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja anawatangazia wananchi wote wenye sifa ya ufundi kuomba kazi kwa ajili ya Ujenzi wa Wodi ya wanawake, Wanaume, chumba cha Upasuaji na chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Iringa -Igodikafu iliyopo kijiji cha Mbuyuni Kata ya Itunundu

Photos from Halmashauri  Ya  Wilaya  Ya  Iringa's post 04/02/2022

Tahadhali inatolewa kwa Umma hususani wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa juu ya uwepo wa baadhi ya watu wasio waaminifu wanaouza bidhaa ambazo sio pembejeo sahihi za kilimo.

Wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika Ofisi za serikali za Vijiji na Kata katika maeneo mara waonapo watu hao ambao wanajipenyeza kwa njia za panya bila kutoa taarifa katika maeneo ya Utawala wala kuwa na barua kutoka kwa Viongozi ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Wilaya.

04/02/2022

Ewe mwananchi wa Tanzania lips Kodi kwa Maendeleo ya Nchi yako.

04/02/2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa za kumilili ardhi wafuke katika Ofisi ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa ajili ya kuchukua fomu ya maombi ya Ardhi na kulipia.

Viwanja vipo karibu na huduma zote za muhimu za Kijamii karibuni sana

30/01/2022

Ofisi ya Rais Tawala za Mikia na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wametoa orodha ya Watumishi waliomba uhamisho wa kubadilishana tafadhali tembelea tovuti za Wizara k**a zinavyoonekana katika tangazo hili.

27/01/2022

Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tunakutakia afya njema Rais wetu Mh.Samia Suluhu Hassan

Want your business to be the top-listed Government Service in Iringa?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

PO. BOX 108
Iringa

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30
Saturday 07:30 - 12:00