06/05/2026
Taarifa ya Kikao β 5 Aprili 2026
Tarehe 5 Aprili 2026, Jumuiya ya Mbomipa ilikutana na kampuni ya Carbon Tanzania kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu mradi wa uvunaji wa hewa ukaa ndani ya hifadhi.
Kikao kilifanyika katika hali nzuri na yenye tija, kikionyesha mwelekeo chanya wa ushirikiano. Lengo kuu la majadiliano lilikuwa kuhakikisha mradi huu unachangia maendeleo ya jumuiya pamoja na kuboresha ustawi wa wananchi wake kwa ujumla.
Kikao hicho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali muhimu wakiwemo Shirika la STEP, Honeyguide, Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Jamii (CWMAC), pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
Kwa pamoja, wadau walionesha dhamira ya kuendelea kushirikiana ili kufanikisha malengo ya mradi kwa manufaa ya jamii na uhifadhi endelevu wa mazingira.
27/04/2026
Tarehe 25 Aprili 2026, Baraza la Jumuiya ya MBOMIPA lilifanya kikao chake cha kikatiba cha robo ya tatu. Katika kikao hicho, Menejimenti iliwasilisha taarifa mbalimbali, zikiwemo:
β’ Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za robo ya tatu
β’ Taarifa ya fedha kuhusu mapato na matumizi kwa robo ya tatu
β’ Taarifa nyingine mbalimbali za Jumuiya
Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa uhifadhi wanaoshirikiana na MBOMIPA, wakiwemo mashirika ya uhifadhi pamoja na wawakilishi kutoka Serikalini.
05/04/2026
Heri ya Sikukuu ya Pasaka! π³
Mbomipa WMA, tunawatakia heri ya sikukuu ya Pasaka iliyojaa upendo, amani na matumaini mapya.
π³
27/03/2026
Kupitia Mradi wa SEGA, tarehe 03β04/03/2025 timu ya menejimenti kwa kushirikiana na wawakilishi wa vijiji wanachama na iliwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kuanzia robo ya kwanza hadi robo ya pili ya MBOMIPA. Aidha, taarifa ya mgao wa fedha wa awamu ya kwanza kwa wananchi wa vijiji hivyo iliwasilishwa rasmi.
Zoezi hilo pia liliambatana na utoaji wa elimu kuhusu uzuiaji wa shughuli haramu, hususan zinazohatarisha rasilimali za uhifadhi.
Wananchi walionyesha furaha na kuipongeza Jumuiya kwa kuendelea kuzingatia uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa jamii katika masuala yanayohusu maendeleo yao.
21/03/2026
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA inawatakia Waislamu wote Sikukuu njema ya Eid al-Fitr.
Siku hii ikawe chanzo cha furaha, amani na mshikamano miongoni mwetu, huku ikiimarisha moyo wa kujali na kuhifadhi rasilimali za asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
ππ
16/02/2026
Kupitia mradi wa , tarehe 13 na 14 wiki iliyopita, Jumuiya yetu ya MBOMIPA kwa kushirikiana na Shirika la Honeyguide Foundation tuliendesha kikao maalum kilichowakutanisha wadau wetu muhimu.
Lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili na kuimarisha ushirikiano wetu, kwa kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kufikia malengo ya pamoja kwa ufanisi na uwajibikaji zaidi.
Tunaamini kuwa kupitia mshikamano na ushirikiano thabiti, tunaweza kuleta matokeo chanya na endelevu kwa jamii tunazozihudumia. Kwa pamoja tunaweza. πͺπΏ
17/01/2026
Hongera kwa Ayoub Ngoko, Mshindi wetu katika shindano la (Facebook).
01/01/2026
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA inawatakia Heri ya Mwaka Mpya 2026 uliojaa furaha na mafanikio! π
25/12/2025
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori MBOMIPA inawatakia heri ya Krismasi π²na msimu mwema wa sikukuu.