29/05/2026
Afisa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Bi. Anna Tesha amewataka Vijana kuwa na nidhamu na Uadilifu katika Matumizi ya fedha wanazokopeshwa na Serikali kwani bila kufanya hivyo ni ngumu kufikia Malengo yao.
Ameyasema hayo Mwishoni mwa juma liliopita alipokua akizungumza na Vijana kwenye kikao cha Maelekezo na ujazaji wa Mikataba kwa Wanufaika wa Mkopo wa asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo jumla ya Vikundi vya Vijana 37 vimepatiwa Mkopo wa fedha za Kitanzania Shilingi 1,242,423,500.
Bi. Tesha amesema kuwa kundi la Vijana ndio linaloongoza kwa kutofanya Marejesho kwa wakati hivyo inapelekea uaminifu kupungua dhidi yao.
29/05/2026
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imetoa Fedha za Kitanzania 1,575,123,500 kwa vikundi 55 ikiwa ni Mkopo unaotokana na asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu katika robo ya tatu ya Mwaka 2025/2026.
Katika Mkopo huo Wanawake ni Vikundi 15 wamepata Shilingi 299,400,000, Vijana Vikundi 37 Shilingi 1,242,423,500 na Watu wenye Ulemavu Vikundi 3 Shilingi 33,300,000.
Akizungumza wakati wa Semina kwa Wanufaika wa Mkopo huo Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Ndg. Hamis Mnubi amewataka kuzitumia fedha hizo kulingana na Mipango na maandiko yao ili kuweza kutimiza malengo yanayokusudiwa.
27/05/2026
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mapema leo imesaini Mkataba wa umaliziaji ujenzi wa Barabara za Mjini ikiwa ni Mkataba Mpya baada ya Kuvunjwa kwa Mkataba wa Mkandarasi wa awali M/s Sichuan Road and Bridge (Group) Corporation Ltd) .
Mkataba huu wa sasa ni Baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Mkandarasi M/s China Civil Engineering Construction Corporation na ni Mkataba Miezi 8 kuanzia tarehe 01/06/2026 hadi tarehe 31/01/2027 na una thamani ya TZS: 25,547,162,432.04 bila Kodi ya ya Ongezeko la thamani.
Akitoa neno baada ya Utiaji Saini Mkataba huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anatekeleza Mradi huo ndani ya Muda uliopo kwenye Mkataba na hakutokuwa na Kuongezewa Muda wa utekelezaji.
22/05/2026
Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kahama Wamepatiwa Mbinu mbalimbali za Ukusanyaji wa Mapato ya Madini kutoka kwa Majirani zao wa Manispaa ya Geita.
Akizungumza katika Kikao cha Pamoja cha Kubadilishana Uzoefu kati ya Manispaa hizo mbili kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Geita, Naibu Meya wa Manispaa ya Kahama Mhe. Shabani Mikongoti amesema kuwa kuna vitu vingi ambavyo wamejifunza kuhusu Makusanyo yatokanayo na Chanzo cha Madini ambapo wao kwa nafasi yao wataona namna ya kwenda kuyafanya wakirudi Kahama.
Awali akitoa neno la Ukaribisho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita Ndg. Yefred Myenze amesema kuwa Halmashauri zinatakiwa kuhakikisha zinakusanya Mapato ili kuweza kutoa huduma na kutekeleza Miradi ya Maendeleo, kusikiliza na kutatua Kero za Wanachi.
22/05/2026
Waheshimiwa Madiwani Wilayani Kahama wamepatiwa mafunzo ya maadili na sheria ya Kuzuia na Kupambana na rushwa kifungu kwa kifungu ili kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa Majukumu yao.
Mafunzo hayo yamefanyika Jana Mei 21, 2026 kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Kahama na kujumuisha Madiwani kutoka Halmashauri zote tatu za Wilaya ya Kahama (Ushetu, Msalala na Manispaa).
Akiwezesha Mafunzo hao Afisa wa Takukuru Bw. Maxmillian Kyabona amewaelezea Madiwani majukumu yao na wajibu wao katika kusimamia miradi ya maendeleo katika Kata zao.
Aidha waheshimiwa Madiwani wameelezwa kuwa ni vyema wanapokuwa wanasimamia kanuni za kuwajibisha watendaji ambao siyo waadilifu kuhakikisha wanafanya pasipo kumuonea mtu na kuhakikisha wanasimamia almashauri na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha.
21/05/2026
Tumempata Mkandarasi Mpya, Njoo uwe Shuhuda wa Tukio la Utiaji Saini wa Mkataba
17/05/2026
Kesho hiyo, Stendi ya Malori Majengo.