07/07/2026
Karibu sana MH. RIDHIWANI KIKWETE
Ukurasa Rasmi kwa ajili ya Maendeleo kwa Kata ya USINGE chini ya Mheshimiwa Kulwa Maendeleo Kajoro Diwani Kata ya Usinge 2025-2023. Mawasiliano 0764537216
07/07/2026
Karibu sana MH. RIDHIWANI KIKWETE
24/06/2026
Diwani wa Kata ya Usinge, Mhe. Kulwa Kajoro akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, Japhael Lufungija, na Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Joseph E. Tama, amefuatilia mjadala na upitishaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2026/2027 kupitia Wizara ya Fedha.
Mhe. Kajoro amewapongeza wabunge kwa kuipitisha bajeti hiyo, akisema itasaidia kuharakisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi katika maeneo tofauti nchini Tanzania.
Cc : Ofisi Ya Diwani Kata Ya Usinge
20/06/2026
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC), Richard Abwao amefariki dunia leo Juni 20, 2026 akiwa kwenye matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha amesema Kamanda Abwao alikuwa akipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo, lakini leo wamepokea taarifa hizo za kusikitisha.
Amemueleze hayati Abwao k**a kiongozi shupavu aliyepambana kwa nguvu zote dhidi ya vitendo vya uhalifu mkoani Tabora.
19/06/2026
https://youtu.be/sX1sUzeipWc?si=ExQlNA7xPXJ9wyir
#ZIARAUSINGE : Kipaza kikafunguliwa na Luck Kipaji kisha kikatua kwa mwenye Ziara Kulwa Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.
: Kipaza kikafunguliwa na Luck Kipaji kisha kikatua kwa mwenye Ziara Kulwa Kajoro nae akatoa pasi kwa Wananchi wa Ugansa wafunguke kisha Maafisa wa Idara husika wakatoa majibu....
Cc : Ofisi ya Diwani Kata ya Usinge & Usinge Tv YouTube 📺
🎥 Lugali
18/06/2026
Diwani wa Kata ya Usinge, Mhe. Kulwa M. Kajoro, amehitimisha rasmi ziara yake ya siku saba ndani ya Kata ya Usinge kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika eneo la Usinge Kati. Katika ziara hiyo, aliambatana na viongozi mbalimbali pamoja na maafisa wa kata kwa lengo la kusikiliza, kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.
Ziara hiyo imekuwa jukwaa muhimu lililowapa wananchi nafasi ya kueleza kero zao moja kwa moja kwa viongozi, jambo ambalo limeongeza matumaini na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi na uongozi wa kata.
Miongoni mwa masuala yaliyopatiwa ufafanuzi na hatua za utatuzi ni pamoja na huduma za afya, elimu, usalama barabarani, migogoro ya uharibifu wa mazao unaosababishwa na mifugo, ujenzi wa machinjio ya kisasa, eneo la muda la maegesho ya mabasi, uchongaji wa barabara za mitaa, matumizi sahihi ya vyoo vya soko, upanuzi wa huduma za umeme katika vitongoji na mitaa pamoja na huduma ya ukusanyaji wa taka katika soko la Usinge.
Wananchi wengi wameeleza kuridhishwa na ziara hiyo, wakisema imewapa fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa uwazi na kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa viongozi. Baadhi ya vijana wa Usinge walimpongeza Mhe. Kajoro kwa kuanzisha utaratibu huo na kumuomba aendelee kuitisha mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi na viongozi.
Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo, Mhe. Kajoro aliwashukuru wananchi wote kwa kujitokeza kwa wingi na kwa kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni, kero na mapendekezo yao. Aliwahimiza kuendelea kushirikiana na viongozi wa kata na kujitokeza kwa wingi zaidi katika mikutano ijayo ili kwa pamoja wajenge maendeleo endelevu ya Kata ya Usinge.
Ziara hiyo ya siku saba imeweka historia ya kuwa ziara ya kwanza kwa Diwani wa Kata ya Usinge kuzunguka vijiji na vitongoji vyote vya kata hiyo akiwa pamoja na viongozi na maafisa wa kata, kwa lengo la kusikiliza wananchi, kutatua changamoto zao na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
"Maendeleo ya Usinge yatachangiwa na ushiriki wa wananchi wenyewe. Tukisikilizana, tukishirikiana na kutatua changamoto kwa pamoja, tutafikia maendeleo tunayoyataka." – Mhe. Kulwa M. Kajoro.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Diwani Kata ya Usinge
16/06/2026
Kesho ni hitimisho la Ziara Ya Siku Saba ya kusikiliza Kero na kuzitatua kwa wananchi wa kata ya Usinge, Wananchi wote wa Kata ya Usinge mnakaribishwa kufikisha kero na malalamiko Yenu...
16/06/2026
Wananchi
MWAMAPULU NA NKOKOTO TUMEKUFIKIA Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.
Maswali ya Wananchi wetu wa Usinge
15/06/2026
Luganjo Mlimani, Kaliua – Diwani wa Kata ya Usinge, Kulwa M. Kajoro, amewataka viongozi wa Kijiji cha Luganjo Mlimani kushirikiana kwa pamoja ili kuimarisha maendeleo ya kijiji hicho na vitongoji vyake.
Akizungumza katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika Luganjo Mlimani, Mhe. Kajoro alishughulikia kero iliyokuwa imejitokeza kati ya Mwenyekiti wa Kijiji na wajumbe, ambapo alisisitiza umuhimu wa viongozi kufanya kazi kwa umoja na kuheshimu majukumu yao kwa manufaa ya wananchi. Aidha, aliwakumbusha viongozi kutunza siri za vikao vya ndani na kuhakikisha wanaitisha mikutano ya wananchi mara kwa mara ili kujadili masuala ya maendeleo ya kijiji.
Kuhusu changamoto ya barabara ya Usinge hadi Luganjo, Mhe. Kajoro aliwataka wananchi kuwa na subira, akieleza kuwa Halmashauri tayari imepata mkandarasi mpya ambaye ataanza kazi ya matengenezo na maboresho ya barabara zenye changamoto katika Kata ya Usinge.
Katika sekta ya maji, Kaimu Katibu wa Maji wa RUWASA Kata ya Usinge aliwahakikishia wananchi wa Luganjo Mlimani kuwa huduma ya maji safi na salama itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho, akieleza kuwa pampu ya maji inayohitajika kwa mradi huo tayari imepatikana.
Akizungumzia mgogoro unaohusu ujenzi wa Zahanati ya Luganjo Mlimani, ambao umekuwa chanzo cha malalamiko kutokana na wananchi kulazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za afya, Mhe. Kajoro aliwaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu huku akibainisha kuwa suala hilo linaendelea kufuatiliwa na Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Joseph E. Tama.
Diwani huyo pia alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano inayotishwa na viongozi wa kijiji ili kupata taarifa za mapato na matumizi ya serikali ya kijiji pamoja na maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ziara hiyo ilifanyika katika Kijiji cha Luganjo Mlimani na kuhudhuriwa na wananchi kutoka vitongoji vya Luganjo Mlimani na Kiloleni, ambapo walipata fursa ya kuwasilisha changamoto zao na kupokea majibu kutoka kwa viongozi.
Imetolewa na:
Idara ya Habari na Mawasiliano
Ofisi ya Diwani, Kata ya Usinge.