10/06/2026
Ofisi ya mbunge kaliua
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ofisi ya mbunge kaliua, Political organisation, .
10/06/2026
MHE. TAMA AISHUKURU SERIKALI KWA KUTENGA FEDHA ZA BARABARA YA MPANDA–KALIUA–KAHAMA
Mheshimiwa Joseph Enock Tama, Mbunge wa Jimbo la Kaliua, amechangia hoja wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi Bungeni, ambapo ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mpanda–Kaliua–Kahama.
Akichangia hoja hiyo, Mheshimiwa Mbunge alieleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi, kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao pamoja na kufungua fursa za biashara na uwekezaji kwa wananchi wa maeneo husika.
Mheshimiwa Tama ameendelea kuonesha dhamira ya kusimamia miradi ya maendeleo yenye manufaa makubwa kwa wananchi wa Jimbo la Kaliua na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na:
Ally J. Kallah
Katibu wa mbunge - jimbo la kaliua
10/05/2026
TANZIA.
10/05/2026
HAPPY MOTHER'S DAY
04/05/2026
SERIKALI YAANZA NA KATA YA KALIUA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI
Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa kuboresha upatikanaji wa maji kwa kuanzia Kata ya Kaliua, ambapo mabomba ya usambazaji wa maji yameanza kuwasili tayari kwa hatua za utekelezaji.
Hatua hii inalenga kupunguza changamoto ya uhaba wa maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa uhakika zaidi.
Mheshimiwa Joseph Enock Tama, Mbunge wa Jimbo la Kaliua, ameendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma bora.
Kuanza kwa mradi huu katika Kata ya Kaliua kunaashiria dhamira ya Serikali ya kutatua changamoto ya maji kwa vitendo na kuleta matumaini mapya kwa wananchi.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Kaliua
NSIMBO,MPONGOLO,ISUNDA,LUYEMBE, CENTER L KUWASHWA UMEME.
💪🏾
26/04/2026
HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA FPCT - KALIUA
Leo tarehe 26/04/2026, mimi Ally J. Kallah, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kaliua nimeshiriki ibada ya harambee ya ujenzi wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) k**a Mgeni Rasmi, nikimuwakilisha Mhe. Joseph Enock Tama, mbunge wa jimbo la kaliua.
Katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mungu, jumla ya zaidi ya shilingi milioni 36 zimechangishwa, jambo linaloonesha mshik**ano mkubwa wa wananchi wa Kaliua katika kuunga mkono maendeleo ya kiroho na kijamii.
Kwa niaba ya Mheshimiwa Mbunge, tunatoa pongezi kwa viongozi wa kanisa, waumini na wananchi wote waliojitokeza kwa moyo wa kujitolea. Ushirikiano huu ni ishara ya umoja, upendo na dhamira ya pamoja ya kuijenga Kaliua yenye maendeleo.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kaliua itaendelea kuwa karibu na wananchi, kusikiliza changamoto zao, kushirikiana nao katika maendeleo, na kuunga mkono taasisi za dini na kijamii. Mheshimiwa Joseph Enock Tama anaendelea kuwa kiongozi mwenye maono, anayejali watu na anayetekeleza wajibu wake kwa vitendo.
Imetolewa na:
Ally J. Kallah
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kaliua.
MHE. MBUNGE AHOJI UJENZI WA KITUO CHA AFYA IGWISI
Mheshimiwa Joseph Enock Tama, Mbunge wa Jimbo la Kaliua, amehoji katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Igwis.
Akijibu swali hilo, Naibu wazili wa Afya imeeleza kuwa suala hilo liko kwenye mchakato na kwamba muda wowote zoezi la ujenzi litaanza.
Pamoja na mpango huo wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo yenye wakazi zaidi ya elfu sabini na mbili (72,000) Mheshimiwa Mbunge ameendelea kuonesha dhamira yake ya kusimamia upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa Jimbo la Kaliua kwa ujumla.
Imetolewa na:
Ally J. Kallah
Katibu wa mbunge - jimbo la kaliua
