ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA

ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA, Karagwe.

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 24/11/2023

Huduma za Ambulance zilikuwa za shida hivyo watu walilazimika kutumia vitanda vya kutengenza lakini kuhakikisha wagonjwa wanafikishwa Hospitali. Lakini pia akina Mama waliongoza na wagonjwa kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya chakula kila aina kinapatikana. Hapo mama akiwa kijanjabo ana andaa chakula

24/11/2023

Elct Nyakahanga Hospital Administration block

24/11/2023

Elct Nyakahanga Hospital wodi B katika ubora wake miaka ile

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 24/11/2023

Elct Nyakahanga Hospital hatuwezi kusahahu kuwaenzi wazee wetu na viongozi wetu waliokwisha tangulia mbele ya haki na wengine bafo wapo lakini wanahitaji faraja yetu. Tunaendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki viongozi wetu wa Hospitali na wastaafu wote.
Hapo ni jengo la kanisa yetu kabla ya kufanyiwa marekebisho. Pia picha nyingine inaonyesha siku ya maafari ya kuhitimu wanafunzi wa Pre-Nursing enzi zile

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 24/11/2023

Hospitali ya Elct Nyakahanga imekuwa ikitoa huduma za kimwili na kiroho.

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 24/11/2023

Elct Nyakahanga Hospital enzi hizo wakati wa black and white dhima yetu ilikuwa ni kutoa huduma bora za afya na tiba. Tumetoka mbali na bado safari ni ndefu. Mungu wetu tunakuomba uendelee kutupa moyo wa kutenda kazi yako kwa wahitaji ili wauone uwepo wako katika Hospitali yetu. Mungu utubariki na zaidi wabariki viongozi wetu wa Hospitali na Dayosisi yetu ya karagwe

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 24/10/2023

Kusimikwa kwa viongozi wa Hospitali ya Nyakahanga. Tarehe 22/10/2023 ilikuwa siku ya furaha na tulivu, siku muhimu na ya kumbukumbu kwani Viongozi wawili Dr Furaha Kahindo - Mganga Mkuu na Mr Justine Kataraia - Muuguzi MKuu walisimikwa rasmi na Baba Askofu Benson Bagonza Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Dayosisi ya Karagwe kuongoza Hospitali kwa kipindi hiki.

Akisoma Hati ya Dayosisi ya karagwe kwa ajili ya viongozi wateule wa Hospitali ambao ni Dr Furaha Mganga Mkuu na Justine Kataraia Muuguzi Mkuu, Katibu mkuu wa Dayosisi Mch Jeremiah M Rugimbana alisema, kwa mujibu wa katiba ya Dayosisi ya Karagwe, ukurasa wa 27, kifungu cha 1.14.2.i kuna kazi za Halmashauri kuu. Halmashauri kuu ya Dayosisi ya Karagwe namba 142 iliyofanyika Karagwe Hoteli kayanga tarehe 7/6/2023, katika agenda yake namba HK/142/9 ilimchagua Dr Furaha Darlene aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mganga Mkuu kuwa Mganga mkuu kamili. Aidha Manejimenti ya Dayosisi ya Karagwe kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya KKKT Dayosisi ya karagwe ilimteua Bwana Justine Kataraia kuwa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Nyakahanga kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Kwenye nafasi hiyo ya Uongozi.

Hivyo baada ya kusomwa kwa hati hiyo Baba Askofu aliwasimika viongozi hao kila mmoja kwa nafasi yake. Mhesh Baba Askofu waombea kwa Mungu wa Mbinguni asiwapungukie wanapoamka, wanapoingi na kutoka na kuwatakia mafanikio katika wajibu huu mpya. Aidha aliwakumbusha kwamba kuwa kiongozi kuna garama zake, na nyingi ni chungu sana. Aliendelea kusema kuwa ukiwa kuongozi unapoteza uhuru wako binafsi,hutavaa k**a unavyopenda, hutakunywa k**a unavyopenda, hutakula popote unavyopenda, hutaenda popote k**a unavyopenda, utajichunga badala ya kuchungwa, utasengenywa lakini wewe huma haki ya kusengenya wengine, utalalamikiwa lakini wewe huna haki wala mahali pa kulalamika, waliochini yako wana haki ya kuonywa lakini wewe huna hiyo haki maana kosa moja unaondoka.

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 21/08/2023

Maendeleo ya ujenzi wa Private Elct Nyakahanga Hospital unaendelea vizuri. Uko kwenye hatua za finishing

Photos from ELCT/NYAKAHANGA DD.HOSPITAL KARAGWE-TANZANIA's post 03/01/2023

Tukio la kuweka jiwe la Msingi kwenye jengo la Private ward lililofanyika tarehe 31/12/2022 na Baba Askofu Dr Benson Kalikawe Bagonza. Katika salaam zake, Mhesh Baba Askofu benson Bagonza aliupongeza Uongozi wa Hospitali kwa hatua hiyo iliyofikiwa, pia aliwatahadhalisha mafundi wajenzi wa kampuni ya Shubtec Group LTD kuhakikisha jengo hilo linaisha kwa muda muhafaka.

14/06/2019
Want your business to be the top-listed Government Service in Karagwe?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Karagwe