Halmashauri ya Mji Kasulu

Halmashauri ya Mji Kasulu

Share

Kasulu ni yetu sote, Karibu sana

20/03/2026

EID AL FITR MUBARAK 🤲 🌙 ♥️

07/03/2026

Sisi Halmashauri ya Mji Kasulu tunatambua na kuthamini mchango wa mwanamke katika familia,jamii na taifa kwa ujumla kwa pamoja tunasema Heri ya siku ya mwanamke Duniani ❤️.

Photos from Halmashauri ya Mji Kasulu 's post 05/03/2026

KAYA 2,114 ZENYE UHITAJI MAALUMU HALMASHAURI YA MJI KASULU KUNUFAIKA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amezindua zoezi la uandikishaji na ugawaji wa Bima ya Afya kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wanaotoka katika familia zenye uhitaji maalumu huku akiwataka wataalam kuhakikisha wanawafikia wanufaika wote waliokusudiwa.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi huo katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Nyalumanga na kubainisha kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imegharamia bima hizo kwa wananchi wasiokuwa na uwezo ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu kwa urahisi na kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma za afya.

" Awamu hii ni kwa wale watu ambao hawana uwezo wa kugharamia upatikanaji wa Bima , sasa Mhe. Rais amegharamia gharama zote na tunagawa bima za afya lengo kubwa ni kuwezesha wananchi kufikia huduma za matibabu na kuondoa vikwazo vyote na kuleta usawa kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini hadi kitaifa "

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mbelwa Abdallah Chidebwe amebainisha kuwa ahadi ya Chama ni kuhakikisha kila mwananchi anapata Bima ya Afya.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu Ayubu Ngalaba Kilugu amewatoa hofu wananchi ambao bado hawajapata Bima na kuwataka kuwa na subira kwa kuwa zoezi hilo bado linaendelea.

"Swala la afya ndugu zangu ni swala nyeti sana watu wengi wanapoteza maisha kwa sababu ya kukosa gharama za matibabu kwa hiyo hiki kitu anachokifanya Mhe. Rais ni kitu kizuri sana kwa hiyo wanakigondo tunamshukuru sana na Kwa wale ambao hamjapata huduma kwa leo bado zoezi hili ni endelevu msife moyo "

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Nurfis Azizi amesema amethibitisha kuwa vifaa vya BVR vilivyopo vinafanya kazi vizuri na vinasaidia kurahisisha usajili wa wanufaika.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Gwamaka Mwakyoma, ameahidi kusimamia utekelezaji wa Bima kwa weledi na uadilifu, kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.

Baadhi ya wanufaika wanamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuwawezesha kupata Bima za Afya ambazo zinaenda kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa urahisi.

Awamu ya kwanza ya zoezi hilo limejumuisha jumla ya kaya 2114 Halmashauri ya Mji Kasulu ambapo watu 9360 wenye uhitaji maalumu watanufaika.

Photos from Halmashauri ya Mji Kasulu 's post 05/03/2026

WAMILIKI WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA MAELEKEZO YA MTAALA WA ELIMU ULIOBORESHWA

Wamiliki wa shule zisizo za serikali Halmashauri ya Mji Kasulu wametakiwa kuzingatia kikamilifu maelekezo ya utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa wa Elimu ya Msingi na Sekondari kwa lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kuimarisha ustawi wa shule zote.

Wito huo umetolewa na Afisa Udhibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Kasulu, Sadock Rusekwa wakati akiwasilisha mada kuhusu Maboresho ya Mitaala katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kasulu akiwahimiza wamiliki wa shule kuwa karibu na walimu ili kuhakikisha wanaelewa kwa kina michepuo yote.

“Kwanza kabisa niwapongeze wamiliki na wasimamizi wa shule zote kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya na niwaombe sana kaeni karibu na walimu ili wayafahamu vizuri maelekezo ya utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa na kufahamu michepuo yote”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya wamiliki wa shule zisizo za serikali ( TAMONGSCO)
Kanda ya Magharibi Erick Mtondo amewasisitiza wamiliki wa shule kusimamia nidhamu kwa walimu na wanafunzi pamoja na kuajiri wafanyakazi kwa mikataba rasmi na kuwapatia barua za majukumu ili kuepusha migogoro na usumbufu katika uendeshaji wa shule.

Naye Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Kasulu Gaspar Kulikiza amewaomba wamiliki wa shule kusimamia kwa makini utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati.

“Niwaombe sana wamiliki wa shule wasisitizeni wakuu wa shule watoe taarifa sahihi na kwa wakati pale zinapohitajika ili kurahisisha utendaji wa kazi kwa kila upande”

Katika hatua nyingine, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Felician Ferdinand amewasisitiza kuzingatia ukaguzi na matengenezo ya magari yanayotumika kusafirisha wanafunzi.

“Nimepokea maoni yote na tunaendelea kuyafanyia kazi niwaombe sana sisitizeni ukaguzi na marekebisho ya magari yanayotumika shuleni ili yaendelee kuwa bora kila siku pia hakikisheni usalama wa watoto”

Aidha, Afisa Elimu wa Kata ya Murusi Agnes Seth Mwaikamila amewakumbusha wamiliki wa shule kuwasisitiza wazazi kutekeleza wajibu wao wa kuwaandaa watoto mapema kwenda shuleni na kuhakikisha wanawapokea kwa wakati wanaporejea nyumbani.

Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Nurfis Azizi kikiwashirikisha wamiliki wa shule,maafisa,maafisa Elimu kata, Elimu msingi na sekondari.

04/03/2026

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu atazungumza na Waandishi Habari kuhusu Mpango wa Bima ya Afya kwa wote katika Ofisi ya Mtendaji Kigindo.

Photos from Halmashauri ya Mji Kasulu 's post 03/03/2026

WAKAZI WA KATA YA MURUSI WAISHUKURU SERIKALI KWA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Wakazi wa Kata ya Murusi Halmashauri ya Mji Kasulu wameishukuru Serikali kwa kuleta mpango wa Bima ya Afya kwa Wote wakieleza kuwa huduma zinazotolewa ni bora na zitasaidia familia nyingi kupata matibabu kwa urahisi.

Zoezi la uandikishaji na ugawaji wa kadi za bima limefanyika katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Murusi ambapo kaya zenye uhitaji maalumu zimeendelea kunufaika na mpango huo ikiwemo kupunguza mzigo wa gharama za matibabu na kuwawezesha kupata huduma katika vituo vya afya mbalimbali.

"Tunaishukuru serikali kwa huduma hii ya Bima ya afya kwa wote hapa tumepata huduma vizuri, wanatuhudumia vizuri na hizi bima zitasaidia kuondoa gharama na kupata huduma nzuri hospitali yoyote tutakapoenda kutibiwa"

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Murusi Frank Bruno ameeleza kuwa mwitikio wa wananchi ni mkubwa na unaendelea kuongezeka na kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza muda wa zoezi hilo ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi kujiandikisha na kunufaika na mpango huo.

"Uandikishaji na ugawaji wa Bima za afya ni jambo la kitaifa na hapa kwetu wananchi wamejitokeza kwa idadi kubwa na tunatamani kuona watu wengii zaidi naiomba serikali iongeze muda k**a kuna uwezekano ili wananchi wengi wanufaike "

Zoezi hilo linasimamiwa na Ofisi ya Bima ya Afya Mkoa wa Kigoma, Mratibu wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mratibu wa TASAF, Maafisa Watendaji pamoja na Wenyeviti wa Mitaa.

03/03/2026

Kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Kigoma kupitia Kamati ya Ushauri ya Wafanyakazi Wanawake wa Halmashauri ya Mji Kasulu kitawatembelea watoto yatima katika Kituo cha Matumaini (Center of Hope) siku ya Ijumaa tarehe 6 Machi 2026.

27/02/2026

MADIWANI KASULU WAPATIWA MAFUNZO MAALUM, WASISITIZWA UWAJIBIKAJI NA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Nurfis Azizi amefungua rasmi mafunzo ya Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu akisisitiza umuhimu wa kuzingatia misingi ya utendaji kazi kwa manufaa ya wananchi na kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfis amesema kuwa Madiwani ni daraja muhimu kati ya wananchi na Serikali hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwajibikaji na weledi ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati.

Amebainisha kuwa Serikali za Mitaa zina jukumu kubwa la kusimamia rasilimali na miradi ya maendeleo jambo linalohitaji uelewa mpana wa masuala ya uongozi, utawala bora na maadili ya uongozi.

Katika mafunzo hayo, jumla ya mada kumi zitafundishwa ikiwemo mada ya uongozi na utawala bora, maadili ya Madiwani, usimamizi wa miradi ya maendeleo na masuala mengine ya kiutendaji yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Kwa upande wao, baadhi ya Madiwani wameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatawasaidia kuboresha utendaji wa kazi na kuongeza tija katika kuwatumikia wananchi.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu yakiwa na lengo la kuwajengea Madiwani uwezo wa kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Photos from Halmashauri ya Mji Kasulu 's post 25/02/2026

WAKUU WA DIVISHENI HALMASHAURI YA MJI KASULU WAPATIWA MAFUNZO MAALUMU YA MPANGO MKAKATI.

Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wakiwemo Wakuu wa Divisheni wamepatiwa mafunzo maalum ya tathmini ya Mpango Mkakati wa mwaka 2021/2026 pamoja na maandalizi ya Mpango Mkakati mpya wa 2026/2027–2030/2031.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Kasulu yakilenga kuimarisha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuchochea maendeleo kwa kipindi kijacho.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Dk. Bikolimana Muhihi amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo ili kujenga msingi imara wa mpango mpya utakaoakisi mahitaji halisi ya wananchi.

Aidha, washiriki wa mafunzo wamesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwa kuwa wamepata uelewa mpana juu ya mbinu za kisasa za uandaaji wa mpango mkakati na namna bora ya kuweka vipaumbele vitakavyochochea maendeleo endelevu ya Halmashauri ya Mji Kasulu katika miaka ijayo.

Want your business to be the top-listed Government Service in Kasulu?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

475
Kasulu
48500