Tawi La MwembeTayari/CCM

Tawi La MwembeTayari/CCM

Share

KARIBU KATIKA UKURASA RASMI WA TAWI LA MWEMBE TAYARI, KATA YA MKUZA| WILAYA KIBAHA MJINI| MKOA PWANI

25/03/2026

TAARIFA KWA UMMA

23/03/2026

SAVE THE DATE.. ZOEZI LA KUPATA KITAMBULISHO/NAMBA YA NIDA SASA LIMEREJEA KWENYE KATA YAKO MANISPAA YA KIBAHA. PONGEZI ZIMFIKIE MKUU WA WILAYA NICKSON SAIMON (NIKI WA PILI) KWA KUHAKIKISHA SERIKALI YA DR SAMIA SULUHU HASSAN INAENDELEA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA UKARIBU ZAIDI

30/01/2026

πŸ”₯ KIBAHA MJINI πŸ”₯
πŸ’ͺ🏾 VIJANA TUNASONGA MBELE!

Kesho Jumamosi tarehe 31/01/2026, tunafikia KILELE CHA MBIO ZA BENDERA

πŸ“ Viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini

Ni siku ya umoja, mshik**ano na uthibitisho wa nguvu ya vijana ndani ya Chama chetu.

Vijana wa CCM tuko tayari kulinda misingi ya taifa na kusukuma mbele maendeleo πŸ‡ΉπŸ‡ΏβœŠπŸΎ

πŸ“‘ Tukio litarushwa LIVE kupitia:
πŸ”΄ Facebook
πŸ”΄ Instagram

πŸ—£β€œTUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU” πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
πŸ“£ Karibuni nyote – vijana, wanachama na wananchi!
CCM OYEE! VIJANA OYEE!

13/01/2026

MBIO ZA BENDERA – MIAKA 49 YA CCM πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

UVCCM Kibaha Mjini, chini ya uongozi thabiti wa Mwenyekiti wa Vijana Ndugu Ramadhani Kazembe, wanakuletea Mbio za Bendera zenye lengo kubwa na la kizalendo πŸ’ͺ🏾

Ni mbio za hamasa, umoja na mshik**ano, zikibeba ujumbe mzito wa:
βœ… Kutangaza na kuelimisha utekelezaji wa Ilani ya CCM
βœ… Kuhamasisha ushiriki wa vijana, wakina mama na wananchi wa rika lote
βœ… Kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi – chama cha ushindi, amani na maendeleo πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Mbio hizi si za kasi pekee, bali ni mbio za fikra, mshik**ano na uzalendo, zikilenga kuwakutanisha wananchi wote bila kujali umri wala jinsia, kushiriki kwa pamoja katika kujenga uelewa, moyo wa kujitolea na uzalendo kwa Taifa na Chama.
πŸ”₯πŸ™‹β€β™‚οΈ Vijana jitokezeni kuonesha nguvu na ari ya kizazi cha sasa
πŸ‘©Wakina Mama mshiriki k**a nguzo muhimu ya jamii
πŸ‘΄πŸ½πŸ§’πŸΎ Wazee na watoto – mkaribishwa kushuhudia na kushiriki shamrashamra
Kauli mbiu yetu: β€œKULINDA NA KUJENGA UJAMAA”





πŸ‘‰ CCM ni Historia, CCM ni Leo, CCM ni Kesho
Usikose kushiriki – Coming Soon!

23/12/2025

Mwalimu Mwajuma AMIR Nyamka, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini, anawatakia wana-CCM wote heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wenye baraka tele.
Tunawahimiza kuendelea kusherehekea sikukuu hizi kwa amani, upendo na mshik**ano wa dhati, tukidumisha maadili ya utu, heshima na umoja ambayo yameijenga CCM na Taifa letu kwa ujumla. Tuutumie Mwaka Mpya k**a fursa ya kuimarisha mshik**ano wetu, kuongeza bidii katika kuwatumikia wananchi, na kuendeleza mapambano ya maendeleo, haki na ustawi wa jamii. Umoja wetu ni nguvu yetu, tushik**ane, tushirikiane na kulinda amani ya nchi yetu kwa vitendo na maneno.



Photos from Tawi La MwembeTayari/CCM's post 19/12/2025

TAARIFA KWA UMMA

Kuhusu Ushiriki wa Meya Dkt. Nicas Mawazo katika Kikao cha Kazi cha Mkuu wa Mkoa na Ziara za Kimaendeleo

Meya wa Jiji, Dkt. Nicas Mawazo, ameshiriki katika kikao cha kazi kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa, kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika kikao hicho, Meya alieleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya jiji, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali ya Mkoa, Halmashauri na taasisi nyingine za umma ili kuhakikisha malengo ya Rais yanafikiwa kwa ufanisi.

Aidha, Meya alikutana na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ajili ya kujadili hali ya miundombinu ya barabara, hususan utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara, pamoja na mikakati ya kuboresha usafiri kwa wananchi.

Katika kuendelea na majukumu yake, Dkt. Mawazo alifanya ziara katika kituo cha afya kilichopo mkoani, ambapo alipata fursa ya kujionea maendeleo ya huduma za afya, miundombinu iliyopo, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya. Meya alisisitiza umuhimu wa kuboresha huduma za afya ili kuendana na mahitaji ya wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.

Meya alihitimisha kwa kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote wa maendeleo kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta tija kwa wananchi na kuendana na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita.

08/12/2025

TAARIFA MUHIMU KWA GEN Z UPATO UJUMBE HUU MWAMBIE NA MWENZIO

06/12/2025

SHUKRANI SHUKRANI πŸ™

MIMI SARAH PETER ULED
KWA UNYENYEKEVU MKUBWA NAOMBA NITOE SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA CHAMA CHANGU CHA MAPINDUZI KWA KUNILEA NA KUNITEUA NIKAWA MGOMBEA NA BADAE KUCHAGULIWA KWA KURA NYINGI KATIKA NAFASI YA UDIWANI VITI MAALUM TARAFA YA KONGOWE.

DUA SALA NA BARAKA ZENU NDUGU ZANGU NDO ZIMEFANYA MPAKA SIKU YA TAREHE 4/12/2025 TULIAPISHWA MADIWANI WOTE WA MANISPAA YA KIBAHA NA KUPATA KIBALI CHA KUANZA KAZI RASMIπŸ™

NIWAOMBE NDUGU ZANGU TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUENDESHA GURUDUMU LA MAENDELEO KATIKA KATA ZETU TUNATAMBUA IMANI YENU KWETU NA SISI TUNAWAAHIDI HATUTAWANGUSHA

TUISHI KWA UMOJA UPENDO NA MSHIKAMANO HILI TUWATUMIKIE WANANCHI KWA MOYO WETU WOTE

SINA NENO KUBWA LA KUSEMA ZAIDI YA KUSEMA ASANTENI SANA TUKO PAMOJA KATIKA KUZIJENGA KATA ZETU NA MANISPAA YETU KWA UJUMLA

WENU KATIKA UTUMISHI
SARAH P. ULEDπŸ™

02/12/2025

TAARIFA KWA UMMA TOKA OFISI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIBAHA

πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Photos from Tawi La MwembeTayari/CCM's post 01/12/2025

HONGERENI SANA KWA KUAMINIWA

Want your business to be the top-listed Government Service in Kibaha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

MBELA Road
Kibaha

Opening Hours

Monday 11:00 - 20:00
Wednesday 11:00 - 20:00
Friday 11:00 - 20:00
Sunday 11:00 - 20:00