ACT Mkoa wa Mwambao

ACT Mkoa wa Mwambao

Share

official page ya ACT-WAZALENDO Mkoa wa Mwambao

06/05/2025

Mwenyezi Mungu ameijaalia ardhi ya Pwani Mama Mwenye hekma, Elimu na maono mapama . Mpanbanaji , fikra zake wakati wote anaiwaza Pwani yake na Mafia yake. Leo imekuwa siku ya kumbukumbu muhimu ya kuzaliwa kwa Mama yetu Mama wa ACT Mkoa wa Mwambao Riziki Shahari Kila la hera Allah akupe afya njema kwa ajili ya kuwapambania watu wako. Happy Birthday Mama

01/05/2025

Rufiji ilipita miaka mingi tangu alipozaliwa Bibi T**i sasa mpaka kuzaliwa mwamba mwingine k**a yeye ni . Kila la heri mlezi wa Mkoa wa Mwambao Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kikuu cha upinzani Tanzania

18/03/2025

Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo inaupa pongezi Mkoa wa Kichama wa Mwambao kwa kuwa kinara kwenye maandalizi ya hatua za awali za uchaguzi wa Serikali za mitaa wa tarehe 27 Novemba 2024.

Halmashauri Kuu ya ACT imesema kuwa Mkoa wa Mwambao umeweza kuwa kwenye mikoa mitano bora nchini kwa kufikia asilimia 78 ya wagombea kwa kuwa na wagombea 190 kati ya wagombea 250 katika vijiji na mitaa ya mkoa huo.

16/03/2025

Viongozi wa wamesema, Rais wa Angola Joao Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola hatoshi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kwa kushindwa kuheshimu Diplomasia na Demokrasia nchi kwake na kwamba hataweza kusimamia misingi hiyo kwenye nyingine.

13/03/2025

Msafara wa Viongozi wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Dorothy Semu na Mwenyekiti wa Chama Ndugu Othman Masoud Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar umezuiwa kuingia nchini Angola na mamlaka za Serikali ya Angola.
Taarifa ya Katibu wa Mambo ya Nje ya chama hicho, Mwanaisha Mndeme iliyotumwa kwenye vyombo vya habari jioni hii inasema kuwa viongozi hao wanashikiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda na hati zao za kusafiria zinashikiliwa.

Serikali ya Angola, bila kueleza sababu yoyote imetoa amri ya viongozi hao kurejesha Tanzania kupitia Ethiopia.

Viongozi hao waliwasili Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Brenthrust Foundation yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 13-16 Machi 2025.

Mbali na viongozi wa ACT Wazalendo, viongozi wengine zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali Afrika ambao pia walikuwa wanahudhuria Mkutano huo wamezuiliwa na Serikali ya Angola.

Moja ya viongozi waandamizi waliotarajiwa kushiriki kwenye Mkutano huo ni pamoja na Marais Wastaafu Ian Khama (Botswana) na Andres Pastrana Arango (Columbia). Wengine ni Waziri wa Kilimo wa Afrika ya Kusini na Kiongozi wa Chama cha DA Ndugu John Steenhuisen na
Kiongozi wa Chama cha PODEMOS cha nchini MsumbijiNdugu Venancio Mondlane.

Kwenye taarifa ya Mndeme inasema kuwa chama hicho

ACT Wazalendo imesema kuwa chama hicho kinalaani kwa nguvu kitendo cha udhalilishaji kilichofanyika dhidi ya viongozi wetu na viongozi wengine kwa kuzuiliwa na kushikiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Luanda.

"Tunamtaka Balozi wa Angola nchini Tanzania kutoa maelezo ni kwa sababu gani viongozi wetu akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wamezuiliwa na kunyang'anywa hati zao za kusafiriria" imeeleza taarifa hiyo.

ACT imeitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imuite na kumhoji Balozi wa Angola nchini juu ya kadhia hii.

Taarifa ya Mndeme inasema kuwa chama hicho kinatoa wito kwa serikali ya Angola kuziachia mara moja hati za kusafiria za viongozi wetu walizoshikilia na kuwaruhusu kuendelea na ratiba yao nchini Angola.

*Mwisho*

12/03/2025

Nchi hii si ya Mama yake mtu nchi ni ya Watanzania wote lazima hilo tulioneshe kwa vitendo , tusilichukulie hili kuwa ni siasa tuchukulie hili ni uchumi kwa sababu uchaguzi ndio Mama wa uwajibikaji , leo unasikia Mama katuletea Mama yenu huyu kazipata wapi, yeye ndio tumempa ardhi yote ya nchi hii , migodi yote ya nchi hii sasa mnataka tusimwajibishe tusipomwajibisha nchii itakuwa na ufisadi , na ufisadi tunaouona Leo hii kwa sababu hakuna uwajibishaji" Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman

12/03/2025

Leo tarehe 12 Machi 2025, Wakili wa ACT-WAZALENDO Mwanaisha Mndeme, amewawakilisha wagombea wa chama hicho katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kijiji cha Tambani wilayani Mkuranga.

11/03/2025

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kuwa kimesitisha ushiriki wake kwenye vikao vya Baraza la Vyama vya Siasa kwa sababu ya kushindwa kushughulikia changamoto za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na maboresho ya mfumo wa uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025.

08/03/2025

"Wengi tulidhani Rais Mwanamke angetupa kipaombele wanawake Miaka minne ya Rais Samia imekuwa ya kuendelea kupuuzwa kwa madai ya wanawake. Rais Samia ametusaliti wanawake wenzake .Wanawake wanakufa kwa kukosa fedha za kugharamia matibabu. Wanawake wanapoteza maisha kwa kukosa gharama za huduma za uzazi na njaa." Dorothy Semu kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo.

07/03/2025

Leo tarehe 7 Machi Wakili amewawakilisha waliokuwa wagombea wa uchaguzi wa serikali ya kijiji cha Mchungu,Kata ya Mwambao, Wilaya ya Kibiti kupitia chama cha ACT Wazalendo kwenye shauri la uchaguzi lililofunguliwa Mahak**a ya Wilaya Kibiti,Mkoa wa Pwani.

Shauri hilo la uchaguzi ambalo leo limetajwa kwa ajili ya kusikilizwa limefunguliwa kupinga matokeo na mwenendo wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Wakili Mwanaisha aliambatana na Viongozi wengine wa ACT akiwemo Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Mwambao , Mlezi wa Jimbo la Kibiti na Mwenyekiti wa Jimbo la Kibiti Mzee Mketo.

01/03/2025

Kila la kheri.

01/03/2025

Heri ya kuzaliwa Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa ACT-WAZALENDO - Mkoa wetu ndugu Hawa Mwangia .

Want your business to be the top-listed Government Service in Kibiti?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address

Jaribu Mpakani
Kibiti