Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Government Organization, P. O. BOX 44, Kigoma.

10/01/2023

Wanafunzi wa Kidato Shule ya Sekondari Gungu ilipokea kiasi cha Million 220, kwa Ujenzi wa Vyumba 11, Angalia Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza Walivyoishukuru Serikali kwa Miundombinu iliyopo Msemaji Mkuu wa Serikali Ikulu Mawasiliano Ofisi ya Rais - Tamisemi

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 05/01/2023

UPASUAJI WA KWANZA KITUO CHA AFYA CHA GUNGU MANISPAA YA KIGOMA/UJIJI WAFANYIKA

Posted On: January 5th, 2023
Na Mwandishi Wetu
Upasuaji wa kwanza kwa Mama mjamzito katika kituo cha afya cha Gungu umefanyika Leo January 5, 2023 Mara baada ya uzinduzi wa kuanza kwa huduma hiyo

Upasuaji huo umeanza Mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. kuzindua kuanza rasmi kwa huduma hiyo ya Upasuaji katika kituo hicho cha Afya cha Gungu

Akizindua huduma hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza na kushukuru Serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuboresha huduma za afya katika Wilaya hiyo ikiwemo uboreshaji wa huduma na Ujenzi wa Majengo katika Kituo cha afya kipya cha Buhanda na uboreshaji wa huduma kituo cha afya cha Ujiji

Aidha amewataka Watumishi wa Afya kufanya kazi kwa weredi na kuonesha upendo kwa Wagonjwa wanaofika kupata huduma ya matibabu katika kituo hicho wakiwemo Wajawazito watakaokuwa wakipata huduma ya upasuaji mara baada ya uchungu pingamizi katika kipindi cha kujifungua

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. imefanikisha Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara, Jengo la kufulia, jengo la wodi ya Wazazi na Upasuaji katika kituo hicho cha afya cha Gungu kwa gharama ya fedha za Kitanzania Millioni Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya Upasuaji pamoja na vifaa vya uhifadhi damu salama

Amesema Serikali imeendelea kufanya uboreshaji wa huduma katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuongeza damu kutokana na uwepo wa vifaa vya utunzaji damu salama
Amesema kupatikana kwa huduma hizo kutaondoa utoaji rufaa kwa Wagonjwa kuelekea katika hospitali ya Babtisti na Hospitali ya rufaa ya Maweni kupata huduma ya Upasuaji pamoja na kuongezewa damu

Nao baadhi ya Wananchi Waliohudhuria katika ufunguzi huo akiwemo Samsoni Nathani na Bi. Grace Nashoni wameipongeza Serikali kwa jitihada za uboreshaji na upatikanaji wa huduma bora za afya huku wakisema huduma hizo utahakikisha Usalama wa maisha ya Mama na Mtoto pindi Mjamzito anapojifungua

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 24/12/2022

WATAALAMU WAAHIDI KUSIMAMIA KIKAMILIFU MRADI MPYA WA BOOST

Posted On: December 24th, 2022
Na Mwandishi Wetu
Wataalamu wa Halmashauri na Mikoa ya Kigoma na Kagera wameahidi kutekeleza mradi wa BOOST kikamilifu Ili kuleta ufanisi na matokeo yaliyokusudiwa

Wameyasema hayo Mapema Jana Desemba 23, 2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili (02) yaliyokuwa na lengo la kuzijengea timu za utekelezaji wa mradi huo wa BOOST

Akizungumza katika katika mafunzo hayo kwa niaba ya Wahandisi wengine Mhandisi wa Ujenzi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Joel Shirima alisema katika Mradi wa BOOST ambao utahusisha Ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa watahakikisha wanasimamia kikamilifu katika kutoa Ushauri wa Kitaalamu na Kiutendaji

Naye Afisa Mipango, Uchumi na Mipango kutoka Halmashauri ya Biharamuro Mkoani Kagera Ndugu. Jasphone issanzu Mkurugu alisema Halmashauri zipo tayari katika kupanga bajeti za utekelezaji kikamilifu kwa kushirikiana na idara mbalimbali na kuhusisha mapato ya Ndani na ushirikishaji wa Jamii

Awali akihutubia washiriki hao kabla ya kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma Bi. Paulina NdigezĂ  aliwataka Wataalamu hao kutekeleza kikamilifu afua mbalimbali zilizofundishwa

Mradi wa BOOST unatarajiwa kutekelezwa kwa mda wa miaka mitano (05) kwa Mwaka 2021/2022 hadi Mwaka 2025/2026 kwa fedha za Kitanzania Trillion 1. 15 sawa na Dola za Kimarekani Million Mia tano (500)

Katika fedha hizo Dola za Kimarekani Million 480 zitatumika katika program ya lipa kulingana na matokeo na Dola za Kimarekani Million 20 ni gharama za utekelezaji wa uwekezaji wa miradi

Jumla ya vyumba vya Madarasa 12, 0000 vinatarajia kujengwa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya Tehama kwenye Shule zaidi ya mia nane (800) za Msingi na Vituo vya Walimu, na uandaaji wa vifaa vya kufundishia na Kujifunzia kwa elimu ya awali

Wataalamu Waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa elimu, Walimu wakuu, Waratibu elimu Kata, Wahandisi, Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Wahasibu, Maafisa mipango na Uchumi, Maafisa Manunuzi, Wadhibiti ubora wa elimu pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 22/12/2022

Baadhi ya Washiriki waliohudhuria mafunzo ya siku mbili (02) ya mradi mpya wa BOOST yaliyoanza leo Desemba 22, 2022 yakihusisha Wataalamu mbalimbali kutoka ngazi za Mkoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Kigoma na Kagera katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu kwa lengo la kuzijengea timu za utekelezaji wa mradi huo

Wataalamu hao Waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa elimu, Walimu wakuu, Waratibu elimu Kata, Wahandisi, Maafisa Maendeleo ya jamii, Wahasibu, Maafisa mipango na Uchumi, Maafisa Manunuzi, Wadhibiti ubora wa elimu pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 22/12/2022

NAMNA MRADI WA BOOST UTAKAVYOINUFAISHA JAMII KATIKA MASUALA YA ELIMU NCHINI

Posted On: December 22nd, 2022
Na Mwandishi Wetu
Wataalamu mbalimbali kutoka ngazi za Mkoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Kigoma na Kagera Leo Desemba 22, 2022 Wamekutana katika mafunzo ya siku mbili (02) katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu kwa lengo la kuzijengea timu za utekelezaji wa mradi mpya wa BOOST

Wataalamu hao Waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa elimu, Walimu wakuu, Waratibu elimu Kata, Wahandisi, Maafisa Maendeleo ya jamii, Wahasibu, Maafisa mipango na Uchumi, Maafisa Manunuzi, Wadhibiti ubora wa elimu pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini

Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma Bi. Paulina NdigezĂ  akihutubia Washiriki wa mafunzo hayo amewataka kuzingatia mafunzo hayo kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi

Awali Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka OR-TAMISEMI Ndugu. George Jackson Mbijima amesema mradi wa BOOST unatarajiwa kutekelezwa kwa mda wa miaka mitano (05) kwa Mwaka 2021/2022 hadi Mwaka 2025/2026 kwa fedha za Kitanzania Trillion 1. 15 sawa na Dora za Kimarekani Million Mia tano

Amesema katika fedha hizo Dola za Kimarekani Million 480 zitatumika katika program ya lipa kulingana na matokeo na Dola za Kimarekani Million 20 ni gharama za utekelezaji wa uwekezaji wa miradi

Ameendelea kusema katika Mradi huo jumla ya vyumba vya Madarasa 12, 0000 vinatarajia kujengwa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya Tehama kwenye Shule zaidi ya mia nane (800) za Msingi na Vituo vya Walimu, na uandaaji wa vifaa vya kufundishia na Kujifunzia kwa elimu ya awali

Aidha malengo mengine ya mradi ni kuongeza uandikishaji wa elimu ya awali kutoka 76.9% mwaka 2021 hadi zaidi ya 85%, mafunzo endelevu ya Walimu kazini (MEWAKA), na Halmashauri kusimamia utawala bora katika elimu kwa kuzingatia miongozo na usimamizi wa Shule

Amehitimisha kwa kusema Shule za Msingi 6,000 zitateleleza mradi wa programu ya Shule ya Msingi Salama na kufanya Wanafunzi 50% wa darasa la pili kufikia kiwango cha chini cha kumudu stadi za Kusoma na kuandika na 35% katika kuhesabu

Mradi wa BOOST tayari Umeanza kutekelezwa Nchini Tanzania kwa Mikoa ya Tanzania bara kwa kutoa mafunzo mbalimbali na utambulishaji wa mradi na unatarajia kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu Ofisi ya Rais - Tamisemi Msemaji Mkuu wa Serikali Ikulu Mawasiliano

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 21/12/2022

CCM WILAYA YA KIGOMA YARIDHISHWA NA UJENZI WA VYUMBA MADARASA KIGOMA/UJIJI

Posted On: December 21st, 2022
Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Jana Desemba 20, 2022 walifanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 57 unaoendelea Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya chama hicho

Katika ziara hiyo Viongozi na Wajumbe wa Kamati hiyo waliridhishwa na ujenzi huku wakipongeza usimamizi wa Wataalamu chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo

Manispaa hiyo ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion moja na milion mia moja arobaini na Sita (Tsh 1, 146, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ujenzi wa vyumba hivyo vya Madarasa ikiwa ni maandalizi na mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa Mwaka 2023

Akizungumza Katika ziara hiyo Katibu wa itikadi uenezi wa CCM Wilaya ya Kigoma Ndugu. Haruna Kambiro aliwapongeza Wataalamu wa Manispaa hiyo kwa Usimamizi wa ujenzi wa Madarasa kwa Shule kumi na sita (16) huku akiwataka kuendelea kukamilisha ili kuwanufaisha wanafunzi pindi Shule zitakapofunguliwa

Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Shabani Ng'enda alisema ujenzi wa miundombinu hiyo unaendelea kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya Madarasa katika Manispaa hiyo na kufanya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya upili kuanza kwa wakati mmoja

Mjumbe wa Kamati hiyo na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe aliwataka Wananchi kuitunza Miundombinu hiyo kwa kutoruhusu uhalibifu wowote huku akiwataka Wazazi kuhakikisha kila Mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na masomo ya upili anaripoti kwa wakati

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila alisema ujenzi wa vyumba vya Madarasa unaendelea kukamilishwa katika hatua za mwisho ili kuanza kutumika mapema mwezi Januari 2023

Alihitimisha kwa kusema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali na inatarajia kuleta fedha zingine za Maendeleo katika Ujenzi wa Miundombinu ya vyumba vya Madarasa kwa Shule za Msingi kupitia mradi wa Boost

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 14/12/2022

"WALIMU ZINGATIENI MAFUNZO " Bi. PANGANI MRATIBU MSAIDIZI WA MRADI WA SHULE BORA

Posted On: December 14th, 2022
Na Mwandishi Wetu
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Shule Bora OR- TAMISEMI Bi. Adelaida Pangani amewataka walimu kuzingatia mafunzo yenye lengo la kuinua ubora wa elimu Nchini

Aliyasema hayo Jana Desemba 13, 2022 katika Mafunzo ya siku mbili (02) ya Walimu Kazini (MEWAKA) yanayoendelea katika Shule ya Msingi Kigoma yakihusisha Watendaji Kata, Waratibu Elimu Kata, Walimu Wakuu, Walimu Wataaluma na Walimu Mahili wa Shule za Msingi zilizopo Kata za Kigoma na Bangwe

Alisema lengo la Mafunzo hayo ni kuwawezesha Walimu kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza za mfano zinazopatikana miongoni mwao ili kutatatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji ili kuinua ubora wa elimu nchini

Aliwataka Wasimamizi wa elimu ngazi za Kata kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa kuwashirikisha Wazazi na wadau mbalimbali wa elimu katika kukuza elimu Nchini

Mradi wa Shule bora umelenga kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa Wanafunzi wote wa k**e na wa kiume katika Shule za Serikali za Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid , gharama za mradi zikiwa ni Shilingi za Kitanzania bilion 271 na utafanya katika ngazi zote za mradi katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Tanga na Pwani ambapo utafikia kikomo mwaka 2027

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 12/12/2022

MAFUNZO YA WALIMU NA WASIMAMIZI WA ELIMU MRADI WA SHULE BORA

Posted On: December 12th, 2022
Na Mwandishi Wetu
Walimu na wasimamizi wa elimu ngazi ya kata jana Desemba 11, 2022 walihitimisha mafunzo ya siku mbili (2) yaliyokuwa na lengo la kuwawezesha walimu kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza za mfano zinazopatikana miongoni mwao ili kutatatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji ili kuinua ubora wa elimu nchini

Mafunzo hayo yaliendeshwa katika taasisi ya Ahlulbayt Islamic Centre yakihusisha Watendaji Kata, Waratibu Elimu Kata, Walimu Wakuu, na Walimu Wataaluma wa Shule za Msingi zilizopo Kata za Majengo, Kipampa, Businde na Rusimbi

Katika mafunzo hayo Watendaji kata walijadiliana na Walimu namna bora ya Ukuzaji elimu na ufaulu kwa kushirikisha Wazazi na Wadau wengine wa elimu katika maeneo yao

Aidha katika mafunzo hayo walijifunza namna kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza kwa mfano kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji

Mkufunzi na Mkuza mitaala kutoka taasisi ya elimu Tanzania Ndugu. Hwago Hassan Hwago alisema kutumia hadithi za mafanikio katika kufundisha na kujifunza zitamfanya mwanafunzi kuwa mbunifu ambapo atakuwa na uwezo wa kuibua tatizo, Ufumbuzi wa tatizo na kupata matokeo yaliyo bora

Mafunzo haya ya mradi wa Shule bora yanaendelea katika Halmashauri za Mikoa ya Kigoma, Singida, Katavi na Pwani kwa lengo la kukuza viwango vya elimu katika Mikoa hiyo yakiandaliwa na Mradi wa Shule unaofadhiliwa na mfuko wa Uk aids chini ya Usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 05/12/2022

Walimu na wasimamizi wa elimu Kata ya Mwanga Kusini na Kata ya Mwanga Kaskazini leo Desemba 05, 2022 wamehitimisha mafunzo kwa Walimu waliopo kazini (MEWAKA) baada ya Mafunzo hayo kuanza Jana Desemba 04, 2022

Mafunzo hayo yamehitimishwa katika Shule ya Msingi Muungano yalipokuwa yakifanyikia na yakiandaliwa na Mradi wa Shule unaofadhiliwa na mfuko wa Uk aids chini ya Usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 04/12/2022

MAFUNZO YA SHULE BORA KWA WASIMAMIZI WA ELIMU NA WALIMU KAZINI KIGOMA/UJIJI

Posted On: December 4th, 2022
Na Mwandishi Wetu
Walimu na wasimamizi wa elimu ngazi ya kata wametakiwa kuibua hadithi za mfanikio za kujifunza kwa mfano kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa Wanafunzi katika mafunzo ya Siku mbili (02) yaliyoanza Leo Desemba 04, 2022 katika Shule ya Msingi Muungano

Ameyasema hayo Mkuza mitaala kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Ndugu. Hwago Hassan Hwago alipokuwa akitoa mafunzo kwa Walimu waliopo kazini (MEWAKA) yakihusisha Wasimamizi wa elimu ngazi ya kata na Walimu wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Mwanga Kusini na Kata ya Mwanga Kaskazini

Amesema hadithi za mafanikio ya kujifunza kwa mfano zinasaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji, kutia moyo katika utendaji kazi, kuamsha ari ya kutenda kazi, na kukuza ushirikiano miongoni mwa wadau wa elimu

Amesema hadithi za mafanikio za kujifunza kwa mfano zinapatikana miongoni mwa Walimu, Jamii, Taasisi za Elimu, Viongozi wa dini, Wanasiasa na Wadau wote wa elimu

Mafunzo hayo yameandaliwa na Mradi wa Shule unaofadhiliwa na mfuko wa Uk aids chini ya Usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Miradi wa Shule bora unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) Nchini Tanzania ukihusisha Halmashauri sitini na saba (67) na Shule elfu tano mia saba hamsini na saba ( 5, 757) na Unatarajia kuwanufaisha Wanafunzi zaidi ya Milioni tatu na laki nane ( 3, 800,000) na Walimu zaidi ya elfu hamsini na nne ( 54, 000)

Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 03/12/2022

WIKI YA MAADHIMISHO MIAKA 61 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAMEENDELEA KWA UPANDAJI MICHIKICHI KIGOMA/UJIJI

Posted On: December 3rd, 2022
Na Mwandishi Wetu
Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Desemba 3, 2022 wameendelea na maazimisho ya wiki ya Sherehe ya Miaka sitini na Moja (61) tangu Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika ilipojipatia Uhuru wake Desemba 9, 1961

Maadhimisho hayo yameendelea kwa Wananchi, Viongozi na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kasimbu iliyopo katika Manispaa hiyo kushiriki zoezi la upandaji wa zao la Mchikichi

Akizungumza katika tukio hilo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Idrisa Naumanga amewataka Wakazi wa Manispaa hiyo kuendelea na zoezi la upandaji wa miche ya kisasa ya zao hilo kutokana na uzalishaji wa mafuta ya Mawese kuwa mengi pamoja na malighafi zingine

Ameendelea kuwataka Wananchi kuendelea kuitunza na kuithamini miche hiyo iliyopandwa katika Shule ya Sekondari ikiwa ni alama ya kusherehekea miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika

Kaimu Mkurugenzi huyo ameiagiza idara ya Misitu na Mazingira kupandwa kwa miti mingine ya Matunda na kivuli katika Shule hiyo

Wakizungumza katika tukio hilo baadhi ya Wanafunzi wa Shule hiyo Ndugu. Ismail Samweli na Mashuma Swalehe wameipongeza Serikali kwa maadhimisho ya wiki ya Uhuru ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara huku wakisema mazao waliyopanda itakuwa ukumbusho huku wakiahidi kuilinda na kuitunza

Katika Shule hiyo zaidi ya Miche hamsini (50) ya Miche ya Kisasa ya zao la michikichi imepandwa na Wananchi, Walimu, Wanafunzi na Viongozi mbalimbali wa Kata na Mitaa walihudhuria maadhimisho hayo

Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika kwa sasa inafahamika kwa jina la Tanzania kutokana na Muungano wake na Zanzibar mwaka 1964 na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".

Photos from Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji 's post 02/12/2022

Picha Mbalimbali za Wananchi na Wafanyabiashara wa Soko la Buzebazeba walipojitokeza Leo Desemba 02, 2022 katika ufanyaji Usafi katika Soko la Buzebazeba katika wiki ya maadhimisho ya Sherehe ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara

katika kuadhimisha maadhimisho hayo Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".

Want your business to be the top-listed Government Service in Kigoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

P. O. BOX 44
Kigoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00