Nyang'hwaledc Online

Nyang'hwaledc Online

Share

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale - GEITA

29/05/2026
29/05/2026

29/05/2026

Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri jana Mei 28, 2026, wamepatiwa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, afya ya akili pamoja na maambukizi ya VVU katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha afya za watumishi ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.

Elimu hiyo iliyotolewa na wataalamu wa afya ilijikita katika uelewa wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la damu (presha), kisukari, magonjwa ya kifua, selimundu, saratani na changamoto za afya ya akili.

Wataalamu hao wamesisitiza umuhimu wa kuboresha mitindo ya maisha kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kula lishe bora, kupunguza matumizi ya pombe na tumbaku pamoja na kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kutambua hali zao mapema.

Aidha, washiriki wameelimishwa kuhusu visababishi vya maambukizi ya VVU, njia za kujikinga pamoja na umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara.

Pia, wajumbe wamepata mafunzo ya namna ya kutumia vifaa vya kujipima VVU wenyewe majumbani (self-test), huku vipimo hivyo vikigawiwa kwa watumishi walioonyesha uhitaji.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Ndg. Ezekiel Ntiriyo amewataka watumishi kuweka kipaumbele katika kulinda afya zao, akieleza kuwa mtumishi mwenye afya njema ana uwezo mkubwa wa kutoa huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi kwa wananchi.

“Afya ya mtumishi ni msingi wa utendaji kazi wenye tija. Ni muhimu kila mmoja kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa ili kuendelea kulitumikia taifa kwa ufanisi,” amesisitiza.

26/05/2026

Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma kwa kutekeleza ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, ambapo hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 85 ya utekelezaji.

Mradi huo unalenga kuhakikisha viongozi wa Serikali wanakaa karibu na vituo vya kazi ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi, sambamba na kupunguza changamoto zinazoweza kuathiri utendaji wa majukumu ya kila siku.

Ujenzi wa nyumba hiyo unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma kwa kuwapatia makazi yaliyo karibu na maeneo ya huduma.

Kukamilika kwa nyumba hiyo kutamuwezesha Mkurugenzi Mtendaji kuishi karibu na kituo chake cha kazi, jambo litakalorahisisha uratibu wa shughuli za maendeleo na kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi wakati wote.

Aidha, mradi huo unatarajiwa kusaidia Serikali kupunguza gharama zinazotumika katika upangishaji wa nyumba kwa viongozi pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa viongozi wa Serikali wanapotekeleza majukumu yao.

Wananchi wa Wilaya ya Nyang’hwale wanatarajiwa kunufaika zaidi kupitia ongezeko la ufanisi wa utendaji wa viongozi na huduma bora zitakazotolewa kutokana na uwepo wa mazingira rafiki ya kazi na makazi kwa watumishi wa umma.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwekeza katika miundombinu muhimu ya kiutumishi kwa lengo la kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na maendeleo ya huduma kwa wananchi.

25/05/2026

Jiandae kufuatilia toleo maalum la JARIDA LA MIRADI YA CSR MWAKA 2025 litakalokujia hivi karibuni. Ndani ya jarida hilo utafahamu miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale kwa kushirikiana na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia CSR kwa mwaka 2025, Jumla ya fedha zilizotumika, faida za miradi hiyo kwenye jamii, na Mengine mengi.

Kaa tayari🔥🔥🔥

25/05/2026

Wananchi mnakaribishwa kwenye kliniki ya huduma za Macho na Meno zitakazotolewa katika Zahanati na Kijiji cha Busolwa Mei 26, 2026 kuanzia Saa mbili kamili Asubuhi.

24/05/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Ndg. Husna Toni jana Mei 23, 2026 amefanya ukaguzi wa maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi ametembelea maeneo mbalimbali ya miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa lengo la kujionea hatua za utekelezaji pamoja na hali ya maandalizi ya mapokezi ya mbio hizo muhimu kitaifa.

Aidha, amewataka wataalamu na watendaji kuhakikisha mazingira ya miradi yanaendelea kuboreshwa na shughuli zote zinazohitajika kukamilishwa kabla ya ujio wa Mwenge wa Uhuru ili kuonesha utendaji na maendeleo ya Halmashauri kwa Wananchi na wageni watakaoshiriki katika tukio hilo.

23/05/2026

Watendaji wa Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale jana Mei 22, 2026 wamemkabidhi zawadi ya Mbuzi Mkurugenzi Mtendaji ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake katika kusimamia maendeleo na kuimarisha ushirikiano mahali pa kazi.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Husna Toni amewashukuru Watendaji hao kwa upendo na mshikamano wao, huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana katika kuhakikisha huduma bora zinawafikia Wananchi.

Want your business to be the top-listed Government Service in Kigoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Pox 352 Nyang'hwale
Kigoma
30201