Hudatz

Hudatz

Share

Maarifa kwa Wote

Photos from Hudatz's post 04/05/2026

HOJA YA KUHALALISHA MIRUNGI YAZUA MJADALA MKALI.
🌠🌠🌠🌠🌠🌠🌠

=================
Kauli ya Mbunge wa Kondoa Mjini (CCM), Mariam Ditopile, ya kutaka kilimo cha mirungi ihalalishwe imeibua upinzani mkali kila kona, huku Ansaar Muslim Youth Centre (AMYC ikiitaja kuwa hatari kwa mustakabali wa taifa.
=================

Mbunge Ditopile alitoa pendekezo hilo Aprili 29, 2026 bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya kilimo, akidai mirungi inaweza kuongeza mapato ya taifa na kuwasaidia wakulima, huku akihoji msingi wa kisheria ulioifanya iwekwe katika kundi la dawa za kulevya.

Hata hivyo, AMYC wamesema hoja hiyo “si tu dhaifu kitaalamu, bali ni hatari kwa mustakabali wa taifa,” wakisisitiza kuwa kuhalalisha mirungi kunapingana moja kwa moja na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2015.

Katika tamko lao refu na la kina kupinga hoja hiyo, AMYC wamesema “kuhalalisha mirungi kutasababisha kudhoofisha mamlaka ya sheria, kudharau juhudi za kitaifa za kupambana na dawa za kulevya, na kufungua mlango wa uhalifu na mmomonyoko wa maadili.”

Kuhusu hoja ya mapato, AMYC wameeleza kuwa ni “upotoshaji mkubwa” kudai mirungi inaweza kuleta maendeleo, wakionya kuwa faida za muda mfupi haziwezi kufidia madhara ya muda mrefu k**a gharama za matibabu ya uraibu, kupungua kwa nguvu kazi, pamoja na kuongezeka kwa umaskini na uhalifu.”

Aidha,wamekumbusha wajibu wa Serikali kulinda ustawi wa wananchi:

“Serikali ina wajibu wa kulinda afya na maadili ya jamii, si kukusanya mapato kwa gharama ya maisha ya wananchi.”

Wameongeza kuwa mirungi “hulewesha akili, husababisha utegemezi na hupunguza tija,” hivyo kuhalalishwa kwake ni “sawa na kuhalalisha uharibifu wa kizazi cha vijana.”

Kwa mtazamo wa kidini, taasisi hiyo imenukuu hadithi ya Mtume (rehema na amani zimshukie): “Kila kinacholewesha ni haramu,” na kufafanua kuwa wanzuoni wameweka wazi kuwa kila kinachoathiri akili, iwe ni kinywaji au kitu kingine, kinaingia katika hukumu hiyo.

AMYC pia wamegusia maslahi ya umma, wakisema: “Maslahi ya jamii yanapaswa kutangulizwa kuliko faida za kifedha,” wakionya kuwa kuhalalisha mirungi ni “kuweka fedha mbele ya utu wa binadamu.”

Katika ngazi ya kimataifa, wameeleza kuwa hatua hiyo inaweza kuiweka Tanzania katika mgongano na mikataba ya kudhibiti dawa za kulevya, na kuharibu taswira ya nchi.

Kwa msimamo wao wa mwisho, AMYC wamesisitiza: “Kuhalalisha mirungi si sera ya maendeleo — ni sera ya maangamizi,” huku wakiiomba Serikali ikatae pendekezo hilo na kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo inaongeza uzito wa mjadala
unaoendelea nchini kuhusu mustakabali wa zao la mirungi na athari zake kwa jamii.

Ukiacha tamko la AMYC, wadau wengi wametoa maoni mitandaoni kupinga vikali maoni ya mbunge huyo, wakiyataja k**a yamepotoka na baadhi wakisema mirungi itaongeza ulevi na kuliingiza taifa katika anguko zaidi la kimaadili.

Mwanamke mmoja, mkazi wa Chanika, anayeishi na mume mtumiaji wa mirungi, ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake litajwe amesema maoni ya mbunge, mwanamke mwenzao, yamemshtua mno.

Akifafanua alisema ndoa yake inatetereka kwa sababu ya ulevi wa mumewe wa mirungi na asingependa wanawake wengine wapitie shida anazopitia.

Alisema ukiacha madhara mengi ya kiafya anayopitia mumewe, uraibu umesababisha pesa zote kuishia kwenye matumizi ya mirungi.

Huko Kenya, wadau nao wametoa maoni wengi wakiisikitikia Tanzania kutamani mirungu ihalalishwe ilhali wao nao wanatamani ingeharamishwa nchini kwao.

Watangazaji wa radio maarufu ya 47 Alex Mwakideu na Captain Emmanuel Mwashumbe katika kipindi chao cha asubuhi wameonya Watanzania kuwa mirungi ina madhara mengi na ni bora iendelee kupigwa marufuku.

=================
CHANZO:
IMAAN: ISSN 5618 - NO. 582 (Mei 4, 2026)
=================




"Maarifa Kwa Wote"

01/05/2026

"Mtoto mwema atakapodumu kumuombea msamaha baba yake, naye atasamehewa na atainuliwa darja ya PEPONI."

Ewe Mwenyezi Mungu tujaalie nasi tuwe miongoni mwao. Aamin.


Photos from Hudatz's post 01/05/2026

KIGOMA FUTA ZIRO
SEMINA YA EDK WILAYA YA UVINZA-ILAGALA
🌠🌠🌠🌠🌠🌠🌠

Semina ya wanafunzi wa KIDATO CHA PILI imefanyika vizuri na muhtasari wa mahudhurio ni k**a ifuatavyo:

✔️Kioo Sec: ME 01, KE 06, JML=07
✔️Ilagala Sec: ME 17, KE 25, JML=42
✔️Mwakizega Sec:ME 06, KE 15, JML=21
✔️Sunuka Sec: ME 08, KE12, JML=20
✔️Kirando Sec: ME 00, KE 04, JML=04.
JUMLA KUU: ME 32, KE 62, JML=94

Mwenyezi Mungu awajaalie Wanafunzi hawa wapate ufaulu mzuri kwenye mitihani yao na wawe vijana wema.



"Maarifa Kwa Wote"

18/02/2026

*MATAIFA AMBAYO MUDA WA KUFUNGA RAMADHANI UTAKUWA MREFU ZAIDI 2026*

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan 2026, unatarajiwa kuaanza Jumanne February 17 na kwa mataifa mengine itakuwa Februari 18.

Kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, ni mojawapo wa nguzo tano ya dini ya kiislamu, na inamlazimu kila muumini wa Kiislamu ambaye ametimiza vigezo kufunga.

Watu hufunga kwa siku 29 au 30 mwezi huo, kuanzia alfajiri hadi jua linapotua.

lakini, muda wa kufunga hutofautiana katika kila taifa, na ndio maana kuna utofauti wa jinsi Ramadhan huadhimishwa kote duniani.

Msimu wa majira ya joto haswa katika mataifa ya Ulaya, wao hushuhudia siku ndefu kabla ya jua kutua, huku mataifa mengine ya bara Afrika yakishuhudia joto kali, suala ambalo huathiri ratiba yao ya kufunga.

SABABU YA TOFAUTI YA MUDA

Ili kuelewa tofauti za ratiba ya Ramadhan, BBC ilizungumza na Simwal Usman Jibril, mwanachama wa k**ati ya wanaotazama mwezi nchini Nigeria, ambaye alielezea kuwa kuna vipengele tofauti ambavyo huzingatiwa.

Alisema kuwa katika maeneo mengine duniani, waumini wa Kiislamu wanaweza kufunga hadi kwa saa 20 kwa siku, ila kuna maeneo mengine ambayo huwezi kufunga zaidi ya saa 10," alielezea katika mahojiano na shirika la BBC idhaa ya Hausa.

MAENEO AMBAYO MSIMU WA KUFUNGA NI MREFU

Simwal Usman Jibril, anaelezea kuwa mfungo wa muda mrefu hushuhudiwa kaskazini mwa Ulaya na maeneo ya Aktiki, ambapo jua huonekana wakati wa jioni msimu wa majira ya joto.

Miongoni mwa miji inayoshuhudia mfungo wa muda mrefu ni:

🌙Tromso-Norway kuanzia saa mbili hadi saa nne usiku,

🌙Reykjavik – Iceland kuanzia saa mbili hadi saa tatu usiku,

🌙Murmansk, Urusi, Stockholm - Uswidi, kuanzia saa kumi na mbili hadi saa moja jioni.

Kulingana na mtaalamu huyu, miji hii itashuhudia mfungo wa muda mrefu 'kwa sababu yako mbali na ikweta, ambapo jua hudumu kwa muda mrefu majira ya joto yakikaribia.'

Anaelezea kuwa msimu wa Ramadhan huja karibu na majira ya joto, kwa hivyo jua huonekana kwa muda mrefu, kwa hivyo kufanya mfungo kuwa wa muda mrefu.

Kulingana naye "Ramadhan hufuata kalenda ya mwezi wa Kiislamu ambayo huwa na siku 10 chache au 11 kila mwaka.

Mwezi wa Ramadhan hubadilika kila mwaka, hii ni kumaanisha muda wa kufunga hubadilika kila mwaka. "

Maneo ambayo mfungo utakuwa mfupi
Mtaalam huyo anaelezea kuwa mataifa yaliyo kusini mwa ikweta yatashuhudia mfungo wa muda mfupi.

Mji hii ni k**a:

🌙Ushuaia – Argentina masaa 11,
🌙Punta Arenas- Chile masaa 11,
🌙Christchurch-New Zealand masaa 11,
🌙Cape Town - Afrika Kusini takriban masaa 12.

Simwal anasema Ramadhan mwaka huu inatarajiwa kuanza mwezi Februari "hii inaendana na majira ya kiangazi kusini mwa ikweta, kipindi ambacho hushuhudia siku fupi.

Aidha maeneo haya huwa karibu na ikweta kwa hivyo hayashuhudii jua kali."

Mazingira ya kufunga nchini Nigeria
Simwal anadai kuwa kuna mataifa yaliyokaribu na ikweta ambapo siku za kuanza mfungo huwa hazibadiliki kila mwaka.

Miji hii ni k**a:
🌙Abuja-Nigeria,
🌙Jakarta-Indonesia,
🌙Kuala Lumpur- Malaysia na
🌙Nairobi Kenya.

Simwal anasema muda wa kufunga katika miji hii ni takriban saa 12 hadi 13.

Hii ni kutokana na miji hii kupokea kiwango sawia cha mwangaza na giza kila mwaka huku kukiwa na utofauti ndogo sana ya muda ambao jua linachomoza na kutua.

Muda wa kufunga huamuliwa vipi?

Simwal anaelezea kuwa vipengele muhimu vinavyozingatiwa kuamua muda wa kufunga ni:

🌙Ikweta,
🌙Hali ya hewa,
🌙Maeneo ya kaskazini na kusini mwa dunia na
🌙Kalenda ya kila mwezi ya Kiislamu.

"Ingawa muda wa kufunga hutofautiana, Ramadhan ni mwezi ambao waumini wa Kiislamu kote duniani huimarisha ibada kwa kufunga na kuomba."

NANI ANAPASWA KUFUNGA?

Yeyote anayekidhi vigezo vifuatavyo ni lazima afunge:

1. Aliyebalehe kufikia wastani wa umri wa balehe wa miaka kumi na nne na nusu katika kalenda ya Gregorian).

2. Mwenye akili timamu - mtu yeyote anayesumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ama huwafanya wasijue kufunga, au wasiweze kuelewa wazo la kufunga (k**a vile wale wanaosumbuliwa na Down Syndrome) hawatalazimika kufunga.

3. Ikiwa si mgonjwa na mwenye magonjwa sugu ambayo huzuia kufunga, k**a vile kisukari kali, au hata udhaifu kutokana na uzee.

4. Msafiri ambaye haendi safari ya zaidi ya maili arobaini na nane.

5. Kufunga hakutamdhuru mtu au mtoto wake (ikiwa mwanamke ni mjamzito au ananyonyesha).

https://www.bbc.com/swahili/articles

Wabillahi Tawfiiq!



"Maarifa Kwa Wote"

08/02/2026

MBINU ZA MALEZI CHANYA KWA MAMA WA KIISLAMU.
💡💡💡💡💡💡💡

________________
Media
--------------------------

Malezi chanya ni safari ya kujenga uhusiano wa karibu na wa kudumu kati ya mzazi na mtoto kwa misingi ya heshima, mawasiliano na mfano mwema.

Katika Uislamu, mtoto si mali ya mzazi bali ni amanah kutoka kwa Mwenyezi Mungu
Aliyetukuka.

Hivyo, jukumu la mzazi—hasa mama ambaye mara nyingi huwa karibu zaidi na mtoto—ni kumlea mtoto kwa upendo, busara na mwongozo unaomwandaa kuwa binadamu bora duniani na Akhera.

Malezi chanya yanasisitiza kumlea mtoto kwa msukumo na uthibitisho chanya badala ya hofu na ukali.

Mtoto anapaswa kuheshimiwa k**a mtu binafsi mwenye hisia, fikra na utu wake.

Badala ya mtazamo wa “fanya kwa sababu nimesema,” Uislamu unahimiza maelezo, majadiliano na kueleweshana kulingana na
umri wa mtoto.

Ingawa malezi hubadilika kulingana na hatua za ukuaji wa mtoto, misingi yake inaweza kutumika katika umri wowote.

UKWELI KATIKA HALI ZOTE
💡💡💡💡💡💡💡

Kwanza kabisa, ukweli ni nguzo muhimu ya malezi chanya.

Watoto hujifunza zaidi kwa kuangalia wazazi wao kuliko kusikiliza wanachosema.

Mama anaposema uongo, hata kwa mzaha au kwa lengo la kumtisha mtoto, humfundisha mtoto kuwa uongo ni njia halali ya kutatua mambo.

Ahadi hewa, vitisho vya kubuni na kauli zisizotekelezwa huvunja imani.

Hata pale ambapo ukweli unapokuwa hauwafai watoto kwa umri wao, ni busara kuwaambia kwa uaminifu kuwa watapewa maelezo wanapokuwa wakubwa.

MAPENZI YA DINI
💡💡💡💡💡💡💡

Ni muhimu pia kumtambulisha mtoto katika Uislamu kwa njia ya kupendeza itakayomfanya aupede Uislamu.

Dini isiwasilishwe k**a mzigo au adhabu, bali k**a chanzo cha faraja na furaha.

Kusikiliza Qur’an, kujifunza dua fupi, kusimuliwa hadithi za Manabii na kuzoea taratibu za Kiislamu mapema hujenga uhusiano wa mapenzi na imani.

Mtoto anayefurahia kujifunza dini hukua akiipenda bila kulazimishwa.

MAZUNGUMZO
💡💡💡💡💡💡💡

Mazungumzo ni mhimili mwingine wa malezi chanya. Mtoto anapaswa kuzungumziwa kwa heshima, kwa sauti ya upole na kwa lugha anayoielewa.

Kukaa chini na kuzungumza naye uso kwa uso huonyesha huruma na kuthamini mawazo yake.

Mazungumzo ya kila siku kuhusu maisha, mipango na hisia huwasaidia watoto kujifunza kwa urahisi na kujenga ujasiri wa kuwasiliana.

USALAMA WA KIHISIA
💡💡💡💡💡💡💡

Nyumbani panapaswa kuwa mahali pa utulivu na usalama wa kihisia.

Kelele, matusi na migogoro ya wazazi mbele ya watoto huathiri sana afya ya kisaikolojia ya mtoto.

Mtoto anayekulia katika mazingira ya amani hujenga utulivu wa ndani.

Pale mzazi anapochoka au kukerwa, ni busara kuchukua muda wa kupumzika kabla ya kushughulikia mtoto.

Malezi chanya pia yanahusisha kuangazia mema kuliko mabaya.

Mtoto anapofanya jambo jema, pongezi humjenga zaidi kuliko lawama za mara kwa mara.

Badala ya kuwatisha watoto kwa adhabu, ni bora kuwaeleza faida za kufanya jambo sahihi.

Mtazamo huu huwasaidia kujenga motisha ya ndani.

STADI ZA MAISHA
💡💡💡💡💡💡💡

Kadhalika, watoto wanapaswa kuzoeshwa katika mtindo wa maisha wa wazazi badala ya wazazi kubadilisha maisha yao yote kwa ajili ya watoto.

Kwa kutafuta suluhisho za kuwajumuisha watoto katika shughuli za wazazi, watoto hujifunza kubadilika na kushiriki.

Hii huenda sambamba na kuanzisha tabia njema mapema k**a kusoma, kula vyakula vyenye afya, kusalimia watu na kupenda hadithi.

💡CHANZO:
Imaan ISSN 5618-NO.569

Media.

"Maarifa Kwa Wote"

24/01/2026

QUR'AN NI MUONGOZO WA MAISHA

Tusihesabu miaka tu, bali tubesabu tuliyoyafanya katika miaka hiyo Kwa mujibu wa Qur'an.

Je, tunazo Aya ngapi za Qur'an zinazoongoza maisha yatu?

VIDEO KAMILI:
https://youtu.be/24F4d5KIaVU?si=yoHRQVaVIZWVuV6x.

KUMBUKA:

KU-SUBSCRIBE
KU-SHARE
KU-COMMENT
KU-LIKE

.
.
"Maarifa Kwa Wote"

11/01/2026

AGENDA YA VENEZUELA NI MAFUTA

✔️Ya Maduro yalimkuta pia Aristide wa Haiti.
✔️Co***ne, bangi haijawa tatizo kwa Amerika!
✔️Ilimkumbatia Noriega mshirika wa Escobar.

Jioni ya tarehe 2 Januari, 2026 jeshi la Marekani pamoja na makachero wa FBI walivamiaCaracas, hususwan makazi ya Rais Nicolas Maduro.

Kikosi hicho maalumkiliingia makazi ya Maduro na kumteka yeye na mkewe, Cilia Flores wakiwa ndani ya chumba chao cha kulala.

Wakiwa wamezibwa macho na kufungwa pingu mikononi, walisafirishwa hadi New York (Metropolitan Detention Center, Brooklyn), ambapo Trump anadai wanakabiliwa namash*taka ya ‘ugaidi wa madawa’ ya kulevya na utakatishaji wa fedha.

“Venezuela ni namba moja kwa utoaji wa mafuta na gesi duniani".

Inatatiza akili na kwa hakika ni upuuzi mtupu kudai kwamba Venezuela inashirikiana na Colombia kufanya biashara ya madawa ya kulevya.”

Anasema Prof. Michel Evgeny Chossudovsky.

Wakati tukitafakari hoja ya Prof. Michel Chossudovsky, gazeti la New York Times la tarehe 3 Januari, 2026 linatuambia:

“Before Nicolás Maduro, There Was Manuel Noriega”.

Kwamba, Nicolas Maduro si wa kwanza.

Kabla yake yalimkuta Manuel Noriega.

Manuel Antonio Noriega Moreno (Februari 11, 1934 – Mei 29, 2017) alikuwa Rais wa Panama kipenzi cha Wamarekani na ‘Kifaa’ cha Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) ambaye alipata mafunzo yake katika Chuo cha Kijeshi cha Marekani SOA (U.S. Army’s School of the Americas), Panama Canal Zone (Fort Gulick).

Kuanzia miaka ya 1970s Noriega akiitumikia Marekani katika kukabiliana na wanaharakati wa siasa za kijamaa na kikomunisti Amerika ya Kati na Kusini.

Noriega anatajwa kuhusika katika kupitisha pesa na silaha kutoka Marekani kwenda kwa magaidi wa Contras wa Nicaragua.

Kwa hiyo alikuwa “mchezaji” muhimu katika ile kashfa ya “Iran-Contra Affair (1985–1987)".

Pamoja na kuwa mtumishi wa CIA, Noriega alikuwaakitumiwa pia na wababe wa madawa ya kulevya.

Anatajwa kutumiwa na mbabe wa madawa ya kulenya wa Colombia aka “King of Pablo Emilio Escobar Gaviria.

Akimsaidia kuingiza co***ne Marekani na kisha kupitishia pesa zake katika benki za Panama.

Bila shaka hili liliwezekana kutokana na nafasi yake katika CIA huku akiwa mkuu wa nchi Panama.

Serikali ya Marekani ilijua namna Manuel Antonio Noriega Moreno alivyokuwa akihusika na kuingiza madawa ya kulevya Marekani.

Aidha, ilijua pia namna alivyotakatisha pesa za “Mfalme wa Co***ne”, lakini maadhali alikuwa ‘kifaa’ muhimu cha CIA, haikujali.

(Tazama: Kerry Committee na “Dark Alliance”).

Mambo yaliharibika pale Washington ilipogundua kwamba Noriega alikuwa akiuza baadhi ya siri za masuala nyeti ya Marekani, ikiwemo tekinolojia kwa nchi nyingine.

Wakati huo huo, ulikuwa umefikia muda wa kukamilika muda waMkataba wa Mfereji wa Panama uliokuwa chini ya uangalizi wa pamoja baina ya Marekani na Panama toka Septemba 7, 1977 ambapo ikifika saa sita mchana wa tarehe 31 Desemba, 1999, Marekani ilitakiwa kukabidhi mamlaka ya kusimamia mfereji huo kwa Panama Canal Authority (PCA) ya Serikali ya Panama.

Kwa kuona kwamba Noriega anaweza kuwa kikwazo, Rais Ronald Wilson Reagan akamtaka wafanye makubaliano wamlipe kiasi cha fedha na kumhakikishia mafao, ulinzi na fursa mbalimba aondoke serikalini, akaishi nje ya Panama. Noriega akakataa.

Ashaonja ‘tamu’ ya ubabe na k**a ni pesa anazipata nyingi kupitia mtandao wa “Medellin Cartel”.

Kufikia hapo ndio Washington ikaja na mash*taka ya ‘madawa’ ya kulevya.

Alipokuja Rais George H. W. Bush, ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa CIA miaka ya 1970s wakati Noriega akiwa ‘kifaa’ muhimu cha CIA , akamuamuru Generali Colin Luther Powell, wakati huo akiwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi, kuivania Panama.

Operation Just Cause, lilikuwa ndio jina la operesheni hiyo.

Askari 26,000 wakavamia Panama tarehe 20 Desemba, 1989.

Operation Just Cause ulikuwa uvamizi wa kikatili ambapo vifaru vilikuwa vikikanyaga na kusagasaga watu waliothubutu kujitokeza njiani huku zaidi ya nyumba 4,000 za makazi ya raia zikiangamizwa na kuacha mamia kwa maelfu ya watu wakiwa maiti.

Maiti zilifukiwa katika makaburi ya jumla, kwa hiyo haikuwa rahisi kujua kwa uhakika idadi ya waliouliwa.

Miaka 36 baada ya kuk**atwa Noriega na kupelekwa jela Miami (FCI Miami), Donald John Trump naye kaja na madai yale yale dhidi ya Nicolás Maduro Moros.

Lakini kabla ya kuzungumzia kadhia ya Maduro, tumuangalie Jean - Bertrand Aristide.

Septemba 1991 Rais wa Haiti Jean-Bertrand Aristide, alilazimishwa kuikimbia nchi yake baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi.

Wakati ule Taasisi za Fedha za Kimataifa World Bank Group, European Commission, pamoja na nchi za Marekani, Brazil, Canada, Norway, n.k, zilikusanya mabilioni ya Dola kuchangia Mfuko uliojulikana k**a “Haiti Reconstruction Fund” (HRF) kusaidia kuijenga upya Haiti baada ya kukumbwa na tetemeko baya la ardhi mwaka 2010.

Serikali ya Clinton ilitaka kusimamia Mfuko huo ili kuhakikisha pesa hizo zinarudi katika mabenki ya Marekani kupitia tenda mbalimbali .

Clinton akaona Rais Jean-Bertrand Aristide, atakuwa kikwazo .

Yakafanyika mapinduzi ambapo CIA inatajwa kuhusika.

Inaelezwa kuwa katika mabilioni ya Dola yaliyokusanywa, ni asilimia 10% iliyofika kwa wananchi wa Haiti.

William Jefferson Clinton alipata alichotaka.

Akafanya “Sherehe kwa Pesa za Matanga” katika msiba wa tetemeko la ardhi Haiti! (Angalia:

How the Clintons robbed and destroyed Haiti.

Tazama pia: How the U.S. Destroyed Haiti and the Clintons Failed to Rebuild It).

Lakini kwa Aristide kulikuwa na jambo jingine.

Baada ya Aristide kupinduliwa tarehe 29 Septemba 1991, pamoja na kuwa na Rais wa Mpito, mamlaka hasa yalishikiliwa na Kamanda Joseph Raoul Cédras, Afisa wa ngazi za juu wa jeshi na Idara ya Usalama (SIN), ambayo iliundwa na kuendelea kupewa pesa na CIA.

Joseph Raoul Cédras na genge lake la mapinduzi wakituhumiwa kuwa washirika wa wababe wa biashara ya madawa ya kulevya Spanish: Cartel de Cali) ilikuwa kundi la wababe wa madawa ya kulevya likiwa na makao yake katika miji ya Valle del Cauca, Colombia waanzilishi wakiwa ndugu watatu:

✔️Gilberto Rodríguez Orejuela,
✔️Miguel Rodriguez Orejuela na
✔️José Santacruz Londoño.

Wakidhibiti biashara ya Co***ne duniani kwa zaidi ya aslimia 80% katika miaka ya 1990s.

Awali ndugu hawa wanne, walikuwa katika kikosi cha Pablo Escobar, wakajitenga.

Aristide anasema kuwa, anaamini dhamira yake na hatua alizoanza kuchukua kuwak**ata washirika wa wababe wa biashara ya madawa ya kulevya walio ndani ya jeshi na Idara ya Usalama wakiwemo Raul Cedras na Michel Francois, ni moja ya sababu zilizopelekea yeye kupinduliwa mwaka 1990.

Mwakilishi wa Bunge la Congress la Marekani John James Conyers Jr (D-Michigan) akielezea masikitiko yake dhidi ya Serikali ya Clinton namna inavyoshirikiana na wababe wa madawa ya kulevya walio ndani ya Serikali ya Haiti alisema kuwa, pamoja na ushahidi ulio wazi unaotolewa na Chombo cha Serikali kinachoshughulikia uhalifu wa madawa ya kulevya, White House na CIA bado wameendelea kushirikiana na wahalifu hao ndani ya SIN badala ya kuchukua hatua k**a ilivyofanyika kwa Manuel Noriega.

Hiyo ndiyo Marekani!

Kinyume na Noriega aliyekuwa ‘kibaraka mtiifu’ kwa CIA kabla ya kuasi, kosa la Nicolas Maduro mbele ya Trump ni kuendeleza siasa za Hugo Chaves za kutumia mafuta na gesi ya Venezuela kwa maendeleo ya Wana wa Venezuela.

Wabillahi Tawfiiq!

CHANZO:
An-nuur: ISSN 0856 - 3652 TOLEO NA. 1693.


"Maarifa Kwa Wote"
[email protected]

06/01/2026

SONGOMBINGO YA TAREHE ZA KUZALIWA.

Kuna watu hawatasherehekea BIRTHDAY mwaka huu, watake wasitake.

Kwa nini? Sababu ni hii:

Hii ni Kwa wale Waliozaliwa tarehe 29 Februari. Kwa sababu, mwaka huu wa 2026 mwezi Februari utaishia tarehe 28.

Au mimi sijaelewa? Fanya utafiti kisha uniandikie kwenye "COMMENT" k**a nimepatia.



"Maarifa Kwa Wote"

03/01/2026

TAARIFA ZA MSIBA

Innalillahi Wainna Ilayhi Rajiuun.

🏮MUM ALUMNI IMEFIWA
🏮KKUT IMEFIWA
🏮FAMILIA IMEFIWA
🏮UMMA UMEFIWA

____________
03-01-2026
-------------------

"Allahumma Ighfirlahu Warhamhu Waskannahu Filjannat"

"Mwenyezi Mungu tunakuomba umsamehe, umrehemu na umpe makazi ya peponi"

Aamin.

Ndugu yetu, mhasibu wa Mkoa Kamati ya Kuendeleza Uislamu Tabora, Br. Masesa Maganga Masesa, amefariki usiku wa leo (03.01.2026).

Br. Masesa alikuwa safarini kutoka Tabora kuelekea Dar es Salaam kwa mabasi ya usiku.

Walipokaribia Gairo hali ya kiafya ilibadilika, na kupatwa na hali ya strock.

Konda alitoa taarifa kwa familia, kwa kuwa ilikua usiku saa saba familia walimuunganisha konda na ndugu yetu mmoja yupo morogoro ili ampokee na kumpeleka hospitalini.

Wakati wanakaribia Morogoro konda alimuomba yule ndugu aje na usafiri kabisa hadi geti la kutokea magari stendi.

Baada ya kufika akampokea akiwa kashafariki.

Allaah amsamehe makosa yake na amuepushe na adhabu za moto.

Ndugu yetu ni mume wa wake wanne. Kikazi ndugu yetu alikuwa mwajeshi.

Masesa alikuwa mwanachuo mwenzangu, kitivo kimoja na masomo yetu yalifanana isipokuwa somo moja tu. 2011 - 2014. Muslim University of Morogoro.

Ninaweza kusema kitivo Cha "Bachelor of Islamic Studies with Education" kimeondokewa na kifaa muhimu.


[email protected]

Want your business to be the top-listed Government Service in Kasulu?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Kasulu