28/02/2026
Subhaanallahhi sheikh amesema haya kuhusu mahari...
Gusa hiyo video link kamsikilizee📸📸
Visit TikTok to discover videos!
Watch, follow, and discover more trending content.
19/01/2026
Al-Jumu'ah 62:8
قُلۡ إِنَّ ٱلۡمَوۡتَ ٱلَّذِي تَفِرُّونَ مِنۡهُ فَإِنَّهُۥ مُلَٰقِيكُمۡۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Sema ewe Muhammad (waambie)
Hakika ya umauti wanaoukimbia watakutana nao, kisha Kwa Allah watarejeshwa mjuzi WA mambo ya (ghaib) na washuhudishiwe Yale waliyotenda na waliyoyatanguliza...
Ndugu zangu tusibweteke katika kutenda mema na kulet istighfaar hakika ya umauti huja ghafla...
Wassalamu alaykum warahmatullahhi wabarakatuhh...
13/01/2026
Assalamu alaykum warahmatullahhi wabarakatuhh...
✍️ Amani iwe juu yako ewe rafiki yangu.
• Usiwe na hofu, hakika mambo huenda namna ambavyo Allah amekadiria.
• Qadari zote za Allah kwako ni kheri, hata k**a zitakupa maumivu.
• Unamuomba Allah jambo fulani kwa kung'ang'ania. Wala hakupi, kisha wewe wahuzunika.
• Wala hujui kuwa wewe ni k**a mtoto mdogo ambaye analilia dawa ya vidonge ambavyo vimepakwa rangi (anadhani kuwa ni p**i).
• Mtoto anataka dawa, mama yake anamzuia. Kwa sababu mama anajua kwamba kile anachokitaka mtoto lazima kitamuangamiza.
• Allah anapokunyima kitu, basi atakupa kitu (kilicho bora zaidi).
• Unakikosa kitu kizuri, kisha moyo wako unatawaliwa na huzuni. Wala hujui kwamba Allah anachukua kitu ili akupe kitu kingine.
• Wakati Al-khadhwir alipomuuwa kijana, mwanzoni jambo hilo lilionekana baya na ni ukatili mkubwa.
• Hata Nabii Musa (amani iwe juu yake) alidhani hivyo pia.
• Na wala hakuna shaka kwamba mioyo ya wazazi wa kijana huyo ilipasuka.
• Kisha mambo yaliyofichwa yakawekwa wazi, na ikabainika kwamba kilele cha rehma za Allah ni kuuliwa yule kijana.
• Allah Mtukufu huichukua dunia yako ili akuhifadhie dini yako.
✍️ Ewe rafiki yangu.
• Hakika Allah hupangilia mambo kwa hekima na rehma, hekima zake hazijawahi kupita kwenye akili yetu.
• Kwa sababu hatuna uwezo wa kuona mbali, na pia fikra zetu zina kikomo (hatuna uwezo wa kufikiria mbali zaidi), wala hatuyaoni mambo ila kwa uchache wake.
• Lakini Allah anaona kila kitu.
• Lau k**a ungekuwa pamoja na wale masikini pindi jahazi lao lilipotobolewa, huenda ungesema: Hivi umasikini tulionao hautoshi hadi tunapewa mtihani kwenye chanzo chetu cha kujipatia riziki?!
• Lakini wala usingekaa muda mrefu ila ungeliona kundi lililotumwa na mfalme dhalimu, wakiyapora majahazi ambayo ni mazima (hasiyo na dosari).
• Wakati huo sasa ndiyo ungezijua rehma za Allah.
• Hakika kutobolewa jahazi ilikuwa ni rehma kubwa mno kuliko lingeachwa (bila kutobolewa).
• Utukufu ni wa Allah ambaye anakupa mtihani mdogo, ili akuokoe na balaa zito ambalo lipo mbele yako.
✍️ Ewe rafiki yangu, jambo lolote likifungamana na Allah, basi kuwa na adabu.
• Hivi umemsahau Yule ambaye alikuwa akikuletea riziki yako hali ya kuwa upo tumboni kwa mama yako?!
• Hivi umemsahau Yule ambaye aliulainisha moyo wa mama yako kwako ulivyokuwa mtoto mchanga?! Mama yako alikuwa akiamka usiku wa manane kwa ajili yako bila ya kuchoka, alikuwa k**a vile kijakazi anayemuhudumia mfalme wake.
• Hivi umemsahau baba yako jinsi alivyokuwa akikutafutia mkate licha ya maisha kuwa magumu ili uweze kukua?!
• Hivi umewahi kujiuliza ni nani ambaye amekufanya uwe kipande cha moyo wa baba yako?! Ilifika hatua baba yako alikuwa tayari kuikata nyama yake ili akulishe wewe (yaani alikuwa tayari kuumia mwili wake kwenye harakati za kutafuta riziki ili tu wewe upate chakula).
• Alieyaweka mapenzi hayo kwa wazazi wako ni Allah.
• Amejitosheleza kwako ila hawezi kukuacha (kwenye kila hali yupo nawe).
• Allah ni Mwenye nguvu ambaye hakuhitaji lakini anakuita.
• Umeyasahau haya yote. Kisha ukipatwa na Qadari yake ambayo huipendi, unaanza kulalamika na kuchoka.
• Subiri siku zipite, utafunguliwa pazia ya mambo yaliyojificha, utatambua kwamba Allah hakuchukua kitu kwako ila kwa lengo la kukupa kitu kingine, wala hakukupa mtihani ila ili akutengeneze. Na hakukuondoshea jambo isipokuwa alitaka kukupa kilicho bora zaidi.
✍️ Amani iingie ndani ya moyo wako ewe rafiki yangu.
*نستودعك يارب حالنا فاجعله*
*في خير وعلى خير وإلى خير*
06/01/2026
Follow on tiktok as
kaka salim on TikTok
.tittok.kakasalim22 32 Followers, 41 Following, 33 Likes - Watch awesome short videos created by kaka salim
06/01/2026
Allah awarehemu masheikh zetu na wengine wengi Kwa jitihada za kutuelimisha..
...
Ila mbora katika wanaokosea ni wenyew kutubiaa....
Twawapenda sanaaa
28/12/2025
Kaka SALIM...
This is my new page naomba ni follow, like comment and share ukiwa k**a funs wangu...
Nawapenda saanaaa