Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro

Share

Akaunti Rasmi ya Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro

Photos from Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro's post 06/02/2026

UJENZI WA DARAJA LA MTO POLOLETI UMEKAMILIKA

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Ngorongoro wamekamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Pololeti lililopo katika Kata ya Oloipiri. Daraja hilo lina urefu wa mita 22 na limegharimu jumla ya shilingi 314,737,557.62, likiwa linaunganisha Kata ya Oloipiri na Soitsambu.

Ujenzi wa daraja hilo ulianza tarehe 6 Juni 2024 na kukamilika leo tarehe 6 Februari 2026. Kukamilika kwa daraja hili kunalenga kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi, hususan katika kipindi hiki cha msimu wa mvua, kwa kuhakikisha usalama na upatikanaji wa huduma kwa wakati.

TARURA inaendelea kutekeleza miradi ya miundombinu kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Ngorongoro.

06/02/2026

MBUNGE KUWAUNGA MKONO WANANCHI WA KITONGOJI CHA HARARA

Wananchi wa Kata ya Samunge wameonyesha mshik**ano na uzalendo wa hali ya juu kwa kujenga daraja la Mto Rima lililopo kwenye barabara ya kwenda Mojenenane, Kitongoji cha Hahara, Kijiji cha Samunge. Daraja hilo limejengwa kwa nguvu zao wenyewe na kugharimu jumla ya shilingi milioni 11.
Mheshimiwa Mbunge amepongeza juhudi hizi na kuahidi kuwaunga mkono wananchi kwa hatua waliyochukua. Aidha, amewahimiza wananchi wengine kuiga mfano huu wa kujituma na kuibua miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jamii nzima.

05/02/2026
05/02/2026

Pongezi Kidato cha Nne

29/01/2026

UTEUZI

Photos from Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro's post 29/01/2026

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amemvisha cheo na kumuapisha Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Ibrahim Badru.

Hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 29 Januari, 2026 Arusha ni baada ya uteuzi wa Kamishna huyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 26 Mei, 2025 kisha Kamishna Badru kuhitimu mafunzo ya Jeshi la uhifadhi kwa mujibu wa sheria na hatimae kuvishwa cheo na kula kiapo kwa ajili wa utekelezaji wa Majukumu yake ya kuiongoza Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Ngorongoro Conservation Area Authority

28/01/2026

Swali :Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza maeneo ya malisho kutoka hekta 3 hadi 6 k**a Ilani ya CCM inavyosema?

Aliuliza Mhe Yannick Ndoinyo (MB) Jimbo la Ngorongoro

28/01/2026

Taarifa

Want your business to be the top-listed Government Service in Loliondo?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Loliondo
1