Afisa Mwandamizi wa Masoko kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Hamis Msham Kiimbi, ametoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Mpombo kuhusu upimaji wa ubora wa maziwa, usajili wa wadau wa sekta ya maziwa na umuhimu wa unywaji wa maziwa.
Akizungumza na wananchi katika shule ya msingi Mapambano, Bw. Kiimbi amesema Bodi ya Maziwa Tanzania ina jukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza sekta ya maziwa nchini kwa kuhakikisha uzalishaji, ukusanyaji, usafirishaji, usindikaji na uuzaji wa maziwa unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama.
Aidha, amewahimiza wafugaji, wakusanyaji, wasindikaji na wafanyabiashara wa maziwa kujisajili na Bodi ya Maziwa Tanzania ili kutambuliwa kisheria, kupata huduma za kitaalamu na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya maziwa.
Amewahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kunywa maziwa kila siku ili kuboresha afya na lishe katika jamii.
Busokelo District Council
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO . Lwangwa, Tukuyu
S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Wajumbe wa kamati ya zhule, wawakilishi wa Wazazi pamoja na Walimu katika shule ya msingi Mapambano kata ya Mpombo wameupokea mradi wa unywaji maziwa shuleni kwa furaha na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha unatekelezwa kwa mafanikio na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Dkt. Mackrina Nombo, Mtaalamu wa Lishe kutoka Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, ametambulisha Mradi wa Unywaji Maziwa Shuleni kwa Kamati ya Shule, wawakilishi wa Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Mapambano Kata ya Mpombo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Akizungumza wakati wa utambulishaji huo, Dkt. Nombo amesema mradi huo unatekelezwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), ukiwa na lengo la kuboresha lishe kwa wanafunzi, kuongeza kipato cha wafugaji, kukuza uzalishaji na soko la maziwa pamoja na kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026, ambapo wanafunzi watanufaika na huduma ya unywaji maziwa shuleni, hatua inayolenga kupunguza utapiamlo na udumavu, kuboresha afya na kuongeza uwezo wa wanafunzi kujifunza na kufanya vizuri darasani.
18/07/2026
SHULE YA MSINGI MAPAMBANO YAPOKEA MRADI WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI
Leo Julai 18, 2026, Dkt. Mackrina Nombo, Mtaalamu wa Lishe kutoka Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, ametambulisha Mradi wa Unywaji Maziwa Shuleni kwa Kamati ya Shule, wawakilishi wa Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Mapambano Kata ya Mpombo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Akizungumza wakati wa utambulishaji huo, Dkt. Nombo amesema mradi huo unatekelezwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), ukiwa na lengo la kuboresha lishe kwa wanafunzi, kuongeza kipato cha wafugaji, kukuza uzalishaji na soko la maziwa pamoja na kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026, ambapo wanafunzi watanufaika na huduma ya unywaji maziwa shuleni, hatua inayolenga kupunguza utapiamlo na udumavu, kuboresha afya na kuongeza uwezo wa wanafunzi kujifunza na kufanya vizuri darasani.
Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati ya Shule, wawakilishi wa Wazazi pamoja na Walimu wameupokea mradi huo kwa furaha na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha unatekelezwa kwa mafanikio na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Kamati za Shule, wawakilishi wa Wazazi pamoja na wawakilishi wa Viongozi wa Dini kutoka Shule ya Msingi Mbambo iliyopo Kata ya Kambasegela na Shule ya Msingi Itete iliyopo Kata ya Itete, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, wamepokea kutambulishwa kwa Mradi wa Unywaji Maziwa Shuleni unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Oktoba 2026.
KAMATI ZA SHULE, WAZAZI NA VIONGOZI WA DINI BUSOKELO WAPOKEA MRADI WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI.

Zoezi la utambulishaji wa mradi huo limefanyika leo 17/07/2026 na kuongozwa na Dkt. Mackrina Nombo, Mtaalamu wa Lishe kutoka Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, ambao unatekelezwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Akizungumza wakati wa utambulishaji huo, Dkt. Nombo amesema lengo kuu la mradi ni kuboresha kipato cha wafugaji na wananchi, kuongeza uwezo wa jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuboresha lishe, hususan kwa watoto wa shule za msingi kupitia programu ya unywaji maziwa shuleni.
17/07/2026

Programu hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha afya na maendeleo ya wanafunzi kwa kuhakikisha wanapata lishe bora, kupunguza utapiamlo na udumavu, kuongeza umakini darasani na hatimaye kuchangia kuimarika kwa ufaulu wa wanafunzi.
Katika kikao hicho, Kamati za Shule, Wawakilishi wa Wazazi na Viongozi wa Dini walipatiwa elimu kuhusu utekelezaji wa mradi na wajibu wa kila mdau katika kuhakikisha unafanikiwa. Viongozi wa Dini walisisitiza umuhimu wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu faida za unywaji wa maziwa, huku wakihimiza wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika kuunga mkono utekelezaji wa mradi huo.
Aidha, washiriki walielezwa kuwa mradi huo utasaidia kukuza uzalishaji wa maziwa, kuongeza soko la maziwa kwa wafugaji, kuhamasisha utamaduni wa unywaji maziwa shuleni na kuboresha hali ya lishe kwa watoto, hatua itakayochochea maendeleo ya sekta ya mifugo na kuinua ustawi wa jamii kwa ujumla.
Mradi wa Unywaji Maziwa Shuleni unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Oktoba 2026, ukiwa sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha lishe kwa wanafunzi na kukuza uchumi wa wafugaji kupitia sekta ya maziwa.
Kikundi cha Wanawake Kikuba kilichopo Kata ya Lufilyo Halamshauri ya Wilaya ya Busokelo kimeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Kikundi hicho, kinachojishughulisha na biashara ya uuzaji wa vitenge, kimenufaika na mkopo wa Shilingi Milioni 8 uliotolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, fedha ambazo zimewawezesha kuongeza mtaji na kupanua shughuli zao za biashara.
Akizungumza kwa niaba ya kikundi, Katibu wa Katibu wa kikundi hicho B.Rehema Godwin Swallo amesema mkopo huo umeleta chachu ya maendeleo kwa wanachama na kuongeza kipato cha familia zao.
Aidha, washukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki yanayowezesha vikundi kujikwamua kiuchumi na kuahidi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha kinarejesha mkopo kwa wakati.
15/07/2026
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI BUSOKELO AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO, ASISITIZA UBORA WA UTEKELEZAJI NA UREJESHAJI WA MADENI YA MIKOPO.
Leo Julai 15, 2026 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. John Kipingi, ameongoza Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (Council Management Team - CMT) kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi, kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana na kutoa maelekezo yatakayoharakisha kukamilika kwa miradi hiyo.
Katika ziara hiyo, Kamati ilikagua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafi (Sanitation) na mfumo wa maji (Water Supply System) katika Zahanati ya Lupata, Kata ya Lupata, unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 43.3 kupitia fedha za SRWSS.
Aidha, Kamati ilitembelea mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafi na mfumo wa maji katika Zahanati ya Kibole, Kata ya Itete, unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 42.5, ukiwa pia umefadhiliwa kupitia fedha za SRWSS.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Bw. Kipingi amesisitiza wasimamizi wa miradi na wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyowekwa ili wananchi waendelee kupata huduma bora za afya katika mazingira salama na rafiki.
Katika ziara hiyo, Kamati pia ilikagua ujenzi wa matundu mawili ya choo katika Soko la Mbambo, Kata ya Kambasegela, unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 7 kupitia fedha za Mapato ya Ndani.
Katika hatua nyingine Kamati ilitembelea vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ambapo Kikundi cha Lusubilo kilinufaika na mkopo wenye thamani ya Shilingi Milioni 9, huku Kikundi cha Wanawake Kikuba kinachojishughulisha na biashara ya vitenge kikinufaika na mkopo wa Shilingi Milioni 8.
Kamati ya CMT Imevitaka vikundi vyote vinavyonufaika na mikopo hiyo kuhakikisha vinaitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wengine wenye sifa kuendelea kunufaika na mpango huo wa uwezeshaji wa kiuchumi.
13/07/2026
Leo tarehe 13 Julai 2026, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. John Kipingili, ameongoza kikao cha maandalizi ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe wa kamati ndogo mbalimbali zinazohusika na maandalizi ya mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa lengo la kupitia hatua zilizofikiwa, kujadili utekelezaji wa majukumu ya kila kamati, kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
Mbeya
53529