CANT STOP LAUGHING
Beatho fancy page
The home of story
10/07/2022
MAMA
MWANDISHI: Beatho Benedict.
SEHEMU YA THERATHINI NA MBILI.
MAWASILIANO;
▶️WhatsApp- 0767464146.
▶️ Gmail- [email protected]
▶️ Website- storiesandscriptwriter.worldpress.com
👉TULIPOISHIA......
Aliingia chumbani na kujifungia mwenyewe! Nafasi yake ikiwa ni yenye kujuta kwa yote aliyo fanya, Kila akiyakumbuka ni k**a nyundo kichwani ama wembe na makali yake alichanjwa nao machoni, ama vile radi ipigayo ingali unatembea na umenyeshewa kwelikweli.
Kumbukumbu zilimrudia za upuuzi alio kwisha kuifanya kwenye maisha yake. Naweza kusema ni k**a mtu alie kua akiishi nje ya ufahamu wake sasa akili zimemurejerea na anaonyeshwa mambo yote aliyo fanya kipindi chote! Alitamani kusema si yeye, lakini hapana angekumbuka vipi mambo ambayo hakuyafanya?
"Kwanini mimi, kwanini niliishia kwenye njia hiyo? Kwanini sikujitambua wakati wote mbaka nakutwa na adhabu k**a hii!!
"Mwisho wa yote hivi ndivo ulivo amua kuniadhibu mimi Mungu baba? Na k**a nikitubu nitasanehewa mimi kweli?"
Endelea........
"Hello mama!"
Alisema Yubeti baada ya kupokea simu na kuiweka sikioni, mpigaji alikua ni mkwewe, yaani mama yake Vivie ama Vivian.
"Samahani mwanangu, haijarishi naomba leo jioni tuonane! Niko na maongezi na wewe ni mhimu sana"
"Bila shaka itakua k**a ulivopanga wewe!"
Walielekezana mazingira ya kukutana na mda.
Akiwa chumbani amejifungia mwenyewe, kitu pekee alichagua ni kulia! Machozi si kumdondoka bali naweza kusema yalimmiminuka hakua wa kula wala kunywa. Lakini ni k**a alipata wazo, akayafuta machozi yake na kusimama akijiuliza ataanzia wapi kwenda na mipango yake.
Alitoka kwa kujiamini na kuingia jikoni, njaa ilikua imemuuma kweli kweli, kwa mda k**a ule mama yake alikua kwenye mizunguko yake mara kwa jilani huyu mara kwa jilani yule! Na alikua na heshma yake kwa sasa kila anako pita alikaribishwa vizuri, wengi walihitaji kuweka nae ukaribu, labda niseme Yubeti ndio alie leta heshma yote hiyo. Kila mtu alitamani kuweka ukaribu.
Hapakua pamepikwa chochote, Prisca alihaha huku na huko, akapata wazo la kupika lakini anakumbuka hajawai kumiliki ata sufuria ama sahani wala kijiko tangu wakati ule akiwa binti mdogo anaishi na mama yake! Hakuwai kupika kwa kipindi chote, alikua akila humohumo kwa mabaa na mahoteli alikisha chukuliwa kutoa huduma za kuburudisha wenyewe wanapesa zinasumbua mifuko yao.
Swala la kupika alijistukia kwamba hawezi, ikabidi ajikague pochi Ina bei gani aende akanunue chakula.
Baada ya mambo yote na mda kupitia mama yake alireje nyumbani, kabla ya yotee alimpigia magoti na kuanza kumwomba msamaha kwa Kila gumu alilomsababishia mama yake.
"Nisamehe mimi mama yangu, sina mwingine wa kumulilia akanielewa mimi! Naomba nisame sana mama!"
"Umekula?
Ni swali alilo uliza bibi, jambo lililo mfanya Prisca ashindwe kumwelewa kabisa maana yeye alitamani kuambiwa amesamehewa ama laa!
"Umekula nini wakati hujapika?"
Swali jingine baada ya bibi Yubeti ama mama yake Prisca kuangalia jikoni, akagundua ata moto haukua umepulizwa. Kabla hajasema chochote mama yake aliendelea kusema;
" Unatakiwa kula vizuri Ili uwe na afya, nilikwambia k**a unahitaji kulia lia sana! Ila kujifungia ndani na kulia tena bila kula wala kunywa haisaidii chochote, unachotakiwa kufanya ni kubadilika sio kuomba omba msamaha apa!
"Msamaha nenda kamwombe mwanao ulie mfanyia ukatili"
Hapakua na laziada, kazi ni kwake kubadilia na kuishi maisha mazuri. Alimpigia simu Yubeti lakini haikupokelewa, alijaribu kurudia mara kadhaa lakini bado Yubeti hakua na mda wa kupokea simu yake. Alijiskia vibaya sana…, akaona amwandikie ujumbe wa maandishi;
"Natambua unahasira sana na mimi japo huonyeshi wazi, lakini chuki ya kweli inatokana na upendo wa dhati. Sifahamu chochote ni kwajinzi gani nilikusababishia wakati mgumu kwa wakati wote mbaka ulipofikia, Nafahamu sasa k**a yote ni makosa yangu! Najua pia ulisha wai jiuliza kuhusu baba yako........
Yubeti ndio alikua akisoma ujumbe huo na wakati huo tayali alikua kashafika pale alipo ombwa afike, lakini alipo soma Habari ya baba kwenye Ile meseji alijikuta akistuka sana na Ile kutupa macho mbele kadri ya maelekezo aliyo pewa, alimwona mkwewe yaani Bi.Fanista lakini hakua ameketi pale mwenyewe!
Yubeti alijikuta anashindwa kuendelea kusogea baada ya kumwona mtu alie kua ameketi pamoja na mkwewe wakimsubili yeye!
Akajikuta anarudi kwa simu kuendelea kusoma Ile meseji, Prisca mama yake aliandika;
"Najua pia ulisha wai jiuliza kuhusu baba yako, baba yako yupo! Nilifanya ujinga mwingi lakini baba yako natambua, k**a umesha nijua mimi unatakiwa kumjuza na baba yako pia! Na usije kumchukua kwa lolote yote ni makosa yangu, mimi ndio sababu yeye kushindwa kuchukulia uangarifu wa malezi yako, naomba sana usije kumchukia baba yako Hana kosa juu Yako"
🤙 Nikumbushe TV wanasababisha tunapata hii burudani fanya kuwa yani💪
Endelea.......
Ni mengi aliyo andika kuonyesha kujuta kwa yote aliyo kwisha kufanya, aliandika ujumbe huo kwa hisia sana, na alionekana kumtetea sana mwanaume alie mpea mimba ya Yubeti.
Yubeti alijikuta akiwa na hisia za tofauti na yule mwanaume alie kaa pale na mkwewe, mwanzo alitamani hata kuondoka lakini kulingana na maelezo ya ujumbe mama yake alimtumia, akaona hana sababu ya kua na hasira kwa mtu asie mjua.
Alisogea na mkwewe alimkarimu vema, zaidi ni salamu na polojo za hapa na pale lakini mara kwa mara Yubeti aligongana macho na yule mwanaume alie keti pamoja nao hapo! Kwani wote alikua wakitizamana kwa kuiba ibiana.
Baada ya mda kupita wakipoza Koo taratibu, utulivu ukiwa wa kutosha, hapo ndipo Bi.Fanista akaona ni mda mwafaka wa kuzungumza kile alicho mwitia Yubeti!
Alianza kwa kusema;
"Yubeti!"
"Naamu mama!"
Naomba nisamehe mimi, na naomba unielwe kwa hichi ninachokwenda kumwambia leo!"
Yubeti ni k**a alishaanza kuelewa nini anakwenda kuambiwa,ila aliwekea umakini zaidi kujua kile kilicho kusudiwa!!!
🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐
Usisahau kuacha comment, nambie umeelewa Nini au na wewe ni k**a Yubeti unawekea umakini kujua Nini mama Vivian anakwenda kuzungumza?
*Tukutane jumapili ijayo apa apa? STORE OF STORIES
👉 We baki na mimi!
Like, comment and share na a,usisahau a kulike ukulasa huu ili usipitwe na simulizi zangu.
Niwatakie wakati mwema na muwe na bahati njema tukutane kwenye comments
🙏🙏🙏🙏🙏
03/07/2022
MAMA
MWANDISHI: Beatho Benedict.
SEHEMU YA THERATHINI NA MOJA.
MAWASILIANO;
▶️WhatsApp- 0767464146.
▶️ Gmail- [email protected]
▶️ Website- storiesandscriptwriter.worldpress.com
👉TULIPOISHIA......
Apo Yubeti ndio akakumbuka k**a alivuliwa pale hotelini, lakini hakua na chakujieleza.
"Ivi Yubeti! Unakaribia kua chizi siyo, ivi inawezekanaje wewe kutembea na mama yako!"
"Inawezejana nishakua chizi, vipi unafikiri kwa akiri ata za kuanza kua chizi mi naweza kufanya Ivo!"
"Kwahiyo unataka kubisha sio? Basi nambie ulikua wapi leo!"
Vivian alikua kavurugwa kweli, alikwenda jikoni na kutoka na kisu na alihitaji kumdhuru nacho, lakini bahati nzuri Yubeti akiona, kisu kilikua kinaenda kumkita kifuani akakizuia kwa mkono!
Endelea.......
Basi mkono ndio ulio dhurika kwani alizuia kisu kwenye makali, Vivian alishuka mpini wake! Inaelekea hakupata maumivu yoyote Yubeti kwani aliendelea kushikilia kile na damu zilianza kuchuruzikapale mkononi!!!!
Vivian aliogopa sana, tena kwa jinzi Yubeti alivo kua kamokodolea macho bila ya kupepesa pembeni! Vivian alianza kutetemeka misiri ya mtu alie pigwa baridi ya alfajiri pale Njombe mwezi wa sita ama pale Arusha!
"K**a ukitaka kuuwa basi hustahili kutetemeka k**a hivo, hata hivo mikono Yako ni laini sana Mungu alikuumbia utumie kunikandakanda mimi nipate raha hivo haifai wewe kushika visu k**a hivi!
"Lakini sijaumia na nafurahi kuona mke wangu anajari sana kuhusu mimi na hapendi nifanye makosa mimi!"
🤙Iko tv channel pale YouTube inaitwa Nikumbushe TV , ukipita huko subscribe channel hii pia wako hapa pia wanapatikana na follow them👈
Endelea........!
Alisema Yubeti akimtaka Vivian aachie kile kisu, Kisha akakirusha pembeni. Alizama mfuko mwake na kuzama mfukoni, alitoka simu yake na kumpigia mtu! Baada ya kupiga alisikika akisema-;
"Nitumie izo video!"
Ndivo alivo sema Yubeti, na haikumchukua mda inaonekana alipokea izo video alizo omba!
Alicheza na simu yake naona mwisho alikua ameweka Ile video aliyo tumiwa tayari kwa kutizamwa, aliunganisha kwa tv yao na kwa tv alionekana yeye akiwa anaingia kwenye Ile hoteli aliyo kwenda kukutana na mama yake ambapo ilisadikika walikwenda kufanya visivyo fanyika, isipo kua kwa yule mmakonde anaweza pengine maana aliimba akisema 🎶yeye anafanya visivyo fanyika🎶
Mda wote Vivian alikua kajikunyata misiri ya mtu alie subilia tu kufanywa kitoweo na simba alie kua kashambananisha kwenye kumi nanane zake!
"K**a nikisema chochote ni ngumu kuamini Ili hali umenitilia mashaka we kwenye moyo wako, nafikiria ukitizama hii video utapata majibu ya maswali unayo jiuliza mwenyewe!"
Kumbe Yubeti alikua na mawasiliano na alishaa andaa Kila kitu kabla ya yeye kwenda pale hotelini alisha onana na ulinzi wa pale! Kwa vile ilikua hoteli ile ilikua na hazi ya nyota tano basi ilikua na kamera za ulinzi hivo Yubeti aliomba yeye arekodiwe kuanzia anavo ingia mbaka kutoka kwake na mwisho wamtumie video hizo!
Na ndivo kila kitu kilikwenda, Yubeti alifahamu endapo kitajulikana kile anacho kwenda kufanya itakua ngumu watu kumwamini kwamba hakufanya chochote.
Baada ya Vivian kutizama ile vision ambayo ilionekana vile vile k**a Prisca alivo simulia kila kitu ndivo ilivo onekana kwa ile video.
Vivian alijikuta mwenye kujilaumu kwa kushindwa kumwamini Yubeti mmewe, na wakati huo Yubeti alikua zake kwa bafu akijisafisha na kujipea huduma ya kwanza jeraha alipata baada ya kuzuia kisu alicho zuia kisimchome.
"Nisamehe Yubeti, kweli mimi ulinichanganya mme wangu!"
"Nilijua pengine ungehitaji kuachana na mimi baada ya mi kufanya mambo ya aibu k**a haya lakini ulicho fanya inaonyesha kabisa wewe ndio hatma ya maisha yangu mimi, nakupenda sana mke wangu!"
Ndivo alivo sema Yubeti, Wala hakujari kwa lolote! Vivian alimulukia na kumkumbatia kwa nguvu! Kumbato la huba, kumbato la kuleta hisia, kumbato lenye joto na lenye kusheheni utamu usingependa kung'atuka.
Kijijini anaoneka Prisca, kinyongo sana anatia timu nyumbani kwa mama yake na mabegi yake! Alilikimbia jiji kwa lazma, alifika na kutizama sana kinyumba alichowajengea marehemu baba yao, na kilinganisha na unyama alio fanya Yubeti pale kijijini, haijawai fanyika kabla.
"Mama kwanini hukunambia mimi!"
Aliangua kilio Prisca baada ya kumwona mama yake, alijikuta akimulauma mama yake ili hali makosa yote ni yake! Alimulaum mama yake kwa kunidanganya siku zota kuhusu Yubeti mwanae.
Aliendelea kulia akiwa amejiegemesha mwilini mwa mama yake ambae nae mawazo yalikua mbali sana. Alikumbuka miaka kadhaa iliyo pita Yubeti aliporudi kwa mara ya kwanza toka mjini akimwambia-;
"Bibi nimefanikiwa kumwona mama yangu mimi, bibi nakuaahidi nitamrudiaha hapa nyumbani na ataishi vizuri!"
Alimwapia Yubeti siku hiyo, na bibi alimtakia bahati njema. Kwahiyo kwa ujio ule wa Prisca bibi aliamini Yubeti kasha sababisha, bibi alimuuliza bintie;
"Inamaana umerudi kwangu tena au umekuja kunilaumu tu!"
"Nitaificha wapi sura yangu mimi mama! Kwanini uliruhusu mimi kwenda mjini wakati ule? Ulitakiwa kua mkali na kunizuia mimi!"
Naona ilikua ni njia pekee ya yeye kupunguza mizigo ya mabaya aliyo beba, alichagua kumulaumu mama yake kwa kila kitu.
"Asie funzwa na mamae atafunzwa na ulimwengu hivi ndivo ilivo maanishwa mama?"
"Hata mi naona!"
music Niko pale YouTube lakini Niko na page yangu and follow me, YouTube uko wimbo bomba unaitwa karibu nenda na ucheki
Endelea........!
Kwa jinsi alivo kua akilia hata mama yake alimwinea huruma, ingawa alisha mkosea sana! Alimwachia amalize kuzungumza yote anayo hitaji kuyasema Kisha akamwanbia;
"Sina namna yoyote ya kukusaidia kulingana na vile unavojiskia, hivo unatakiwa kupambana mwenyewe na hiyo hali! K**a ni maumivu sijui ni kiasi gani unapata? Lakini k**a unachochote cha kusema Ili upunguze maumivu unayo apata usisite kuzungumza! K**a ni kumulaumu mtu mlaumu kwelikweli na k**a ni kujuta na utahitaji kulia basi lia sana, jifungie ndani na ulie kwelikweli utakapo nyamaza utakua umeipata thuruhu ya tatizo lako! Kitakacho kunyamaziana ndio tiba ya maumivu unayo yapata!
"Lakini njia pekee ya kujitoa huko ni kutubu na kusahau kila kitu ukiishi k**a kiumbe mwingine ambae hajawai kuwepo duniani"
Maneno pekee ambayo mama aliona yanafaa kuzungumza kwa wakati ule katika hali k**a ile.
Ni kweli baada ya pale Prisca alijitoa mwilini mwa mama yake, aliangaza huku na kule alikuta picha ya familia! Yaani bibi, Yubeti na mkewe Vivian lakini upande mwingine kulikua napicha yake nzuri tu pia iliwekwa kwamba nae ni mmoja kati ya watu wa mle ndani.
Picha hiyo aliiweka Vivian, Prisca alijisikia tumaini kuona licha ya mambo yote bado Yubeti alijari kuhusu yeye na hata kutafuta picha zake na kumuweka kwa nyumba.
Aliingia chumbani na kujifungia mwenyewe! Nafasi yake ikiwa ni yenye kujuta kwa yote aliyo fanya, Kila akiyakumbuka ni k**a nyundo kichwani ama wembe na makali yake alichanjwa nao machoni, ama vile radi ipigayo ingali unatembea na umenyeshewa kwelikweli.
Kumbukumbu zilimrudia za upuuzi alio kwisha kuifanya kwenye maisha yake. Naweza kusema ni k**a mtu alie kua akiishi nje ya ufahamu wake sasa akili zimemurejerea na anaonyeshwa mambo yote aliyo fanya kipindi chote! Alitamani kusema si yeye, lakini hapana angekumbuka vipi mambo ambayo hakuyafanya?
"Kwanini mimi, kwanini niliishia kwenye njia hiyo? Kwanini sikujitambua wakati wote mbaka nakutwa na adhabu k**a hii!!
"Mwisho wa yote hivi ndivo ulivo amua kuniadhibu mimi Mungu baba? Na k**a nikitubu nitasanehewa mimi kweli?"
🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐
🏹Je? Akitubu atasamehewa?
Nitakwenda kuwauliza wachungaji, lakini tutapata majibu kwenye sehemu inayo fuata?
*Tukutane jumapili ijayo apa apa? STORE OF STORIES
👉 We baki na mimi!
Like, comment and share na a,usisahau a kulike ukulasa huu ili usipitwe na simulizi zangu.
Niwatakie wakati mwema na muwe na bahati njema tukutane kwenye comments
🙏🙏🙏🙏🙏
26/06/2022
MWANDISHI: Beatho Benedict.
SEHEMU YA ISHIRINI NA THERATHINI.
MAWASILIANO;
▶️WhatsApp- 0767464146.
▶️ Gmail- [email protected]
▶️ Website- storiesandscriptwriter.worldpress.com
👉TULIPOISHIA......
"Ebu, kwahiyo unataka kusema Ile mimba Prisca hakuitoa si ndiyo!"
"Iligoma kutoka?"
"Yuko wapi sasa mwanangu?"
Ikiwa ni siku inayo fuata ndio Ile ya mwanzo kabisa mwasimulizi yetu, mimi nilipo mkuta kijana nje ya nyumba yake akiwa na mwanamke alie jiita mwenyewe kua ni mama mtu!
Basi hao walikua ni Yubeti na mama yake, Prisca! Na yote uliyosoma ndiyo yaliyo pelekea kuto kua na maelewano mazur kati ya mama na mtoto yaani Prisca na Yubeti.
Endelea.........
Ni Serina alie amua kumfwa rafiki yake Prisca, amwsmbie nini walifanya kule kwa hoteli kati yake na Yubeti.
"Kumbe ulikua unafahamu siku zote kua yule ndio Yubeti, lakini hukutaka kuniambia! Kwani laki Serina?"
Akilalama Prisca baada ya kumwona rafiki yake wa siku nyingi kamtembelea.
Na hopo ndio tunapata kujua ilikuaje kule hotelini?
Baada ya maandalizi yote Prisca alifanya na kukubaliana kukutana na Yubeti kwaajiri ya faragha yao ya kwanza tangu wawe wapenzi!
Kila kitu kulikua shwali mbaka pale Yubeti alipo ingia, kwa mahaba na furaha kubwa alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu the na wakatulia Ivo kwa mda.
Na vile Prisca ni fundi, mtundu kwa maswala mazima ya chumbani hakutaka kusubiri alianza kumsaula Yubeti! Alimtoa koti lake la suti akamtoa na tai...... Lakini alipo taka kumfungua mkanda, Yubeti akamuzuia!
🤙Hello watu wangu wa nguvu mkipita pale YouTube Niko na kawimbo kangu mnaweza kukatizama kidogo channel inaitwa na utaona vingi tu uko karibuni 🎶🎶🎶🎶🎶🎶
🏹Usisahau;🤏 KU_ SUBSCRIBE
🤏 LIKE
🤏 COMMENT & SHARE
👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌👌
"Kwanini? Au mkeo hajawai kukufanyia ivi na unajiskia aibu!"
Aliuliza Prisca, lakini Yubeti hakumjibu alichukua begi yake ya mkononi maarufu k**a blufukesi na kuifungua, na alionekana kushika picha, picha flani iliyo choka kidogo, dhahiri ilionekana kua ni ya zamani kidogo!
Kwa vile alikua amemgeuzia mgongo! Prisca hakuweza kuona chochote, na Yubeti aliendelea kusimama vile kwa mda akiitizama Ile picha.
"Maisha uliyo ishi, uliishi kwasababu ya pesa, ukafanya kila kitu kwaajili ya pesa na hukuhofu chochote mbele ya pesa!"
Alisema Yubeti akiwa ameshika Ile picha na alipo geuka, aligeuka na Ile blufukesi na ilikua imekaa pesa!
"Kelvini mbona sikuelewi?"
Aliuliza kwa mshangaao Prisca, kwani Yubeti alimfahamu k**a Kelvini yeye alivo tambulishwa.
"Sijui ni kiasi gani cha pesa ulikua unahitaji katika maisha yako Ili uishi k**a wa binadamu mwenye hisia na aibu hata hofu!"
Kwa vile Prisca hakujua kinacho endelea, hakua na mda wa kuikataa Ile pesa! Na hakika zilikua millioni kadhaa.
"Sikuja kwa jambo lolote mimi apa, ila Nina jambo dog Naomba unisaidie!"
Yubeti alimkabidhi Prisca mama yake Ile picha, ni picha Yubeti alipatiwa na bibi yake, mwanzo kabisa alipo kua akimpa hadithi ya kuzaliwa kwake, picha ya Prisca kipindi angalia binti mdogo, tena angali kijijini.
Prisca alistuka sana alipo mwona mtu yule wa kwenye picha, akamwangalia Yubeti Vuzuri! Kunataswira ilimjia kichwani mwake, Kila alipo mtizama Yubeti kuanzia kimo chake, mwili wake flani sio kubwa sio dogo, bashasha na malingo yake anapo ongea lazima atenbeetembee k**a amesimama lakini pia mikono huenda kwa vitendo!
Kumbukumbu flani mfano wa radio ziligonga kichwani mwake, alikumbuka takribani miaka ishirini iliyo pita kuna mwanaume k**a huyo alisimama mbele yake namna Ile na kumulaumu sana!
"Kwasababu ya pesa, ndio unafanya yote haya! Huna hofu, huna hisia wewe? Yule mwanamke anakuhalibia maisha yako wewe! Kwanini lakini wewe, nikisema nitafanya Kila kitu angalau unidhalie uyo mtoto, mwisho wa siku umetoa mimba yangu Prisca
"Inamaana Mungu alikupa uzuri akakunyima upendo wewe! Mbona hufanani na matendo Yako we mwanamke?"
🤙Kuna online tv channel inaitwa Nikumbushe TV wapo na kule fanya kuwa na k**a kawaida like, comment, share kwenye post zao na Usisahau ku_
Alikua akilalama sana mwanaume huyo!
Hiyo ni kumbukumbu ya Prisca, lakini bado hakupata picha kamili kujua ni nani huyo mwanaume kwani ni zaidi ya miaka ishilini ilishapita tangu yote ayo yatokee.
"Unamfahamu huyo wa kwenye picha?
"Ni mtu ambae nilitamani kumfahamu na nikamtafuta kujua kuhusu yeye tangu ningari mdogo sana!
"Bibi yangu alinambia huyo ndio mama yangu! Mama alie nipatia zawadi ya jina zuri la Yubeti lakini akaninyima Kila kitu nilichostahili toka kwake kwa pumziko lote la maisha niliyo ishi!
"Anaitwa Prisca ye jina lake, k**a ukimwona mwambie natamani sana kumwona japo mara moja, na umwambie ni Yubeti ndio anataka kuona!"
Wakati Yubeti anaongea yote ayo, ilikua k**a ndoto kwa Prisca, hakuamini k**a inawezekanaj mambo yote yakaishia k**a vile!
Na Yubeti hakua na lakusubili pale k**a ni picha na pesa vyote alimwachia mama yake ambae alishindwa kabisa kufanya chochote ni k**a kupalalaizi, hakua ata na nguvu za Julia adondoshe chizi labda.
Yubeti alitoka zake, na vile alitoka akiwa anavaa Vuzuri baada ya yote yaliyo tokea, na walio mwona walimtafsiri k**a katoka kufanya maangamizi! Hasa kwa upande wa Vivian ambae alimvisha tai mmewe wakati anaondoka lakini alishangaa kuona hana tai shingoni! Mana yake k**a wamevuana nguo hakuna usalama kabisa! Hivo ndivo aliamini Vivie ama Vivian.
Na hata kule Yubeti alimwitia hakutaka kwenda kabisa. Siku iyo Yubeti alikua na kusubiri sana lakini mkewe hakutokea. Na simu yake haikupatikana.
Hapo to alipata wazo la kukagua jumbe za maandishi alizo tumiwa kwa simu yake.
Akagundua mchongo ulivuja, na k**a ulivuja basi huenda hata mkewe kapata habari! Ikambidi awai nyumbani.
Nikweli hali ya hewa haikua shwali, baada ya kiingia tu ndani na mkewe kumwona alisimama na kumnasa vibao ye kwenye shavu lake hata bila maelezo!
"Nambie umefanya nini wewe, tai niliyo kufunga nani huyo kaifungua?"
Apo Yubeti ndio akakumbuka k**a alivuliwa pale hotelini, lakini hakua na chakujiekeza
"Ivi Yubeti! Unakaribia kua chizi siyo, ivi inawezekanaje wewe kutembea na mama yako!"
"Inawezejana nishakua chizi, vipi unafikiri kwa akiri ata za kuanza kua chizi mi naweza kufanya Ivo!"
"Kwahiyo unataka kubisha sio? Basi nambie ulikua wapi leo!"
Vivian alikua kavurugwa kweli, alikwenda jikoni na kutoka na kisu na alihitaji kumdhuru nacho, lakini bahati nzuri Yubeti akiona, kisu kilikua kinaenda kumkita kifuani akakizuia kwa mkono!
🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐
🏹unataka kujua kilichotokea baada ya hapo?
Kwa wakati k**a huo Yubetiatamweleweshaje Vivian k**a hajafanya chochote na mama yake.
*Tukutane jumapili ijayo apa apa? STORE OF STORIES
👉 We baki na mimi!
Like, comment and share na a,usisahau a kulike ukulasa huu ili usipitwe na simulizi zangu.
🙏🙏🙏🙏🙏
19/06/2022
MAMA
MWANDISHI: Beatho Benedict.
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA.
MAWASILIANO;
▶️WhatsApp- 0767464146.
▶️ Gmail- [email protected]
▶️ Website- storiesandscriptwriter.worldpress.com
👉TULIPOISHIA......
Alifika mapokezi na kupokelewa vema na alipo toa maelezo akaelezwa pa kwenda!
Aliambiwa ni ghorofa ya tatu chumba number 54. Ni chumba ambacho Prisca alikupo nae alikua amekwisha jipamba akapambika!
Unaweza sema binti wa miaka 22 kumbe tayari mwanamke wa miaka 38. Alikua amevalia kagauni kafupi kaliko shindwa japo kusitiri ye mapaja yake, akiinama kidogo unaona adi nguo ya ndani! Kiufupi alitoka bomba yani!
Akiwa Bado kwa dressing table (meza ya kujitengenezea yani)
Mlango uligongwa, hakua na shaka alikua mgeni wake kaja! Na ndivyo ilivyo Yubeti alikwesha kufika pale! Chumba Namba 54, chumba kisicho na dirisha.
Wakati huo Stella alikua akijaribu kupiga gia, aki_overtake magari mwingine na kujaribu kutafuta njia za mkato Ili tu wawai!!!!!!!?
Endelea........
Licha ya jitihada zote alizo zifanya Stella, ikiwa ni pamoja na kuvunja Sheria za barabarani, lakini bado walichelewa!
Wakati wanaingia kwenye maegesho ya hoteli ile ambayo walikua na Imani kwamba ndiko Prisca anaenda kukutana na Yubeti k**a mpenzi wake bila kujua ndio mwanae.
Wakati wao wanaingia ndio kwanza Yubeti alikua tayari anatoka! Alionekana mwenye amani kiasi kwamba kashamaliza shughuri iliyo mpelekea. Alikua akiwekaweka sawa mavazi yake, na kwa mawazo ya halaka ni kwamba mavazi hayo alikua ametoka kuyavaa baada ya kuyatoa mwilini mwake.
Moja kwa Moja bila kupoteza mda alizama kwa Gali Yubeti na kusepa zake, akiwa anatoka alimpigia simu Vivian! Bila kujua kumbe Vivian kamwacha hapohapo anapo toka yeye! Vivian hakua na uwezo kabisa wa kupokea simu ile, Stella ikabidi kufanya Ivo!
"Hello shemeji!"
"Mmmmmmhh Stella!"
"Ni mimi ndio!"
"Inamaana Vivian kakuachia simu yake!"
"Ndio hayupo mbali lakini, we uko wapi?"
"K**a akija mwambie, niko na mudi nzuri leo! Mwambie atanikita maeneo!"
"Hivo tu ataelewa!"
"Ataelewa!"
_Waarabu wa pemba, hujuana kwa vilemba_ hivo ndivyo ilivyo! K**a Yubeti ama Vivian akimwambia mwingine 'tukutane maeneo' basi wao wanaelewa kipi kinamaanishwa.
"Dada, Yubeti anasema mkutane maeneo"
"Sitamani hata kumwona!"
"Usiseme Ivo, inabidi uende ukamsikilize nini anataka kusema! Tusimuhukumu kwanza wenda alikua na sababu ya kufanya yote ayo!"
"Sababu? Sababu gani zakupelekea yeye kua na mahusiano ya kimapenzi na mama yake tena mzazi!"
Hakuna alie kua na namna ya kumwamini Yubeti, isipo kua Stella tu ye aliuitaji Yubeti apewe nafasi ya kujieleza kwa yale aliyo yafanya.
Serina ye alihitaji wamwache apo akamwone rafiki Ake uko ndani lakini Vivian na ndugue Stella walikubaliana waende uko maeneo, ambalo Yubeti kasema.
Serina alishuka kwa gari na kuacha ndugu wawili wakiondoka nae alielekea ndani apate kumwona Prisca rafiki yake, Ili apate pia kujua k**a wameharibu au shetwani kashindwa kufanya kazi yake.
Lakini alikua amechelewa sana!
"Samahani, kuna rafiki yangu Yuko apa, chumba namba 54, aliniita ila bahati mbaya nimefika apo nje najaribu kupiga simu haipokelewi!"
"Ooh! Pole sana dada, mteja alie chukua chumba Iko kasharudisha funguo dakika chache tu zilizo pita, na amesha ondoka!"
Serina alibaki njia panda bila kujua ukweli ni upi? Lakini hakua na lakuendelea kumbakisha pale ikabidi aondoke, baada ya kutoka akijaribu kupiga simu ya Prisca mara kupiga lakini haikuweza kupokelewa.
Tukiachilia mbali hayo yote, hatimae ile siku, siku iliyo subiliwa kwa hamu, siku ambayo watu lakini pia yeye mwenyewe, nikiwa na maana ya Bi.Fanista akiwa ndani ya gauni lefu jeupe, maarufu k**a shera na lilikua likiburuza chini wakawepo watoto wa kushikilia lisichafuke! Suti aliyo vaa bwana harusi nahisi ilitengenezwa huko Korea kusini kwa wakali wa mitoko.
Hakika ni siku iliyo faana, nyomi ya watu mithiri ya utitiri, lakini pongezi nyingi kwa k**ati zote yalivutia mapambo, Kila sehem bomba kwa kupigia picha!
Na kana ni chakula, kulikua na chakula cha kutosha labda tumbo lako litosheke.
Ilikua ni siku ya furaha kwa familia nzima ya mzee Patrick kwamaana, hawakua wakiamini k**a ipo siku k**a hio maishani! Hawakujua kwa Mungu kila kinawezekana labda.
Kulingana na Mengi ambayo alisha kwisha kuyafanya kwenye maisha yake hakuna alie amini k**a yupo mwanaume anaweza kukaa na kufikilia sio kuoa ila japo kufanya kimada Bi.Fanista.
Lakini maajabu ya Mungu alijipatia mme wakwake mwenyewe.
Yote kwa yote, sherehe zilimalizika salama na maisha mengine yakaendelea, na mama Vivian ama bibie Fanista alikua ndani ya maisha ya ndoa lasmi! Wazazi na ndugu wa pande zote mbili wakiwa wametoa balaka zote kwao.
Zilipita karibuni wiki mbili tangu ndoa ifungwe! Ikawa ni siku ya ijumaa, ndani ya hoteli flani Bi.Fanista alipata kuonekana, na alionekana akimsubilia mtu ambae walipeana ahadi ya kukutana hapo. Mda mwingi alitizama huku na kule k**a kuna ujio wa mtu alie kua akimsubilia pale.
Haikupita mda mwingi hatimae mwanaume flani alie enda hewani kiasi, licha ya kuvaa nguo pana Bado hakuweza kuficha kifua chake kilichokosekana kukaa kwelikweli, bila shaka alikua ni mtu wa mazoezi!
Licha ya umri wake kuonekana si haba ujana unamtupa lakini bado, alionekana mjanja mjanja k**a yuko na miaka 28 hivi, ni kulingana na alivo jiweka weka.
"Hatimae tumeonana tena!"
"Mungu mkubwa Irenio, namii nashukuru kwa kunitafuta maana nilikua na deni kubwa la kulipa kwa mwanao!"
Alisema Bi.Fanista, to na mwanaume yule alie itwa Irenio na bibie Fanista alionekana kua na shauku kubwa ya kutaka kujua juu ya mambo hayo!
"Ebu, kwahiyo unataka kusema Ile mimba Prisca hakuitoa si ndiyo!"
"Iligoma kutoka?"
"Yuko wapi sasa mwanangu?"
Ikiwa ni siku inayo fuata ndio Ile ya mwanzo kabisa mwasimulizi yetu, mimi nilipo mkuta kijana nje ya nyumba yake akiwa na mwanamke alie jiita mwenyewe kua ni mama mtu!
Basi hao walikua ni Yubeti na mama yake, Prisca! Na yote uliyosoma ndiyo yaliyo pelekea kuto kua na maelewano mazur kati ya mama na mtoto yaani Prisca na Yubeti.
🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐
🏹 Je! Unataka kujua kilicho tokea kule hotelini kati ya Yubeti na mama yake Prisca?
🏹 Na vipi kuhusu Irenio, inawezekana kua ni baba wa Yubeti?
*Tukutane jumapili ijayo apa apa? STORE OF STORIES
👉 We baki na mimi!
Like, comment and share na a,usisahau a kulike ukulasa huu ili usipitwe na simulizi zangu.
🙏🙏🙏🙏🙏
11/06/2022
MAMA
MWANDISHI: Beatho Benedict.
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE.
MAWASILIANO;
▶️WhatsApp- 0767464146.
▶️ Gmail- [email protected]
▶️ Website- storiesandscriptwriter.worldpress.com
👉TULIPOISHIA......
"Baada ya mambo yote hatimae leo unaolewa, si vibaya k**a nitakupongeza! Lakini je? Unafikili nitaacha kukulaumu kwa yote uliyo nifanyia!
We mwanamke, unafikiri ni kiasi gani mi nilimpenda yule binti! Nikafanya kila kitu kwake ili atulie na mimi lakini wakini we ukaona biashara zako ndio za maana zaidi kuliko mtu kuolewa! Mbaya zaidi alishabeba hata mimba yangu nayo mkaitoa!
Nilikuwa pesa nyingi uniachie yule mwanamke we ukachukulia poa ukaniona mi fala wa kuchunwa,
Ila sawa yote anajua Mungu!"
Alishindwa kua na majibu Bi.Fanista zaidi ya Julia tu! Mbaka mpigaji alipo amua kukata simu yake kwani salio lilikua likiisha kwake wakati anae ongea nae hana Cha kumjibu!
Endelea.....
Kwa siku Ile ilipita Bi.Fanista akiwa na mawazo tele, lakini kwa siku iliyo fuataaaliaamua kumpigia simu yule mwanaume alie onekana kumulaumu sana yeye!
Nae hakuacha kupokea simu hiyo, lakini alionekana mwenye kinyongo sana na Bi.Fanista.
"Unataka kusema nini wewe, unataka kuniambia unafurahia maisha yako ama utakua na furaha na ndoa yako Ili hali umesha halibut maisha ya mabinti wengi tu!
Kwao hata kuja kua na familia ni ndoto, we ulitakiwa kufa maana umeuwa wengi pia! Si zani k**a ustahili hata kusamehewa wewe!"
Alionekana kua na hasira na kuongea mengi, na yote yalichangiwa na kukosa kwake kua na mwanamke alie mpenda sababu ikiwa ni Bi.Fanista ye kwa mapenzi yake.
"Najua nilikukosea sana Irenio, lakini nahitaji kukuomba uwe mpole angalau lipite hili la mimi kufunga ndoa!
Kikubwa naomba ujue mimba Yako haikutolewa na mwanao yupo!"
"Unasama?"
Alihamaki mwanaume huyo alie itwa Irenio ye jina lake, lakini ombi la Bi.Fanista lilikua moja! Awe mpole angalau yeye apate kufunga ndoa yake kwa amani.
Kwakweli maneno ya Irenio yalionekana kumuumiza sana Bi.Fanista, lakini kwa vile alikua mtu wa Mungu tayali! Aliamua kumushirikisha Mungu juu ya swala k**a lile.
"Eh Mungu baba mwenye haki, ni kweli mimi nastahiri kifo, nihukumu mimi kwasababu mimi sina haki ya kufanya hivo! Sistahili mimi kuishi Naomba kwa mapenzi yako ichukue pumzi yangu!"
Alilia sana Bi.Fanista pale kanisani, na aliendelea kubaki kwa mda zaidi mbaka pale Vasco alipo mpigia kujua Yuko wapi, na ndie alie kwenda kumchukua pale kwa kabisa.
"Vipi mke wangu! Mbona k**a hauko sawa?"
"Basi tu siamini k**a mimi hapa hatimae nakwenda kuishi maisha ya ndoa!"
Hivo ndivo alivo sema, hakutaka kumuweka wazi juu ya mambo yote yaliyo kua yakimsibu.
Ndani ya nyumban flani yenye hadhi ya uchumi wa kati! Ni nyumba nzuri na Kila kitu kimo kasoro alie ishi hapo alikua ni mwanaume mmoja peke yake, kilichokosekana ni mke na watoto.
Mwanaume huyo, mda mwingi akirejea nyumbani kwake anayo picha moja aliyoiweka ukutani kwenye chumba ambacho ye analala! Picha kubwa ambayo alionekana kua na kumbukumbu nayo isiyo futika, kumbukumbu na mtu alie pichani. Pichani alilia ni mwanamke mrembo sana, nilipo itizama picha Ile kuanzia miguuni na kwa vile alivalia suruali, suruali flani ya kubana huitwa modo na wajanja wa kijijini! Jambo ambalo lilifanya nisipate taabu kugundua yaliyomo.
Ye alikua na guu la bia, nilivo panda kidogo kwa paja tayali niliaza kumpa vyeo muumbaji! Lakini nilipo fika kwa kiuno nikagundua kuna vinono endapo mmiliki ni mpishi mzuri. Unafikiri niliishia hapo, nikapanda kidogo kwa tumbo, apo nikabaki na maswali! Na mduwao nikijiuliza hio pisi kali hua inakula tongue moja kwa siku ama? Kwamaaana kalibinyia kwa ndani ye katumbo lake na mbaya zaidi ye hakusitiri na chochote maeneo hayo zaidi alikuja kusitiri chuchu zake maana apo kifuani kijana wa kuanzia 2002 akiona lazima ajisaidie mwenyewe na kwa mwanaume rijali lazima kudindisha mkonga.
Nikaendelea kupanda nikatua shingoni apo palikua kawaida, labda kipindi Cha ukuaji walimbebesha sana ndoo za maji shingo ikashindwa kurefuka.
Lakini nilistuka sana nilipomwangalia usoni pake! Alikua ni Prisca, mwite Recho ama mama yake na Yubeti.
Maskini, mapenzi ni Nini?
Irenio alikua akilalama kumbe mwanamke aliekua akimpa uchizi ni Prisca.
Mda mwingi alitumia kuzitizama picha za mwanamke alie mpenda, mwanamke alie amini ni mke wa maisha yake Ili hali mwanamke mwenyewe alikua mdangaji.
Serina baada ya kuona mambo hatarishi yanaweza kutokea mda wowote akaamua kumpigia simu Prisca ajue anampango gani aswa na Kelvini wake ambae hakumjua Bado k**a ndio Yubeti mwanae!
Lakini naweza kusema alikua amechelewa tayali! Baada ya simu kupokelewa alimskia Prisca akisema-;
"Samahani Serina, tutaongea badae ngoja nijiamdae kumpokea me wangu kadai yupo njiani!"
"We Prisca!"
Simu ilikatwa na alipo jaribu kupiga tena simu haikupokelewa akatuma sms kumjuza k**a Kevin ndio Yubeti mwanae lakini Prisca hakua na mpango na kusoma jumbe zake alicho waza yeye ni kula rahaa na mpenzie alie kwisha mtaarifu kua yupo njiani.
Serina akaona amtafute Yubeti mwenyewe, lakini Bado alisha kwisha kuchelewa maana simu ya Yubeti haikua hewani kabisa.
Alianza kuhisi akili yake haina akili! Ni k**a alichanganyikiwa, lakini baadae akapata wazo labda amwendee Vivian amweleze ukweli wote wa mambo, licha ya kwamba hakujua ataanzaje kumweleza na atampata wapi kwa mda huo?
Alichukua boda moja kwa moja Hadi kwenye maduka yao, na k**a bahati alimkuta Vivian nae akiwa na ndugue Stella ndio alikua anatoka, inamaana angechelewa kidogo asinge mkuta...
Kulingana na Presha aliyo kua nayo alijikuta karopoka kila kitu! Vivian nae akajikuta anapandwa wazimu lakini mdogo wake Stella akamsihii aweze kua mpole ila watafute namna ya kuwasiliana nao.
"Ivi kweli Yubeti ni wakufanya upuuzi k**a huu kweli!"
Alikua akilalama Vivian, wakihangaika bado kupiga simu zao bila mafanikio.
"Wewe siumesema uliwasiliana na mama yake kabla akiwa kwenye hiyo hoteli?"
Aliuliza Stella na Serina aliitikia kwa kichwan kuashilia ndio! Na Stella alionekana kua na wazo, nae si mtoto wa jiji, alicho fanya ni kufwatilia kwa mtandaon simu hio ilipigwa kutokea wapi na alipo para tu eneo ilipo pigwa simu! Basi akajua pia ni hoteli gani wapo, hivo akaomba waongozane huko halakat....
Ni kweli pia Yubeti alionekana, kiingia ndani ya hoteli flani yenye hadhi ya nyota tano akiwa na begi lake la mkononi maarufu k**a blufukesi. Alitinga ye suti nyeupe kwa langi akini shati jeusi bila tai chini moka iliyo enda kwa chuo mwendo wa kibosi alitembea, alionekana anakwenda amejipanga kwa jambo analo liendea.
Alifika mapokezi na kupokelewa vema na alipo toa maelezo akaelezwa pa kwenda!
Aliambiwa ni ghorofa ya tatu chumba number 54. Ni chumba ambacho Prisca alikupo nae alikua amekwisha jipamba akapambika!
Unaweza sema binti wa miaka 22 kumbe tayari mwanamke wa miaka 38. Alikua amevalia kagauni kafupi kaliko shindwa japo kusitiri ye mapaja yake, akiinama kidogo unaona adi nguo ya ndani! Kiufupi alitoka bomba yani!
Akiwa Bado kwa dressing table (meza ya kujitengenezea yani)
Mlango uligongwa, hakua na shaka alikua mgeni wake kaja! Na ndivyo ilivyo Yubeti alikwesha kufika pale! Chumba Namba 54, chumba kisicho na dirisha.
Wakati huo Stella alikua akijaribu kupiga gia, aki_overtake magari mwingine na kujaribu kutafuta njia za mkato Ili tu wawai!!!!!!!?
🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐🌐
Next episode coming 🔜🔜🔜🔜
Je unafikiri watawai❓
👉 We baki na mimi!
Like, comment and share na a,usisahau a kulike ukulasa huu ili usipitwe na simulizi zangu.
🙏🙏🙏🙏🙏
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Website
Address
Mbeya
Opening Hours
| Friday | 20:00 - 23:00 |
| Sunday | 19:30 - 12:00 |
