07/01/2025
BRAIN FOOD
“Technology is best when it brings people together.” ...
07/01/2025
The less you care, the more happier you become
BRAIN FOOD
“Technology is best when it brings people together.” ...
14/05/2022
Wauguzi na wakunga hospitali ya wilaya ya Chunya wameadhimisha siku yao kwa kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi na wakunga duniani hufanyika kila inapofika Mei 12 kila mwaka ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa, “Wauguzi ni sauti inayo ongoza, wekeza kwenye uuguzi na heshimu haki na kulinda afya kwa wote."
Akizungumza wakati wa kuwapatia zawadi wagonjwa, Afisa Muuguzi katika hospitali ya wilaya, Dkt. Osman Simbeye amesema, wanayo furaha kuadhimisha siku hii na kumkumbuka mwanzilishi wa siku ya wauguzi duniani Mama Florence Nightingale.
“Ni siku yetu ya furaha kwa kuhudumia wagonjwa ndio maana mnaona tunapita kwenye wodi humu kuwaona na kuwapa zawadi." Alisema Simbeye.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaasa wauguzi wote kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagongwa wote wanaokuja kupata huduma katika hospitali hiyo ya wilaya.
“Niwaombe sana wauguzi wenzangu tuhakikishe tunatoa huduma bora na stahiki kwa kila mgongwa anayefika hapa hospitalini,” alisema simbeye.
Naye Kaimu Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Dkt. Issa Mbande amesema, wao k**a Halmashauri wameamua kufanya maadhimisho hayo kwa kuwapatia zawadi wagonjwa waliopo wodini.
"Tumefanya hivi kwa ajili ya kuonesha upendo kwa wagonjwa wetu na kumuenzi Mama Florence Nightingale mwanzilishi wa siku hii muhimu kwa wauguzi.
“Sisi kawa Wauguzi tunayo furaha kuadhimisha siku hii muhimu na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu." Alisema Dkt. Mbande
31/12/2021
Kheri ya mwaka mpya 2022
25/12/2021
Pokea salamu za kheri ya sikukuu ya Krismas kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya
Je unapata changamoto yeyote ya namna bora ya kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako? Fika ofisi ya TEHAMA wilaya kupata msaada wa kitaalam bure kabisa.
TEHAMA kwa maendeleo yako na nchi kwa ujumla
WAZIRI MKUU AKABIDHI MAGARI 184 KWA HALMASHAURI NCHINI.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 21, 2021 amekabidhi jumla ya magari 184 kwa maafisa elimu wa Halmashauri ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibasila, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri zilizopokea magari zizingatie taratibu za serikali katika matumizi na matengenezo ya magari hayo na kuhakikisha magari hayo yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Maafisa elimu na wakurugenzi wa Halmashauri Magari haya mmekabidhiwa tukute gari limepaki kisa limekosa ‘Service’ utakuwa umekosa kazi, lazima tuambiane ukweli, magari haya lazima yafanye kazi kwa zaidi ya miaka mitano hadi sita”
Amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya Maafisa Elimu wa msingi wa Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara. Na kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia mchakato wa ununuzi wa magari mengine 184 yatakayogawiwa kwa Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri zote pamoja na magari matatu kwa utekelezaji ngazi ya Wizara.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema Magari hayo yamenunuliwa na Serikali kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Sekta ya Elimu (EP4R) kwa gharama ya shilingi bilioni 16.4.
19/12/2020
Tembelea tovuti ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya ambayo ni www.chunyadc.go.tz kuona majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa shule zilizopo ndani na nje ya wilaya ya Chunya. Pia utaweza kupata join instruction forms kwa shule husika aliyepangiwa mwanao
Mwanzo A default home page
Wanachunya tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa kwa kunawa mikono yetu kwa maji tiririka na kwa sabuni jwa angalau sekunde 20, tuepuke mikusanyiko isiyo yalazima.
.
Namba za kupiga simu bure endapo utaona una dalili au utaona mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Korona
0800110124
0800110125
Namba hizi kupiga Ni bure hata k**a hauna salio kwenye simu yako.
DALILI ZA UGONJWA WA CORONA
Dalili zionekanazo mara kwa Mara:
• Homa
• Kikohozi kibichi
• Uhemaji wa tabu
• Maumivu ya mwili
• Kuuma kwa koo mfano wa
matonses (tonsillitis)
• Kukosa hamu ya kula
Dalili za mara chache:
• Kuhara
• Kutapika
• Kichwa kuuma
• Kukohoa damu
• Maumivu ya kifua
Nani hupatwa na korona?
• Watu wote (wakike kwa kiume) waweza
kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.
KINGA:
• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa
Kirusi cha korona katika mwili wa
binadamu:
• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Telephone
Website
Address
Mbeya
