Salvation is the best sustainable choice

Salvation is the best sustainable choice

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Salvation is the best sustainable choice, Library, P. O. BOX 225, Mbinga.

05/11/2024

Bwana Yesu asifiwe;
Mtu yeyote anayependa kuwa na afya nzuri ya kimwili halafu Hana kiu na njaa ya kula chakula hawezi kuipata afya Bali atakuwa dhaifu sana.
Vilevile katika ulimwengu wa ROHO, mtu ambaye Hana kiu na njaa ya kula chakula Cha rohoni yaani NENO LA MUNGU na maombi atakuwa dhaifu sana kiasi Cha kwamba ataangushwa Kwa urahisi na adui shetani.

NB:PENDA SANA KULA CHAKULA CHA ROHONI ILI UWE NA AFYA / UNENEPE ROHONI.
Mungu akubariki sanaaaa!!

23/05/2022

SOMO: CHUKI YA WAKUCHUKIAO.

BAADA YA GEREZA KUNA KITI CHA ENZI KINAKUSUBIRI.
Mwanzo 41: 37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu k**a huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima k**a wewe. 40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. 41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. 42 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.

WALIOKUCHUKIA UTAWALISHA, USIWACHUKIE.Mwanzo 45:1 Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. 2 Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. 3 Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. 4 Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. 5 Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

NJAMA ZAO MBAYA JUU YAKO ZINAKWENDA KUWAANGAMIZA. Daniel 6:1 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote;2 na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu kwao, mfalme asipate hasara. 3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote. 4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumsh*taki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. 5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumsh*taki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake. 6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele. 7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba. 8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, k**a ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.

SIMBA HAWATAKUTAFUNA WEWE, BALI WALIOPANGA HILO SIMBA HAO HAO WATAFUTA KUMBUKUMBU LAO.19 Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. 20 Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? 21 Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. 22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. 23 Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danieli katika lile tundu. Ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.24 Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomsh*taki Danieli, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.

BAADA YA CHUKI YAO MUNGU WAKO ATAABUDIWA NA WOTE.25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu. 26 Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho. 27 Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba.28 Basi Danieli huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.

21/05/2022

SOMO: CHUKI YA WAKUCHUKIAO KWA AJILI YA KITU MUNGU AMEWEKA JUU YAKO IMEBEBA NGUVU YA KUKUPELEKA KWENYE KITI CHA HESHIMA, USIIANGALIE CHUKI MWANGALIE MUNGU.

Mwanzo 37:5 Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; 6 akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. 7 Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. 8 Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake.23 Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa,
24 wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji.25 Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. 26 Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? 27 Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu.

INAKUINGIZA NYUMBANI MWA POTIFA. 1 Basi Yusufu akaletwa mpaka Misri naye Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari, mtu wa Misri, akamnunua mkononi mwa hao Waishmaeli waliomleta huko. 2 Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.

UNAINULIWA NYUMBANI MWA POTIFA. 3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.

USIMTAZAME MKE WA POTIFA KWA SURA KUKUANGAMIZA, BALI JUA ANAFANYIKA NJIA ANAKUSUMA UFIKE HARAKA KWENYE KITI CHA HESHIMA.18 Ikawa nilipopaza sauti yangu, nikalia, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.19 Ikawa bwana wake aliposikia maneno ya mkewe aliyomwambia, akisema, Mtumwa wako amenitendea mambo k**a haya, hasira yake ikawaka.20 Bwana wake akamtwaa Yusufu, akamtia gerezani, mahali walipofungwa wafungwa wa mfalme, naye akawamo humo gerezani.21 Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. 22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya.

13/11/2021

DINI NI MBAYA,TENA HATARI KULIKO SHETANI,NI RAHISI KUMTOA PEPO NDANI YA MTU,SIO KUITOA DINI NDANI YA MTU.

Dini inawekeza rohoni kwa mafundisho yake ya uongo,NA WATU WANAPENDA KUDANGANYWA KULIKO KUAMBIWA UKWELI.

Mfumo wa kidini unapoteza raia wengi wanaelekea jehanamu bila kujua k**a ng'ombe anavyopelekwa machinjioni akiwa hajui,ndivyo dini inavyoua raia wengi.

DINI IMEMFUNDISHA MTU KUABUDU SANAMU WAKATI MUNGU AMEKATAZA,DINI INABATIZA VITOTO VICHANGA WAKATI MUNGU ANASEMA,Aaminiye ndiye anapaswa kubatizwa tena ubatizo wa maji mengi kwa kuzamishwa.

MAFARISAYO WALIMSH*TAKI YESU KWA UONGO KWAAJILI YA KUTETEA DINI ZAO,WALIPOONA WATU WENGI WANAMWENDEA YESU,WALIMSULUBISHA KWA HILA,WAKAWA TAYARI KUCHUKUA LAANA YA DAMU YAKE ILIMRADI TUU DINI ZAO ZIWE SALAMA.

Dini huondoa ufahamu ili usimjue Mungu,acha kushikilia dini Yesu anakupenda,mwamini Yesu akuweke huru ili uifahamu Kweli ya Mungu nawe uwe huru kwelikweli.

YESU NDIYE NJIA,KWELI NA UZIMA,HAKUNA MTU ATAKAYEMWONA MUNGU BILA KUPITIA KWAKE.

12/11/2021

Yakobo alikuwa na watoto wangapi?

Yakobo, mjukuu wa Ibrahimu, alipewa neema na Mungu ya kuwa na Watoto 13, Kati ya hao 12 ni wa kiume na 1 wa k**e aliyejulikana k**a Dina.

Yakobo alikuwa na wake wawili, Na hao wake zake kila mmoja alikuwa na kijakazi wake mmoja, ambao baadaye walikuja kufanyikiwa kuwa masuria wa Yakobo.

Mke wa kwanza aliitwa Lea, Na mke wa pili aliitwa Raheli. Kijakazi wa Lea aliitwa Zilpa Na kijakazi wa Raheli aliitwa, Bilha.

Wafuatano ni Watoto wa Yakobo waliozaliwa na Lea.
Rubeni
Simeoni
Lawi
Yuda
Isakari
Zabuloni
Dina(wa k**e)
Wafuatao ni Watoto wa Yakobo waliozaliwa na Raheli.
Yusufu
Benyamini
Wafuatao ni Watoto wa Yakobo waliozaliwa na Zilpa (Suria)
Gadi
Asheri
Wafuatao ni Watoto waliozaliwa na Bilha (Suria)
Dani
Naftali
Habari yote ya uzao wao utaipata katika kitabu cha Mwanzo, kuanzia sura ya 29 na kuendelea.

Mwanzo 29:31 “Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.

32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.

33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.

34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.

35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa…………..”

Bwana akubariki.

12/11/2021

Mwanzo 35 (Maswali & Majibu)

[1] Nani wahusika wakuu katika sura hii? (Mwanzo 35) Yakobo, Debora, Rebeka, Raheli, Benyamini, Reubeni, Bila, Isaka, Esau.

[2] Yapi mawazo makuu katika sura hii? (Mwanzo 35)

(a) Mungu anamwamuru Yakobo akae Betheli, na kujenga madhabahu huko (1)
(b) Yakobo anaamuru familia yake iondoe sanamu: wajisafishe, na kubadili mavazi, katika maandalizi ya kwenda Betheli. Hili wanatii. (2-3)
(c) Kisha Yakobo anazika miungu yake migeni chini mti karibu na Shekemu, na kambi linasafiri kwenda Betheli (4)
(d) Wakanaani wanaogopa familia ya Yakobo, hivyo hakuna anayethubutu kuwafuatilia katika safari yao (4)
(e) Wanapofika Betheli, Yakobo anajenga madhabahu na kupaita mahali hapo El-Bethel (6–7). Debora, mjakazi wa Rebeka, anakufa, naye anazikwa chini ya Betheli chini ya Mwaloni. (8)
(f) Mungu anamtokea Yakobo, anathibitisha jina lake kuwa Israeli, na kurudia upya ahadi (9-13)
(g) Hivyo anajenga mnara, anamimina mafuta hapo, na kupaita mahali hapo Beth-eli (14-15)
(h) Wanaposafiri kutoka Beth-el kwenda Ephrathi; Raheli anakufa akiwa anamzaa Benyamini (16-18)
(i) Raheli anazikwa akiwa njia kuelekea Ephrathi (yaani, Bethlehemu). ~ (19)
(j) Naye Yakobo anajenga mnara kwenye kaburi lake, ambao ni mnara wa kaburi la Raheli hadi leo. (20)
(k) Reubeni analala na mkewe baba yake: analala na Bilha suria wa babaye (22)
(l) Sura hii hubainisha orodha ya wana kumi na mbili wa Yakobo (23-26)
(m) Yakobo anamtembelea Isaka, babaye, huko Mamre, au Kirjath Arba (yaani, Hebroni), alikokuwa ameishi Ibrahim una Isaka (27)
(n) Sura hii huhitimisha kwa taarifa ya mauti ya Isaka na tukio lililofuatia la maziko ya wanawe, Yakobo na Esau (28–29).

[3] Ni tukio gani la Biblia linalofanyika/lililotajwa katika sura hii? (Mwanzo 35)

MATUKIO YANAYOFANYIKA:
(a) Yakobo anahamia Betheli • Mwa 35:1–7
(b) Mlezi wa Rebeka anafia Betheli • Mwa 35:8
(c) Mungu anatokea Betheli • Mwa 35:9–15
(d) Raheli anamzaa Benyamini halafu anakufa • Mwa 35:16–20
(e) Reubeni analala na Bila • Mwa 35:21–22
(f) Isaka anafia Hebroni • Mwa 35:27–29

MATUKIO YALIYOTAJWA:
(a) Lea anawapata wana wanne • Mwa 29:31–35 (Mwa 35:23)
(b) Lea anawapata wana watatu wengine • Mwa 30:17–21 (Mwa 35:23)
(c) Raheli anamzaa Yusufu• Mwa 30:22–24 (Mwa 35:24)
(d) Bila anawapata wana wawili • Mwa 30:5–8 (Mwa 35:25)
(e) Zilpa anapata wana wawili • Mwa 30:10–13 (Mwa 35:26)

[4] Nini ambacho Mungu alitamani Yakobo afanye? Mungu alimwambia Yakobo arudi wapi? (1) Aende kuishi Betheli.

[5] Je umewahi kupata uzoefu wa “Kurudi Betheli”? Jadili.

• Mungu anamwita kila mmoja wetu “arudi Betheli" (v. 1), mahali pa njozi na nadhiri; mahali pa maombi na saumu. Mtu anapotanga mbali k**a ilivyokuwa kwa Yakobo, hana lolote la kufanya isipokuwa kurejea mahali pa wakfu na kufanya upya nadhiri zake.

• Najua hili kutokana na uzoefu wangu binafsi na Bwana. Kumbuka: “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” (Isaya 59:1–2)

[6] Yakobo alijiandaaje kwa ajili ya safari hii? Aliwahimiza watu wa nyumba yake wafanye nini? (2-4) Waweke mbali sanamu, na kujisafisha, na kubadili mavazi yao.

“Matarajio ya kukutana na Mungu huko Betheli ilisababisha kazi makini ya matengenezo. Kulikuwepo mambo mengi ya kufanywa kabla Yakobo na nyumba yake kuwa tayari kukutana uso kwa uso na Bwana (angalia Amosi 4:12; 1 Yohana 3:3). Nje ya mazingatio kwa ajili ya wakeze, Yakobo alikuwa amevumilia uwepo wa sanamu katika mahema yao. Miungu hii migeni pengine ilihusisha terafimu ambayo Raheli alikuwa ameiba kutoka kwa babaye (Mwa. 31:19), sanamu za watumishi wake, na zingine zilizomilikiwa na wanawe kupitia nyara za Shekemu.”

“Utakaso wa nje wa mwili na kubadilisha mavazi mengine kuliwakilisha utakaso wa kiroho na kimaadili wa akili na moyo (angalia Isa. 64:6; 61:10). Huduma ya Mungu haipaswi kuanzwa bila maandalizi husika (angalia Luka 14:28).” (The Seventh Day Adventist Bible Commentary, Vol. 1/ Genesis 35:1–2)

 (kwa taarifa zaidi angalia sehemu ya 1-BSG-35T katika Mwongozo huu)

[7] Mungu alimwambia nini Yakobo alipomtokea tena? (10-12) Alimbariki na kurejesha upya agano.

[8] Ni vidokezo gani mahususi vilivyorudiwa katika agano hili lililofanywa upya katika 35:9-12?

(a) “Jina lako ni Yakobo; … lakini Israeli litakuwa jina lako.”
(b) “Mimi ni Mungu Mwenyezi.”
(c) “uzidi ukaongezeke”
(d) “Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako,” na
(e) “wafalme watatoka viunoni mwako.”
(f) “Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.”

Sasa, hebu tufanye marudio ya kile ambacho Mungu anamwahidi Yakobo hapa:

(a) Jina jipya,
(b) Uhakikisho,
(c) Kuzaa,
(d) Umati mkubwa,
(e) Mataifa & Wafalme kutoka kwa Ibrahimu >>>Isaka >>>Yakobo,
(f) Nchi/ Umiliki.

Linganisha maandiko yafuatayo:

(a) Mwa 26:23–24
(b) Mwa 28:14a
(c) Mwa 35:11b
(d) Mwa 46:3
(e) Mwa 48:3–4
(f) Law 26:9

[9] Nini kilitokea baada tukio hili la kukutana na Mungu? Yakobo aliitikiaje? (14-15)

 Mwanzo 35:14–15 — 14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake. 15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.

[10] Nini kilimtokea Raheli wakati ule Benyamini alipozaliwa? (16-19) “akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.”

[11] Ni upotevu gani mkuu uliompata Yakobo alipokaribia Bethlehemu? (19) Kifo cha Raheli.

[12] Raheli alifia wapi? Alizikwa wapi? (17–19) Familia hii inaposafiri kutoka Beth-eli hadi Ephrathi. Raheli alizikwa akiwa njiani kuelekea Ephrathi (yaani, Bethlehemu).

[13] Yakobo alikumbukaje kifo cha mkewe mpendwa? (20) Alisimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

[14] Ni jina gani lingine alilopewa Benyamini? (18) Ben-oni

“Kuzaliwa kwa Benyamini kuliashiria utimizwaji wa shauku ya Raheli katika kumpatia jina Yusufu, kwamba Mungu angempatia mwana mwingine (angalia katika sura ya 30:24). Anapokuwa katika hali ya kufa wakati wa kuzaa anamwita mwana huyu Ben-oni, “mwana wa uchungu wangu” au “mwana wa msiba wangu.” Katika mazingira haya, kwa mtazamo wake, lilikuwa jina sahihi.” (SDABC1/ Genesis 35:18)

[15] Ni dhambi gani aliyotenda Reubeni? (22) Alilala na suria wa Yakobo na mjakazi wa Raheli, Bila. Huu ulikuwa uhusiano mbaya sana; kwa vile Masuria walikuwa k**a wake halali.

“Hili liliongeza mateso yake (Yakobo), na kuifanya maradufu, kumpoteza Raheli kwa mauti, na mjakazi wake Raheli, suria wake, kunajisiwa na mwanawe, na ambaye inawezekana kabisa aliachana naye baada ya hapo. Hili, japo ni dhambi ovu sana ya mwanawe, lakini inaweza kuchukuliwa k**a marudi kwa Yakobo, kwa kuwachukua masuria.” (John Gill)

[16] Yakobo alikuwa na jumla ya wana wangapi? (22) Kumi na mbili

 Wana wa Lea: Reubeni (mwana wa kwanza wa Yakobo), Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni.
 Wana wa Raheli: Yusufu na Benyamini.
 Wana wa Bila ~ (mjakazi wa Raheli): Dani na Naftali.
 Wana wa Zilpa ~ (mjakazi wa Lea): Gadi na Asheri.

Palikuwa na wana wa Yakobo waliozaliwa huko Padan Arani.
 Zingatia: Dina hatajwi hapa, kwa sababu hakuwa kiongozi wa kabila.

[17] Je ni umbali gani kusini alikoenda Yakobo? (27) Mbali kadiri ya Mamre, au Kirjath Arba (yaani, Hebroni),

[18] Akina nani waliokaa huko? (27) Wazee wake zamani: Ibrahimu na Isaka. Pengine Yakobo alikufa miaka mitatu baadaye.

[19] Sura hii inahitimishaje? (28-29) Sura hii huhitimishwa kwa taarifa ya mauti ya Isaka na tukio lililofuata la maziko kutoka kwa wanawe, Yakobo na Esau.

Esau na Yakobo wakamzika. “Esau na Yakobo sasa walikuwa wamepatana kikamilifu kwa miaka 23. Hivyo si ajabu kumwona Esau akiungana na Yakobo katika desturi ya mwisho kwa ajili ya baba yao waliyemheshimu. Katika mazingira ya namna hiyo Isaka na Ishmaeli alikuwa ameshiriki katika maziko ya Ibrahimu (sura ya 25:9). Isaka alikuwa mtauwa na mwenye kujisalimisha kwa unyenyekevu mbele ya Mungu, mchangamfu na mkarimu kwa wanadamu wenzake. Ikilinganishwa na ile ya Yakobo mwanawe, tabia yake mwenyewe ilikuwa bora zaidi.” (SDABC1/ Genesis 35:29)

Less
MORE FROM MWANZO

Mwanzo 41 (Maswali & Majibu)
November 22, 2018 • Mwongozo wa Biblia.

Mwanzo 38 (Maswali & Majibu)
November 19, 2018 • Mwongozo wa Biblia.

Mwanzo 37 (Maswali & Majibu)
November 18, 2018 • Mwongozo wa Biblia.

19/11/2020

[11/19, 3:53 PM] +255 713 957 050: _*HATUA ZA KUFUATA TUNAPOKUWA TUNAFANYA MAOMBI YA KUMUGUSA MUNGU:*_

_*I.* Hatua ya KWANZA; Kuomba rehema mbele za Mungu; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 1 Yohana 1:9_
[11/19, 3:55 PM] +255 713 957 050: _*II* . Hatua ya PILI; Amini kwamba Mungu yupo na huwasikia wale wamuombao; “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Waebrania 11:6. “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” *Marko 11:24.*_
[11/19, 3:57 PM] +255 713 957 050: _*III.* Hatua ya TATU; Omba kwa kutumia jina la Yesu. Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. *Yohana 14:13-14.*_
[11/19, 4:00 PM] +255 713 957 050: _*IV.* Hatua ya NNE; Mahali pa kuombea, Unaweza kuombea mahali popote penye utulivu mfano chumbani au sehemu yoyote iliyo na utulivu; “Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.” *Mathayo 6:6*_
[11/19, 4:04 PM] +255 713 957 050: _*V.* Hatua ya TANO; Muda wa kuomba unaweza kujipangia kulingana na muda wako lakini Biblia inasisitiza kiwango cha chini cha Muombaji angalau iwe SAA moja; “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?” *Mathayo 26:40*_
[11/19, 4:07 PM] +255 713 957 050: _*VI.* Hatua ya SITA kusimamia Neno la Mungu (kuomba kwa kutumia Neno la Mungu); “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.” *Yohana 15:7,* “Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.” *Yeremia 1:12*_
[11/19, 4:09 PM] +255 713 957 050: _*VII.* Hatua ya SABA na ya mwisho kwa maandalizi yangu ni Kushukuru; “Dumuni sana katika kuomba, mk**esha katika kuomba huku na shukrani” *Kolosai 4:2.* “Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, k**a vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.” *2 Timotheo 1:3*_
[11/19, 4:14 PM] +255 713 957 050: _*AINA ZA MAOMBI YANAYOMGUSA MUNGU:*_

_*1* . Maombi ya Usiku au alfajiri: Haya maombi ukisoma vifungu vifuatavyo vizuri, utagundua ni Maombi yanayofungua vifungo mbalimbali na kumuweka mtu kuwa huru zaidi, naomba mpitie vifungu hivyo, ili maswali yapatikane._

_“Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.” *Mwanzo 32:24-28*_
[11/19, 4:16 PM] +255 713 957 050: _“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.” *Luka 6:12*_

_“Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.” *Marko 1:35*_

_“Na alipokuwa akifikiri haya akafika nyumbani kwa Mariamu, mamaye Yohana, ambaye jina lake la pili ni Marko; na watu wengi walikuwa wamekutana humo wakiomba.” *Matendo ya Mitume 12:12*_
[11/19, 4:18 PM] +255 713 957 050: _“Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.” Matendo ya *Mitume 16:25-26*_
[11/19, 4:20 PM] +255 713 957 050: _*2.* Maombi ya kufunga: Haya Maombi yanaleta majibu haraka kuliko tunavyofikiri, mara nyingi hutupa Neema na kibari Mahali ambapo hatustahili kupata uhitaji wetu, na pia ni Maombi yanayotuepusha na majaribu mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Somo maandiko hapa chini._

_“Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.” *Kutoka 34:28*_

19/11/2020

KWANINI KITABU CHA KUMBUKUMBU LA TORATI?

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Leo ninazungumzia Kitabu cha Kumbukumbu la torati.

Tunafahamu kwamba kitabu cha Mwanzo kinazungumzia historia ya uumbaji pamoja na matukio ya awali ya wanadamu na jinsi walivyokuwa na uhusiano na Muumba wao, pia Kitabu cha Mwanzo kinazungumzia jinsi wanadamu walivyoanza kukengeuka na kufuata uovu badala ya utakatifu. Lakini pia kitabu hicho kinazungumzia Mwanzo wa Taifa la Israeli na jinsi walivyokwenda Misri.

Tunafahamu kuhusu kitabu cha Kutoka kwamba kinazungumzia Waisraeli kutoka utumwani Misri na katika Kutoka huko Misri walipewa Sheria na taratibu za kutembea nazo ili mataifa wengine wajifunze kwa Israeli jinsi ya Kumcha MUNGU.

Kitabu cha Mambo ya walawi kinazungumzia ukuhani na jinsi ya kufanya mapenzi ya MUNGU.

Kitabu cha Hesabu kinaendeleza safari ya Waisraeli ya Miaka 40 Jangwani kikianza na kuhesabiwa kwao idadi kulingana na kila kabila.

Baada ya kitabu cha Hesabu kinafuata Kitabu cha Kumbukumbu la torati.

Kitabu hiki kimeandikwa na Musa k**a ilivyo kwa vitabu vinne vya kwanza vya Biblia, lakini Mwishoni mwa kitabu hicho hajaandika Musa bali wateule wa MUNGU walioishi na Musa katika kipindi chake cha Mwisho cha uhai Duniani, inawezekana ni Joshua au wengine waliofuata.

Musa katika kitabu cha Kumbukumbu la torati alikuwa anaongea na kizazi kipya, maana waliotoka Misri wakiwa watu wazima wakati huu walikuwa wameshakufa(Kwa kosa la kuabudu ndama, wakati Musa amepanda Mlimani kukutana na MUNGU',Angalia Kutoka 32:1........)

Wakati huu watu waliotoka Misri wakiwa watu wazima walikuwa ni Musa, Joshua na Kalebu tu. Kipindi hiki wallikuwa jirani na Mto Yordani ili wakivuka wanafika Kaanani(Hata Musa hakuvuka Yordani kwa kosa la kutokumwamini MUNGU. angalia Hesabu 20:12)

Sasa katika kitabu cha kumbukumbu la Torati ambacho ndicho Mimi nakizungumzia leo kinaanza Musa akizungumza maneno haya '' BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao. Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu. BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi. BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, k**a alivyowaahidi.-Hesabu 1:6-11''

Huu sasa ulikuwa ni mwaka wa 40 tangu Watoke Misri

Kumb 1:3 '' Ikawa mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli k**a yote aliyopewa na BWANA ya kuwaamuru; ''

Kwanini kinaitwa kitabu cha Kumbukumbu la torati?

Kinaitwa kitabu cha kumbukumbu la Torati kwa sababu kinazungumzia mambo yote pamoja ya tangu Waisraeli wanatoka Misri hadi mto Yordani, ili wakivuka wanaangia nchi yao.

Kitabu cha Kumbukumbu la torati kinarudia yaliyofanyika kutokea kitabu cha Kutoka, Mambo ya Walawi na Hesabu.

Maana yake yanayozungumzwa katika kitabu cha kumbukumbu la torati yana chanzo chake kutoka vitabu vitatu vya kabla yake na mengine ni ufunuo wa wakati huo huo.

Ujumbe huu mimi Peter nilipewa na ROHO wa MUNGU k**a ufunuo na sasa ndio nataka ujue kiini cha somo la leo.

Tunafahamu kwamba Waisraeli zaidi ya Milioni 2 walitoka Misri lakini watu wazima waliotoka Misri hadi kuingia Kaanani walikuwa wawili tu yaani Joshua na Kalebu.

Safari ya Wana wa Isareli kutoka Misri kwenda Kaanani inafananishwa na safari ya wateule wa MUNGU waliookolewa na Bwana YESU ya kutoka duniani kwenda uzima wa milele.

Waisraeli waiotoka Misri hadi Kaanani walikuwa wawili tu, naamini Wateule wa MUNGU watakaofika uzima wa milele ni wengi sana lakini ni muhimu sana tukajifunza vyanzo vilivyosababisha Waisraeli waliokoka kutoka Misri wakashindwa kufika nchi ya ahadi.

Andika kwa makini katika moyo wako mambo haya ili wewe katika safari ya uzima wa milele usiishie njiani.

Kuna mambo mengi yaliyosababisha waisraeli wasifike Kaanani isipokuwa hao wawili.

Biblia imeyaweka vizuri sana mambo hayo yaliyosababisha waisraeli japokuwa wameokoka k**a wewe lakini hawakufika kaanani.

Biblia inatujulisha katika 1 Kor 10:1-12 mambo yaliyosababisha Waisraeli wasifike Kaanani, mambo k**a hayo yanaweza yakasababisha baadhi ya wateule wa MUNGU wasiingie uzima wa milele. Jifunze kwa makosa haya ya Waisraeli ili usiyatenda katika maisha yako ya safari ya kwenda uzima wa milele.

SABABU ZILIZOSABABISHA WAISRAELI WALIOTOKA MISRI WASIFIKE KAANANI.

1. Kutamani mabaya.

1 Kor 10:6 '' Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, k**a wale(Waisraeli) nao walivyotamani.''

Ndugu usikubali kutamani mabaya ya zamani kabla hujaokoka, ishi maisha matakatifu sasa na usikubali kujihusisha na dhambi za zamani kabla hujampokea YESU k**a Mwokozi wako.

2. Kuabudu Sanamu.

1 Kor 10:7 '' Wala msiwe waabudu sanamu, k**a wengine wao walivyokuwa;''

Ndugu usiabudu sanamu, kuiheshimu wala kuisujudia.

Sanamu ni Sanamu tu na haina uhusiano wowote na MUNGU wala na YESU KRISTO.


3. Uasherati na uzinzi.

1 Kor 10:8 ''Wala msifanye uasherati, k**a wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.''

Kufanya uzinzi na uasherati huko ni kuitafuta jehanamu, ndugu usikubali kufanya dhambi hiyo mbaya.

4. Kumjaribu MUNGU.

1 Kor 10:9 '' Wala tusimjaribu BWANA, k**a wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.''

Ndugu usikubali kumjaribu MUNGU bali mtii na kutii Neno lake la Wokovu wa YESU KRISTO.

5. Kunung'unika

1 Kor 10:10 '' Wala msinung'unike, k**a wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.''

Manung'uniko ni silaha ya shetani kuwatesa Kanisa, na Manung'uniko ni dhambi kwa MUNGU hivyo ndugu kataa kunung'unika katika maisha yako ya Wokovu.

Kumbuka Kaanani ya Waisraeli ni mfano wa uzima wa milele kwetu hivyo inapasa kuishi maisha matakatifu siku zote huku tukikataa mambo ya dhambi yote pamoja nanyi mambo mitano hapo juu yaliyowaponza waisraeli.

Kitabu cha Kumbukumbu la torati kiliandikwa kipindi ambacho waasi walikuwa wameshakufa kwa sababu ya uovu wao na dhambi zao.

Musa katika kumbukumbu la torati alikuwa anawasaidia waisraeli ambao wakati maagizo ya kwanza yanatolewa walikuwa watoto wadogo na wengine walikuwa hawajazaliwa.

Sisi mambo ya Torati yanatusaidia nini?

1 Kor 10:11-12 '' Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.''

Hatuko chini ya torati leo lakini ukiisoma Biblia kwa jinsi ya KRISTO utajifunza mambo mengi muhimu sana katika Wokovu wako leo.

Ninafurahishwa na Neno la Mwisho la Musa katika Biblia ambalo linatoka Kumb 33:29 Kwamba '' U heri, Israeli. Ni nani aliye k**a wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.''

Nimelipenda Neno la Musa la Mwisho.

Kumbuka Hajawahi kutokea Nabii k**a Musa katika Israeli na manabii wote wa Biblia walitokea Israeli.
Kumb 34:10 ''Wala hajainuka tena katika Israeli nabii k**a Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;''

Ndugu, Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante k**a umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU K**a Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

0 7 1 4 2 5 2 2 9 2(Ni namba hii kupiga, kuandika meseji na hadi whatsapp).

Uki-share somo hili kwa maandishi naomba share k**a lilivyo,usibadili jina wala chochote.

Want your business to be the top-listed Government Service in Mbinga?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

P. O. BOX 225
Mbinga