Bavicha Morogoro

Bavicha Morogoro

Share

Kurasa maalum ya vijana wa CHADEMA Morogoro

04/09/2020

Tushinde pamoja

29/01/2020

IFAHAMU CHADEMA
SEHEMU YA TANO (5)
______________________
3. Madhumuni ya Kijamii
-----------------------------
Kuendeleza juhudi za kuhakikisha haki za wanawake, watoto na mila potofu za ukandamizaji wa kijinsia, kuwanyima watoto haki za malezi bora na za kupata elimu ya kutosha, umuhimu wa kuwajali wenye ulemavu na kuwatimizia mahitaji yote ya msingi, pamoja na kutekeleza makubaliano na mikataba ya kimataifa kuhusu haki za watoto, wanawake na walemavu.

Kuboresha, kutunza na kutoa huduma za jamii, kwa mfano Afya, Elimu, Maji, Makazi na Usalama wa Raia, kwa ajili ya kukuza hali ya maisha ya watu.

Kuhifadhi na kuboresha utamaduni wa Taifa ili kujenga hadhi na heshima ya watanzania na kuendeleza nyanja zote za utamaduni, burudani, michezo, sanaa na historia ya nchi.

Kutoa huduma za kukidhi maisha kwa wastaafu na makundi yasiyojiweza katika jamii hususan wenye ulemavu, watoto yatima na wazee, ambao hawapo katika mkondo wa kujipatia kipato cha kujitosheleza.

Kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na janga la VVU / UKIMWI (HIV/AIDS) sambamba na kutoa huduma muafaka kwa waathirika.

Itaendelea...
Ref: Katiba ya CHADEMA Media ya mwaka 2006 toleo la mwaka 2016.

12/01/2020

SEHEMU YA PILI (2)

FAHAMU Itikadi ya CHADEMA
_____________________________
CHADEMA ni Chama cha itikadi ya MRENGO
WA KATI (Center Party).

CHADEMA ni Chama kinachoamini kukuza
na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia
rasilimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa
Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla
unanufaika na rasilimali zao.

CHADEMA inaamini katika kujenga na
kuimarisha uchumi wa soko jamii (social
market economy), utakaoheshimu na kulinda
haki na mali za watu, biashara huru na sekta
ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya
umma katika maeneo nyeti hususani pale
penye hitilafu ya soko au penye maeneo
nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko
huru si katika soko holela.

CHADEMA inaamini katika kuhakikisha
matumizi bora ya rasilimali asilia za nchi
ili zichangie kikamilifu katika pato la Taifa
na hasa kuboresha huduma za kiuchumi
zinazotumiwa na wananchi wote.

CHADEMA inaamini katika uzalendo na
kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.

CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya
sheria zilizo za haki.

CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi
maslahi ya Taifa.

CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee
katika familia k**a moja ya taasisi muhimu
ya kijamii.

CHADEMA inaamini katika umuhimu wa
uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya
mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini
kuwa sehemu ya dola.

CHADEMA inaamini Taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.

CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.

CHADEMA inaamini kumiliki rasilimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa
uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga Chama
na baadaye Taifa lenye kutoa fursa, ambapo
kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza
kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

Itaendelea sehemu ya tatu.
(Ref: Katiba ya chama toleo la 2006)

09/01/2020

SEHEMU YA KWANZA (1)
_______________
FAHAMU FALSAFA NA ITIKADI YA CHADEMA

Falsafa ya Chama
_________________
Falsafa ya Chama ni kuamini katika “Nguvu na
Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.

Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa Umma ndio wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na Taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na
viongozi, watawala au wageni.

Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.

Historia inaonyesha kuwa “Umma” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea
enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza Serikali na kuwakandamiza wananchi.

CHADEMA inaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu haupo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.

CHADEMA inaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamlaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwa shawishi na kuwaandaa watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya
Umma” uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

SOMO LITAENDELEA SEHEMU YA PILI YA ITIKADI.

(Rejea ni katiba ya chama ya mwaka 2006)

Photos from Bavicha Morogoro's post 09/01/2020

Kumeibuka vurugu kwenye kikao cha baraza la madiwani Jiji la Dar es Salaam kilichopanga kuamua hatima ya Meya Isaya Mwita baada ya kuwepo madai ya "mtu mmoja" kusaini mahudhurio lakini hayupo kikaoni.

Mh. Boniface Jacobo akiwa anaonesha "forgery" hiyo pichani.

09/01/2020

Twende sawa

08/01/2020

Mwenyekiti Kanda ya Kaskazini Mh. Godbless Lema atakuwa live kupitia

https://bit.ly/2QAm5qr
Subscribe sasa.

Photos from Bavicha Morogoro's post 08/01/2020



"Taifa hili sasa hivi tumeingizwa kwenye utamaduni ambao siyo asili yetu, na tunaelekea kuingia kwenye shimo lakini kila Mtanzania ameamua kuwa mpole kukaa kimya. Akifikiria kuna Mtanzania mwingine mwenye wajibu waziada kulioko yeye"


:
"Hatu wezi kuruhusu kwenye nchi yetu iwe ni jambo la kawaida, wananchi kumiminiwa risasi hadharani"


:
"Kwamba iwe ni utamaduni wakawaida kwa Watanzania kubambikiwa kesi za Uhujumu Uchumi, kwasababu eti tunaikosoa serikali, hatuwezi kunyamaza”


:
"Leo mmeshuhudia vijana wanapewa kesi za uhujumu uchumi, wafanyabiashara wanafilisiwa, na serikali wanawapiga chini k**a utani"


:
"Lakini tungeisikiliza ilisema nini, tukaielewa inawezekana kabisa tungeweza kuzuia haya mambo mapema"


:
"Vyombo vya habari mnajua sasa hivi mnamachaguo, ama muandike taarifa inayoipendeza serikali, ama mjifanye mko ‘neutral ‘ hamuoni, ama muamue kupotezwa"


:
“Hatuwezi kuruhusu tunakuwa na chaguzi za kihuni alafu Watanzania hamzungumzi yaani mnakaa kimya, tunatoa comment kwenye mitandao ya kijamii tunaandamana huko alafu maisha yanaendelea”


:
"Sisi tumeamua k**a ngwai naiwe ngwai na tunamaanisha kwasababu ifike pahala tuwaonee huruma mama zetu namkumbuka Mama Kabendera siku kadhaa kabla hajafariki alinukuliwa akimwambia Rais huyu mtoto uliye mueka ndani ndiyo anaye nifanya mimi niwe na uhai


:
"Mwaka 2016, wakati Magufuli anaingia madarakani na serikali yake. Na kina Mkapa wote deni la taifa lilikuwa Trl. 49 kwa miaka ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete"


:
"Huyu jamaa ameingia anamiaka minne, tumetoka Trl.49 mpka 65 alafu anataka tumpe miaka 5 mingine haliwezekani"


:
"Takwimu za BOT zinaonyesha deni la taifa ni Trl. 65, na Waziri Mpango analidanganya taifa kwasababu anajua wamekopa kupitiliza"

Photos from Bavicha Morogoro's post 08/01/2020

''Rais Magufuli alizuia Mikutano ya Vyama vya Siasa na akasema Mikutano Mpaka 2020 na sasa ni 2020 Sisi Baraza la Wanawake wa CHADEMA Tutazunguka Nchi nzima kukiwasha K**a tulivyofanya hapo nyuma" Mh. Hawa Mwaifunga Makamu M/Kiti Bawacha Taifa (MB)

Photos from Bavicha Morogoro's post 06/01/2020

Ayubu Sikagonamo, Diwani Kata ya Chipaka - Songwe, anayekabiliwa na kesi No. 10/2019 ya uhujumu uchumi, ambayo alibadilishiwa kesi ya awali ya umiliki wa silaha na kupewa kesi ya uhujumu uchumi, Leo Januari 06, 2019 Mahak**a Kuu Mbeya imempatia dhamana.

05/01/2020

Hongera

Leo k**anda na Mwenyekiti Mkuu Bavicha Taifa Mh. Pambalu, leo amepokelewa hapa Mwanza katika ofisi za Kanda ya ziwa amepokelewa pamoja na wazazi wake.

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Morogoro