18/03/2026
Kikao cha pamoja na Wakuu wa Wilaya kilifanyika kwa lengo la kutoa mrejesho wa mafunzo ya kukabiliana na majanga yaliyowezeshwa na Norwegian Church Aid Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa Anglikana Dayosisi ya Morogoro.
Malengo ya kikao hicho yalikuwa ni:
1. Kujitambulisha rasmi kwa ofisi husika kuhusu ushiriki wa DDSCDO-Kupitia Kanisa Anglikana Dayosiai ya Morogoro katika juhudi za kusaidia Serikali katika maandalizi na mwitikio wa dharura ya majanga, hususan mafuriko katika maeneo ya Wilaya ya Mvomero.
2. Kuwasilisha mrejesho wa awali wa mafunzo yaliyofanyika tarehe 13–14 Machi 2026, ambayo yalilenga kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya wadau katika kukabiliana na majanga.
3. Kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya DDSCDO na Serikali ya Wilaya pamoja na Halmashauri ili kuhakikisha hatua za maandalizi na mwitikio wa majanga zinafanyika kwa uratibu na ufanisi.
Katika kikao hicho, pia tulijadiliana kwa kina namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya wadau mbalimbali pamoja na kubainisha mahitaji muhimu ya msingi kwa wananchi waliopo katika kata zilizoathirika na mafuriko katika Wilaya za Kilosa na Mvomero. Aidha, tulitambua baadhi ya kata zilizoathirika zaidi, zikiwemo Doma, Mhonda na Sungaji (Mvomero), pamoja na Tindiga, Mhenda na Myombo (Kilosa).
14/03/2026
Day 2 – Orientation on Emergency Preparedness and Flood Response in Morogoro Region
Today we continued with Day 2 of the Orientation Program on Emergency Preparedness and Flood Response organized through the collaboration between NCA and the Anglican Church Diocese of Morogoro. The training focused on strengthening the capacity of local stakeholders to respond effectively to emergencies, particularly flooding, which continues to affect many communities in Morogoro.
The orientation brought together representatives from several Local Government Authorities (LGAs), including Kilosa, Gairo, Mvomero, and Morogoro Municipal. These are key areas where our Economic Empowerment Programmes are currently being implemented, with a strong focus on food security and waste management as part of building resilient communities.
Using the latest data and seasonal outlook from the Tanzania Meteorological Authority (TMA), the training emphasized the growing risks of flooding in Morogoro due to the area’s geographical characteristics and recurring heavy rainfall patterns. Participants discussed practical strategies for early preparedness, coordinated response, and community awareness to reduce the impact of floods on livelihoods, infrastructure, and food systems.
This orientation is an important step toward building stronger partnerships between faith-based institutions, local governments, and community programs to ensure timely, organized, and effective emergency response in Morogoro and surrounding districts.
29/05/2025
Utoaji Elimu katika shule ya Msingi Miembeni iliyopo katikq kijiji cha Mvomero ikiwa na lengo la kujenga uelewa kwa mabinti wadogo ambao wamefikia umri wa kubalehe kwa kutambua hitaji muhimu la kujisitiri pindi wanapokuwa katika Hedhi.
Elimu hii imewezeshwa na Afisa ustawi wa Jamii kutoka Halimashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na uongozi wa Mradi.
Kanisa Anglikana kwa kushirikiana na wadau wake wa Norwegian Church Aid Tanzania wamewezesha ugawaji wa taulo za k**e ambazo zinatumika tena (Re-usable pad)baada ya kufuliwa na kusaidia kupunguza gharama ya manunuzi kwa jamii ya hali ya chini.
17/05/2025
Utambulisho wa mradi mpya wa EDFS(Economic Development and Food Security) utakao tekelezwa kwa miaka mitano (2025-2029)ukihitimishwa kwa Wilaya tatu ambazo mradi huu utatelezwa kwa Kilosa,Mvomero na Gairo katika vijiji 11.
Mradi huu unafadhiliwa na Norwegian Church Aid Tanzania na kutekelezwa na Kanisa Anglican Dayosisi ya Morogoro kupitia shirika lake la DDSCDO.
Mradi huu utakuwa na unalenga kutoa elimu na kuwezesha katika nyanja zifuatazo Usalma wa chakula,uhifadhi wa Mazingira,kupinga Ukatili wa Kijinsia,Kupambana na Usawa,Ujenzi wa amani.
Ili kufikia matokeo tarajiwa ya Mradi njia zitakazo tumika ni pamoja na uundaji wa vikundi vya VICOBA, ushirikiano na taasisi wezeshi za Kiserikali na Binafsi,Kujengea jamii uwezo wa kusimamia mradi kupitia mitandao ya vikundi,uundaji wa kamati mbalimbali za kufuatilia Rasimali za Umma(PETS/SAM),Ujenzi wa amani kupitia jukwaa la usuruhushi la mahusiano ya Dini mbalimbali.
Katiia utambulisho ulihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Wakuu wa Wilaya,makatibu Tawala, Wakurugenzi pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali.
14/11/2024
Ufungaji wa mfumo wa sola kwa ajili ya kuvuta maji ya kisima katika shamba darasa lilipo katika umoja wa vikundi vya Dini mbalimbali kwa wilaya ya Mvomero(MVIRVICA) ukiwa umekamilika.
Kupitia ushirikiano uliopo baina ya wanavikundi na uongozi wa serikali ya kijiji ulituma mwakilishi wake ambae ni Bwana shamba wa kijiji kwa ajili ya ushiriki na kutoa utalaamu wa ufungaji wa mifumo ya umwagiliaji.
Kanisa la Anglikani kupitia shirika lake la DDSCDO linashukuru wafadhili wake wa Norwegian Church Aid Tanzania kwa kufanikisha zoezi hili katika kuifanikisha jamii kujikomboa na mabadiliko ya tabia nchi
05/11/2024
It has been a privilege to host various visitors from NCA who have come to the Morogoro region to observe and learn how we implement our projects. These initiatives are carried out with the support of local structures (Agripreneurs and Coordinators), all working together under the umbrella of MVIRVICA and KIRVICA. We are pleased to welcome them and share our experiences… Asanteni sana😁