Wami Ruvu Basin

Wami Ruvu Basin

Share

Taasisi ya Serikali unayohusika na utunzaji wa rasilimali za Maji.

04/04/2024

Uwekaji wa alama za kudumu za mipaka na Mabango ya makatazo katika Bwawa la Mindu chini ya Bodi ya Maji, Bonde la Wami/Ruvu.

01/03/2024

Wajumbe wa Bodi ya Sita, Bodi ya Maji, Bonde la Wami/Ruvu wamefanya ziara ya kutembelea mito iliyokumbwa na uharibifu kutokana na mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwezi wa kwanza katika Wilaya za Kilosa na Morogoro pamoja na kujione jitihada zilizochukuliwa na Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu za kuzuia madhara zaidi yasiweze kujitokeza hasa katika kipindi hiki cha mvua za Masika zinazotarajiwa kunyesha kwa kipindi hiki kuanzia wiki ya 4 ya mwezi wa Pili hadi Wiki ya Pili ya Mwezi wa Tano.

01/03/2024

"Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu hapa duniani, kuwa hadithi nzuri kwa wale ambao watasimuliwa habari zako." - Buriani
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Photos from Wami Ruvu Basin's post 19/02/2024

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inatekeleza mradi wa kutengeneza Mfumo wa kutabiri Mwenendo wa Maji katika Mto Ruvu utakaosaidia kufanya utabiri wa majanga ya mafuriko na ukame na kisha kutoa taarifa kamili zitakazotumiwa na wadau mbalimbali wanaotegemea maji ya mto huo katika shughuli zao za kichumi na kijamii.

Akizungumza katika warsha fupi ya kufunga mafunzo yaliyodumu kwa siku 7 yaliyotolewa na mtaalamu mshauri kutoka M/S DIT ya kuwajengea uwezo watalaam kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu juu ya uendeshaji wa mfumo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dkt. George Lugomela ameipongeza Wami/Ruvu kwa kuja na Mradi huu utakaoweza kutoa taarifa za awali juu ya majanga mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Dkt. Lugomela ameitaka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kutekeleza kwa weledi mradi huu na kuwa chachu ya kutoa mafunzo kwa Mabonde mengine hapa nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amebainisha kuwa Mfumo huo utaweza kutabiri kila baada ya siku 10 lengo likiwa ni kupata taarifa sahihi kutokana na umuhimu wa Mto Ruvu.

Mradi huu wa mfumo wa kutabiri mienendo wa maji mtoni unatekelezwa kwa fedha kutoka Benki ya Dunia kwa kupitia Mradi wa Kusaidia Sekta ya Maji (WSSP II) unaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 325,700,000.

Photos from Wami Ruvu Basin's post 17/02/2024

TATHMINI KUFANYIKA BONDE LA MZAKWE, WAKAZI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO.

Wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na Bonde la Mzakwe wametakiwa kutoa ushirikiano katika zoezi la tathmini linalofanyika na timu ya watalaam ambayo imeundwa kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za maeneo hayo ili kusadia ushauri na maamuzi yatakayotolewa katika harakati za kunusuru bonde hilo ambalo ndio chanzo kikuu cha Maji kwa Mkoa wa Dodoma.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule Februari13,2024 wakati akiitambulisha timu hiyo kwa wananchi wanaoishi maeneo ya Bonde hilo na maeneo jilani ambapo utambulishi huo umefanyika katika Ukumbi wa Veyula Jijini Dodoma.

" Kuna timu ya watalaam itapita kwenu kuja kupata taarifa ni watu wanaokuja kwa amani na wakute amani ,watafanyakazi kwenye maeneo yanayozunguka Bonde watapita nyumba kwa nyumba Ili kupata taarifa za Msingi na hiyo kazi kuanzia tarehe 14 hadi 21 Februari ", Amesema Senyamule

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri amewaomba na kuwaagiza wenyeviti wa Mitaa na Vijiji ambao tathmini hiyo itafanyika katika maeneo yao, kuwatumia wazee maarufu na wazaliwa wa wa maeneo yao ili wawasaidie kukusanya taarifa zisizo na mkanganyiko na zenye maslahi katika tathmini hiyo ambayo Ina lengo la kulinusuru bonde hilo.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Mundemu akizungumza kwa niaba ya wakazi wanaolizunguka bonde hilo Bw.Ayub Chimuli amemshukuru Mhe.Senyamule kwa kuja na mchakato huo wa kupatia ufumbuzi wa eneo hilo la Bonde kwani imekuwa ni changamoto ya muda mrefu kwa wakazi hao.

Timu ya Tathmini hiyo imeundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutokana na uwepo wa shughuli za kibinadamu ikiwemo kuchunga mifugo ndani ya hifadhi, kilimo na ukataji Miti ambazo zinaathiri upatikanaji wa Maji Mkoani humo.

Tathmini hiyo itafanywa na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Maji, Bonde la wami ruvu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,DUWASA, Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na wadau mbalimbali wa Maji na mazingira.

Photos from Wami Ruvu Basin's post 08/02/2024

ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA UHIFADHI WA BWAWA LA MINDU.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea na zoezi la utoaji elimu na kuwataka wananchi pamoja na wakulima wanaofanya shughuli za kilimo pembezoni mwa hifadhi ya Bwawa la Mindu kuachana na kilimo cha kutifua udongo hali inayosababisha uharibifu wa mazingira na kuhimizwa kujikita katika upandaji wa miti ili kurejesha uoto wa asili katika Hifadhi hiyo.

Zoezi hili la uotoaji elimu limekuwa shirikishi ambapo maafisa kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wameungana na Viongozi wa kata, maafisa watendaji pamoja na wenyeviti wa mitaa ambapo mpaka sasa Bodi imeshaandaa vitalu vya miti rafiki na mazingira pamoja na miti ya matunda ambayo wakulima hao watapatiwa kwa utaratibu maalumu na kisha kuwepo na ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha miti hiyo inakuwa salama.

Ikumbukqe kuwa Bwawa la Mindu ndio chanzo pekee kinachotegemewa katika manispaa ya Morogoro kwa zaidi ya asilimia 75 ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunakilinda na kukihifadhi chanzo hiki kwa maslahi ya kizazi cha sasa na cha baadae.

05/02/2024

TAHADHARI YA MAFURIKO NA ONGEZEKO LA WINGI WA MAJI KATIKA MTO RUVU.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea kutoa taarifa za tahadhari ya mafuriko Pamoja na mienendo ya maji katika vyanzo vya Maji katika kipindi hiki chenye ongezeko la maji Lisilo la Kawaida.

Bodi imeendelea kufanya tafiti zinazoonyesha kuwepo kwa Ongezeko kubwa la Maji katika vyanzo vyake ikiwem mto Wami na mto Ruvu, ambapo ongezeko hili linasababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika Milima ya Uluguru, Ukaguru na Milima ya Nguu
Bodi inatoa tahadhari kwa wadau wake hususani wadau wa Kilimo, kuacha kabisa kufanya shughuli za kilimo kando kando ya mito, na kuwakumbusha wadau wa Uvuvi kuendelea kufanya shughuli zao kwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la Maji.

Kwa watu mbalimbali wanaotumia maeneo yanayotiririsha maji kwa ajili ya vivuko kuchukua tahadhari katika kipindi hiki kabla ya kuvuka lakini Bodi inaendelea kuwahakikishia wadau wake wanaochukua maji mtoni kuendelea kuwepo kwa kiwango cha maji cha kutosha kinachotosheleza mahitaji yao.

Photos from Wami Ruvu Basin's post 18/01/2024

WAMI/RUVU YAENDELEA NA JITIHADA ZA KUPUNGUZA MAFURIKO KILOSA.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea na jitihada za kupunguza athari za mafuriko katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro hususani wilaya ya Kilosa katika mto Kisangata kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imetengeneza njia mbadala za matoleo ya maji ili kupunguza kiasi kikubwa cha maji kinachopita katika mkondo mmoja na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara pamoja na kuvamia makazi.

Aidha Bodi imeendelea na tathimini ya athari za mafuriko katika maeneo ambayo yameathirika na mafuriko ikiwemo Mto Miyombo, Mto Msowero na Mto Mazinyungu wilayani Kilosa sambamba na kutoa Elimu kwa wananchi kuacha kufanya shughuli zisizo rafiki na mazingira pembezoni mwa mito na ujenzi holela wa makazi katika njia za maji ili kuepukana na atahari za na mafuriko maji yajaapo.

"Tone la Maji lazima lihifadhiwe”

Photos from Wami Ruvu Basin's post 12/01/2024

Timu ya Majanga na Maafa kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imetembelea na kufanya Tathmini ya maeneo yanayokumbwa na Mafuriko na kusababisha Uharibifu na Upotevu wa Mali za Wananchi wanaoishi katika hifadhi ya Bonde la Wami/Ruvu.

Aidha Maeneo yaliyotembelewa na wataalamu ni Bigwa Mgolole, Mbuyuni, Kihonda kwa Chambo na Shule ya Azimio , kupitia Hilo Bodi inawataka Wananchi kufuata sheria ,Kanuni na Taratibu za Utunzaji wa Rasilimali maji ili kuepukana na Majanga hayo.

12/01/2024

Heri ya siku ya Mapinduzi…!!

25/12/2023

Tunawatakia Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya.

24/12/2023

HERI YA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA.!

Bodi ya Maji, Bonde la Wami/Ruvu inapenda kuwashukuru Wadau, Taasisi na Wanachi wote kwa kipindi chote cha Mwaka huu 2023 katika ushiriki wao wa kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Bodi inapenda kuwashukuru wote na kuwatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya pamoja na kuwakumbusha kusheherekea sikukuu hizi kwa kulinda na kuhifadhi Rasilimali za Maji.

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya….!!!

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Mazimbu Road
Morogoro