Elimu Kwa Jamii

Elimu Kwa Jamii

Share

Elimu kwa jamii

15/05/2019

ZIFAHAMU GROUP (KUNDI) ZA DAMU PAMOJA NA AINA YA ULAJI NA TABIA ZAKE.
Kundi lako la damu linaweza kukufanya uwe dhaifu au imara katika kukabiliana na magonjwa fulani.Ni vema kujua kundi lako la damu sawa na ilivyo vema kujua mambo mengine yanayochangia kuwa na afya njema. Kujua kundi lako la damu Kunaweza kukuza uwezo wako wa kufahamu hatari zinazo kukabili kutokana na kundi la damu Ulilo nalo na kuepuka hatari hizo kwa kutumia mtindo wa maisha unaofaa.Hata hivyo, K**a vilivyo viungo vingine vya mwili, damu nayo ina changamoto ya kukumbana na maradhi mbalimbali, magonjwa yanayoathiri utendaji kazi wa damu yanaweza kugawanywa katika makundi k**a vile ya kurithi, kuambukiza, mabadiliko ya kimwili na saratani tofauti. Damu ya binadamu imegawanyika katika makundi makuu manne ambayo ni A, B, AB, na O, binadamu yeyote lazima awe na moja wapo ya makundi hayo.

GROUP A
✔Hawa ni vegetarians. Yaani wala mboga mboga hasa za kijani. Pia wanahitaji sana mananasi na zabibu kwa wingi.
✔ Mara nyingi ni wale watu ambao hawaambiliki yaani wakiamua kitu wameamua mpaka wakitekeleze hata k**a ni kibaya.
✔ pia ni watu ambao ni wabishi sana au wabishani na hawakubali kushindwa hivi hivi.
✔Watu Wa kundi hili pia huwa wana changamoto ya kuwa na upungufu Wa acid mwilini hivyo hushindwa kuiprocess protini tumboni hasa itokanayo na nyama nyekundu.
✔Ni watu ambao hushambuliwa sana na saratani za mishipa ya fahamu,utumbo,mifuko ya mayai,mfuko wa kizazi na mlango wa uzazi kwa wanawake,kibofu cha mkojo,figo,kongosho na saratani ya kinywa, tezi za mate na umio.
✔Wana hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya Moyo,kupata lehemu mbaya mwilini,kwenye Moyo,wako hatarini pia kupata kiharusi na ugonjwa Wa shinikizo la damu Wa Moyo.
☑Vyakula wanavyotakiwa kula kwa wingi ni mbogamboga za Majani na nyama nyeupe nyama nyekundu sio nzuri sana kwa watu hawa.
☑ Hawatakiwi kugusa kabisa au kutumia Mara kwa Mara vyakula hivi :-nyama nyekundu,ngano,machungwa,na maziwa.
☑ wakila ndizi,maembe na mapapai huwasababishia waamkapo asubuhi kutokwa na mak**asi kwa wingi.
☑ Watu wa kundi hili wanapenda sana wali na Mara nyingi ndio Chakula chao kikuu.
Hawatakiwi kugusa kabisa ngano na mahindi na endapo wakatumia vyakula hivi hasa kwa wanawake huwasababishia kupata hedhi Mara mbili kwa mwezi.

Tabia zao ni hizi hapa:-
👉​​​​​ni watu Wa gharama sana hasa wadada au wanawake.
👉​​​​​huishiwa au wanakuwa na upungufu Wa damu sana.
👉​​​​​ni wavivu nikiwa na maana hawawezi Kazi ngumu ngumu.
👉​​​​​Ni waongo sana na sio wadanganyifu,ni wakweli (they don't like cheating)
👉​​​​​ni wasiri sana.
👉​​​​​wanapenda kujifichajificha k**a ni usiku hupenda kukaa gizani sana.
👉​​​​​ni waaminifu sana na hapa Mara nyingi unawakuta Maafisa utumishi kwani hufuata sheria.
👉Ni watu ambao pia wanaumwa Mara kwa Mara, kutokana na upungufu wa mwilini.
👉Wanapenda kuwa wao wao.Ni watu ambao wanafanya maamuzi wakiwa pekeyao. 👉Sio wazurulaji(Anaweza jifungia ndani asubuh mpaka jioni na ukadhani hamna mtu). 👉Wakipenda wanapenda kweli. 👉Wanahitaji handle with care, tunapokuja kuongelea mahusiano. Wanadeka mnoo.
GROUP B
✔Hili ni kundi la watu ambao ni wazungumzaji yaani ukiwapa nafasi ya kuzungumza ni k**a vile umekosea na hapa Mara nyingi unawapata watu k**a MCs, Wasanii, Radio presenters.
✔Ni watu ambao wana tabia zilizojitosheleza yaan wamekamilika.
✔ Wanapenda kuonekana ,hapa utawakuta waimbaji Na watangazaji.
✔Ni watu ambao husumbuliwa sana au wako hatarini kupata magonjwa k**a uvimbe Wa fizi,na pia wanawake walioko katika kundi hili wako hatarini kupata ugonjwa Wa kisukari aina ya pili.
✔ Mara nyingi ni watu ambao wakipata maambukizi ya virusi vya aina yoyote ile huwa machizi au vichaa kutokana na kwamba vinaenda kuharibu mfumo wake Wa fahamu, wana uwezo mkubwa kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.
✔Wana hatari kubwa ya kupata saratani ya koo.
☑Watu Wa kundi hili hawashauriwi sana kula vyakula vya aina ya kuku(Mara nyingi wao wenyewe tu hawapendi kuku ingawa hawaruhusiwi kula),Karanga,korosho,na nyanya, hizi pia hawashautiwi kula. ✔Ni watu ambao wanaamini sana kupitia maamuzi yao binafsi. ✔Si rahisi kuingia katika project yeyote unless, umempa derails za kutosha kuhusiana na hiyo project. ✔Ni watu wa malengo, yuko radio kupambana kuhakikisha anapata matokeo.

GROUP AB
✔Hawa ni watu ambao Mara nyingi hawaeleweki yaani wana tabia za A na pia tabia za B wakati mwingine.
✔Kundi hili la Damu husadikika ni kundi linalopenda sana dini. Na mara nyingi washehe, mapadre, wachungaji utakuta wengi wapo kundi hili. ✔Ni wakarimu sana na wanapenda sana watu. ✔Hujitolea kwa ajili ya wengine. Mtu wa jamii hii anaweza kukupa kila kitu akabaki hana yeye. ✔Ni watu ambao wanaweza akaanzisha kitu asikimalizie ukakuta kaishia katikati halafu kaanzisha kingine.
✔Ni watu ambao wako hatarini Kupata magonjwa k**a kiharusi,dengue,magonjwa ya Moyo,shinikizo la Moyo,na lehemu kujaa kwenye mishipa ya damu.
✔Watu Wa kundi hili Mara nyingi wakifikia uzeeni uwezo wao Wa kufikiri hupungua kwa haraka.Lakini Mara nyingi kupungua kwa uwezo Wa kufikiri hutokana na magonjwa k**a shinikizo la Moyo,kisukari na lehemu kuwa nyingi sana mwilini.
✔ ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana Wa kukabiliana na magonjwa yaani kinga yao ya mwili ni imara ukifananisha na makundi mengine yote ya damu. ✔Ni watu ambao wako na hasira za ndani kwa ndani sio rahisi kuexpose hasira zake ukamtambua kirahisi. ✔Hubadilika kulingana na mazngira(Hawana tofauti na vinyonga). ✔Wanasifa ya uongozi.

GROUP O
✔Hawa ni watu ambao ni jeuri na kiburi na wanajiamini sana.
✔Wanasifa ya uongozi. Wanapenda kuongoza watu(They're Leaders). ✔Wazurulaji mono. ✔Wako very much Open minded. Yaani ni watu wa Kureason mambo. ✔Watu ambao ni wababe,wagumu, na wanafanya maamuzi yao pale wanapoamua na sio kulazimishwa. ✔watu ambao wana roho nzuri sana ila hawapendi uongo hivyo usije ukajaribu kuwadanganya hata siku moja.
✔Ni watu ambao wanaweza jihusisha na mahusiano zaidi ya moja na wakaona wako sawa. ✔Ni Watu ambao sio rahisi sana kupata shambulio la ghafla la Moyo k**a ilivyo kwa watu wenye makundi mengine ya damu.
✔Hawana kinga ya kutosha dhidi ya kipindupindu lakini wana kiasi fulani cha kinga dhidi ya Kifua Kikuu (TB), Malaria isiyo kali, saratani za kongosho, tumbo, matiti na mlango wa kizazi.
✔Ni rahisi kupata magonjwa ya maambukizi ya ngozi,na vidonda vya tumbo.Wanapata sana maumivu ya kiuno,magoti pamoja na mgongo.
✔Ni watu wasiopenda vitu vichachu kutokana na uwepo Wa acid kwa wingi mwilini mwao hivyo wanasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo na huwa wanasumbuliwa sana na tatizo la choo (constipation) pamoja na kisukari.
✔Kundi hili pia hutokewa na mvi za mapema sana.
✔Kwa wanaume hapa ndipo unawakuta ambao wana mapaja yasiyolingana yaani moja kubwa lingine Dogo.

☑Hawatakiwi kula ngano na mahindi Mara kwa Mara au kutokula kabisa.
☑ Hawapaswi kabisa kugusa au kula machungwa,passions,ukwaju,maembe mabichi, zabibu nk na vyote vyenye acid.
☑Hawatakiwi kabisa kula ugali au wali,mahindi ya kuchoma au kukaanga au kupika hayawafai kabisa.
☑Wanaume walioko katika kundi hili wanahitaji protein kwa wingi kuliko wanawake kutokana na kuhitaji nguvu kwa sana katika shughuli zao na miili yao kwa ujumla.
☑Kwa wanaume wanatakiwa kula matunda sana k**a maembe,mananasi,ndizi,matikiti maji (ule na mbegu zake) hapa pia k**a ni tunda unakula lote mfano nanasi unalimaliza,papai unalimaliza,na pia matunda ya rangi moja kula kwa pamoja.
☑Ukitengeneza kitu k**a juice ya matunda unywe yote kwa wakati huo na sio kutengeneza ya wiki au siku kadhaa.
☑Vyakula vinavyowasaidia au wanavyohitaji sana mwilini ni matunda ,mboga za Majani,protein kwa wingi yaani nyama,maharage,mayai na maziwa.

*NB:Magonjwa mengi yanaweza kuepukwa kwa kuzingatia usafi wa mwili na mazingira, mlo kamili(kula kilingana na Uhitaji wa group lako la damu), kufanya mazoezi, kupunguza uzito uliozidi na kuepuka matumizi ya tumbaku, pombe pamoja na madawa za hospital mara kwa mara..*

12/08/2018

*K**a ilivyopokelewa kutoka kwa mtendaji mkuu wa Polisi.*

*UFAHAMU KWA UMMA!*

Tafadhali chukua dakika chache kupitia maoni haya

Polisi wametupa maoni yafuatayo katika tukio la wezi wanaoweza kuingia kwenye majengo yetu au ndani ya nyumba zetu. Natumaini yana manufaa kwako na inaweza kusaidia kuokoa maisha.

1. Majambazi kwa kawaida huanzisha mashambulizi yao kupitia mlango wa nyuma (kawaida milango ya jikoni) kwa sababu kwa kawaida hawaonekani. Weka milango mizuri jikoni kwako. Tumia "chuma cha kukatisha" ama "Kizuiawezi" nyuma ya milango ndani ya nyumba. K**a una funguo "Kizuiawezi," kamwe usiache ndani ya kufuli. K**a inawezekana, tumia kufuli kwa kuongeza. lengo ni kuleta ugumu kadiri inavyowezekana kwa wezi kuingia ndani ya nyumba na kukuongezea wewe muda wa kuwaita watu kwa msaada.

2. Unaposikia mtu anavunja mlango wako, k**a huna unahakika kabisa vitendo vyako vitazuia kuingia ndani ya nyumba, usijaribu kuwa shujaa kwa kusukuma nyuma ya mlango (Wanaweza kukupiga risasi kupitia mlangoni), au kuweka vitu vizito k**a jokofu au makochi (Wanapatwa na hasira zaidi na k**a watafanikiwa kuingia ndani wanaweza kufanya ukatili vibaya mno).

3. K**a unalala bila nguo au na nguo kidogo, Vaa haraka mara tu uwasikiapo. Kwa wanawake hasa, usijaribu kubaki na nguo za kulalia. Vaa suruali na blauzi isiyovutia.

4. Iwapo umepiga simu kwa mtu kwa msaada, weka simu mbali nawe k**a vile huitaki ili usijulikane kuwa umepiga simu.

5. Angalia sehemu ya kukatia umeme kwenye nyumba yako kisha zima umeme iwe giza nyumba yote (hii itawachanganya na kusababisha wakimbie.

6. K**a una bunduki, imesajiliwa au la, itumie lakini tu k**a una unauhakika kuwa unaweza kuwasababishia madhara. Huu siyo muda wa kupiga risasi juu kuwatisha! Mauaji ya mvamizi katika eneo la nyumba yako wakati wa kujilinda mwenyewe na mali zako ni halali kisheria upande wa utetezi. Pia hata ukitumia silaha nyingine yoyoyte k**a vile kisu.

7. Wakati Majambazi wamefanikiwa kuingia wape chochote wakitakacho. Usifiche chochote. Usijaribu kuwa Jasiri wala kujadiliana nao.

8. Usiwatazame moja kwa moja (au usiwafanye wajue kuwa unafanya hivyo). K**a unamfahamu yeyote kati yao usioneshe dalili zozote za kumtambua na wala usitaje jina lake. Hata hivyo kariri maumbile yoyote unaweza kusaidia na kutambulisha katika uchunguzi.

9.Wakati hatimaye wanaondoka katika nyumba yako usiwafukuzie ..

10. Kuwa mlinzi wa jirani yako k**a utasikia uvunjaji katika nyumba zao, piga simu polisi kwa msaada.

11. Wakati Majambazi yanaingia kwenye eneo la nyumba yako, usiwashe taa yoyote katika chumba chako. Washa taa za nje lakini zima taa za ndani zote ili majambzi/wezi wasiweze kukuona.

Mbwa Walinzi wanakubalika sana majumbani kwa ajili ya kutoa taarifa mara kitu kigeni cha hatari kinapokuwa kwenye eneo. 🐕

Yeyote anaweza hitaji hii taarifa !

03/06/2018

MAMBO 15 YA MSINGI SANA KUYAJUA ILI UISHI NA WENZIO VIZURI.

1. Epuka hasira za hovyo na kila mtu, kuwa msikivu kabla ya kukimbilia maamuzi (elewa kuwa ukiwa na hasira huwezi kupata suluhu ya jambo)

2. Usiwatendee wengine ubaya ukadhani kuwa utakuwa salama (ubaya ulipwa kwa ubaya, ipo siku ubaya wako kwa wengine utakurejea k**a sio kuwarejea watu wa uzao wako)

3. Usichukue maamuzi kabla ya kutafiti ukweli (pengine wapo wanadamu wanaopenda kuonekana wao wema kwa kuumiza wengine). Mtuhumu mtu lakini mpe muda wa kumsikiliza, usimshambulie mtu kwa maneno makali bila kuujua ukweli, ukijua ukweli nafsi inaweza kukusuta.

4. Mchukulie kila mwanadamu ni mkosaji (tambua kuwa hata wewe unawakosea sana wengine na wanakuvumilia. Hivyo usiwe mwepesi wa kuwaadhibu wenzio kwa ubaya).

5. Usipande mbegu ya chuki na ubaya katika jamii unayoishi ukadhani itakuacha salama (chuki ukuwa k**a mti utambaao wa (passionfruit), ukiipanda ndani ya jamii yako, haitatoka kwako na inaweza kutafuna uzao wako ukajutia.

6. Tambua kuwa yule unayeishi nae ni mwanadamu k**a wewe, mpe heshima na mwonyeshee upendo hata k**a huoni anafanana nawe. Maisha ni duara huenda ulikuwa k**a yeye au utakuja kuwa k**a wewe baadae (Wapo wapi kina Firauni "Farao"??), wapo wapi waliokuwa matajiri wa Dunia hii, wapo wapi kina Idd Amin, Gadaffi, Hi**er, Saddam Hussein nk...ipo siku yanaweza kuja kwako pia.

6. Usiwe muongeaji ovyo ovyo na usiye na subira. Kuongea sana kunapoteza busara.

7. Jiepushe na maisha ya kusukumwa na wengine kufanya jambo usilojua manufaa yake. Jifunze kujitegemea kiakili. Sio kila unayemdhania rafiki moyoni mwake yupo pamoja nawe, na ukashirikiana nae, wengi wa marafiki zetu hututumia sana kuliko tunavyoweza kuwatumia wao.

8. Usipende sana kugombana na watu kwa njia ya maongezi yanayodumu k**a vile, ujumbe wa maandishi, mawasiliano ya simu au ujumbe wa maneno (SMS). Kumbuka kuwa maneno yanaishi kuliko ugomvi au uadui, ipo siku yatakurudi na utajiona mpumbavu na kukosa pa kujificha. Jifunze kusubiri.

9.Usifumbue mdomo wako kutamka ubaya au kunyanyua kidole chako kuandika ubaya juu ya mwenzio bila kujiuliza mara mbili moyoni mwako hatima ya unachokitoa kwa mwingine.

10. Jishushe na jifunze kusikiliza wengine wakati wa mazungumzo ili uweze kujifunza kabla ya kukurupuka kujibu, usikifu ni kipimo cha busara, mtu anayekurupuka kujibu jibu kila anachosikia hawezi kuwa kiongozi, Mume au Mke mwema kwani mara nyingi atapotoka tu.

10. Usitunze hasira nyingi moyoni kwani hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Jitahidi pia kuepuka kuwa na hasira mara kwa mara na zisizo na maana. Elewa kuwa hasira zisizo maana ukupunguzia maisha na kukupa maumivu wewe mwenye kuliko yule uliyemfanyia hasira, utakufa kwa magonjwa kabla ya wakati ufaao.

11. Thamani yako inategenezwa na watu wengine, wewe k**a ni mtoto, mheshimu sana mzazi wako na k**a umeoa au kuolewa, heshimu wazazi na familia ya mke au Mumeo kwa kuwa bila wao, usingekuwa hivyo ulivyo leo, unajivunia ndoa njema kwa kuwa yupo mtu alimzaa huyo mwenzio. Mheshimu kwa lolote liwe jema au baya, utalipwa kwa wakati ufaao.

13. Usijibizane na mtu usiyemjua au ambaye hawezi kukupunguzia kitu katika maisha yako. Tambua kuwa unapunguza sehemu kubwa ya maisha yako kwa kutafuta magomvi na mtu wa mbali nawe.

14. Kumbuka asili yako, kumbukumba upo hapo kwa kuwa kuna mahali ulitoka, maisha yanabadilika, usidhalau pale ulipokuwa zamani kwa kuwa ndipo palipokufanya leo uwe hapo.

15. Subiri, sikiliza, elekeza, vumilia..Elewa sio kila mtu ana uelewa k**a wako. Jitahidi kuwa mvumilivu katika kila jambo, usiinuke kuwafokea au kuwakaripia wengine kwa jambo ambalo pengine nao wanahitaji muda kueleweshwa ili walifanye vyema. Kumbuka sana, kuna wakati nawe ulikuwa huelewi kabisa lakini wapo wenzio walikuvumilia, wakakuelekeza njia njema, kufokea wengine mara kwa mara sio njia njema ya kuwafundisha bali ni kuwaweka mbali nawe.

: Ishi kwa kumpendeza Mungu. #

IKIKUGUSA, SHIRIKISHA MWINGINE 🧠✍🏼👣

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Mlimba Morogoro
Morogoro