18/07/2026
TAMASHA LA WASANII LAFANYIKA SHELUI KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
Tamasha la wasanii limefanyika tarehe 18 Julai, 2026 katika ukumbi wa Wembele, Shelui likiwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya ya Iramba likiwa ni tamasha maalumu la kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24 Julai 2026. tamasha hilo lilikuwa jukwaa la kuonesha vipaji vya wasanii wa ndani kupitia muziki, ngoma na maigizo.
Mbali na burudani, tamasha hilo lilitumika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, huku likiendelea kuibua vipaji, kuimarisha mshik**ano wa jamii na kukuza sanaa na utamaduni wa Wilaya ya Iramba.
18/07/2026
DC MWENDA AONGOZA MAZOEZI YA PAMOJA KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaj Suleiman Mwenda, leo tarehe 18 Julai 2026 ameongoza mazoezi ya pamoja yaliyowashirikisha watumishi wa Halmashauri, taasisi za umma, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24 Julai 2026.
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Dc Mwenda, amewataka wananchi wa Iramba kuendelea kushiriki mazoezi ya pamoja kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuimarisha afya, kujenga mshik**ano na kudumisha ushirikiano miongoni mwa wananchi na Serikali.
pia Amesisitiza kuwa ushiriki wa kila mmoja ni muhimu katika kuhakikisha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanafanyika kwa ufanisi na mafanikio.
18/07/2026
SHELUI SPORTS CENTER WAIBUKA WASHINDI BONANZA LA MICHEZO KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU IRAMBA
Timu ya Shelui Sports Center imeibuka bingwa wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo tarehe 18 Julai, 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Boda Boda fc katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Shelui.
Mbali na michezo, bonanza hilo lilihusisha utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu salama, upimaji wa hali ya lishe, upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza k**a kisukari na utoaji wa elimu ya afya kwa wananchi.
Shughuli hizo zililenga kuhamasisha jamii kushiriki katika michezo, kuboresha afya na kuendeleza mshik**ano kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru tarehe 24 Julai, 2026.
MKUU WA WILAYA YA IRAMBA Singida RS OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI Maelezo News
18/07/2026
KARIBU MWENGE WA UHURU WILAYA YA IRAMBA
🗓 JULAI 24, 2026
Kauli Mbiu: "Tanzania ni Yetu Sote; Tushik**ane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo"
MKUU WA WILAYA YA IRAMBA Singida RS OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI Maelezo News
18/07/2026
BONANZA LA MICHEZO KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
Leo tarehe 18 Julai, 2026 linafanyika bonanza la michezo lenye jina la Iramba DNA katika viwanja vya Shule ya Sekondari Shelui likishirikisha timu za Shelui Sports Center, Gereji FC, Boda Boda FC na Young Boys FC.
Bonanza hilo ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba, yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24 Julai 2026, likilenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi, kuimarisha afya na kudumisha mshik**ano katika jamii.
MKUU WA WILAYA YA IRAMBA Singida RS OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI Maelezo News