Kilindi District Council

Website

Kilindi District Council ๐Ÿ›๏ธ Karibu katika Ukurasa Rasmi wa Halmashauri ya Wilaya Kilindi
๐Ÿ“ Kilindi, Tanga - Tanzania
๐ŸŒhttps://kilindidc.go.tz
Makao Makuu ya Ofisi Songe

18/09/2026
KILINDI YAGAWA PIKIPIKI TATU KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMIIKatika kuadhimisha Mwezi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Halma...
02/09/2026

KILINDI YAGAWA PIKIPIKI TATU KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII

Katika kuadhimisha Mwezi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi imekabidhi pikipiki tatu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa ngazi ya kata, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao na kurahisisha huduma kwa wananchi.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata za Mkindi, Jaila na Kisangasa, kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza kwa ufanisi shughuli mbalimbali, ikiwemo ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo, uhamasishaji wa jamii pamoja na shughuli nyingine za maendeleo.

Akikabidhi pikipiki hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Mikopo, Ndugu Lucas Mirambo, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuzitumia kwa ufanisi katika kuwahudumia wananchi na kuchochea maendeleo ya jamii.

Amesisitiza kuwa pikipiki hizo zinapaswa kutumika kwa lengo lililokusudiwa, hasa katika kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma za maendeleo.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ndugu Nhojo Kushoka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dtk Samia Suluhu Hassan kwa kuridhai urejeshwaji wa kutolewa kwa mikipo ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watuwenye ulemavu. Akipongeza kanuni mpya za mwaka 2024 ambazo zimeruhusu kutenge fedha za Mafunzo, Ufuatiliani na Tathimini. Afisa Maendeleo Jamii akafafanua kwamba hata fedha fe ununuzi wa pikipiki hizo zimetoka katika sehemu ya fedha hizo.

Kamati ya siasa yakagua  miradi mbalimbali ya maendeleo.
01/09/2026

Kamati ya siasa yakagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hongera sana Mhe.Deogratius John Ndejembi Kwa kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
29/08/2026

Hongera sana Mhe.Deogratius John Ndejembi Kwa kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

29/08/2026

Mafunzo ya shule jumuishi chini ya programu ya shule bora.

Address

Kilindi
Tanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kilindi District Council posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share