Halmashauri ya Wilaya Ya Kusini

Call

Halmashauri ya Wilaya Ya Kusini Huu ni ukurasa rasmi wa Baraza la Mji Kusini Unguja

07/10/2026


HABARI PICHAZoezi la usafi wa Shehia katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kusini ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya usaf...
03/10/2026

HABARI PICHA
Zoezi la usafi wa Shehia katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kusini ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya usafi wa kila Jumamosi katika Mkoa wa Kusini Unguja

02/10/2026
MWEZI SEPTEMBA 2026
01/10/2026

MWEZI SEPTEMBA 2026

30/09/2026


MKUU WA WILAYA YA KUSINI ATOA WITO KWA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA MVUA KUBWA ZA EL NINOMkuu wa Wilaya ya Kusin...
29/09/2026

MKUU WA WILAYA YA KUSINI ATOA WITO KWA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA MVUA KUBWA ZA EL NINO
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mhe. Othman Ali Maulid, amewataka wananchi wa Wilaya ya Kusini kuchukua tahadhari mapema na kujiandaa kukabiliana na mvua za Vuli zinazotarajiwa kuambatana na mvua kubwa za El Niño.
Mhe. Othman ametoa kauli hiyo wakati wa Ziara ya Kamati ya kukabiliana na Maafa ya Wilaya ya Kusini ya kutembelea maeneo mbalimbali yanayoweza kuwa hatarishi na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hatua za kuchukua ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
Amesema kuwa, wananchi wanaoishi katika maeneo yanayotuama maji wanapaswa kuanza utaratibu wa kuhama mapema kwenda katika maeneo salama, badala ya kusubiri hali kuwa mbaya hatua ambayo inaweza kuhatarisha maisha pamoja na mali zao.
Aidha, Mhe. Othman amewataka wananchi kuimarisha usafi wa mazingira kwa kusafisha maeneo yanayozunguka makazi yao, ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ikiwemo maradhi ya matumbo na malaria pamoja na kusisitiza matumizi ya vyoo, huku akizitaka familia ambazo hazina vyoo kuchukua hatua za kuvijenga kabla ya mvua kubwa kuanza.
Katika hatua nyingine Mhe. Othman amewataka wananchi kuhifadhi nyaraka zao muhimu katika maeneo salama, hususan kwa familia zinazoishi katika maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko ili endapo mafuriko yatatokea ziweze kupatikana na kutumika bila usumbufu.
Mhe. Othman pia amewahimiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika kuhusu hali ya hewa na tahadhari za maafa pamoja na kuchukua hatua stahiki ili kupunguza athari zinazoweza kutokezea.
Ziara hiyo ya Kamati ya kukabiliana na Maafa ya Wilaya ya Kusini imelenga kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu maeneo hatarishi, kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua kubwa pamoja na kuhamasisha jamii kuchukua hatua za kinga kabla ya maafa kutokea.
Maenep yaliyotembelewa katika ziara hiyo ni Shehia ya Muyuni A, Muyuni B, Muyuni C, Mtende, Mzuri, Kiongoni, Paje na Bwejuu.

28/09/2026

DIWANI WA WADI YA PAJE MHE. IBRAHIM CHAGUWA ABDALLA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA PAJE KATIKA UFUNGUZI WA VYOO VYA JAMII

Address

Kitogani
Zanzibar

Opening Hours

Monday 01:30 - 15:30
Tuesday 01:30 - 15:30
Wednesday 01:30 - 15:30
Thursday 01:30 - 15:30
Friday 01:30 - 15:30

Telephone

+255776889893

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halmashauri ya Wilaya Ya Kusini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share