PPP Centre Tanzania

  • Home
  • PPP Centre Tanzania
Call Directions Website Contact the organization

PPP Centre Tanzania Welcome to PPPC Page!We forge impactful partnerships between Public and Private sectors.

Happy Nyerere day.
14/10/2026

Happy Nyerere day.

30/09/2026

📍kibaha-Pwani
KAFULILA AELEZEA JINSI YA KUFUNGUA SOKO, ANAFAFANUA FALSAFA YA PPP.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, ametoa ushuhuda binafsi wa uongozi wake akiwa Mkuu wa Mkoa k**a somo linaloeleza falsafa halisi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).

Kafulila ametoa ushuhuda huo Ijumaaa, Septemba 25, 2026, alipozungumza katika uzinduzi wa kongamano la PPP mjini Kibaha, mkoani Pwani.

Alisema alipokutana na sheria iliyowabana wakulima wa pamba kuuza mazao yao kwa vyama vya ushirika pekee, aliamua kufungua soko na kuruhusu wanunuzi binafsi kushindana na vyama vya ushirika, jambo lililomnufaisha moja kwa moja mkulima.

Kafulila alitumia mfano huo kueleza kuwa lengo la PPP si kupinga serikali au taasisi zake k**a vyama vya ushirika, bali kuhakikisha muundo wowote wa kiuchumi unaangalia tija kwa mwananchi wa mwisho.

“PPP inaleta ushindani unaolazimisha kila upande kuwa na ufanisi, na matokeo yake ni huduma bora na bei nafuu kwa wananchi,” alibainisha.

Alifafanua kuwa Sheria ya PPP imeweka kinga maalum kwa mtanzania na kubainisha kuwa kuna kanuni ya dhahabu inayosema kampuni ya kigeni inaposhirikiana na kampuni ya ndani katika kuomba mradi wa PPP, hupata unafuu na alama za ziada kuliko inapoomba peke yake.

“Hata k**a huwezi kujenga barabara yote, unaweza kuingia katika mnyororo wa thamani wa mradi huo,” alisema.

29/09/2026

📍Kibaha-Pwani

“WAWEKEZAJI WA NDANI SI WAPINANI, NI WASHIRIKA KATIKA PPP", ASEMA KISSANGA WA TNCC

Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Biashara ya Tanzania (TNCC), Oscar Kissanga, amesema ubia baina ya sekta ya umma na binafsi ni muunganiko wa mitaji, teknolojia, utaalamu na soko la ndani.

Amesisitiza kuwa uwekezaji wa ndani si mpinzani wa uwekezaji wa nje, bali ni mshirika katika kujenga uchumi.
Kissanga aliyasema hayo Ijumaa, Septemba 25, 2026, mjini Kibaha, Pwani, wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Fursa za Uwekezaji na Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Miradi ya Ubia (PPP).

Katika hotuba yake, Kissanga alitoa picha halisi ya hali ya miradi ya PPP nchini.

“Hadi kufikia mwaka 2026, katika kituo cha ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPPC), kulikuwa na jumla ya miradi 113...” alibainisha.

“Mchanganuo wa miradi hiyo ni: miradi tisa ipo katika hatua ya utekelezaji, mitatu katika majadiliano, mitatu katika manunuzi, 21 katika hatua ya upembuzi yakinifu wa awali, sita katika upembuzi yakinifu kamili na 42 katika hatua ya wazo,” alisema Kisanga.

Kwa mujibu wa Kissanga, takwimu hizo zinaonesha uwepo wa bomba kubwa la miradi, lakini kiwango cha utekelezaji bado kiko chini.

Pia aligusia mipango ya maendeleo ya Taifa, akieleza kuwa Mpango wa Tatu wa Maendeleo (FYDP III) ulihitaji Sh114.8 trilioni, ambapo Sh40.6 trilioni zilitazamiwa kutoka sekta binafsi.

SALAMU ZA PONGEZI.Wizara ya Fedha
28/09/2026

SALAMU ZA PONGEZI.

Wizara ya Fedha

28/09/2026

PWANI NI ‘NCHI ’ YENYE RASILIMALI TATU AMBAZO HAZIPO MKOA MWINGINE WOWOTE TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amefafanua kuwa uamuzi wa kuanzia Mkoa wa Pwani katika uzinduzi wa Kongamano la Fursa za Uwekezaji kupitia PPP haukufanyika kwa bahati mbaya, bali umetokana na tathmini ya kina ya uwezo wa kipekee wa mkoa huo.

Kafulila ametoa kauli hiyo Ijumaa, Septemba 25, 2026, mjini Kibaha, mkoani Pwani, wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Fursa a Uwekeaji Kupitia PPP, lililofanyika mkoani humo.

Alisema Pwani haipaswi kutazamwa k**a mkoa wa kawaida, bali k**a nchi yenye uchumi wake binafsi, na kubainisha kuwa mkoa huo una ukubwa wa kilomita za mraba 33,000.

Kafulila alisema k**a Pwani ingekuwa nchi huru, ingeshika nafasi ya 139 kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa

Hata hivyo, Kafulila alitumia methali ya Kiswahili isemayo, “Ukikaa karibu na waridi lazima unukie”, kueleza kuwa Pwani ndiyo mkoa unaonufaika zaidi na uwepo wa Dar es Salaam kuliko mkoa mwingine wowote

“Vietnam inakua kwa kasi kwa sababu iko karibu na China, huku Korea Kusini, Japan na Singapore zikikua kwa sababu ziko katika maeneo yenye fursa kubwa za biashara za kimataifa,” alitoa mifano hiyo kuunga mkono nadharia aliyoisema.

Kwa mantiki hiyo hiyo, alisema Pwani inapaswa kuitumia Dar es Salaam k**a Singapore inavyotumia bahari k**a lango la biashara.

“Pwani ina bahati ya kuwa na rasilimali tatu ambazo hakuna mkoa mwingine nchini unazo kwa pamoja ikiwemo Kisiwa cha Mafia, ambacho ni kisiwa cha tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, chenye ukubwa wa kilomita za mraba 394,” alisema.

“Pili ni Bwawa la Julius Nyerere, ambalo peke yake lina ukubwa wa kilomita za mraba 530, sawa na asilimia 90 ya eneo lote la Jiji la Dar es Salaam and tatu ni Mto Rufiji,ambao ni mkubwa nchini,” alisema.

Kafulila alisema mto huo humwaga maji yake Bahari ya Hindi kwa takriban lita trilioni nane za maji kila mwaka, na kubainisha kuwa maji hayo yanapotea baharini bila matumizi yoyote ya kiuchumi.

“Maji hayo hayapaswi kuendelea kupotea, bali yanapaswa kugeuzwa kuwa rasilimali ya kiuchumi kupitia miradi ya PPP,” a

Kibaha-Pwani📍PPPC, TNCC wazindua kongamano la fursa za uwekezaji wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi mkoani PwaniKi...
25/09/2026

Kibaha-Pwani📍
PPPC, TNCC wazindua kongamano la fursa za uwekezaji wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi mkoani Pwani

Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), kwa kushirikiana na Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) kimezindua kongamano la fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya ubia (PPP).

Uzinduzi huo umefanyika leo, Ijumaa, Septemba 25, 2026, mjini Kibaha, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Hafla hiyo, ilienda sambamba na
uzindua wa kaulimbiu ya kongamano hilo isemayo: “Kufungua Fursa za Uwekezaji kupitia Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa Maendeleo Endelevu.”

Kaulimbiu hiyo inalenga kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika miradi ya maendeleo kupitia ubia (PPP), kwa lengo la kuchochea maendeleo endelevu mkoani humo na taifa kwa ujumla.

Uzinduzi huo unafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila, na Mkurugenzi Mtendaji wa TNCC, Oscar Kissanga, na kuhudhuriwa na wadau wa ubia mkoani Pwani.

Salamu za Pole.
23/09/2026

Salamu za Pole.

SALAMU ZA POLE.
07/09/2026

SALAMU ZA POLE.

03/09/2026

03/09/2026

Bungeni📍
ZUNGU: HALMASHAURI ZITUMIE PPP KUSAFISHA DAR ES SALAAM

Spika Zungu akemea urasimu wa TAMISEMI kukwamisha miradi ya PPP

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. M***a Azzan Zungu, ametoa onyo kwa watendaji wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Halmashauri za Miji mikubwa nchini, akiziagiza kutumia mifumo ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutatua kero ya uchafu jijini Dar es Salaam badala ya kuweka urasimu unaokwamisha wawekezaji binafsi.

Spika Zungu ametoa msimamo huo leo, Septemba 3, 2026, bungeni jijini Dodoma katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Nne, Kikao cha Saba, kufuatia kile alichoeleza kuwa ni mwenendo wa watendaji wa serikali kuchelewesha majibu ya uwezeshaji kwa miradi ya ubia inayowasilishwa na halmashauri.

Akirejea maelekezo yaliyotolewa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais ya kukemea uchafu katika Jiji la Dar es Salaam, Spika Zungu alibainisha kuwa mojawapo ya sababu zinazofanya miji kuendelea kuwa michafu ni tabia ya watendaji wa TAMISEMI kutotoa majibu au kuchelewesha majibu pindi halmashauri zinapoleta mapendekezo ya ubia na sekta binafsi.

"Watu wetu wa TAMISEMI wabadilishe fikra zao., Tunakwenda kwenye Vision 2050, Bunge hili ndilo lililoidhinisha uwekezaji wa dira hii asilimia 70 unatoka sekta binafsi. Ninawaomba sana watendaji wa Serikali, badilikeni msipobadilika, mtabadilishwa," alihitimisha Spika Zungu alikumbusha kuwa Bunge hilo ndilo lililoidhinisha Dira ya Maendeleo 2050, ambapo asilimia 70 ya uwekezaji wote unategemewa kutoka kwenye sekta binafsi.

Address

Government City-Mtumba,Hazina Street

+255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PPP Centre Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to PPP Centre Tanzania:

Shortcuts

  • Want your organization to be the top-listed government service?

Share