HabariLeo

HabariLeo

Share

HABARILEO Gwiji la Habari Tanzania| Kwa habari za uhakika na kina | Sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania
Tanzania Standard Newspapers (TSN)

15/06/2026

ARUSHA: SERIKALI itaendelea kuongeza nguvu katika uhifadhi wa wanyamapori aina ya faru ambao wapo haratini kutoweka kwa kuimarisha Mradi wa Kimkakati wa Uhifadhi wa Faru Weupe ili kuongeza chachu ya ongezeko la uhifadhi na utafiti wa wanyamapori waliopo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hasaan Chande wakati wa hafla maalumu ya kuwaachilia huru faru weupe 17 waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ikiwa ni mradi maalumu uliofadhiliwa kupitia Shirika la Andbeyond kwa ushirikiano na Serikali ya Afrika Kusini

“Kwa kweli mmebuni kitu kizuri ambacho kinaleta tija na ufanisi na kuleta lmaendeleo kwa nchi yoyote, lengo kuu ikiwa ni kuongeza utafiti, uhifadhi na kupata elimu.

"Wako wengi duniani watakuja kujifunza kupitia Faru hawa weile wakiwa ama ni wanafunzi, au wakufunzi," Chande.

Amempongeza na kumshukuru mhifadhi namba moja nchini katika uhifadhi na muongoza watalii, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa utayari na utashi wake katika uhifadhi huku akiishukuru pia Serikali ya Afrika Kusini kwa ushirikiano mzuri na Tanzania kwa ufadhili wa faru hao.

Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imendaliwa na Mwandishi Wetu

15/06/2026

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo, amesema serikali imehakikisha kuna mazingira tulivu ya uwekezaji, kwa kuweka masharti ya kikodi ambayo ni rafiki, huku ikiondoa kanuni zilizokuwa kikwazo zaidi 370.

Londo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati utambuzi wa kampuni bora 100 za chapa za Afrika zinazotengeneza bidhaa zilizoko barani humo, jijini Dar es Salaam.

Amesema kwamba pia bajeti ya fedha kwa mwaka 2026/2027 imekuwa ya kwanza katika kuanza utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku kwa asilimia 70 ikitegemea utendaji kazi wa sekta binafsi.

“Tunatambua mchango wa sekta binafsi, watoa huduma na serikali inaunga mkono juhudu hizo za watanzania na wanakuwa washiriki wa kweli katika mnyororo wa thamani,” amesema.

Mratibu wa tuzo hizo, Deogratius Kilawe, amesema kwamba lengo la kuandaliwa kwa tuzo hizo ni kutengeneza ushindani wa soko kwa bidhaa za Afrika, na kuongeza huduma bora kwa wananchi.

“Mwaka wa nne tunawatambua wazalishaji hao sasa, watu walioshiriki kuwania ni takribani 5,000 hadi kufikia mchakato wa kampuni 500, kutoka katika nchi zaidi ya saba,” amesema Kilawe.

Photos from HabariLeo's post 14/06/2026

Kurasa za mbele HabariLEO Jumatatu Juni 15, 2026
Soma nakala yako kupitia kiunganishi cha http://epaper.tsn.go.tz

14/06/2026
14/06/2026

LINDI: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Hamid amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina thamini jasho la kila kwa Mtanzania, hivyo serikali itakikisha kila kundi la kijamii linaguswa ili kuhakikisha linafanikiwa na shughuli zote za kujitafutia mali sambamba na huduma zote zinatokana na serikali.

Rabia ameyasema hayo leo Juni 14, 2026 mkoani Lindi alipo kutana na kuongea na makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, vyama vya ushirika, baba lishe na mama lishe, maofisa Usafirishaji, wajane, wenye mahitaji maalum, viongozi wa Serikali za mitaa, viongozi wastaafu pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiliamali.

“Ndugu zangu Wanalindi, CCM inatambua jasho lenu katika kujitafutia mali kupitia shughuli zenu mbalimbali k**a kilimo, biashara na ujasiliamali, Serikali ya CCM itahakikisha inaweka mazigira wezeshi ili mnufaike na shughuli zenu zote” amesema Rabia.

Aidha, ameyaomba makundi mbalimbali ya kijamii, kuendelea kushirikiana na CCM kwa ukaribu zaidi, kwa kukipa ushauri, mawazo na kutoa changamoto ili kupitia hayo serikali ya CCM itazitafutia ufumbuzi.

Ameongeza kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuacha tabasamu la kweli kwa kila mtanzania na kwa makundi yote ya kijamii hivyo ni dhamira yake kuona anaugwa mkono, ili kuliletea maendeleo endelevu Tanzania letu na ndio maana katika mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali 2026/2027 imekusudia kutenga asilimia 15 ya mapato ya halmashauri kutoa asilimia 10 ya awali ili kuongeza wigo katika upatikanaji wa mikopo.

Pamoja na hayo ameelekeza Serikali ya Mkoa wa Lindi na Uongozi wa Chama kutenga muda na kufanya mikutano maalum ya kuyasikiliza makundi ya kijamii.

14/06/2026

DAR ES SALAAM; MBIO za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2025/26 zimezidi kunoga, baada ya leo Juni 14, 2026 Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
-
Kutokana na matokeo hayo Simba imefikisha pointi 61 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 63, huku kila timu ikiwa imebakisha michezo minne kumaliza ligi.
-

14/06/2026

DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara mbobezi wa masuala ya uchukuzi, usafirishaji na biashara za bandari ambaye pia ni Mkurugenzi wa MB KUU Group of Companies, Athumani Zuberi Mwesongo, amesema Tozo ya Maendeleo ya Miundombinu ya Bandari (PIDL) inayotarajiwa kuanza kutumika Julai 1, 2026 ni moja ya hatua muhimu za uwekezaji zinazolenga kuwezesha Tanzania kuendelea kuboresha na kupanua miundombinu ya bandari kwa viwango vinavyoweza kuhimili ukuaji wa biashara wa sasa na wa baadaye.
-
Amesema mataifa yaliyojenga bandari kubwa na zenye ushindani duniani k**a Singapore na Uholanzi kupitia Bandari ya Rotterdam yalifanikiwa kwa kuwa na mifumo endelevu ya kufadhili uwekezaji wa miundombinu ya bandari kwa muda mrefu.
-
Mwesongo amesema bandari ndiyo ateri kuu ya biashara ya dunia kwa sasa, huku zaidi ya asilimia 80 ya biashara zote za kimataifa zikisafirishwa kwa njia ya bahari.
-
Kwa mujibu wake, mafanikio ya bandari kubwa duniani hayakupatikana kwa bahati mbaya, bali yalitokana na uwekezaji mkubwa na endelevu uliowezesha maboresho ya miundombinu, ongezeko la uwezo wa kuhudumia mizigo na kuimarika kwa ushindani wa biashara za kimataifa.
-
Alisema hatua ya Tanzania kuendelea kutafuta vyanzo vya kugharamia maendeleo ya bandari ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na ukuaji wa biashara na mahitaji ya uchumi wa kisasa.
-
"Tukiiangalia Rotterdam peke yake, uwekezaji mkubwa uliofanyika umeiwezesha kuwa miongoni mwa bandari bora duniani. Mifumo ya tozo za maendeleo k**a hii imechangia kuiboresha, kuifanya iwe ya kisasa na kuongeza uwezo wake wa kuhudumia biashara za kimataifa. Hili si jambo geni, mataifa mengi yaliyofanikiwa kupitia biashara ya bandari yalishapitia njia hii miaka mingi iliyopita," amesema Mwesongo.
-
Ameongeza kuwa jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinasimamiwa kwa uwazi, zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wananchi kuendelea kupewa taarifa kuhusu matokeo ya uwekezaji huo.

14/06/2026

GEITA: KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilayani Bukombe imefanikiwa kuk**ata na kuwatoa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kigosi zaidi ya ng’ombe 11,700 walioingizwa kinyume cha sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Pasikasi Muragili alitoa taarifa hiyo juzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita katika mkutano wa hadhara wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Msangila.

Amesema ng’ombe zaidi ya elfu 10 waliondolewa kwa hiari baada ya tangazo la serikali huku ng’ombe 1,700 walipigwa faini baada ya wafugaji kukaidi tangazo la kutoa mifugo yao kwa hiari.

Muragili amesema kikao cha k**ati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bukombe na wafugaji kiliazimia kutoa siku saba mifugo yote iondolewe hifadhini na waliokaidi wamechukuliwa hatua.

“Baada ya muda wa hiari kuisha anayekutwa kule faini yake ni shilingi laki moja kwa ng’ombe mmoja, vinginevyo huyo ng’ombe anataifishwa”, amesema Muragili.

Amesema ofisi ya mkurugenzi imeshaandika barua kwa watendaji wa kata na vijiji vyote kuelekeza mtu yeyote ambaye siyo mkazi wa halmashauri hiyo hapaswi kuingiza mifugo bila utaratibu.

“Tumeanza kutoa elimu kwa wafugaji kwanza wamiliki maeneo ya malisho, kwa sababu uchunguzi unaonyesha wengi wao hawamiliki maeneo k**a ilivyo kwa wakulima.

“Mwaka huu tumeanzisha mashamba darasa la malisho ya mifugo kwa ajili ya wafugaji wajifunze, na tayari kuna mbegu zimetolewa na wizara ya mifugo”, amesema.

Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Yohana Shida

14/06/2026

GEITA: SERIKALI mkoani Geita imetangaza mpango rasmi wa kupokea taarifa za wauguzi na watumishi wa afya wanaofanya vitendo visivyo vya kiungwana kwa watu wanaohitaji huduma ya matibabu.

Mpango huo pia unahusisha upokeaji wa taarifa za watoa huduma wanaokaidi kwa makusudi sera ya huduma bure kwa watoto, wajawazito na wazee kwenye vituo vya huduma za afya.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dk Omari Sukari ametoa taarifa hiyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa alipotembelea ujenzi wa kituo cha Afya cha kijiji cha Msangila wilayani Bukombe.

Dk Sukari amesema ili kufanikisha hilo, kila kituo cha kutolea huduma za afya kitabandikwa eneo la wazi namba za mawasiliano za Mganga Mfawidhi wa eneo husika na Mganga Mkuu wa Mkoa.

Amesema hatua hiyo itasaidia kila mtu anayehitaji huduma anapokutana na kadhia ya makusudi inayosababishwa na jeuri ya mtoa huduma basi atoe taarifa mara moja kwa viongozi hao.

Dk Sukari amewataka watumishi wa afya kuendelea kuishi kiapo cha kazi na maadili kwa kuwatendea haki na kuwahudumia wagonjwa bila ubaguzi na unyanyasaji wa aina yeyote.

Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Yohana Shida

Want your business to be the top-listed Government Service?

Telephone

Opening Hours

Monday 07:30 - 05:30
Tuesday 07:30 - 05:30
Wednesday 07:30 - 05:30
Thursday 07:30 - 05:30
Friday 07:30 - 05:30
Saturday 09:00 - 04:00
Sunday 10:00 - 04:00