Mombasa Republican Council (MRC)

Mombasa Republican Council (MRC)

Share

It is not surprising that the MRC has frequ Introduction. So just who are the MRC? And exactly what are their motives? Secession.

The Mombasa Republican Council (MRC) has recently resurfaced in the media spotlight again after the government arrested some of its suspected members during an alleged oathing ceremony in Likoni, Mombasa County. It is not surprising that the MRC has frequently been getting in trouble with the law as it was among the 33 groups that were declared ‘illegal organized criminal groups’ by the Government

06/07/2016

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
6th. July 2016.
Tangazo! Tangazo! Tangazo!
Wapwani sote tunatangaziwa na kuhimizwa kwamba; kesi zetu za Rufaa (Appeal) Dhidi ya IEBC zilizoko Mahak**a Kuu Nairobi zinafanyiwa uamuzi Ijumaa tarehe 08/07/2016.
Tuhimizane, tuende na tujitokeze kwa wingi Nairobi tukazisikize sisi wenyewe kesi zetu mbali na kufanya kuambiwa. Gari ni Watu, nalo hili ndilo gari letu litakalo tuvukisha kwenye Ulimwengu wa Haki na usawa. Tudumishe Amani popote tulipo kwani viongozi wetu hawalali kwa kututafutia haki yetu kwa njia ya Amani. Tusikubali kuchochewa tukaingizwa msituni na mtu yeyote ili kuharibu utaratibu wa Amani uliopo.
Tushik**ane na UMOJA kwani Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu ( UNITED WE STAND DIVIDED WE FALL)
Tunawaombea Wapwani wenzetu walio Waislam EID yenye furaha.
ASANTENI

02/03/2016

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
3rd. March 2016.
Tangazo! Tangazo! Tangazo!
K**ati/ Branches zote za MRC munahitajika kuhakikisha kila Branch imegharamikia na kupeleka wafuasi wanne (4) au zaidi siku ya kesi mnamo tarehe 03/06/2016 Nairobi. Hala hala tuonyeshe ghera ili tuikamilishe tondo ya MPWANI. Branch itakayo keuka amri hii haitatambuliwa wala kuorodheshwa tena.
Michango iendelee k**a kawaida ili kukimu ada ya mawakili na kuwawezesha viongozi wetu kuhudhuria kesi hizo bila tatizo.
Tunawaomba mudumishe amani na tuwe watulivu Pwani kote. Tusikubali kupotoshwa, kutumiwa na wanasiasa pamoja na vitengo vya usalama visvyo. Kwani malengo ya MRC ni kuikomboa nchi ya PWANI kwa amani bila umwagikaji wa damu. Ahsanteni.
UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU!!.

27/02/2016

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
27th. Feb. 2016.
TAARIFA YA KESI:
Enyi ndugu Wapwani Wazalendo, nimatumaini yetu nyote muko wazima.
Tungependa kuwaarifu ya kwamba kesi yetu dhidi ya IEBC imeweza kusikizwa kwa ukamilifu. Mahak**a imeafikia kutoa uamuzi tarehe 03/06/2016. Siku hio pia kutatolewa Maamuzi ya kesi kuhusu uharamu wa Vuguvugu la MRC.
Tunawaomba muzidi kuwa watulivu, wavumilivu, wenye busara, hekima na subra hasa katika kipindi hichi cha lala salama. Tusijihusishe na michafuko na majopo ya kisiasa. Chamsingi tunawaombeni kila Branch/K**ati kujizatiti kwa michango itakayotuwezesha kukimu mahitaji ya mawakili na usafiri. PAMOJA BEGA KWA BEGA KUIKOMBOA PWANI. Ahsanteni.

04/02/2016

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
04th. Feb. 2016.
TAARIFA YA KESI:
Enyi ndugu Wapwani Wazalendo, nimatumaini yetu nyote muko wazima, tunawatangazia tarehe ya kesi yetu ya rufaa (appeal) ni tarehe 26/02/2016 Nairobi, kesi al-maaruf ya IEBC. Tunawaomba muwe watulivu, wenye busara na hekma na wavumilivu. Tunafahamu ndugu mumejawa na huzni na ghadabu jinsi serikali inavyowahangaisha viongozi wetu Mzee Omar Mwamnuadzi na wenziwe bali tunawasisitiza kuwa na subra kwani kila jambo na wakati maadam ni haki yetu ipo siku itasimama. Tunawaombeni kila Branch yetu imchangishie nauli (tikiti) hata k**a ni mtu mmoja kwa uchache, tuhudhurie kwa wingi panapo majaliwa yake Maulana. UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU (UNITED WE STAND, DEVIDED WE FALL) Ahsanteni.

17/07/2015

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
18th. July 2015.
TAARIFA YA KESI:
Enyi ndugu Wapwani Wazalendo, nimatumaini yetu nyote muko wazima. Tunawatangazia tarehe ya kesi yetu ya rufaa (appeal) ni tarehe 23/7/2015 Nairobi. Kesi al-maaruf ya IEBC.
Tungependa kuwatanabahisha Wapwani wasihadaiwe na propaganda zinazoenezwa eti MRC wamepata silaha za kupigana na serikali ya Kenya, huo ni uzushi!!. Pia habari za kuwa mambo yamekwisha nchi tumepatiwa hazina misingi. Hizi ni propaganda kutaka kuzorotesha bidii ya wakereketwa haswa wale wanaojitolea kimichango kuendesha harakati hizi. Tunawafahamisha kesi yetu bado tunaifatilia kwa ustadi na tunawaomba tusichoke kuchangisha kwa ajili ya wakili na viongozi waweze kuhudhuria kotini Nairobi, K**a tujuavyo harakati zetu ni za walala hoi lazima nasi tuwatie moyo na shime.
Hayawi hayawi mwisho yatakuwa, muhimu tuwe watulivu, wenye busara na hekma na wavumilivu, kwani kila kitu na wakati wake maadam haki ipo. Tunawaombeni kila Branch yetu imchangishie nauli (tikiti) hata k**a ni mtu mmoja kwa uchache, tuhudhurie kwa wingi panapo majaliwa yake Maulana. UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU (UNITED WE STAND, DEVIDED WE FALL) Ahsanteni.

Mobile uploads 08/03/2015

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
09th. March 2015.
TAARIFA YA KESI:
Enyi ndugu Wapwani Wazalendo, nimatumaini yetu nyote muko wazima. Tunawatangazia tarehe ya kesi yetu ya rufaa (appeal) ni tarehe 25/03/2015 Nairobi, sawa na barua inavyo onyesha hapo chini. Kesi al-maaruf ya IEBC. Hayawi hayawi mwisho yatakuwa, muhimu tuwe watulivu, wenye busara na hekma na wavumilivu, kwani kila kitu na wakati wake maadam haki ipo. Tunawaombeni kila Branch yetu imchangishie nauli (tikiti) hata k**a ni mtu mmoja kwa uchache, tuhudhurie kwa wingi panapo majaliwa yake Maulana. UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU (UNITED WE STAND, DEVIDED WE FALL) Ahsanteni.

Mobile uploads 22/12/2014

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]
22nd. Dec. 2014.
TAARIFA YA KUAHIRISHWA KWA KESI: Habari zenu Wapwani wazalendo, nimatumaini yetu kila mtu wa Pwani popote alipo ni mzima wa afya, anasikizia ili apate kujuwa kesi yetu ya tarehe 17/12/2014 ilikuwaje. K**a mnavyo ona hiyo barua hapo chini, barua hii ilitoka mahak**ani juzi tarehe ya kesi, ambapo iliahirisha kesi yetu al-maarufu kesi ya IEBC, kesi hii iliahirishwa kwa sababu Mahakimu wawili walienda likizoni na haiwezekani kuzungumzwa na Mahakimu watatu, pia haiwezi kubadilishiwa mahakimu wengine tofauti na wale walioisikiliza ya uharamu. Wapwani wapendwa na Wazalendo, kufuatia hilo, tunawaomba tuwe watulivu na watu wenye busara kwani Wahenga walinena; njia ya mrongo ni fupi, tuwe na subra na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu tutafika tuliko lenga na ikizidi k**a alivyo ahidiwa mwenye kusubiri nikwamba kadiri tunavyozidi kusubiri kheri nayo inazidi kutusongelea, kwani subra huvuta kheri. Natusubirini, Mahakimu watakapo ingia mwezi wa kwanza wataketi chini watupangie tarehe ya kesi yetu. Kingine cha msingi, tafadhalini Wapwani, Mawakili wetu wanahitaji pesa, michango yetu k**a tunavyojuwa ndiyo inawasimamia Mawakili wetu, mwito wetu nikwamba sehemu tunazopeleka michango ya pesa tunazijuwa, basi tufanye hima tuipeleke michango yetu ili iweze kusimamia jambo letu. Ahsanteni! UNITED WE STAND, DIVIDED WE FALL .

27/11/2014

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]


27th. November, 2014.
TAARIFA YA KUTANGAZA TAREHE YA KOTINI.

Ndugu Wazalendo wa Pwani hamjambo? Tuamkeni; k**a mnavyo juwa Vuguvugu letu la The Mombasa Republican Council (MRC), tunafuata sheria ndiyo maana tukapeleka kesi zetu zote mahak**ani. Kunayo kesi yetu moja al-maarufu kesi ya IEBC kesi ambayo tuliish*taki IEBC na vitengo vingine tisa (9) vya serikali vinavyofanya kazi zake pasipo kufuata utaratibu wa sheria yaani kimaonevu, kuwaonea watu hasa wa Pwani, hivyo basi tumeitisha kura ya maoni (referendum) hapa Pwani kwenye kesi hiyo, lengo haswa nikujitoa kwenye minyororo ya wakoloni weusi wanaotukandamiza sawasawa na tulivyokuwa sisi wa Pwani hapo karne za 15, 16, 17, 18 na hata zaidi ya nusu ya karne ya 19 Waingereza walipo peana uhuru Kenya na wakatuchanganya pamoja ili tupate kulindwa kwa vile Kenya watakuwa na serikali kamili, tukadhania eti tutapumzika shida kumbe tunaruka matope tunakanyaga kinyesi. Hivi sasa kesi iliyo mbele yetu ni ile ya IEBC inayosikizwa (Hearing) tarehe 17th December 2014. Wapwani wazalendo, k**a tujuavyo hatuna wafadhili wakutufadhili na shughuli hizi zetu isipokuwa wafadhili ni sisi wenyewe na hivi sasa Mawakili wetu wanahitaji pesa za kugharamia kesi zetu, Enyi wapwani, tuendelee kufuata mtindo aliokuwa akiufanya Baba yetu Baba wa Wapwani mkombozi wetu na shujaa wa Pwani Hayati Ronald Gideon Ngala. Baba yetu huyu alikuwa wakati anafanya shughuli za ukombozi, huitisha michango, nao wapwani kwa uzalendo wao walikuwa wakimchangishia kwa kima akitakacho na akaendeleza shughuli pasipo na kudeteleka huku wala kule. Mpaka ilipofika wakati wa kuiteremsha bendera ya Sultan hapa Pwani, Wapwani wazalendo walifanya kazi ya ziada, wakamchangishia Baba yetu Ronald Ngala akiwa Uingereza kwenye mikutano ya Lancaster House, wakampelekea kukohuko naye kwa heshima yake akamkabidhi pesa hizo kiongozi waliyekuwa wamempisha mbele kuongoza Kenya (Hayati Mzee Jomo Kenyatta) apeane kwa Sultan wa Zanzibar. Pesa hizo ndizo zilizopelekea kuandikwa kwa mikataba hapo mwaka 1963 na hata kuiteremsha bendera ya Sultan hapa Pwani. Basi tunawaomba wapwani sote tuige mfano uohuo na wala tusichoke kwani kupata uhuru sio kazi rahisi wala ndogo.


TAHADHARI.
Tahadhari hii tumeitoa kwa wapwani wazalendo tutahadharini dhidi ya wapwani wenzetu na wanaopata shida k**a sisi tunavyozipata, lakini lakushangaza nikwamba, wapwani wawahawa wanazunguka wakieneza uongo na uvumi usiokuwa na faida yoyote kwa Mpwani ila kumrudisha nyuma mpwani. Propaganda za kuwapotosha wapwani eti mambo yamekwisha, sasa hivi tutapatiwa nchi yetu kwani Wazungu wameshakuja tayari kutupatia nchi yetu. Huu ni uongo na ni njia moja au nyengine ya kumlemaza akili Mpwani aone ugumu wa kuchangisha pesa, hizi ni propaganda potofu na wala hazifai kuketi kwenye akili zetu haswa kwetu sisi jamii ya Pwani. Hawa ni watu wanaotumiwa na maadui zetu wasiotaka kumuona Mpwani akifurahia matunda ya uhuru wake. Watu k**a hawa tunafaa kuwakemea k**a shetani anavyo kemewa na kulaaniwa. Sisi k**a viongozi, tumeketi na kulizungumzia jambo hili na hivi sasa tumepitisha kuwafuatilia watu hawa, mmoja baada ya mwengine na k**a mnavyofahamu sisi kila kitu chetu tunakifuatilia kisheria, sisi tumeshaanzisha uchunguzi wetu dhidi ya watu hawa, pindi tutakapokamilisha uchunguzi wetu, basi watu hawa wajue watakiona cha mtema kuni. Sisi tutawaandama na mkono wa sheria mpaka tuhakikishe wamefika mbele za sheria na wajieleze na kujitambulisha mbele ya watu wa Pwani na mahak**a endapo nyadhifa hizo za kukutana na wafadhili wa Umoja wa Mataifa (UN) kuifadhili MRC na Wapwani kwa jumla walizipata vipi. Itakuwaje k**a kweli ni wafadhili wa MRC kusiwe hata kiongozi mmoja aliyekutana na wafadhili hao? Hayo yote ni maneno ya kufitinisha, basi watu hao tunawajuwa mmoja baada ya mwengine, tunawafuatilia na shughuli zao kila wanapopitia ili tukamilishe uchunguzi wetu. Kila siku wanawadanganya watu tarehe Fulani tutapatiwa nchi yetu na siku zinakuja zikipita watu hawa ni waongo, wanafiki, wachochezi, wafitini wa kutufitinisha sisi wenyewe kwa wenyewe tutofautiane mwisho tuanze kukosana na kuteta ambapo Serikali ndivyo inavyotaka, mwisho wapange njama za kutuuwa. Sisi nasi kwakuwa tumegonganishwa tuanze kuonyeshana vidole wenyewe kwa wenyewe na hata kupelekea kuhasiriana ambapo adui huyo wetu ndio atapata nguvu zaidi kulilemaza jambo letu. K**a mnavyojuwa kunazo njia nyingi za kusafiri; kwa ndege, gari, meli, baisikeli na hata kwa miguu, sisi wenyewe mwendo wetu ni kwa miguu, tusimkubalie mtu yeyote mwenye nia ya kutushika nguo akituregesha nyuma ama kututembeza kwa kifua. Kwa hivyo Wapwani Wazalendo tuwe na subra tusikubali mtu yeyote kututowa kwenye timing ya sheria na tukajiingiza kwenye mitego isiyokuwa mipango yetu, kwa sababu waswahili husema kikulacho kinguoni mwako, basi tusipo kuwa waangalifu kwa jambo hili tutalitia michanga sisi wenyewe kupitia kwa hao maadui wetu wakitutumia sisi wenyewe, “ASHINDWE PEPO”. Ndugu zetu Wapwani, tujue yakwamba kilicho na mwanzo, hakikosi mwisho na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujuwa kilakitu hata mwisho wa ukombozi wa nchi yetu. Kwa hivyo tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kila jambo letu na kumuomba azidi kutupatia “SUBRA”. Sisi viongozi wenu tunapitia wakati mgumu na mitihani mingi sana lakini tuko na subra kwani tunajuwa jambo hili ni lazima liwe na mitihani ya kiaina yake na nilazima pia tuivumilie tukimtegemea Mwenyezi Mungu, nanyinyi pia mtuonee huruma na mtuombee Mola wetu atuzidishie subra tuliyonayo na tuzidi kusonga mbele kuzipigania haki zetu za Wapwani kwa kutumia sheria mpaka tutakapo zitia mikononi haki hizi na kujitawala wenyewe.
Mwisho tujue yakwamba, hakuna mtu yeyote atakaye toka nje ya Pwani atuonee huruma na kutuleta kuwa kitu kimoja pasipo, kubaguana sisi kwa sisi kidini, rangi na kikabila ila ni sisi viongozi wa MRC tukishirikiana na viongozi wa mashinani na wafuasi sote k**a kitu kimoja ndiposa tulishinde “JINAMIZI” hili lililo tukalia na kutukandamiza bila hata ya huruma. Ushirikiano ni kitu bora.

“EWE MWENYEZI MUNGU, IBARIKIE PWANI NA UTUBARIKIE PIA SISI WA PWANI, UTUFUNGULIE MLANGO WAKUONA VILE TULIVYO TAWANYWA NA MAADUI ZETU, UTUONDOSHEE KILA AINA YA BALAA HAPA KWETU PWANI, WANAOTUDHULUMU HAKI ZETU UWAONYESHE NJIA YA KUTUTENDEA HAKI, UTUPATIE AMANI NDANI YA NCHI YETU YA PWANI, UWAADHIRISHE WANAFIKI WOTE WANAOENDA KINYUME NA HATA WALE WATAKAO ENDA KINYUME CHA VIONGOZI WETU WA MRC, UWAONGEZEE NGUVU, MAARIFA NA MSHIKAMANO VIONGOZI WETU WA MRC, TUZIPATE HAKI ZETU, TUIKOMBOE NCHI YETU YA PWANI NA TUISHI KWA AMANI, AMIN !!!
“UNITED WE STAND, DIVIDED WE FALL”.

30/09/2014

WANADAI MRC NI KUNDI HARAMU NA KULINASIBISHA NA SHABABU. TUNAWAAMBIA WAFIKE KOTINI WASAIDIANE KUMPA MKUU WA SHERIA HOJA ZA KUPINGA UAMUZI ULIOTOLEWA MAHAKAMA KUU MOMBASA KULIHALALISHA VUGUVUGU LA MRC.
KESI ZETU ZIKO KOTINI ZIMEWASAKAMA WAMEBAKI KUZIAHIRISHA KIHOLELA.

https://m.facebook.com/home.php?soft=notifications #!/dw.kiswahili

27/08/2014

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]

27thAugust 2014

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, Sifa zote zinastahili zielekezwe kwake.
Hamjambo! wapendwa Wapwani, tunafuraha kuwatangazia tarehe ya kesi ya rufaa (appeal) yetu ya kutaka kura ya maamuzi (referendum) ya hapa Pwani, maarufu kesi ya IEBC. Sasa hivi timewekewa tarehe ni 27/ 10/ 2014 k**a mnavyo iona hapa. Ndugu zetu Wapwani, tunawaomba tuendelee kuwa watulivu, tusikubali kutumiwa na watu wasio ipenda MRC kwa kutudanganya na kujiingiza kwenye vitendo viovu vya kusababisha utovu wa usalama, uhasama na hata kuchukiana sisi wenyewe kwa wenyewe na kumuacha adui akisherehekea. Wapwani tunawaomba kujuwa yakwamba haraka ni ya shetani ndio maana ikanyimwa Baraka na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu atuongoze kikamilifu ili tuyafikie malengo yetu, Amin.
Asanteni

01/08/2014

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]

1st August 2014
TAARIFA TAARIFA TAARIFA
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, Sifa zote zinastahili zielekezwe kwake.
hivi ndivyo appeal yetu dhidi ya IEBC iliyokuwa isikizwe jana tarehe 31/7/14 ilivyoendelea:
Jana ilikusa kesi hii iendelee, lakini kwa sababu zisizoweza kuepukika, wakili anayeiwakilisha serikali kwa jina Njoroge yuko na kesi nyengine katika Supreme court ambayo pia anaiwakilisha serikali dhidi ya vyombo vya habari na mfumo wa Digital.
Kwa sababu hiyo kesi yetu iliweza kuahirishwa. Baada ya siku 21 mawakili wa pande zote mbilli watafika kwa Registrar wachukue tarehe nyengine.
Wafuasi wetu wanaombwa wawe watulivu na tudumisheni amani, tusife moyo na tuwe na subra kwani hakuna refu lisilokuwa na mwisho. Tuvumilieni, kufika tutafika na haki tutaipata kwa uwezo wa Mungu.
Asanteni
Wenu,
Randu Ndzai Ruwa ______________
Richard Lewa Mwadena __________
Malembi Mwatsahu Munga _______
Mwadadu wa Mwamtewe ________
Omar F***j (Suchmore) __________
Pastor William Mzungu __________
Killian Chireri Munga ____________
Mwero wa Dukwe ______________

22/07/2014

THE MOMBASA REPUBLICAN COUNCIL
(MRC)
P.O. BOX 81510 MOMBASA
EMAIL: [email protected]

22nd July 2013
TAARIFA
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, Sifa zote zinastahili zielekezwe kwake.
Tungependa kuchukua fursa hii kuwatangazia ya kwamba kesi zetu zote mbili zimepangiwa kufanyika tarehe 31-07-2014, Alkhamis. Katika mahak**a kuu Nairobi.
Tunawaomba ndugu zetu watakaojaaliwa kupata fursa wafike kwa wingi. Hii ndio itakuwa siku ya uamuzi wa mwisho, na sisi tuko tayari kwa uamuzi wowote kwani tunaelewa mahak**a za kenya zinaendeshwa ki imla. Wala hatutakufa moyo wala kukomea hapo hadi tupate haki yetu.
Tunawasihi ndugu zetu wa Pwani wawe watulivu wala wasitiwe wasiwasi na hali ya utovu wa usalama. Tusijihusishe na vikundi au uhalifu wa aina yoyote, kwani serikali inatafuta sababu ya kusambaratisha vuguvugu na lengo letu la ukombozi kwa jumla. Tulipotoka ni mbali, tunapoenda ni karibu lakini mitihani ndio migumu.
Hatuna mengi kwa sasa. Tudumisheni amani, umoja na tuombeane kheri tutafanikiwa
Ahsanteni,
Wenu,
Randu Ndzai Ruwa ______________
Richard Lewa Mwadena __________
Malembi Mwatsahu Munga _______
Mwadadu wa Mwamtewe ________
Omar F***j (Suchmore) __________
Pastor William Mzungu __________
Killian Chireri Munga ____________
Mwero wa Dukwe ______________

Want your business to be the top-listed Government Service in Mombasa?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


1 Mombasa
Mombasa