NYOTA YA JOMVU

NYOTA YA JOMVU

Share

JOMVU 1 ~ MOMBASA COUNTY 001

Former Mombasa Deputy Mayor

Former MCA Jomvu Kuu

Political Advisor to the president

Photos from NYOTA YA JOMVU's post 01/06/2026

Leo ni siku ya kihistoria kwa taifa letu tunapoadhimisha Madaraka Day katika Kaunti ya Wajir.

Nimefarijika kuona uongozi wa Rais Dkt. William Samoei Ruto ukichukua hatua madhubuti za kurekebisha changamoto za muda mrefu zilizokwamisha maendeleo ya Kaskazini mwa Kenya.

Uwekezaji mkubwa katika elimu, afya, makazi nafuu, miundombinu na sekta ya mifugo ni ushahidi kuwa kila sehemu ya Kenya ina nafasi sawa katika safari ya maendeleo ya taifa letu.

K**a Mshauri wa Kisiasa wa Rais, ninaunga mkono dhamira hii ya kuhakikisha hakuna Mkenya wala eneo lolote linaloachwa nyuma kutokana na historia, jiografia au siasa.

Tuendelee kushirikiana kujenga Kenya yenye usawa, fursa na maendeleo kwa wote.

Hon. Karisa Nzai Munyika
Mshauri wa Kisiasa wa Rais, Ikulu 🇰🇪

01/06/2026

Rais Wa Jamuhuri ya Kenya
Dr.William Samoe Ruto

Happy Madaraka Day 2026

William Samoei Ruto Aden Duale

01/06/2026

Leo ni historia kubwa kwa wananchi wa Wajir na eneo zima la Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Kwa mara ya kwanza katika miongo mingi, Wajir imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa sherehe kuu za kitaifa, jambo linalodhihirisha dhamira ya serikali ya kuhakikisha kuwa hakuna sehemu ya Kenya inayobaki nyuma katika maendeleo na ushirikishwaji wa kitaifa.

Tunapowaenzi mashujaa wetu waliopigania uhuru wa taifa letu, tunasherehekea pia hatua kubwa zinazopigwa katika kuunganisha Wakenya wote kupitia maendeleo ya miundombinu, huduma za kijamii na fursa za kiuchumi.

Uongozi wa Rais William Ruto unaendelea kufungua ukurasa mpya wa maendeleo jumuishi ambapo kila kaunti na kila mwananchi anahesabika.

Heri ya Siku ya Madaraka ya 63. Pamoja, Tujenge Kenya Bora. 🇰🇪

Hon. Karisa Nzai Political Affairs Office of the President 🇰🇪

01/06/2026

Tunapoadhimisha miaka 63 ya Madaraka ya Kenya, tunawakumbuka na kuwaenzi mashujaa wetu waliopigania uhuru, haki na heshima ya taifa letu. Ujasiri na kujitolea kwao ndiko kulikoweka msingi wa Kenya huru tunayoijenga leo.

Kwa wananchi wa Jomvu na Wakenya wote, tuendelee kuimarisha umoja, kudumisha amani, kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana katika kujenga uchumi imara na maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Tukiwa wamoja, hakuna linalotushinda. Pamoja Tujenge Kenya Bora.
Heri ya Madaraka Day 2026!

Hon. Karisa Nzai
Political Affairs
Office of the President 🇰🇪

29/05/2026

Apa kuna Ukweli

4:1

Arsenal

Photos from NYOTA YA JOMVU's post 29/05/2026

Kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate uhuru, eneo la Kaskazini Mashariki linaendelea kushuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa yenye kuleta mageuzi ya kweli kwa wananchi. Ujenzi wa Uwanja wa Wajir, ambao ni wa kwanza wa aina yake katika Kaunti ya Wajir na eneo lote la Kaskazini Mashariki, unaonyesha dhamira ya serikali katika kuhakikisha maendeleo ya usawa na ukuaji shirikishi kwa maeneo yote ya Kenya.

Uwanja wa Wajir ambao sasa umekamilika kwa asilimia 99, uko tayari kabisa kuandaa sherehe za 63 za Madaraka Day. Maandalizi yako katika hatua za mwisho huku wadau wote wakijitolea kuhakikisha hafla hiyo inakuwa ya mafanikio na ya kukumbukwa.

Wajir ipo tayari kikamilifu kuwa mwenyeji wa sherehe hizi za kihistoria za kitaifa. Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. William Samoei Ruto, kuichagua Wajir kuwa mwenyeji wa sherehe za mwaka huu ni heshima kubwa kwa wananchi wa Wajir na eneo zima la Kaskazini Mashariki, pamoja na uthibitisho kwamba kila sehemu ya Kenya inastahili kutambuliwa, kujumuishwa na kuendelezwa kwa usawa.

29/05/2026

Siku ya pili baada ya kuapishwa kuwa Mbunge wa Jomvu Constituency, nitaunda kamati madhubuti ya usimamizi wa utoaji wa bursary ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa heshima, uwazi na wakati unaofaa.

K**ati hiyo itahakikisha hakuna kupanga foleni kwa wananchi katika ofisi za CDF au kwenye kumbi mbalimbali ndani ya Jomvu. Familia zote zitafikiwa mapema na kuhudumiwa kwa utaratibu unaostahili.

Bursary kwa wanafunzi itakuwa kiwango cha KSh 10,000 ili kusaidia watoto wetu kuendelea na masomo bila vikwazo vya kifedha.

Pia tutaanzisha mpango wa “Mtoto Asome” utakaohakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni na kubaki darasani hadi jioni kabla ya kurejea nyumbani.

Tuta jenga TVET na taasisi za mafunzo kwa kutoa mafunzo ya ujuzi mbali mbali, pamoja na vifaa halali vya kazi ili vijana wetu waweze kujiajiri na kupata ajira kupitia ujuzi watakaopata.

Vilevile, kila kampuni iliyopo ndani ya Jomvu Constituency italazimika kutoa nafasi za ajira kwa angalau vijana 10, kila mwaka, kutoka kila ward ya Jomvu ili kuhakikisha vijana wetu wanapata fursa za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.

Photos from NYOTA YA JOMVU's post 28/05/2026

Apa lugha ni moja Tu

"Nataka Kuona Jomvu yenye uwezo."

Ministry of Education

Ministry of Energy

28/05/2026

Hamjambo!

Bila chuki yeyote,

Leo taja Kile kizuri nimewai fanya kwako ama kwa kuskia!

27/05/2026

Ziara Ya Rais ya siku tano zilizopita Juzi tulishuhudia maendeleo mengi na sehemu nyingi za maeneo bunge kufaidi.

Nilitamani sana Ningekuwa Mbunge wenu!

Naona Opportunity nyingi na Njia nyingi za Kusongeza Jomvu mbele ila tu!

Jomvu Nani Alituroga?

Want your business to be the top-listed Government Service in Mombasa?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Mombasa