Rs Katavi

Directions Website

Rs Katavi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Rs Katavi, Government Organization, Toundoute.

07/10/2026

TANESCO KATAVI YAWAKUTANISHA WADAU KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 5 hadi 9, 2026, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewakutanisha wateja wake wakubwa na wadau muhimu mkoani Katavi kwa ajili ya kujadili namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma na kupokea maoni yatakayosaidia kuongeza ufanisi na kuimarisha uhusiano na wateja.

Kikao hicho kilichofanyika leo, Oktoba 7, 2026, katika Ukumbi wa Katavi Resort, ni sehemu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TANESCO katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja. Shughuli hizo ni pamoja na kutoa zawadi kwa watu wenye mahitaji maalum kwa kugawa baiskeli za kutembelea kwa watu wenye ulemavu, pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupikia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Nehemia James, amelipongeza TANESCO kwa kuwakutanisha wadau hao, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuboresha huduma na kuimarisha uhusiano kati ya shirika na wateja wake.

“Hii ni siku ya tatu, lakini ni siku ambayo mmemuwakilisha vyema Mhe. Mkuu wa Mkoa. Niwapongeze na niwashukuru TANESCO kwa juhudi hizi, pia kuitisha kikao hiki cha wadau wakubwa na muhimu kwa shirika kujadiliana na kupongezana. Tunatambua umuhimu wa wateja katika uhai wa taasisi na mashirika yetu, kwani wateja ndio msingi wa uwepo wetu,” amesema Bw. Nehemia.

Kaulimbiu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu ni The Extra Mile, inayolenga kuhamasisha wafanyakazi kuendelea kuongeza juhudi na kufanya zaidi katika kuwahudumia wateja.

TANESCO KATAVI YAWAKUTANISHA WADAU KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja il...

MACHINGA WAJIANDAA KUSHIRIKI WIKI YA MWANAKATAVI 2026, WAAHIDI MAMBO MAKUBWA

Machinga mkoani Katavi wameahidi kushiriki kikamilifu katika Wiki ya Mwanakatavi 2026, huku wakieleza kuwa wamejiandaa na mambo mbalimbali kuelekea maadhimisho hayo.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Bandari ya Karema, Halmashauri ya Wilaya ya Tangan...
06/10/2026

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Bandari ya Karema, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kagwira–Karema, Hal...
06/10/2026

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kagwira–Karema, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

06/10/2026
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Skimu ya Umwagiliaji Mwamkulu, Halmashauri ya Mani...
06/10/2026

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, katika Skimu ya Umwagiliaji Mwamkulu, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

RC MRINDOKO APONGEZA UTENDAJI KAZI BANDARI YA KAREMAMkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amepongeza utendaji...
06/10/2026

RC MRINDOKO APONGEZA UTENDAJI KAZI BANDARI YA KAREMA

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amepongeza utendaji kazi wa bandari ya Karema, akisema maboresho ya miundombinu yaliyofanywa na Serikali yameongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia shughuli za biashara na usafirishaji, ikiwemo kutoka na kwenda nchi jirani.

Mhe. Mrindoko alitoa pongezi hizo jana Oktoba 6, 2026, wakati wa ziara yake katika bandari hiyo, ambapo amesisitiza kuwa uwekezaji katika miundombinu umeifanya Karema kuwa sehemu muhimu ya kuchochea biashara na uchumi wa Mkoa wa Katavi.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya usimamizi wa shughuli katika bandarini hapa, hii inatokana na maboresho yaliyofanywa na Serikali yameongeza uwezo wa Bandari ya Karema na kufungua fursa kubwa zaidi za biashara ndani ya nchi na na nchi jirani,” alisema Mhe. Mrindoko.

Alisema kuimarika kwa bandari hiyo kutarahisisha usafirishaji wa bidhaa, kuongeza shughuli za kibiashara na kutoa mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutumia fursa zinazopatikana kupitia eneo hilo.

Aidha aliwataka watendaji wa bandari ya Karema kuendelea kutoa huduma kwa weledi, ufanisi na kuzingatia viwango vinavyokidhi mahitaji ya watumiaji, ili fursa zinazotokana na maboresho ya miundombinu zitumike kikamilifu.

“Tunataka kuona Bandari ya Karema ikiendelea kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji kwa Katavi na nchi jirani, kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha huduma zinakuwa bora, salama na zenye tija kwa wananchi na Taifa,” alisema.

Mwisho.

RC MRINDOKO: BARABARA YA KAGIRWA–KAREMA SASA MKOMBOZI WA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI KATAVIMkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwa...
06/10/2026

RC MRINDOKO: BARABARA YA KAGIRWA–KAREMA SASA MKOMBOZI WA SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI KATAVI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amesema ujenzi wa barabara ya Kagirwa–Karema wenye thamani ya Shilingi bilioni 112.1 unaoendelea utachochea shughuli za usafirishaji kati ya Katavi na mikoa pamoja na nchi jirani, hatua itakayoongeza fursa za biashara, kilimo na kukuza uchumi wa mkoa.

Akizungumza na wananchi wa Kaseganyama Oktoba 5, 2026, wakati akitembelea kipande cha Kasekese–Ikola katika Wilaya ya Tanganyika, chenye urefu wa kilomita 56.9, RC Mrindoko aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara hiyo ili iweze kuleta tija katika kukuza uchumi wa mkoa wa Katavi.

“Serikali iliahidi, ikapanga mpango, ikaleta fedha na sasa barabara tumeanza kuiona. Siku zote mahali ambapo barabara ya lami imepita, maana yake imekuja kuchochea maendeleo, kuchochea biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi. Niwaombe sana tumieni vizuri nafasi hiyo, tumieni vizuri fursa hiyo,” amesema RC Mrindoko.

Kutokana na ujenzi wa mradi huo kufikia asilimia 60, RC Mrindoko amesema maeneo yanayopitiwa na barabara hiyo yanaendelea kuongezeka thamani na kuwa na fursa zaidi za kiuchumi, hivyo amewataka wananchi kutunza ardhi wanazomiliki kisheria na kuepuka kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya misitu, barabara na ushoroba wa wanyamapori.

“Tunzeni vizuri ardhi zenu kwa sababu ardhi itaongezeka thamani na bei. Sasa usije ukakurupuka kuuza sasa hivi, halafu baadaye ukasema kwa nini nilifanya hivi. Ila tahadhari yake ni kwamba usije ukatamani kutunza ardhi isiyo yako, yaani ardhi iliyotengwa na kuzuiliwa kwa mujibu wa sheria, k**a vile maeneo ya misitu, pembezoni mwa barabara na ushoroba wa wanyama,” amesema Mrindoko.

Katika kipindi hiki ambacho nchi imetabiriwa kupata mvua za El Niño, RC Mrindoko amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufanya usafi katika maeneo yao, kusafisha maeneo ya kutolea taka, kuzibua mifereji na kuhamia maeneo salama iwapo wanaishi katika maeneo ya mabondeni, ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

Address

Toundoute

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rs Katavi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share