Public Procurement Appeals Authority - PPAA

Call Directions Website Contact the organization

Public Procurement Appeals Authority - PPAA Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Public Procurement Appeals Authority - PPAA, Government Organization, Mkandarasi Place, 58 Lusinde Road, 41104 Tambukareli, Arusha.

Public Procurement Appeals Authority – PPAA is an independent institution under the Ministry of Finance and Planning mandated to hear and determine appeals/complaints arising from public procurement processes with a view to check compliance with the law Vision - A dispute resolution organ that commands stakeholder’s confidence

Mission - To determine bidders disputes arising from public procurement process fairly and timely to ensure adherence to the governing Law.

Buriani
22/09/2026

Buriani

MAKUNDI MAALUM LINDI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA ZABUNI ZA UMMA…wanolewa kuhusu njia za kudai haki katika zabuni za...
17/09/2026

MAKUNDI MAALUM LINDI WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA ZABUNI ZA UMMA

…wanolewa kuhusu njia za kudai haki katika zabuni za umma

Na Mwandishi wetu, Lindi
Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika zabuni za Umma ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Lindi, Bi. Alusaria Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima katika Kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) jana mkoani Lindi.

Bi. Mushi amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya kuwainua wananchi kiuchumi kupitia mifumo ya ununuzi wa umma ambapo mifumo hiyo imekuwa ikiwawezesha wazabuni kushiriki kwa haki na uwazi, na haki zao zimekuwa zikilindwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za ununuzi wa umma.

“Sheria na Kanuni zinaruhusu mtu au kikundi cha watu wenye mahitaji maalumu kupata fursa ya mkopo wa kategoria ya makundi maalumu ambapo mmetengewa asilimia 30 kwa vijana, wanawake wazee na watu wenye mahitaji maalumu, sasa kazi kwenu wana-Lindi kuchangamkia fursa hiyo. Ila changamoto kubwa ya ninayoiona kwenu k**a makundi Maalumu siyo fursa, bali ni utayari wa kuchangamkia fursa hizo,” amesema Bi. Mushi

Aidha, Bi. Mushi ameitaka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kuendelea kuwajengea uwezo Vijana, Wanawake, Wazee na Watu wenye mahitaji maalumu uelewa juu ya haki zao katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa.
“Naomba PPAA muendelee kuwajengea uwezo vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kujua namna ya kudai haki zao pale wanapoona hawakutendewa haki katika zabuni walizoomba Serikalini, kwani baadhi yao wamekuwa waoga au hawajui mahali pa kudai haki zao,” ameongeza Bi. Mushi

Pamoja na mambo mengine, Bi. Mushi amewasihi washiriki wa kongamano hilo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na ununuzi wa umma ili kuwawezesha kunufaika kiuchumi na kwa maendeleo yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla lakini zaidi kwa maendeleo ya Mkoa wa Lindi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Sehemu ya Mashauri kutoka PPAA, Bi. Violet Limilabo ambaye alimwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika kongamano hilo, amesema PPAA imeendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu haki na wajibu wa wazabuni katika michakato ya ununuzi wa umma, hususan matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa pale wanapoona hawakutendewa haki.

Bi. Limilabo ameongeza kuwa, elimu hiyo inalenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na imani ya wadau katika mfumo wa ununuzi wa umma, huku ikichochea ushiriki wa makundi mbalimbali katika shughuli za kiuchumi.

“Kwa sasa PPAA inapokea na kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia Moduli ya usimamizi wa Malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST, matumizi ya Moduli hiyo yameleta manufaa mbalimbali ikiwemo kuokoa muda, kupunguza gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni,” amesema Bi. Limilabo.

Kongamano hilo limewakutanisha takribani wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu 150 na kutoa fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mitandao ya kibiashara itakayowawezesha kutumia fursa za uwekezaji, teknolojia na ubunifu zinazotanganzwa na Serikali hususani zile fursa zinazopatikana katika Mkoa wa Lindi.

Bi. Limilabo pia ameyahimiza makundi hayo maalumu kuhakikisha yanajisajili katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kupata fursa ya kushiriki katika zabuni zinazotangazwa na Serikali.

Aidha, amewataka kuwa tayari kuchukua hatua stahiki pale wanapoona hawajatendewa haki katika mchakato wa zabuni, kwa kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. Hatua hiyo itasaidia Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi yake na kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi hiyo kwa wakati uliopangwa.

Salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake M...
07/09/2026

Salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake Mhe. Hafidh Ameir Hassan

29/08/2026
Volunteer Job Vacancy
27/08/2026

Volunteer Job Vacancy

25/08/2026
21/08/2026

Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa yaongeza wigo kwa wazabuni

Wigo umeongeka.   Kufahamu zaidi majukumu ya PPAA
19/08/2026

Wigo umeongeka. Kufahamu zaidi majukumu ya PPAA

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewajengea uwezo makandarasi kuhusu mazingira ya haki katika mchakato wa zab...
14/08/2026

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewajengea uwezo makandarasi kuhusu mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma, ili waweze kudai haki zao pindi wanapoona hawakutendewa haki kwenye michakato ya zabuni za umma walizoshiriki.

Wasilisho la PPAA limewasilishwa na Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi ambaye alimwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika Mkutano wa Mashauriano na Wadau wa Sekta ya Ujenzi kwa Mwaka 2026 ulioandaliwa na Bodi ya Wakandarasi (CRB) tarehe 13 – 14, Agosti, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Bi. Sayi amesema kuwa, ununuzi wa umma ni zaidi ya utaratibu wa kununua kazi za ujenzi, bidhaa au huduma; ni chombo cha sera ya maendeleo kinachochochea ukuaji wa uchumi, ajira, kuwezesha makandarasi wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali na kuhakikisha matumizi bora ya fedha za umma.

“Mazingira ya haki katika mchakato wa zabuni za umma ni mfumo unaohakikisha washiriki wote wanatendewa kwa usawa, wanashindana kwa kutumia masharti yanayofanana, na maamuzi yote yanafanywa kwa kuzingatia sheria, kanuni na masharti ya nyaraka za zabuni,” amesema Bi. Sayi

“Mazingira ya haki katika zabuni za umma ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” Bi. Sayi ameongeza. Kadhalika, Bi. Sayi ameongeza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inahitaji mfumo wa ununuzi wa umma unaozingatia misingi ya haki, uwazi, uwajibikaji na ushindani wa haki.

Address

Mkandarasi Place, 58 Lusinde Road, 41104 Tambukareli
Arusha
255

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Telephone

+255743505505

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Public Procurement Appeals Authority - PPAA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Public Procurement Appeals Authority - PPAA:

Shortcuts

Share