15/05/2026
Huuu ndio muonekano wa uwanja mpya wa yanga ambao wamesaini mikataba leo na kampuni ya GSM na kumbuka UPDATES 👇
Uwanja Mpya wa Klabu ya Yanga utamilikiwa kwa asilimia 50% na Klabu ya Yanga na asilimia 50% na Kampuni ya GSM Tanzania Limited.
Ujenzi wa uwanja wa Yanga SC na Kampuni ya GSM Tanzania Limited upo kwenye mfumo wa PARTNERSHIP (Ushirikiano), Yanga SC wao wamechangia ardhi na GSM anatoa fedha.
Wana yanga mnasemajee
15/05/2026
Mwanaume mmoja mkazi wa Kata ya Songambele wilayani Urambo mkoani Tabora amejeruhiwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na mke wa mtu.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Jionee, Kata ya Songambele, Tarafa ya Urambo ambapo mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Abdala Shaban mwenye umri wa miaka 60 alishambuliwa na kujeruhiwa kwa kukatwa na panga akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu.
Chanzo cha habari hii ambacho hakikutaka jina lake litajwe kimesema kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo aligundua mawasiliano ya kimapenzi kati ya mke wake na mwanaume huyo baada ya kuchukua simu ya mke wake usiku na kuanza kuchati na mwanaume huyo akijifanya kuwa ni mwanamke huyo.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Jionee, Kabati Sengeli amesema alipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa mtuhumiwa mwenyewe ambaye alimweleza kuwa alikuwa na changamoto za kifamilia zinazodaiwa kusababishwa na mahusiano kati ya mke wake na mwanaume huyo.
Baada ya tukio hilo, Jofrey Samweli alijisalimisha katika kituo cha Polisi ambapo baadaye aliachiwa kwa dhamana huku majeruhi Abdala Shaban akikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Urambo kwa matibabu kabla ya kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora – Kitete kwa matibabu zaidi.
15/05/2026
Aliyekuwaa Afissaa habari wa yanga Haji manara amesema kitendo cha diaraa kutoka katika mchezo wao uliopita dhidi yqma dodoma jiji fc kilichangiaa pakubwa timu yao ya yanga kupoteza mcheoz huo
Manaraa masemaa ubora alionao diara hakuna golilipa wa yanga mwenye ubiora huo na sio kwa yanga hata kwa vilabu vingine tanzania
Hajii manara amaesema kitendo alichofanya diara ni tabia mbaya ambayo imegarimu timu huku akimkumbusha diaraa kwamba uko wakati yanga ilishawahi kufukuza wachezaji wote hivyo diaraa anatakiwa kuwa makini
Wana yangaa mnasema kitendo alichofanya diara mmekipokeaa vipi weka comment yako hapo?
15/05/2026
Simba Queens na Yanga Princess zinashuka dimbani leo saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, kusaka pointi tatu zitakazotoa mwelekeo wa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) msimu huu.
Mshambuliaji hatari wa Simba Queens, Aisha Mnunka, ameweka wazi kuwa ushindi wa mechi ya leo ndio utakaofungua njia yao ya kunyakua taji msimu huu.
"Ni mechi kubwa, kila mmoja amejiandaa kwa namna yake. Sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya pointi tatu lakini siwezi kumzungumzia zaidi mpinzani. Yote kwa yote itaenda kujulikana nani mshindi na itaenda kutupa taswira nzuri," amesema Mnunka.
Dabi ya Kariakoo kwa upande wa wanawake haijawahi kuwaacha mashabiki salama! Je, Simba Queens itaendeleza ubabe wake au Yanga Princess itapindua meza ugenini Chamazi?
Unatabiri matokeo gani kwenye mechi hii kubwa ya leo?
Weka utabiri wako hapa chini! 👇
14/05/2026
Katika michezo mi4 iliopita Chama amehusika katika magoli 7 🔥 amefunga magoli ma5 naku assists mara2, leo amefunga mara2 dhidi ya Mashujaa
Katika michezo mi4 iliopita yote Chama kaingia kambani🔥. Anaandika Mchambuzi Makini kutoka wasafifm Nasrikhalfan. Uwanja Wa Maoni Uko Wazi
14/05/2026
DODOMA JIJI “MUKAKA” YANGA SC
Kocha Amani Josiah kutoka Musoma amekuwa wa kwanza “Kuikata Yanga Utepe” baada ya kuifunga mabao 3-2, na kuwa timu ya kwanza kutwaa alama zote 3 kutoka kwa mabingwa hao watetezi msimu huu.
Ilianza kwa bao la mapema la OKELLO kabla ya bao la OFFSIDE la kutoka kwa OKELLO tena, lakini nahodha Mwamnyeto aliipa DFC bao baada ya kujifunga hali ambayo ilionekana wazi kutompendeza kipa wake Djigui Diarra ambaye baadae alitoka kabla ya mapumziko labda kwa majeraha.
Lakini alipofika bench k**a anaonekana kuzidi kuzoza kwa wenzie hali ikiyoashiria k**a anaongelea hilo tukio.
Kipa Masalanga hapaswi kulaumiwa bao la 2 kwakuwa hakuuona mpira ambao Mwamnyeto alijaribu pia kuucheza, siku mbaya kazini kwa Captain.
FT: Dodoma 3-2 Yanga SC, DFC wanakuwa makaka wa mjini kwa Yanga ‘Mukaka’. Ameandika Mchambuzi Makini kutoka Wilson Oruma. Uwanja Wa Maoni Uko Wazi
14/05/2026
Dube kafanya isionekane kazi kubwa iliyofanywa na Okello leo wala mchango mkubwa wa Yao.
Dube peke yake amepoteza nafasi zisizopungua 4, huku Yao peke yake akimtengenezea nafasi k**a 3 za wazi kabisa. Cross za maana zote zile, vipi ile nafasi iliyotokana na pasi ya Okello...?
K**a Mwamnyeto anavyopokea lawama leo, basi na Dube naye anapaswa kupokea lawama hizo hizo. Anaandika Mchambuzi Makini kutoka wasafifm Nasrikhalfani. Uwanja Wa Maoni Uko Wazi
14/05/2026
Nina uhakika k**a djugui diarra angekuwa yupo Simba angekuwa tayari ameuzwa tangu msimu uliopita kwasababu viongozi wa Simba hawataki ujinga ujinga kwenye timu hawataki kukaa na watu ambao hawana despline k**a diarra
Mfano, Simba Wana shida ya mshambuliaji ili Jonathan Sowah wamemtoa kwenye timu kwasababu ya nidhamu
Simba wamewahi kumtoa Augustine Okrah kwasababu ya nidhamu
Wamewahi kumuweka bench na kumtoa kwenye timu kwa muda Jonas Mkude kwasababu ya nidhamu
Na wengine wengi ila kwa Yanga mara nyingi inakuwa ngumu kwasababu inaonekana Wana tabia ya kuogopa wachezaji
Inasemekana tabia ya djugui diarra ambayo kuonyesha jana ndio tabia yake hata akiwa mazoezini na inasemekana hata Azizi ki alikuwa na tabia za namna hii
Hopefully,Yanga watakuwa wamejifunza kwenye hili, mchezaji hatakiwi kuwa mkubwa kuliko timu ,wamtoe diarra watafute golikipa mwingine. Anaandika Mchambuzi Makini kutoka Tv3 Alex Ngereza. Uwanja Wa Maoni Uko Wazi
14/05/2026
Goli zote 3 za mchezo mpaka zimetoka Mguuni Kwa Lango Star boy ,Allan Okello. Amefunga Goli 2 lakini pasi yake Fyongo ndo ametengeneza bao la Dodoma Jiji ambalo captain Bakari Nondo amejifunga..Hii Kitaalamu tunaitaje? 😅
Goli 7 na Asists 7. G/A ya 14 so far .. Anaandika Mchambuzi Makini kutoka Wilson Oruma
14/05/2026
Huyu ndo mchezaji Clinical mbele ya lango kwenye kikosi cha Yanga na ligi nzima ya NBC,takwimu hazidanganyi kafunga goli (6) kwenye dakika na mechi chache alizocheza.
Depu ni mbwa mwitu kwenye Box hususa ni pale ambayo Yanga wanamiliki na kutawala mechi….Depu hana utaratibu wa kukosa sana mbele ya lango.
Jana Dube hakuwa na mechi nzuri ila bado Moalin alimuacha Depu nje hadi dakika ya 88😄
Unaacha mchezaji wa bilion 1 nje hadi dakika ya 88 na wakati unatengeneza nafasi kibao?
Kuna muda makocha wanachanganya mambo🙌. Anaandika Mchambuzi Makini kutoka crown Media Hans Rafael14. Uwanja Wa Maoni Uko Wazi