21/10/2024
WANANCHI JITOKEZENI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA - Mhe. Mchengerwa
Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wananchi wenye sifa za kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa, kujitokeza kuchukua na kurudisha fomu kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi tarehe 1 Novemba, 2024 ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kugombea katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Waziri Mchengerwa ametoa wito huo kwa watanzania wenye sifa, wakati akitoa tathmini ya uandikishaji wa wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kujiandikisha katika kituo cha Michikichini Kijiji cha Umwe Kaskazini Wilayani Rufiji.
“Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafanyika kwa siku zote hizo kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba 01, 2024 na kuongeza kuwa, muda wa kampeni utakapofika zifanyike kampeni za kistaarabu ambazo zitadumisha hali ya utulivu na Amani nchini,” Mhe. Mchengerwa alisisitiza.
Waziri Mchengerwa amewashukuru wananchi wote, wanachama na wapenzi wa vyama vyote vya siasa kwa kuendelea kuonesha ukomavu wa kisiasa kwa kufanya siasa za kistaarabu, siasa za hoja na si za ugomvi mpaka zoezi la uandikishaji likifikia ukomo.
“Niwasihi tuendelee kufanya siasa za kistaarabu na ninawakemea vikali wanaotaka kuleta siasa za ugomvi ambazo zinaweza kuhatarisha amani na utulivu tulionao katika taifa,” Mhe. Mchengerwa ameeleza.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amevisihi na kuvitaka vyombo vya dola viendelee kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo katika kipindi chote cha mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili wananchi waweze kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Sanjari na hilo, Waziri Mchengerwa amewasisitiza wasimamizi wa uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi wa Seriksali za Mitaa kuendelea kuzingatia Sheria na Kanuni za Uchaguzi, ili mchakato mzima wa uchaguzi uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya Sheria na Kanuni zilizowekwa.
09/08/2024
MAFISA TARAFA NA WATENDAJI WA KATA MKOA WA ARUSHA WAFUNDWA🇹🇿
Na. Elinipa Lupembe
Maafisa Tarafa na Maafisa Watendaji wa kata wameaswa kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao kwa kuibua miradi ya maendeleo kutokana na fursa zilizopo kwenye maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo endelevu vya Mapato na kuvisimamia.
Rai hiyo, imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, wakati wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoa wa Arusha, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano kwenye Ukumbi za Mikutano Ofisiya Mkuu wa mkoa huo
Amewasisitiza Watendaji hao kuwa wabunifu wa vyanzo vya mapato ya Serikali na kuhimiza uwajibikaji wa watumishi na ushiriki wa wananachi katika maendeleo.
“Mara nyingi tunate tumekuwa hatuna ubunifu wa usimamizi na uwajibikiaji, tuna fursa nyingi za kiuchumi lakini hatuna ubunifu, hatusimamii, fursa za kijamii zinazopatikana kule hatuzielezei vizuri” alisema Bw. Missaile Musa.
Amesema uwepo wa changamoto zinazotokana na kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wa watendaji hao katika ngazi ya msingi, zitapata suluhu baada ya mafunzo hayo hususani masuala ya maadili, uzalendo na masuala ya kiutumishi.
Aidha, amewataka kutambua majukumu yao kwa kina ili kuepuka muingiliano wa kimajukumu na kimaslahi, zaidi kufahamu masuala ya kisera na kuhimiza utekelezaji wake huku akiwataka Watendaji Kata kuandaa Mpango kazi wa Kata na kabla haujawasilishwa ngazi ya Halmashauri lazima upitie kwa Afisa Tarafa wake ili kuwa na agenda ya pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Naikanuka, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ,amesema mafunzo hayo yatamwongezea weledi wa kazi na kuboresha ushirikiano na watumishi wa Sekta zote katika eneo lake yeye akiwa kiungo muhimu Pamoja na kuweza kutatua kero na migogoro ya wananchi kabla ya viongozi kufanya ziara katika eneo lake.
Awali, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, amebainisha kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na ofisi hiyo, kupitia Programu ya Uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na vyuo vya Serikali za Mitaa Hombolo na Chuo cha Utumishi wa Umma, kikiwa na washiriki 181, Watendaji wa Kata 157 na Maafisa Tarafa 23 kutoka Tarafa na Kata zote za Mkoa wa Arusha.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, awamu hii ya mwisho itahusisha mikoa ya Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Morogoro, Tanga na Ruvuma, ambapo Maafisa Tarafa 203 na Watendaji wa Kata 1,377 watapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo.
14/07/2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura pamoja na viongozi wengine leo tarehe 14 Julai, 2024.
02/07/2024
Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe Paul Makonda amefika walayani Ngorongoro kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na mh Dk Samia Suluhu Hassan rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Na Zacharia James.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Paul Makonda amesema Zaidi ya wananchi milioni 1 ndani ya mkoa wa arusha watanufaika na miradi ya maji katika maeneo yao vikikamilika visima 37 wilayani Ngorongoro kati ya vingi mkoani hapa.
Ameyasema hayo leo Julai Mosi 2024 akiwa wilayani Ngorongoro katika ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa maji mijini na vijijini ruwasa kwa ufadhili wa umoja wa falme za kiarabu (UAE) ambapo mbali na kuwashukuru wafadhili hao amempongeza rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.samia suluhu Hassan kwa kufanikisha mahusiano mazuri na mataifa mengine mahusiano yanayopelekea wahisani hawa kusaidia wananchi kupata huduma hii muhimu ya maji katika maeneo yao.
Mhe. Makonda amewasihi viongozi ngazi za jamii na wananchi kwa ujumla kuwa walinzi madhubuti na kuitunza miradi hio ya maji ili ikafikie malengo yaliokusudiwa wa kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata mbali huduma ya maji pia amewatowa hofu wafugaji kwamba miradi hio mbali na kurahisisha upatikanaji wa maji kwa binadamu pia miradi hii itatoa nafasi kwa mifugo kunywa maji katika maeneo yaliyotengwa jirani na miradi hio huku akiagiza maji yafike katika maeneo yote yenye makazi ya watu hasa wanaoishi maeneo ya vijiji vilivyo katika maeneo magumu kufikika hasa Oloboo huku akiomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wakati wa utekelezwaji wa miradi hiyo ya maji.
Miradi hii inatekelezwa kwa ufadhili wa utawala wa falme za kiarabu ambapo wilayani hapa vimechimbwa visima 18 kati ya hivyo 12 vinatoa maji huku katika ziara hio mkuu wa mkoa amekagua visima vilivyopo Oloboo,shule ya msingi Wasso,Maaloni na uchimbaji wa kisima Sale mbali na ukaguzi huo wa visima vya maji mkuu wa mkoa Makonda amewaahidi wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kua atakua na ziara rasmi ya kuskiliza kero za wanachi maarufu k**a ziara ya kupiga spana wilayani hapa katika kipindi kifupi kijacho.
20/05/2024
📌Maasai Village, Oldonyo Lengai 🇹🇿
Tuambie ni Kijiji Gani???