26/09/2023
TEMDO imetoa Mafunzo kwenye Maonesho na Mafunzo ya Biashara ya Mitambo na Mashine za Uzalishaji wa Bidhaa za Viwanda, Kilimo, Mifugo na Bidhaa zinginezo kwenye ukumbi wa SHIRECU yalio andaliwa na Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
12/09/2023
TEMDO to Produce Mini-Mills to Boost Sugar Production in Tanzania
02/09/2023
TEMDO yashiriki kwenye uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (Pan African Post Uniuon - PAPU) lenye ghorofa 17. Jengo hili litazinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jengo hili lina uwezo wa kuchukua wafanyakazi wa Menejimenti na Utawala wa PAPU wanaowakilisha nchi zote 45 wanachama wa Umoja huu uliopo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika (AU).Umoja wa Posta wa Afrika (PAPU) ni Taasisi maalumu ya Umoja wa Afrika ikiwa na dhima ya kuratibu shughuli zote zinazolenga kuendeleza huduma za posta katika bara la Afrika.
29/08/2023
Taasi ya TEMDO imeshinda nafasi ya kwanza kwenye sekta ya Viwanda Vidogo kwenye mashindano ya Kaizen. Tuzo hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdullah. Picha habari ni Watalamu wa Kaizen Dr. Sigisbert Mmasi na Allice Ndosi wakipokea Tuzo na Cheti kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu.
24/08/2023
Wakurugenzi na Maafisa Wakuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wametembelea TEMDO kwa lengo la kuangalia Maendeleo ya Teknolojia zinazo tengenezwa k**a vile Mradi wa Vifaa Tiba, Mtambo wa Kuchakata zao la Muhogo, Mtambo wa kuchakata Sukari na Mkonge. Viongozi wa Wizara waliridhishwa na waliipongeza Taasisi kwa Mafanikio chanya yalio fikiwa kwenye utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Prof. Kahimba alimkabizi zawadi ya Nembo ya jina la Wizara ya Viwanda na Biashara (WVB) ilichongwa kwenye chuma kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utawala Bi. Ingrid Sanda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
14/08/2023
Mtalamu wa TEMDO akiwa anaelzea teknolojia kwenye Maonesho ya Nane nane
07/08/2023
Mkulima akipata maelezo ya kina ya teknolojia ya kuchakata zao la chikichi ili kupata mafuta ya kula kutoka kwa Mtalamu Mosses Chalamila alipo tembelea banda la TEMDO katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini.
TEMDO ni Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania iliopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Katika maonesho ya 29 Nane Nane (88) TEMDO imeshiriki na Teknolojia mbalimbali k**a vile Mtambo wa kumamua na kusafisha mafuta ya Alizeti, Mtambo wa kuchakata unga wa Muhogo, Mtambo wa kuchakata siagi ya karanga, Mtambo wa kuchakata unga wa lishe, Mtambo wa kuchakata juisi ya matunda, Mtambo wa kuchakata viungo vya chakula, Mashine ya kutoa mjuzi wa zabibu kwaajili ya viwanda vya mvinyo.
Pia Taasisi imeshiriki na vifaa tiba vya hosipitali k**a vile vitanda vya kuwagulia wagonjwa, vitanda vya kulazia wagonjwa na kujifungulia Wamama wajawazito, Majokofu ya kuifadhia Maiti ya ngazi mbili mpaka sita na pia kiteketezi cha taka hatarishi zinazo zalishwa na hosipitali- "Biomedical Solid Waste Incinerator".
06/08/2023
TEMDO ni Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania iliopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara Katika maonesho ya 29 Nane Nane (88). TEMDO imeshiriki na Teknolojia mbalimbali k**a vile Mtambo wa kumamua na kusafisha mafuta ya Alizeti, Mtambo wa kuchakata unga wa Muhogo, Mtambo wa kuchakata siagi ya karanga, Mtambo wa kuchakata unga wa lishe, Mtambo wa kuchakata juisi ya matunda, Mtambo wa kuchakata viungo vya chakula, Mashine ya kutoa mjuzi wa zabibu kwaajili ya viwanda vya mvinyo.
Pia Taasisi imeshiriki na vifaa tiba vya hosipitali k**a vile vitanda vya kuwagulia wagonjwa, vitanda vya kulazia wagonjwa na kujifungulia Wamama wajawazito, Majokofu ya kuifadhia Maiti ya ngazi mbili mpaka sita na pia kiteketezi cha taka hatarishi zinazo zalishwa na hosipitali- "Biomedical Solid Waste Incinerator".
03/08/2023
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Notredame wamefanya ziara ya kimasomo TEMDO kwaajili ya kujionea Ubunifu na Usanifu wa kazi za Kihandisi, lengo kuu la ziara ya shule hiyo ni kuwaandaa Wanafunzi wapende masomo ya Sayansi.
22/07/2023
Uongozi na Watumishi wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) wanapenda kumpongeza Mjumbe wa Bodi Dkt. Liliane Joseph Pasape kwa kupandishwa cheo cha Kitaaluma na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM -AIST) kutoka Mhadhiri Mwandamizi " Senior Lecturer" kuwa Profesa Mshiriki "Associate Professor ". "Hongera sana Prof. Pasape".
10/07/2023
Mwenyeketi wa bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Mhandisi Dkt. Richard Masika (Kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Mhandisi Prof. Frederick Kahimba Wametembelea Banda la TEMDO katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam