HabariLeo

Call Directions Website Contact the organization

HabariLeo HABARILEO Gwiji la Habari Tanzania| Kwa habari za uhakika na kina | Sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania
Tanzania Standard Newspapers (TSN)

22/10/2026

MTWARA; Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema jumla ya kaya 625,000 zinatarajiwa kusajiliwa katika mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili.
-
Mchengerwa amesema hayo leo Oktoba 22, 2026 mkoani Mtwara akieleza hatua zinazochukuliwa na serikali katika kupanua wigo wa wananchi kupata huduma za afya kupitia mfumo wa bima.
-
Imeandaliwa na Daud Manongi

DAR ES SALAAM: Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuongeza uwekezaji katika viwanda na uchakataji wa m...
22/10/2026

DAR ES SALAAM: Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuongeza uwekezaji katika viwanda na uchakataji wa malighafi ili kuacha kupoteza fursa za kiuchumi kwa kuuza bidhaa ghafi nje ya ukanda na baadaye kuagiza bidhaa zilizoongezwa thamani.
-
Wito huo umetolewa leo Dar es Salaam wakati wadau wa sekta ya umma na binafsi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki wakijadili namna ya kuimarisha minyororo ya thamani katika sekta za ngozi, nguo na mafuta ya kula.
-
Mchumi mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema mafanikio ya juhudi za kuendeleza viwanda yanapaswa kupimwa kwa hatua zinazochukuliwa baada ya mikutano, ikiwemo kuongeza uzalishaji, kupanua masoko ya wakulima na kuhakikisha wazalishaji wanapata malighafi kwa wakati.
-
Amesema mazingira bora ya biashara yanahitajika ili viwanda viweze kuongeza uzalishaji, kuwekeza katika teknolojia na kushindana katika masoko ya kikanda na kimataifa.
-
Mshauri wa biashara na sera wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Adrian Njau, amesema ukanda huo unaendelea kuagiza bidhaa nyingi zilizokamilika licha ya kuwa na uwezo wa kuzalisha baadhi ya malighafi zinazotumika katika utengenezaji wake.
-
Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Grace Mkojera

MBEYA; Shirika la Uhifadhi la Six Rivers Africa limezindua mashindano ya michezo kwa shule za msingi zilizopo Kata za Ma...
22/10/2026

MBEYA; Shirika la Uhifadhi la Six Rivers Africa limezindua mashindano ya michezo kwa shule za msingi zilizopo Kata za Madibira na Miyombweni wilayani Mbarali yaitwayo Conservation Cup 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha uhifadhi wa mazingira ya hifadhi za Taifa na kupinga vitendo vya ujangili wa wanyamapori.
-
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mariam Mnozya, amelipongeza shirika hilo kwa kuandaa mashindano hayo, akieleza kuwa michezo ni nyenzo muhimu katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.
-
Kwa upande wake, Mratibu wa mashindano hayo kutoka Shirika la Six Rivers Africa, Justina Kizanye amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kutumia michezo k**a jukwaa la kueneza elimu ya uhifadhi wa mazingira na kupinga ujangili.
-
Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Joachim Nyambo, Mbeya

22/10/2026

DAR ES SALAAM: Msanii wa muziki kutoka Kenya, Bien Baraza ‘Bien’, amesema hatasahau mapokezi na mapenzi makubwa aliyooneshwa na Watanzania alipohudhuria fainali ya Ligi ya Kikapu kati ya Dar City na Stein Warriors iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Salaam.
-
Bien, ni miongoni mwa wasanii wanaotambulika katika muziki wa Afrika Mashariki, ameeleza hisia zake kupitia ujumbe aliouchapisha leo, akitumia msemo unaosisitiza umuhimu wa ujirani mwema.
-
“Jirani mwema ni ndugu wa karibu,” aliandika Bien, akionesha namna alivyoguswa na upendo alioupata kutoka kwa Watanzania.
-
Katika fainali hiyo, Dar City iliibuka bingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata ushindi wa jumla wa michezo mitatu dhidi ya Stein Warriors, na hivyo kutwaa taji hilo mbele ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano hilo.
-
Imeandaliwa na Grace Mkojera

DODOMA: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesajili mafanikio ya utoaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) mi...
22/10/2026

DODOMA: Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesajili mafanikio ya utoaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) milioni 23.7, huku vitambulisho zaidi ya milioni 21.5 vikisambazwa kwa wananchi, hatua inayoakisi maendeleo ya mifumo ya utambuzi wa raia nchini.

Mafanikio hayo yamewasilishwa leo Oktoba 20 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati akiwasilisha taarifa za utendaji wa NIDA na Chuo cha Zimamoto na Uokoaji cha Chogo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, NIDA imezalisha NIN 23,718,060 na vitambulisho 21,526,594, ambapo 21,515,793 vimesambazwa kwa wananchi.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na mamlaka hiyo ni kuunganisha taasisi 152 za umma na binafsi kwenye kanzidata yake, kuanza kutumia teknolojia ya 'Laser Engraving' kuzalisha vitambulisho na kuboresha moduli 24 za mfumo wa usajili na utambuzi.

Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Rahimu Fadhili

22/10/2026

TABORA; Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA, imeteketeza takribani kilo 738 za dawa za kulevya aina ya bangi, kufuatia operesheni na jitihada mbalimbali za kupambana na biashara hiyo haramu.
-
Akizungumza wakati wa uteketezaji huo, Mkuu wa Operesheni DCEA Kanda ya Magharibi, Jackson Jacoub ameeza kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia jumla ya kesi 13 zilizofikishwa mahak**ani, ambapo kati ya kesi hizo 13 zilizohusisha watuhumiwa 16, Jamhuri imeshinda kesi 12.
-
Imeandaliwa na Michael Samwel

IRINGA: Tanzania imeongeza msukumo wa kuwekeza katika uchakataji wa mazao ya misitu wilayani Mufindi mkoani Iringa, huku...
22/10/2026

IRINGA: Tanzania imeongeza msukumo wa kuwekeza katika uchakataji wa mazao ya misitu wilayani Mufindi mkoani Iringa, huku wadau wakisema hatua hiyo inaweza kuongeza thamani ya bidhaa, ajira na mapato yanayotokana na sekta hiyo.

Wadau wa sekta ya misitu wameiomba Serikali na Sekta Binafsi kuweka nguvu zaidi katika teknolojia za uchakataji, viwanda vya samani na uzalishaji wa bidhaa nyingine zinazotokana na mbao, badala ya kutegemea zaidi uuzaji wa mazao ya misitu bila kuongeza thamani.

Wakizungumza katika mkutano wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi ulioandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wadau hao pia wameeleza changamoto zinazokabili sekta hiyo, zikiwemo ukosefu wa mitaji na mikopo nafuu, kodi na tozo, upatikanaji wa masoko na taratibu za vibali.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPSF, Deogratius Massawe, amesema ushirikiano kati ya Serikali na wafanyabiashara ni muhimu katika kutafuta suluhisho la changamoto hizo na kuweka mazingira yatakayowezesha uzalishaji na uwekezaji kukua.

Zaidi tembelea//habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Samweli Swai

DAR ES SALAAM;  Rais mstaafu wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es ...
22/10/2026

DAR ES SALAAM; Rais mstaafu wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete ameishauri Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuangalia uwezekano wa kujenga Bwawa Dogo eneo la Wami mkoani Pwani, litakalosaidia kuongeza upatikanaji wa maji Chalinze ifikapo mwaka 2030 hadi 2050.
-
Taarifa iliyotolewa na DAWASA leo Oktoba 22, 2026, imesema Dk Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya kutembelea na Meneja wa DAWASA Chalinze, Mhandisi Boniface Ole Philemon, nyumbani kwake, Msoga- Chalinze mkoani Pwani.
-
“ Dk Kikwete amesisitiza mahitaji ya maji yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na viwanda, hivyo maandalizi ya muda mrefu yanahitajika.
-
"Pia, ameshauri mazungumzo yafanyike na mashamba ya Mtibwa, mkoani Morogoro, kubaini kiasi cha maji wanachotumia ili kuwezesha maji mengi zaidi kufika mto Wami. Aidha, amependekeza matumizi ya maji kwa Bagamoyo Sugar yazingatiwe.
-
"Dk Kikwete amefurahishwa na hali ya huduma ya maji Mji wa Chalinze na kupongeza kazi inayofanywa na wizara na DAWASA, na kusema kazi kubwa imefanyika chini ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na watumishi wote wa sekta ya maji nchini.
-
“ Dk Kikwete amesema kwa sasa hapokei malalamiko kuhusu huduma ya maji Chalinze na amesisitiza kazi nzuri inayoendelea iendelezwe, huku mapendekezo yake yakilenga kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mahitaji yajayo,” imesema taarifa hiyo.
-
Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM; Watanzania wametakiwa kuweka utamaduni wa kujiwekea akiba ili ziweze kuwasaidua siku za usoni.-Wito huo u...
22/10/2026

DAR ES SALAAM; Watanzania wametakiwa kuweka utamaduni wa kujiwekea akiba ili ziweze kuwasaidua siku za usoni.
-
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Biashara za Kiserikali wa Benki ya Azania, Samson Mahimbi wakati akizindua kampeni ya Piga Ndeefu yenye lengo la kuchochea shughuli za kiuchumi kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
-
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, yakitarajiwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika sekta za utalii, malazi, usafiri na huduma nyingine.
-
Amesema kampeni hiyo inalenga kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuchochea shughuli za kiuchumi zitakazowanufaisha Watanzania wakati wa maandalizi na kipindi cha mashindano ya AFCON 2027.
-
Mahimbi amesema kupitia kampeni hiyo, wateja watapata fursa ya kuweka akiba huku wakinufaika na riba pamoja na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
-
Amesema wateja wanaweza kuanza kuweka akiba kwa kiasi cha shilingi 500,000 na kupata riba ya hadi asilimia 12 kwa mwaka, kwa mujibu wa masharti ya kampeni hiyo.
-
Zaidi tembelea //www.habarileo.co.tz
Imeandaliwa na Robert Okanda

22/10/2026

RAIS SAMIA MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA ZA KIRAIA

Kuelekea Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya Usajili na Usimamizi wa Jumuiya za Kiraia nchini, unaotarajiwa kufanyika kuanzia Tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026 katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inawajulisha viongozi wote wa Jumuiya za Kiraia nchini ambao wangependa kushiriki kwenye Mkutano huo kuingia kwenye Tovuti ya Wizara ya www.moha.go.tz na kwenye tovuti ya mfumo wa RSMIS www.rsmis.moha.go.tz ili kujisajili kwa njia ya mtandao na kupata utaratibu wa kuweza kupata mabanda ya maonesho.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Kauli Mbiu ya Mkutano ni “Jumuiya za Kiraia Msingi wa Umoja,Mshik**ano na Maendeleo ya Taifa Letu”.

Address

Arusha
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 05:30
Tuesday 07:30 - 05:30
Wednesday 07:30 - 05:30
Thursday 07:30 - 05:30
Friday 07:30 - 05:30
Saturday 09:00 - 04:00
Sunday 10:00 - 04:00

Telephone

+255737688205

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HabariLeo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HabariLeo:

Shortcuts

Share