Tanapa Updates

Tanapa Updates

Share

The Official Page for Tanzania National Parks (TANAPA) News and Updates.

Photos from Tanapa Updates's post 03/06/2026

Wengi wetu tunamjua simba k**a mfalme wa nyika, lakini fisi ni miongoni mwa wanyama wanaojulikana zaidi na huenda haukufahamu.

Je, unajua kwamba fisi huwinda pia na wakati mwingine wanaweza kuwafukuza simba kutoka kwenye mawindo yao? 😳

Na k**a ulidhani fisi ni mwizi wa mawindo tu, huenda ukashangazwa na baadhi ya ukweli utakaouona kwenye slides hizi!

Sasa swali ni moja tu...
Nani ni mbabe kati ya Simba na Fisi? šŸ‘€

Swipe slides zote kwanza kabla ya kutoa hukumu yako!

Photos from Tanapa Updates's post 03/06/2026

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaipongeza Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuibuka Mshindi wa Pili katika Mashindano ya ā€œAFCON U-17 2026ā€ katika Fainali dhidi ya Timu ya Vijana - Senegal, mchezo uliochezwa jana June 02, 2026 katika uwanja wa Moulay El Hassan Stadium, uliopo jijini Rabat, nchini Morocco.

Katika kuonesha mshik**ano na kuunga mkono vijana hao, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb.) walihudhuria mchezo huo wa fainali hiyo ambapo uwepo wao uliendelea kuitangaza Tanzania na kuhamasisha ushirikiano kati ya sekta za utalii na michezo katika kuitangaza nchi kimataifa.

Kupitia jina la Serengeti Boys, timu imeendelea kuitangaza Tanzania na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti duniani, na hivyo kuongeza mwamko na uelewa kuhusu vivutio vyetu vya utalii katika jukwaa la Kimataifa.

Photos from Tanapa Updates's post 31/05/2026

TAARIFA KWA UMMA | PUBLIC NOTICE

Cc


Photos from Tanapa Updates's post 31/05/2026

WAZIRI MAKONDA: TANAPA IMEFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI NA UWEKEZAJI KUPITIA UTALII WA MICHEZO NCHINI

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia utalii wa michezo unaohusisha riadha, magari, baiskeli na pikipiki imeendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa wadau wa utalii, uhifadhi na uwekezaji huku ikitoa nafasi ya kutangaza bidhaa, huduma na vivutio vya utalii vya Tanzania.

Akizindua mbio za Cape to Cairo Arusha International Marathon Mei 31, 2026 jijini Arusha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, alisema utalii wa michezo umeendelea kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa na unatarajiwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchi.

Mbio hizo ziliwakutanisha washiriki kutoka China, Korea, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Uingereza na Tanzania, ambapo baadhi walitembelea Hifadhi ya Taifa Arusha huku wengine wakiahidi kurejea tena kwa ajili ya kutalii.

ā€œNimeona kazi nzuri inayofanywa na TANAPA katika kutangaza vivutio vya utalii. Hifadhi ya Taifa Arusha ni miongoni mwa maeneo yenye vivutio vya kipekee. Wananchi na wadau watumie fursa hizi kujitangaza na kukuza uchumi wao,ā€ alisema Makonda.

Aliongeza kuwa mwezi Julai kutafanyika Arusha Tourism Marathon, ambapo washiriki watapata fursa ya kukimbia ndani ya Hifadhi ya Taifa Arusha.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Witness Shoo, alisema utalii wa michezo umechangia kuongezeka kwa wageni na kufungua fursa zaidi za biashara na uwekezaji.

Kufikia Mei 31, 2026, Hifadhi ya Taifa Arusha imeshiriki kuratibu matukio makubwa ya kimichezo yakiwemo Cape to Cairo Arusha International Marathon, Arusha Tourism Marathon na Subaru Festival.

31/05/2026

WOW! Tanzania begins in Mkomazi, showcasing the beauty, diversity, and wonders found in Tanzania National Parks (TANAPA) to Tanzanians and the entire world. Through inspiring visuals and storytelling, we aim to create awareness about wildlife conservation, promote tourism attractions, and celebrate the natural treasures of our nation.

Stay tuned… the journey has just begun.

Photos from Tanapa Updates's post 30/05/2026

Tanzania Shines in Tripadvisor Travellers’ Choice Awards 2026

In the 2026 Tripadvisor Travellers’ Choice Awards – Best of the Best Things to Do, Tarangire National Park was ranked 8th among Africa’s Top Attractions, while the Ngorongoro Crater secured the 10th position.

The awards are based on millions of traveller reviews and ratings collected over a 12-month period on Tripadvisor, one of the world’s largest travel platforms. The Best of the Best award represents Tripadvisor’s highest level of recognition, with fewer than 1% of more than 8 million listings worldwide achieving this distinction.

Joining renowned attractions across South Africa, Egypt and Morocco, the recognition highlights Tanzania’s growing reputation as one of Africa’s premier tourism destinations.

Tarangire is known as the Elephants’ Paradise, renowned for its majestic baobab trees and authentic safari experiences, and continues to inspire travellers from around the world.

Cc

29/05/2026

Je wajua!?

Ukiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Ibanda-Kyerwa unaweza kuziona nchi za Uganda na Rwanda kwa wakati mmoja huku ukiwa umesimama Tanzania?

Ukisimama eneo la nchi tatu ndani ya hifadhi utaona Mto Kagera unaotenganisha mipaka ya Tanzania, Uganda na Rwanda huku ukikupa mandhari nzuri ya kuvutia.

Mbali na mwonekano huo wa mataifa matatu, Ibanda-Kyerwa pia inakupatia fursa ya kufurahia aina mbalimbali za utalii ikiwemo utalii wa gari, utalii wa matembezi ya miguu, utalii wa usiku, utalii wa ndege kuona wanyamapori mbalimbali, mandhari ya asili pamoja na uzuri wa mazingira ya Mkoa wa Kagera.

K**a unahisi umeitembelea Tanzania bado, tembelea Ibanda-Kyerwa leo!

Photos from Tanapa Updates's post 28/05/2026

BINGWA WA DUNIA WA MASUMBWI CRAWFORD KUITANGAZA SERENGETI KIMATAIFA

Katika muendelezo wa kuitangaza Tanzania duniani kupitia utalii wa michezo, leo Mei 28, 2026, bingwa wa masumbwi duniani, Terence ā€œBudā€ Crawford, amekabidhiwa rasmi ubalozi wa utalii baada ya kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji. Tukio hilo limefanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni siku ya tano ya ziara yake nchini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kijaji alisema Serikali ya Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuifungua na kuitangaza sekta ya utalii kimataifa kupitia kampeni mbalimbali ikiwemo filamu za ā€œTanzania: The Royal Tourā€ na ā€œAmazing Tanzaniaā€ ambazo zimeendelea kuvutia wageni na watu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali kutembelea Tanzania.

ā€œMichezo ni sehemu muhimu ya ajira na maendeleo ya uchumi, lakini pia imekuwa daraja la kuunganisha Tanzania na watu mashuhuri duniani. Kupitia michezo tunaendelea kuitangaza Tanzania kimataifa na kufungua fursa mpya za utalii, uwekezaji na ajira kwa vijana,ā€ amesema Waziri Kijaji.

Aidha, Waziri Kijaji amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kupokea watu mashuhuri kutoka mataifa mbalimbali watakaotembelea vivutio vya utalii nchini, hatua itakayoongeza thamani ya utalii wa Tanzania katika soko la kimataifa. Pia amemkabidhi Crawford cheti cha kutambua mchango wake na kumpa ubalozi wa kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

Kwa upande wake, Crawford amepongeza ukarimu wa Watanzania pamoja na uzuri wa vivutio vya asili alivyovitembelea katika Hifadhi za Taifa Tarangire na Serengeti tangu kuwasili kwake nchini Mei 24, 2026, huku akiahidi kuwa balozi mzuri wa utalii wa Tanzania.

Naye, Kamishna wa Uhifadhi, CPA Musa Nassoro Kuji amesema utalii wa michezo unaendelea kuongeza sifa za vivutio vya utalii nchini na kuchangia kukuza pato la Taifa.

Akiwa Serengeti, Crawford atashiriki shughuli mbalimbali za kitalii ikiwemo utalii wa p**o, utalii wa gari na utalii wa usiku, shughuli hizi zitakazosaidia kuitangaza hifadhi hiyo kimataifa.

Photos from Tanapa Updates's post 27/05/2026

ā€œBig Fiveā€ ni jina maarufu duniani
lakini ukweli wake unaujua?

Watu wengi hudhani ni wanyama wakubwa zaidi porini, lakini si kweli,
Kumbe kuna walio wakubwa kuliko simba, warefu kuliko wote, na wenye hasira zaidi ila bado hawakuingia kwenye orodha ya wanyama wakubwa watano (the big five) šŸ‘€

Sasa swali ni… ā€œBig Fiveā€ walichaguliwaje mpaka wakapata heshima hiyo? šŸ¤”

Swipe slides zote ujue siri hii ambayo inaweza kukushangaza, kukuchekesha na kukufanya uangalie wanyama tofauti kabisa na ulivyozoea šŸ˜‚

Kuna mmoja ni ā€œgangsterā€ wa porini, mwingine ninja wa kujificha, na mmoja anaweza kukimbia speed kali huku haoni vizuri 😭

Ukifika mwisho wa slides… utakuwa na mtazamo mpya kabisa kwa Big Five šŸ˜…šŸ‘‡

27/05/2026

WOW! Tanzania inaanza Mkomazi, ikionesha uzuri, upekee na vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Hifadhi za Taifa za Tanzania (TANAPA) kwa Watanzania na Dunia kwa ujumla. Kupitia simulizi na picha zenye mvuto, tunalenga kuhamasisha utalii, kuongeza uelewa kuhusu elimu ya uhifadhi ili kutunza na kuendelea kuenzi hazina na maliasili za Taifa letu.

Endelea kufuatilia… safari ndiyo imeanza.

Want your business to be the top-listed Government Service in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Majengo
Arusha
23104